Mauaji ya Hospitali ya al-Ma'madani
Makala hii au sehemu ya makala hii ni tukio la siku. Inawezekana kwa kupita zama, taarifa zikabadilika kwa haraka. Yumkini habari na taarifa za awali zikawa hazina itibari na habari za hivi punde kabisa kuhusu makala hii huenda zisiakisi tukio lote. Tafadhali chukua hatua ya kuboresha makala hii.
Mauaji katika Hospitali ya al-Ma'madani (Kiarabu: مجزرة مستشفى المَعمَداني) yalitokea 17 Oktoba 2023 kufuatia shambulio la anga la jeshi la Israel. Hujuma hiyo ya anga dhidi ya hospitali hiyo iliyoko Gaza, Palestina ilipelekea zaidi ya watu 500 kuuawa.
Mauaji Dhidi ya Raia
Tarehe 17 Oktoba 2023, jeshi la Israel lilitekeleza shambulio la anga dhidi ya Hospitali ya al-Ma'amadani au al-Ahli al-Arabi huko Gaza ambapo ndani yake walikuweko majeruhi na wakimbizi wa Kipalestina waliokuwa wameomba hifadhi katika hospitali hiyo. Katika shambulio hilo, zaidi ya raia 500 waliuawa. [1] Idadi ya waliouawa karika shambulio hilo imetajwa pia kuwa ni 800 [2] na 1000 pia. [3] Msemaji wa Wizara ya Afya ya Palestina huko Gaza amesema, akthari ya wahanga hao walikuwa wanawake na watoto. [4] Duru za habari zinayataja mauaji hayo kuwa ni Holocaust (mauaji ya halaiki) ya kweli na jinai ya kivita. [5]
Sababu na Lengo
Lengo la shambulio hilo na kuwaua raia ni kuwalazimika wakati wa Gaza wahame na kuondoka katika eneo hilo. Shambulio hilo ni radiamali na jibu dhidi ya Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa, iliyotekelezwa na vikosi vya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina. Oktoba 7, 2023, wanamuqawama wa HAMAS walitekeleza operesheni katika fremu ya kukomboa ardhi za Palestina kutokana na Israel ardhi kuendelea kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina, operesheni ambayo ilikuwa ya aina yake na ambayo kwa hakika haijawahi kushuhudiwa na hata inatajwa kuwa ni pigo dhidi ya Israel ambalo haiwezi kulifidika. Shirika la Habari la Reuters, limelitaja shambulio dhidi ya Hospitali ya al-Ma'madani kuwa tukio kubwa la mauaji ya Israel la kulipiza kisasi dhidi ya mashambulio ya Hamas kupitia Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa. [6] Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa, kwa kufanya mashambulio kama hayo, Israel haiwezi kufidia kipigo na kushindwa kwake katika Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa.
Radiamali
Maandamano dhidi ya Israel katika maeneo mbalimbali ya dunia
Shirika la Habari la Reuters linaripoti kuwa, katika radiamali dhidi ya mashambulio hayo ya kinyama ya Israel, kumefanyika mikusanyiko na maandamano katika mataifa mbalimbali ya Kiislamu na yasiyokuwa ya Kiislamu na watu wamejitokeza katika bararaba [7] na mitaa ya miji mbalimbali na kuandamana kulaani jinai hiyo. Nchini Jordan ubalozi wa Israel umechomwa moto. [8] Mataifa mengi ya dunia ikiwemo Iran, Iraq, Jordan, Ufaransa, Saudi Arabia, Uhispania, Uturuki, Misri, Qatar na Syria yamelaani shambulio hilo na katika nchi kama Iran, Iraq, Jordan, Lebanon, Kuwait na Qatar kumeshuhudiwa maandamano makubwa pia ya kulaani jinai hiyo. [9] Waandamanaji wametoa mwito kwa nchi za Kiislamu kuchukua hatua kama hiyo katika kuwaunga mkono wananchi wa Palestina na kutoa mwito wa kushtakiwa Israel katika asasi na mahakama za kimataifa.
