Nenda kwa yaliyomo

Masunni wanaoshikamana na Maimamu 12

Kutoka wikishia

Masunni wanaoshikamana na Maimamu 12 (Kiarabu: التسنّن الاثنا عشري) ni muelekeo wa kimadhehebu baina ya Waislamu wa madhehebu ya Suni ambao mbali na kuwa na imani na Makhalifa Watatu, wana mapenzi na itikadi pia na Wilaya (uongozi) ya Maimamu Kumi na Mbili wa Waislamu wa madhehebu ya Shia. Inaelezwa kuwa, mazingira ya muelekeo huu yaliibuka katika karne za mwanzo tu za Uislamu na ilikuwa ni katika kukabiliana na kundi la wafuasi wa Othman bin Affan lililokuwa likimpinga Imamu Ali (a.s). Hata hivyo kipindi cha kuenea kwake ni kuanzia karne ya 6 Hijiria na awali pote hilo lilikuwa nchini Iran kisha India na baadaye katika baadhi ya maeneo ya mashariki mwa Khorasan Kubwa na ardhi zilizokuwa chini ya udhibiti wa Ukhalifa wa Othman.

Istilahi ya Masunni wanaoshikamana na Maimamu 12 ni anuani mpya iliyochukuliwa katika utafiti wa historia ya Iran; lakini baadhi ya watafiti, wakitegemea nakala ya hati ya mkono wamesema kwamba ilitumika pia katika zama za utawala wa Safavi. Baadhi ya mambo yaliyopelekea kuundika na kuibuka Usuni wa Maimamu Kumi na Mbili yamesemwa kama ifuatavyo: Kuanguka kwa utawala wa Abbasi, ustahamilivu wa kimadhehebu wa Ilikhan Mongol na Maamiri wa Timuri, kukua kwa Usufi na mamlaka ya Masufi na kukurubiana Usufi na Ushia.

Wanahistoria wanazichukulia Sunnah za Maimamu Kumi na Wawili kuwa ni miongoni mwa sababu kuu za kuenea Ushia katika Mashariki ya Kiislamu hususan Iran na sababu kuu ya kudhihiri serikali ya Kishia ya utawala wa ukoo wa Safavi. Kwa mujibu wao, kuwepo kwa serikali zenye utendaji wa Usuni wa Maimamu Kumi na Wawili katika muda wote wa karne ya 9 na 10 Hijria kulitayarisha uwanja wa mabadiliko ya kidini ya Wairani kutoka Sunni hadi Shia.

Nchini Iran, katika karne ya 9 na 10 Hijiria, kuliundwa serikali zenye muelekeo wa Usuni wa Maimamu Kumi na Mbili. Pia, watu mbalimbali wa kitamaduni wamezingatiwa kuwa wana mwelekeo wa Usuni wa Maimamu Kumi na Wawili, na katika kazi zao, pamoja na kuwataja makhalifa watatu, wamewataja Maimamu wa Kishia kuwa mahuja (hoja) Maasumu wa Kiungu.

Utambuzi wa maana na nafasi

Masunni wanaoshikamana na Maimamu 12 ni muelekeo wa kimadhehebu baina ya Waislamu wa madhehebu ya Suni ambao mbali na kuwa na Imani na Makhalifa Watatu wana mapenzi na itikadi pia na Wilaya (uongozi) ya Maimamu Kumi na Mbili wa Waislamu wa madhehebu ya Shia na Maasumina 14 (a.s). [1] Usuni wa Maimamu Kumi na Wawili unatambuliwa kuwa miongoni mwa sababu kuu za kuenea kwa Ushia katika Mashariki ya Ulimwengu wa Kiislamu hususan Iran kuanzia karne ya 6 na kuendelea. [2] Pia wanahistoria wanachukulia kuenea kwa muelekeo wa Usuni wa Maimamu Kumi na Wawili nchini Iran kama sababu kuu ya kuanzishwa na kutokea kwa dola ya Kishia ya Safavi, [3] na wanasema kwamba hayo ni moja ya mageuzi na matukio muhimu ya kifikra na kimadhehebu nchini Iran na moja ya sababu zilizokuwa na mchango mkubwa katika kupunguza migogoro na mizozo ya kimadhehebu ya kati ya Shia na Sunni baada ya karne ya 7 Hijria. [4]

Utambuzi wa istilahi

Istilahi ya Masunni wanaoshikamana na Maimamu 12 ni anuani mpya iliyochukuliwa katika utafiti wa historia ya Iran [5] Inaelezwa kuwa, anuani hii haijaja katika vyanzo wa kihistoria; [6] lakini baadhi ya watafiti, wakitegemea nakala ya hati ya mkono wamesema kwamba, istilahi hii ilikuweko na ilienea mwishoni mwa zama za utawala wa Safavi (1090 Hijiria). [7]

