Nenda kwa yaliyomo

Kusali kimya kimya

Kutoka wikishia

Ikh-faat (Kiarabu: الإخفات) humaanisha kusoma kimya kimya nyiradi au dhikri za swala bila kunyanyua sauti. Dhikri hizo ni kama vile tasbihi nne maarufu za swala zisomwazo badala ya Surat al-Fatiha, Pia Surat al-Fatihah na Surah zisomwazo baada Surat al-Fatihah. Zote zinapaswa kusomwa polepole katika swala ya Adhuhuri na Alasiri. Pia ni Mustahabbu (ni jambo linalopendekezwa) kusali swala za sunna bila kunyanyua sauti katika kusoma nyiradi hizo. Inapendekezwa na inaruhusiwa katika za swala ya Aayat, ambazo husaliwa kutokana na kutokea hali maalumu ya taharuki za kupatwa kwa jua, mwezi na matetemeko ya ardhi.

Uchambuzi wa Dhana

Ikhfaat (kutodhihirisha) ni kinyume cha Jahr (kudhihirisha), maana yake ni kusoma polepole[1] Katika vitabu vya fiqhi neno hili limezungumziwa katika suala la kusoma swala[2] Mafakihi wengi wanaona kwamba kigezo makini cha Ikhfaat, ni kutodhihirisha kiini cha sauti.[3] Na hukumu ya kusadiki kiwango cha sauti ambacho kitahesabiwa kuwa ni kiwango cha chini, hilo litabaki kwenye mikono na desturi za wanajamii.[4]

Yanayopaswa Kutodhihirishwa Katika Swala

Katika hali zifuatazo, ni wajibu kuswali polepole:

  1. Surat al-Fatihah na Sura isomwayo baada yake, katika swala ya Adhuhuri na Alasiri, isipokuwa swala ya Adhuhuri siku ya Ijumaa.[5]
  2. Tasabihatul Arba’a (tasbihi nne maarufu) zisomwazo katika rakaa mbili za mbili za mwisho za swala ya Adhuhuri na Alasiri, na katika rakaa ya tatu ya swala ya Magharibi, na katika rakaa mbili za swala ya Isha.[6]
  3. Dhikri na nyiradi zote za sala ya maaamuma anayesalishwa katika swala ya jamaa.[7]
  4. Swala ya mwanamke anayeswali mbele au katika eneo lenye watu, inapaswa kuswaliwa kimya, ikiwa sauti yake itakuwa inasikika na maharimu wake na kuhofiwa kuleta fitna.[8]
  5. Surat al-Fatihah katika swala ya ihtiaat (sala ya kuyakinisha).[9]

Kwa mujibu wa fatwa za wanazuoni wengi, kuacha au kutochunga kuswali pole pole (kimya kimya) kwa makusudi, kunasababisha swala yako kuwa batili. Bila shaka, ikiwa umefanya hivyo kwa kusahau au kutojua, basi swala yako ni sahihi.[10]

Ya Wajibu na Yanayojuzu Kutodhihirisha

Yafuatayo ni mustahabu (yaliopendekezwa) kutoyadhihirisha:

  1. Swala za mustahabu ziswaliwazo mchana.[11]
  2. Isti'adha (Audhubillahi mina Shaitani Rajiim) isomwayo kabla ya Surat al-Fatihah.[12]

Katika ibada zifuatazo, yajuzu mtu kutodhihirisha ndani ya swala yake:

  1. Surat al-Fatiha katika swala ya Asubuhi, Magharibi na Isha kwa mwanamke. Mwanamke atakuwa na hiari ya kufanya hivyo, iwapo sauti yake itasikika na asiyekuwa maharimu wake.[13]
  2. Zikri au tasbihi mbali mbali za swala, ukiachana na Surat al-Fatihah na tasbihat Arbaa .[14]
  3. Swala ya Ayaat na Tawafu (swala iswaliwayo kutokana na taharuki maalumu, kama vile kupatwa kwa jua, mwezi na matetemeko ya ardhi).[15]

Falsafa ya Kudhihirisha Swala na Kutodhihirisha

Kwa kulingana na hadithI iliyotajwa katika kitabu cha Ilalu Sharaai'i (Sababu za Sheria), ikizungumziwa juu ya sababu ya kuswali kwa jahr (kudhihirisha kwa sauti) na kuswali kwa ikhfaat (kusali kimya kimya) katika swala. Ni kwamba swala ya asubuhi, Magharibi na Isha zilikuwa zikiswaliwa gizani, kwa hivyo ziliswaliwa kwa sauti kubwa ili kuwatanabahisha wengine waelewe kuwa swala ya jamaa tayari inaswaliwa. Lakini kwa upande wa swala ya adhuhuri na alasiri, kwa vile zilikuwa zikiswaliwa mchana, na kila mmoja alikuwa akishuhudia kuswaliwa kwake.[16], hivyo basi hakukuwa na haja ya kuziswali kwa sauti kubwa (jahr).[17]

