Masoud bin Hajjaj Taymi

Kutoka wikishia
Faili:امگاه شهدای کربلا2.jpg
Makaburi ya halaiki ya mashahidi wa Karbala

Masoud bin Hajjaj Taymi (Kiarabu: مسعود بن حَجّاج تَیْمی) ni mmoja wa masahaba wa Imamu Hussein (a.s) [1] na pia ni katika mashahidi wa Karbala. [2]

Samawi katika kitabu chake cha Ibsar al-Ain amemtambulisha Masoud Hajjaj na mwanawe Abdul-Rahman kwamba, ni katika Mashia na mashujaa mashuhuri wa Kufa. Kwa mujibu wake ni kwamba, Masoud bin Hajjaj akiwa pamoja na mwanawe waliondoka katika mji wa kufa kuelekea Karbala wakiwa pamoja na Omar bin Sa’d. [4] Ajiunga na Imamu Hussein (a.s) katika siku ya saba Muharram [5] na alibakia pamoja na Imamu Hussein mpaka alipokuja kuuawa shahidi Siku ya Ashura katika shambulio la kwanza la jeshi la Omar bin Sa’d. [6] Umri wake wakati anauawa shahidi umetajwa kuwa ni miaka 50. [7]

Hajjaj alikuwa akitokana na kabila la Bani Taym. [8]

Ametolewa salamu katika Ziyarat Rajabiyah ya Imamu Hussein (a.s) [9] na Ziyarat al-Shuhadaa. [10]