Nenda kwa yaliyomo

Maukib

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Maukib "مُوکِب")
Maukib zikihudumia watu wanaokwenda kuzuru Karbala

Maukib (Kiarabu: مُوکِب ) Ni neno au jina ambalo hutumika katika tamaduni na mila za madhehebu ya Shia, humaanisha kituo cha huduma ambacho husambaza chakula, maji, chai sharubati n.k kwa wafanyaji ziara au kwa watu wanaojumuika kwa ajili ya kuadhimisha matukio maalumu ya kidini bure bila ya malipo. Kwenye njia ya masafa ya kilomita kadhaa kuelekea Karbala watu wengi huwa watembea kwa miguu katika mnasaba wa Arbaeen ya Imamu Hussein (a.s). Katika hali hiyo, maukib au kwa jina jengine vituo vya huduma, huwa vipo kila mahala njiani humo vikitoa huduma za malazi, afya na matibabu, masaji ya mwili na miguu, pamoja na ukarabati wa vifaa mbali mbali. Neno hili lilikuwa ni istilahi maalumu katika utamaduni wa Mashia wa Iraq, na liliingia ndani ya tamaduni za watu wa Iran katika miaka ya tisini Shamsia. Kabla ya hapo, watu wa Iran walikuwa na utamaduni wa kuweka vituo vilivyokuwa vikijulikana kwa jina la "vituo vya Salawati" «ایستگاه صلواتی» vyenye kazi sawa na maukib za nchini Iraq.

Neno "maukib" linatokana na lugha ya Kiarabu, ambapo katika tamaduni na mila za Kishia, neno maukib "موکب" lina maana ya kundi la watu wanaotembea kwa mfumo unaofanana maandamano katika kuadhimisha maombolezo ya tukio fulani. Katika nchi ya Iraq, mara nyingi neno hili huwa linatumika katika ibara yenye maneno mawili pacha; «موکبُ الْعَزاء» "Kundi la Maombolezo" na «موکبٌ خِدْمیّ؛ موکب » "Kundi la Kutoa Huduma". Pia desturi ya kuanzisha makundi kama haya, inaonekana kushamiri nchini India na Pakistani. Mara nyingi gharama za kusimamisha makundi haya huwa zinatokana na mfuko wa watu binafsi pamoja na wafadhili maalumu.


Welewa wa dhana

Neno Maukib موکب, limaana ya kituo cha huduma [1] ambacho hutoa huduma za bure kwa wanaofanya ziara [2] au kuadhimisha minasaba maalumu katika madhehebu ya Shia [3]. Vituo vya utoaji huduma, kuwekwa kwenye mahema, mabanda yaliyojengwa kwa maturubali au majengo ya kawida. [4]


usuli

Neno "maukib موكب" katika utamaduni wa Washia wa Kiarabu, humaanisha chama au umoja na ushirika wa kundi la watu wanaojishughulisha na harakati za uombolezaji, [5] mkusanyiko wa waombolezaji, [6] gurupu la watu wanaotembea huku wakiomboleza kwa mfumo wa kimaandamano, [7] [Maelezo 1] katika kitabu Aadabu Al-Taffi kilichoandikwa mnamo mwaka 1347 Shamsia, [8] kimenukuu ya kwamba; unapokaribia msimu wa maombolezo ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), huwa kuna makundi ya watu wanaotoka katika miji na vitongoji mbalimbali na kuja kujenga mahema na mabanda kwenye njia ipitwayo na misafara ya wafanya ziara wanaoelekea Karbala kwa ajili ya kuzuru kaburi la Imamu hussein (a.s), wao hujenga mahema na mabanda hayo kwa ajili ya kutoa huduma kwa wanamsafara hao wanaoelekea Karbala. [9]

Utamaduni wa kuanzisha vituo vya kuhudumia wafanya ziara au waombolezaji, uliingia kutoka Iraq na kuja Iran mnamo miaka ya tisini. [12] Bila shaka kabla ya utamaduni huo kuingia Iran, Wairani walikuwa na utamaduni wa kujenga au kuweka vituo viitwavyo "ایستگاه صلواتی Vituo vya Kumsalia Mtume (s.a.w.w)". [Maelezo 2] vituo hivyo vilivyokuwa vikiitwa "Istigahe Salawatiy ایستگاه صلواتی vituo vya Kumsalia Mtume (s.a.w.w)", vilikuwa na kazi sawa na vile vituo vya Iraq. [13] Majina mawili "Istigahe "ایستگاه صلواتی na "موکب" wakati mwengine Waajemi (Wairani), huyatumia majina hayo kwa maana mbadala. Yaani wakati mwengine hulitumia neno "maukib موکب" kwa maanaya ya kituo, na pia kwa maana ya mkusanyiko wa waombolezaji, na wakati mwengine hulitumia neno "Istigahe Salawatiy ایستگاه صلواتی" kwa maana ya kituo na pia kwa maana ya mkusanyiko wa waombolezaji [14]

Huduma

Huduma zote zinazotolewa katika vituo vya kuwahudumia maombolezaji na wetembeaji kwa miguu katika maadhimisho ya Arubaini ya Imamu Hussein, zikiwemo usambazaji wa chakula, chai pamoja na sharubati [15] na kupiga kiwi (kutia rangi) viatu[16] huwa ni bure kabisa. Katika vituo vilivyoko njiani kwenye barabara ya watembeaji kwa miguu katika maadhimisho ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), watu hupata huduma kadhaa, zikiwemo huduma za chakula, malazi, afya na matibabu, masaji ya mwili na miguu pamoja na ukarabati wa vifaa mbali mbali. [17]