Matumizi na maelezo ya neno hili yamehusishwa na makala ya Muhammad Taqi Danesh Pajouh (1290-1375 AH), mtafiti na mwandishi wa nakala wa Kiirani ambayo imenasibishwa katika mwaka wa 1344 AH. [8] Lakini wanasema kwamba anuani hii imeenezwa na kubainishwa pakubwa katika athari na kazi za Rasul Jafarian. [9]

Historia fupi

Kulingana na baadhi ya watafiti, pote la Sunni wa Maimamu Kumi na Wawili liliibuka takribani karne ya 6 Hijria; [10] msingi wake ulitolewa katika karne za kwanza za Uislamu na hilo lilikuwa kwa ajili ya kukabiliana na Ahlu-Sunna waliokuwa na madhehebu ya Kiothmani ambao hhawakuwa wakitambua uhalali wa Ukhalifa wa Imamu wa Imam Ali (a.s); [11] kwa sura hii kwaba, katika kukabiliana na kundi la Othmania, kuna watu waliokuwa wakifanya juhudi za kueneza fadhila za Imamu Ali (a.s) na Ahlul-Bayt (a.s) wengine wa Mtume. [12] Katika vitabu vya kali vya wasifu wa wapokezi wa hadithi vya Ahlu-Sunna watu hawa wametajwa kuwa ni "Masunni waliongia katika Ushia" au "Masuni wanaotuhumiwa kwa Ushia". [13]

Kwa mujibu wa Ja’farian, juhudi za kiitikadi za kundi hili la Ahlul-Sunna zilipelekea katika karne ya Sita Hijiria kutokea marekebisho na mabadiliko ya namna fulani katika madhehebu ya Kisunni. [14] Marekebisho haya, yaliyojikita kwenye huba na kuwapenda Ahlul-Bayt (a.s), kuandikwa vitabu kuhusu fadhila za Ahlul Bayt (a.s) baina ya Masuni. [15] Miongoni mwa watu waliokuwa na nafasi na mchango mkubwa katika uga huu ni shakhsia wa kimadhehebu na kielimu wenye taathira kama Ahmad bin Hanbal (164-241 Hijiria) mmoja wa mafaqihi wanne wa Kisunni, na Muhammad bin Jarir al-Tabari (aliyefariki dunia: 310 Hijiria). [16]

Baadhi ya mambo yaliyopelekea kuundika na kuibuka Usuni wa Maimamu Kumi na Mbili yametajwa kama ifuatavyo: Kuanguka kwa ukhalifa/utawala wa Abbasi, [17] ustahamilivu wa kimadhehebu wa Ilikhan Mongol [18] na Maamiri wa Timuri, [19] kukua kwa Usufi na mamlaka ya Masufi [20] na kukurubiana Usufi na Ushia. [21]

Inaelezwa kuwa, awali pote hili lilikuweko Iran kisha India na baadaye katika baadhi ya maeneo ya mashariki mwa Khorasan Kubwa na ardhi zilizokuwa chini ya udhibiti wa Ukhalifa wa Othman. [22] Kadhalika kuna ripoti zinazoonyesha kwamba, kuundwa kwa utawala wa Safavi kulipelekea kumalizika na kutokomea kwa utendaji huu nchini Iran. [23]

Masunni wanaoshikamana na Maimamu 12 katika uga wa kisiasa

Kwa mujibu wa baadhi ya wanahistoria, mabadiliko na mageuzi ya kimadhehebu ya Wairani kutoka Sunni hadi Shia yalitokea kupitia kuwekwa kwa Usuni wa Maimamu Kumi na Wawili katika uga wa siasa na mamalka. [25] Ripoti zinaonyesha kuwa, katika karne za 9 na 10 Hijiria, kuliingia madarakani tawala ambazo zilikuwa na utendaji wa Usuni wa Maimamu Kumi na Mbili. [26]

Kabla ya hapo pia katika karne ya 8 Hijiria na katika serikali nyingi za Iran na Iraq, kulikuweko na ishara za kuwepo kwa mwelekeo huu; miongoni mwa watawala wa kwanza wa serikali ya Sarbadaran, walikuwa na mwelekeo huu. [27]

Katika karne ya 9 Hijiria, Sultan Hossein Bayqara, mmoja wa watawala wa Timuri, alikuwa na mwelekeo wa Suni wa Maimamu Kumi na Wawili na alitaka kutoa mahubiri kwa jina la Maimamu Kumi na Wawili (a.s), lakini Abdul Rahman Jami [28] ] na Amir Alishir Navai walimkataza kufanya hivyo. [29] Katika zama hizo, Jahanshah Qara Qoyunlu alitengeneza sarafu ambazo zilikuwa na maneno Ali Waliullah upande mmoja na majina ya Makhalifa khulafaa rashidin. [30] Hatua hii imezingatiwa kama ishara ya mwelekeo wa serikali yake pote la Usuni wa Maimamu Kumi na Mbili. [31]