Kutangazwa Maombolezo ya Umma na Kufungwa Hawza za Kishia
Kufuatia mauaji hayo, nchini Iran kulitangazwa siku moja ya maombolezo ya umma, [10] huku Iraq, [11] na Syria [12] zikitangaza siku tatu za maombolezo ya umma. Nchini Iran rangi ya kuba la Haram ya Imamu Ridha (a.s) imebadilishwa na kuwekwa nyeusi kuonyesha ishara ya huzuni na simanzi. [13] Kadhalika Hawza (vyuo vikuu vya kidini) nchini Iran vilifungwa [14] huku Hawza ya Najaf (15] ikitangazwa kufungwa tarehe 18 Oktoba 2023. Katika mji wa Qom, Iran wanafunzi wa masomo ya dini, walimu, masheikh na viongozi wa kidini walishiriki katika maandamano ya kuulaani utawala wa Kizayuni wa Israel kwa mauaji yake hayo ya Gaza. [16] Ayatullah Noori Hamedani, mmoja wa Marajii Taqlidi wa Kishia anayeishi Qom, Iran, alitoa ujumbe an kulaani shambulio hilo la mauaji na kuyataka mataifa ya Kiislamu na wananchi wa Iran wasisite kutoa msaada wowote ule kwa wananchi wa Gaza.
Katika mazungumzo yake na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), Hussein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alitoa mwito wa kususiwa bidhaa za Israel na kutimuliwa mabalozi wote wa Israel walioko katika mataifa ya Kiislamu na kusitishwa usafirishaji mafuta kuelekea Israel. [17] Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani mauaji ya mamia ya raia na kulitaja shambulio hilo kuwa la kutisha. [18] Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kuitisha kikao cha dharura kwa ajili ya kujadili shujuma na shambulio hilo la kijeshi la Israel. [19] Serikali ya Russia imeyataja mauaji hayo kuwa ni jinai, yasiyo ya kibinadamu na ya kumuacha mtu kinywa wazi. [20] Kanali ya Televisheni ya al-Jazeera imeripoti kuwa, kufuatia shambulio hilo, kikao cha pande nne ambacho kilipangwa kufanyika nchini Jordan kwa kuhudhuriwa na Rais Joe Biden wa Marekani, Rais Abdul-Fattah al-Sisi wa Misri, na Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kimefutwa. [21]
Kutumia Mabomu ya Marekani
Vyombo vya habari vimelinukuu gazeti la Marekani la The Wall Street Journal na kutangaza kuwa, katika shambulio hilo Israel imetumia bomu aina ya MK-84 la Marekani. [22] Pamoja na hayo, viongozi wa Israel na Marekani wamedai kwamba, mlipuko katika Hospitali ya al-Ma'madani ulisababishwa na operesheni iliyofeli ya kombora la Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina. [23]
Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina sambamba na kukanusha madai hayo ya Israel imeeleza kuwa, kukana Israel kuhusika na shambulio hilo ni kukwepa kubeba dhima na masuuliya ya jinai hiyo. Harakati hiyo imesisitiza kuwa, Israel imetoa vitisho mara chungu nzima kushambulia kwa mabomu ya hospitali hiyo na hospitali zingine za Gaza kwa kuwataka walioko waondoke. Kadhalika ripoti zao zinazogongana kuhusiana na mauaji hayo ni ushahidi na ithbati ya uongo wao. [24] Kanali ya televishebni ya NBC imenukuliwa ikitangaza kuwa, Wapalestina hawana silaha yenye nguvu ya kuharibu na kulipua namna hii, na Israel ina historia ya kusema uongo na kuwasingizia wengine. [25] Mwandishi wa habari wa BBC amenukuliwa akisema, kwa kuzingatia ukubwa wa mlipiko huo, ni vigumu kukubali kwamba, shambulio la kombora lililofanyika halikutekelezwa na Israel. [26]
Vyanzo
- Al-Hauzah al-'Ilmiyyah Fī an-Najaf Tu'lin al-Haddād Wa Thu'atthil Durūsahā. Site Alforatnews. Diakses tanggal 18 Oktober 2023.
- al-Urdun Yulghī al-Qummah ar-Rubā'iyah Ma'a Biden Wa as-Sīsī Wa Abbās Ba'd Qashf al-Mustasyfā Bi Gazzah. Site Aljazeera. Diakses tanggal 18 Oktober 2023.
- Amir Abdullahiyan: Khastar-e Tahrim-e Fauri Wa Kamel Rezim-e Sahyunisti Tawassuthe Kasywarha-e Eslami Hastim. Diakses tanggal 19 Oktober 2023.