Ukiachana na huduma za kuwahudumia waombolezaji, pia katika baadhi ya vituo hivyo vinavyosaidia wafanya ziara, husaidia watu katika matukio ya mabalaa yanayotokea bila ya kutarajiwa; kama vile matetemeko ya ardhi na mafuriko. Katika matukio kama hayo, wao huwasambazia watu vitu muhimu wanavyo hitajia kama vile; chakula, mahema, blanketi pamoja na maji. [18] Bajeti ya uendeshaji wa vituo na huduma zinazotolewa vituoni humo hutolewa kupitia michango ya umma [19] na wakati mwingine kupitia mfuko wa serikali. [20]

Wakati na mahali panapojengwa vituo

Maukib zikiwa pembezoni mwa barabara kuelekea Karbala

Ujenzi wa vito kwenye hafla mbalimbali za madhehebu ya Shia, ikiwemo ujenzi wa vituo kwenye njia ya watembeaji kwa miguu katika maadihimisho ya Arubaini, [21] mwezi wa Muharram, [22] mwezi 15 Sha'aban, [23] na kwenye maadhimisho ya kumbukumbu za kuuawa kishahidi na kwenye maadhimisho ya kuzaliwa kwa Maasumina (a.s) [24] katika vitongoji na miji ya Shia. Pia kuna vituo kadhaa vilivyojengwa katika maeneo matakatifu yenye hadhi maalumu mbele ya Mashia; kama vile kwenye maeneo ya makaburi ya Maimamu (a.s). Vituo vimejengwa katika maeneo hayo, ili kutoa huduma maalumu kwa wanaofanya ziara katika maeneo hayo. [25]

Pia huwa kua vituo kadhaa vinavyojengwa kwenye njia ya msafara wa kutoka mji wa Najaf kuelekea Karbala, unaofanyika mwezi 15 Sha'aban. [26] Katika hafla ya maadhimisho ya Idi ya Ghadir (Siku Kuu) ijulikanayo kwa jina la "Mehmaniy Dah Kilomitriy مهمانی ده کیلومتری", yenye maana ya "Wageni wa Kilomita Kumi" inayofanyika mjini Tehran, pia hujengwa vituo kama hivyo kwa ajili ya kuwahudumia watu katika hafla hiyo. Kwa mfano katika sherehe za hafla ya Idi hiyo iliyofanyika mwaka 1401, kulijengwa idadi ya vituo 350 kwa ajili ya kuhudumia watu waliohodhuria katika hafla hiyo. [27]


Kwenye matembezi ya maadhimisho ya Arubaini

Tizama pia: Tamaduni za maandamano ya Arubaini

Ujenzi wa vituo vya huduma kwenye njia ipitwayo na waendao kwa miguu katika maadhimisho ya Arubaini, hutendeka kupitia vikundi vyenye ushirikano katika mambo ya kidini nchini Iraq, pia kupitia wakazi asili wa vitongoji na vijiji vilivyoko karibu na mapito ya watu hao wanaotembea kwa miguu wakielekea Karbala. [28] Ujenzi pamoja na uendesahaji wa vituo hivyo, hushughulikiwa na wakazi wenyewe wa maeneo hayo, bila ya kuwepo mkono wa serikali ya Iraq. [29]

Kwa mujibu wa ripoti ya "Idara ya Usimamizi wa Mbio za Kidini, Vituo vya Huduma na Huseiniyyh huko Iraq" inafanya kazi zake chini ya usimamizi wa "Jumuia ya Quds Hosseini na Abbasi". Katika siku za maadhimisho ya Arubaini ya mwaka 1399 Shamsia, kulikuwa na idadi ya vituo elfu 32 kutoka ndchi nzima ya Iraq, vilivyokuwa vikihudumia watu katika maadhimisho hayo. [30] Kulingana na ripoti ya "Jumuia Quds Abbasi", ya Arubaini ya mwaka 1401 Shamsia, katika eleo la Karbala na barabara zinazoelekea huko, kulijengwa vituo 14,500, ambapo vituo 300 vilianzishwa kutoka nchi nyingine ikiwemo Iran. [31]

Jumuiya ya Astan Quds Abbasi ikitoa takwimu ya idadi ya vyakula ya mwaka 1401 Shamsia, imesema kwamba; kuna zaidi vyakula milioni nne vilivyosambazwa na kugawiwa huko Karbala pamoja na maeneo ya jirani kwa ajili ya watu wafanya ziara na waombolezaji nchini humo. [32]

Vituo katika nchi zinazoishi Mashia

Ukiachana na Iraq na Iran, pia katika nchi nyingine zinazoishi Mashia ndani yake, huwa kuna utamaduni wa kujenga au kutenga maeneo maalumu ya kuwahudumia watu katika hafla mbali mbali za kidini. [33] Nchini Pakistan na India, vituo vitoavyo huduma ya maji huitwa "Sabiil سَبیل", na vituo vitoavyo huduma ya chakula huitwa "Niaz Hussein نیازِ حسین". [Maelezo 3] Nchini Pakistan, Masunni pia nao katika masiku ya Muharam hujenga vituo vya "Sabiil سَبیل" na "Niaz Hussein نیازِ حسین". Mingoni mwa vyakula maarufu vinavyogawiwa katika maadhimisho ya sherehe au maombolezo maalumu ya kidini nchini Pakistan, ni bokoboko na biriyani. [37]