Rejea

  1. Dehkuda. Lughat Nameye Dehkhuda, di bawah kata Ikhfat.
  2. Hashemi Shahrudi. Farhangge Feqh, juz. 1, uk. 113.
  3. Najafi, Jawāhir Al-Kalām, juz. 9, uk. 379; Thabthabai Yazdi. Al-'Urwah Al-Wutsqā, juz. 1, uk. 650, no. 26; Imam Khomeini. Tahrīr Al-Wasīlah, juz. 1, uk. 166, no. 11.
  4. Khu'i. Mausū'ah Al-Imām Al-Khū'i, juzld. 14, uk. 402; Jahr wa Ekhfāt dar Namāz. Site Paygah-e Ettela' Resani Daftar-e Ayatullah Sistani (https://www.sistani.org/persian/qa/0873/) diakses tanggal 21 Agustus 2021.
  5. Najafi, Majma' Ar-Rasā'il (Muhassya Shahib Jawahir), uk. 253, no. 779; Imam Khomeini, Taudhīh Al-Masā'il (Mah'sha), juz. 1, uk. 549, no. 992; Gulpayganni, Majma' Ar-Rasā'il, juz. 1, uk. 171, soal no. 180.
  6. Amili, Jāmi' Abbāsi, uk. 142; Imam Khomeini, Taudhīh Al-Masā'il (Mah'sha) juz. 1, uk. 556, no. 1003
  7. Thabthabai Yazdi, Al-'Urwah Al-Wuthqā, juz. 1, uk. 790, no. 22.
  8. Fadhil Miqdad, Kanz Al-'Irfān, juz. 1, uk. 130; Imam Khomeini, Taudhīh Al-Masā'il (Mah'sha) juz. 1, uk. 549, no. 994
  9. Najafi, Majma' Ar-Rasā'il (Mah'sha Shahib Jawahir), uk. 328, no. 1022; Imam Khomeini, Taudhīh Al-Masā'il (Mah'sha) juz. 1, uk. 660, no. 1216.
  10. Imam Khomeini, Taudhīh Al-Masā'il (Mah'sha) juz. 1, uk. 550, no. 995
  11. Gulpayganni, Majma' Ar-Rasā'il, juz. 2, uk. 116, uk. 326.
  12. Thabthabai Yazdi, Al-'Urwah Al-Wuthqā, juz. 1, uk. 661; Imam Khomeini, Taudhīh Al-Masā'il (Mah'sha) juz. 1, uk. 559.
  13. Imam Khomeini, Taudhīh Al-Masā'il (Mah'sha) juz. 1, uk. 549, no. 994
  14. Mukhayyar Budan Nesbat be Jahr wa Ekhfāt-e Sāyere Azkār-e Namāz Zuhr wa Asr, Paygah-e Ettelah Resani daftar Ayatullah Makarim Syirazi (https://makarem.ir/main.aspx?typeinfo=21&lid=0&mid=258210&catid=45579) diakses tanggal
  15. Fadhil Miqdad, Kanz Al-'Irfān, juz. 1, uk. 130; Gulpayganni, Majma' Ar-Rasā'il, juz. 1, uk. 253.
  16. Sheikh Saduq. 'Ilal al-Shari'i juz. 1, uk. 549, no. 994.
  17. «فلسفه جهر و اخفات نمازها»، Payghah itilaat rasanii daftar hadharat Ayatullah al-udhmah Makarimu Shirazi.

Vyanzo

  • Amili, Baha'uddin & Sawaji Nizam bin Husain. Jāmi' Abbāsi. Qom: Daftar Entesharat-e Eslami, cet. 1, 1429 H.
  • Dehkhuda, Ali Akbar. Lughat Nāme. Tehran: Mu'assese Lughat Name Dehkhuda, 1377 HS/1998.
  • Fadhil Miqdad, Miqdad bin Abdullah. Kanz Al-'Irfān fi Fiqh Al-Quran. Qom: Entesharat-e Murtazawi, 1425 H.
  • Gulpaygani, Muhammad Reza. Majma' Al-Masā'il. Qom: Dar Al-Quran Al-Karim, 1409 H.
  • Hashimi Shahrudi, Mahmud. Farhange Feqh Muthabeq-e Mazhab-e Ahl-e Beyt. Qom: Muassese Da'irah Al-Ma'arif Feqh-e Eslami bar Mazhab-e Ahl-e Beyt, 1426 H.
  • Imam Khomeini, Ruhullah. Taudhīh Al-Masā'il. Qom: Jami'ah Mudarrisin, 1424 H
  • Imam Khomeini, Ruhullah. Tahrīr Al-Wasīlah. Qom: Dar Al-Ilm.
  • Jahr wa Ekhfāt dar Namāz. Paygah Ettela' Resani Daftar-e Ayatullah Sistani, diakses tanggal 21 Agustus 2021.
  • Khu'i, Abul Qasim. Mausū'ah Al-Imām Al-Khū'i. Qom: Mausu'ah Ihya Athar Al-Imam Al-Khu'i(qs), 1418 H.
  • Mukhayyar Budan Nesbat be Jahr wa Ekhfāt-e Sāyere Azkār-e Namāz Zuhr wa Asr. Site Paygah-e Ettelah Resani daftar Ayatullah Makarim Shirazi, diakses tanggal 2 Agustus 2021.
  • Najafi, Muhammad Hassan. Jawāhir Al-Kalām. Beirut: Dar Ihya' At-Turath Al-Arabi, 1404 H.
  • Najafi, Muhammad Hassan. Majma' Ar-Rasā'il. Mash'had: Muassese Shahib Az-Zaman, 1415 H.
  • Thabathabai Yazdi, Muhammad Kazim. Al-'Urwah Al-Wuthqā. Beirut: Muassasah Al-A'lami lil Mathbu'at, 1409 H.