- Ayatullah Nuri Hamedani: Saran-e Kesywarha-e Eslami Be Ja-e Bayaniye Eqdam-e Amali Kunand. Site Farsnews. Diakses tanggal 19 Oktober 2023.
- Bisy Az 800 Syahid Dar Bumbaran-e Bimarestan-e al-Ma'madani Gazze. Mehrnews. Diakses tanggal 18 Oktober 2023.
- Bom-e Enfejari Dar Bimarestan-e Gazze, Amrikai Bud. Site Mehrnews. Diakses tanggal 20 Oktober 2023.
- Cahar Syanbe Dar Sarasar-e Kesywar Aza-e Umumi Ast. Site Farsnews. Diakses tanggal 18 Oktober 2023.
- Darkhast-e Ekhraj-e Safire Sahyunisti Az Turkiye. Site Tasnimnews. Diakses tanggal 19 Oktober 2023.
- Faje'e-e Bumbaran Wa Kusytar-e Bimarestan-e al-Ma'madani-e Gazze; Elal Wa Ahdaf. Site Alalam. Diakses tanggal 19 Oktober 2023.
- Holocaust-e Waqi'i In Tashwir Ast. Site Mashreghnews. Diakses tanggal 18 Oktober 2023.
- Israel-Hamas War Israelis and Palestinians Blame Each Other for Blast at Gaza Hospital That Killed Hundreds. Site The New York Times. Diakses tanggal 18 Oktober 2023.
- Jahad-e Eslami Edde'aha-e Rezim-e Sahyunisti Ra Rad Kard. Site Farsi Palinfo. Diakses tanggal 18 Oktober 2023.
- Lahze Be Lahze Ba Dawazdahumin Ruz-e Amaliyat-e Thūfān al-Aqshā. Site IRNA. Diakses tanggal 18 Oktober 2023.
- Mahkumiyat-e Gustarde-e Bumbaran-e Bimarestan-e Ma'madani Dar Gazze.' Site Farsi Palinfo. Diakses tanggal 18 Oktober 2023.
- Marasem-e Musytarak-e Danesy Amukhtagi Danesyjuyan-e Danesygaha-e Afsari-e Niruha-e Musallah. Site Farsi Khamenei. Diakses tanggal 19 Oktober 2023.
- Moskow: Hamle Be Bimarestan-e Gazze Jenayat Ast. Site IRNA. Diakses tanggal 18 Oktober 2023.
- Nesyast-e Syura-e Amniyat-e Sazman-e Melal Dar Bar-e Bumbaran-e Bimarestan-e Gazze. Site DW. Diakses tanggal 18 Oktober 2023.
- Reactions to strike on Gaza hospital killing hundreds. Site Reuters. Diakses tanggal 18 Oktober 2023.
- Suriye Se Ruz Aza-e Umumi E'lam Kard. Site IRNA. Diakses tanggal 18 Oktober 2023.
- Syuke Jahani Ba'd Az Bumbaran-e Bimarestan-e Gazze/Holocaust-e Waqe'i In Jast. Site Khabaronline. Diakses tanggal 18 Oktober 2023.
- Ta'tili-e Darsha-e Hauze-e Ilmiye Dar Vakunesy Be Hamle-e Wahsyiyane Be Bimarestan Dar Gazze. Site ABNA24. Diakses tanggal 18 Oktober 2023.
- Televiziun-e Amrikai: Israel Durughgust. Site Mashreghnews. Diakses tanggal 18 Oktober 2023.
- Wall Street Jurnal: Bimarestan-e al-Ma'madai-e Gazze Ba Bumb-e Amrikai Bumbaran Syud. Site Alalam. Diakses tanggal 18 Oktober 2023.
- Wezarat-e Behdasyt-e Gazze: Aghlab-e Qurbaniyan-e Faje'e-e Bimarestna-e al-Ma'madani Zan Wa Kudak Hastand. Site Alalam. Diakses tanggal 18 Oktober 2023.
- What we know about the Gaza hospital blast. Site NBC News. Diakses tanggal 19 Oktober 2023.
- What we know so far about the deadly strike on a Gaza hospital. Site Aljazeera. Diakses tanggal 18 Oktober 2023.