Mwenendo wa kimadhehebu wa Safavi pia umesawiriwa kwa namna ambayo walikuwa Masunni mwanzoni, kisha wakafuata Usuni wa Maimamu Kumi na Wawili, na baada ya hapo wakaingia kwenye madhehebu ya Shia. [32] Baadhi ya wanahistoria wanatoa dalili za kuwepo kwa ishara kama hiyo hata katika serikali ambazo zilikuwa nembo ya Usuni kama vile serikali ya Othmania. [33]

Masunni wanaoshikamana na Maimamu 12 katika uga wa kiutamaduni

Watu mbalimbali wa kitamaduni, kuanzia karne ya sita hadi kuporomoka kwa utawala wa Safavi, walikuwa na mwelekeo wa Usuni wa Maimamu Kumi na Wawili. [34] Rasul Ja’farian anaamini kwamba, katikati ya karne ya nane hadi ya kumi, kulizalishwa kazi na athari nyingi kwa mueleo huu na Ahlu-Sunna; [35] athari mbalimbali za kidini, kihistoria na za kifasihi (mashairi na nyinginezo) ambamo, pamoja na kutajwa kwa Khulafaa Rashidin, Maimamu wa Shia wamewataja kuwa hoja Maasumu (zisizo na dosari) za Kiungu.[36] Baadhi ya shakhsia wenye mwelekeo wa Ahlu-Sunna wa Maimamu Kumi na Mbili na kazi zilizoandikwa kwa mwelekeo huu ni kama ifuatavyo:

  • Mwandishi asiyefahamika wa kitabu cha “Mujmal al-Tawarikh wal-Qisas” (kiliandikwa mwaka: 520 Hijiria), kitabu hiki kina muelekeo wa Usuni wa Maimamu Kumi na Mbili. [37] Katika kitabu hiki baada ya kusimulia historia ya makhalifa, mwandishi anajihusisha na kutaja historia ya Maasumina 14 (a.s). [38]
  • Abu Muhammad Abdul-Aziz bin Muhammad Hanbali Junabidhi (aliaga dunia: 611 Hijiria), kitabu cha Maalim al-Itrat al-Nabawiyyah wa Maarifa Ahli-Bayt al-Fatimiyah alalawiyah. Kitabu hiki kinabainisha na kutoa ufafanuzi wa hali ya Maimamu wa Kishia mpaka Imamu wa 11. [39]
  • Muhammad bin Yusuf Ganji Sahi (aliaga dunia: 658 Hijiria), kitabu cha Kifayat al-Talib kimeandikwa kuhusiana na fadhila za Imamu Ali (a.s) na Ahlul-Bayt. [40]
  • Hamdullah Mustawfi (aliaga dunia baada ya 750 Hijiria), ufafanuzi wa hali ya makhalifa na Maimamu (a.s) anawataja Miamamu wa Kishia kuwa ni “Aimamat Maasumina, [41] wa Hujat al-Haqq alal-Khalq” [42] [43]
  • Shamsuddin Muhammad Zarandi Hanafi (aliaga dunia: takribani mwaka 750 Hijiria), katika kitabu cha Nudhum Durari al-Shamtayn na Maarij al-Usul il Maarifat Fadhl Aal al-Rasul. [44]
  • Abdul-Rahman Jami (817-898 Hijiria), mshairi wa Kihanafi na Sufi wa Kinaqshabandi. Katika kitabu hiki licha ya kutokuwa na mtazamno mzuri na Mashia. Lakini anaonyesha huba na mapenzi yake kwa Maimamu wa Kishia. [46]
  • Mulla Hussein Waidh Kashifi (aliaga dunia: 910 H), katika akthari ya athari na vitabu vyake [47] zikiwemo Rawdhat al-Shuhadaa ambacho ni ishara ya kuenea maombolezo ya Imamu Hussein (a.s) baina ya Masuni alifahamika kama Suni wa Maimamu Kumi na Mbili. [48]
  • Fadhlull bin Ruzbahan Khunnji Shafii (aliaga dunia: 953 Hijiria) katika Wasilat al-Khadim ila al-Makhdum. [49]
  • Shamsuddin Muhammad bin Tulun (aliaga dunia:953) katika kitabu chake cha Sharatar al-Dhahabiyah fi Tarajumi al-Amimat al-Ithna Ashar Inda al-Imamiyah. [50]
  • Shahabuddin Ahmad bin Hajar Haythami Shafii (909-974), katika Sawaiq al-Muhriqah. [51]
  • Jamal al-Din Abdallah bin Muhammad Shabrawi Shafii (1092-1172) katika al-It’haf Bihubbi al-Ashraf. [52]
  • Suleiman bin Ibrahim Qunduzi Hanafi (1220-1294) katika Yanabiu al-Mawaddah. [53]
  • Muumin bin Hassan Shablanji Shafii (1250-1308 H) katika Nur al-Absar. [54]