Kundi la Waliofuzu

Kutoka wikishia

Kundi la Waliookoka au Kundi la Wenye Kufuzu (Kiarabu: الفرقة الناجية) ni ibara iliyokuja katika Hadith ya Mgawanyiko (حدیث افتراق) ambapo ibara hii imefasiriwa kama ni kundi la Shia Imamiyyah. katika Hadith iliyonasibishwa kwa bwana Mtume (s.a.w.w) imeeleza ya kwamba, baada yake ummah wa Kiislamu utagawanyika katika madhehebu au makundi tofauti, na ni mmoja tu kati yao ndilo kundi litakalooka. Imepokewa kutoka kwa Mtume na Imam Ali (a.s) ya kwamba; Madhehebu au litakalookoka ni Mashia wa Ali (a.s) tu. Kuna maandishi tofauti yalioandikwa kuhusiana na mfano hai na halisi wa kundi litakalookoka.

Umuhimu wa Kundi Litakalookoka

Makala asili: Hadithi ya Iftraq

Kundi la Wenye Kufuzu (الفرقة الناجية) maana yake ni kundi au madhehebu ambayo yameokolewa na maangamio katika Siku ya Hukumu, ibara iliyotumika kama ni jina la kundi hilo katika Hadithi inayonasibishwa kwa Mtume (s.a.w.w) ni "Kundi la Waliofuzu". Kwa mujibu wa hadithi hii, Mtume (s.a.w.w) alitabiri kwamba baada yake ummah wake utagawanyika katika makundi 73, na kundi mamoja tu miongoni mwayo ndilo kundi la watu waliofuzu. [1] Kila moja ya madhehebu ya Kiislamu yamejaribu kuelezea vigezo kadhaa ili kuonesha kwamba wao ndiwo mfano hai wa kundi hilo. [2]

Uhalali na Hadhi ya Hadihti Iftiraraq

Kuna mijadala mbalimbali kuhusu usahihi wa Hadithi ya Aftiraq. Ibn Hazmi Al-Andalusi (aliyefariki 456 Hijiria), mmoja wa wanavyuoni wa Kisunni, ameitathmini Hadithi hiyo kwa kusema kwamba; Hadithi hiyi si sahihi na wala haina thamani ya kujadiliwa. [3] Kwa maoni ya Ibn Wazir, mwanachuoni na faqihi wa madhehebu ya Al-Zaidiyyah (aliyefariki 840 Hijiria), amesema ya kwamba; ibara ya mwisho ilioko katika Hadithi hii, ambayo ni ibara semayo "Makundi yatakwenda motoni ila kundi moja tu" ni ibara bandia, ambayo imeongezwa ndani ya Hadithi. [4] Hata hivyo, baadhi ya vitabu vya Hadith vya Shia [5] na Sunni [6] na baadhi ya vitabu kuhusiana na madhehebu na makundi tofauti [7] vimeinukuu na kuikubali Hadith hiyo. Kwa hiyo, imesemwa kwamba Hadithi ya Iftiraq sio tu mashuhuri na mustafidh (Hadithi iliyopokewa na zaidi ya watu wawili katika kila tabaka la wapokezi wake), [8] bali pia ni Mutawatir [9] au imekaria daraja ya Hadithi Mutawatar (iliyopokewa kwa wingi kupitia matabaka tofauti ya wapokezi wailioishi katika zama tofauti). [10]

Wengine miongoni mwa wanazuoni wamesama ya kwamba; Kutokana na ukweli wa kwamba Hadith hii ni Khabarun Wahid (Hadhithi ambayo wapokezi wake wote wanaishia kwa mpokezi mmoja tu wa asili ambaye ndiye aliyesimulia Hadithi hiyo) hufanya Hadithi hii isiwezekane kuitegemewa katika kuthibitisha itikadi na kubainisha madhehebu maongofu ya watu waliofaulu [11] Lakini kwa mujibu wa maoni ya Ayatullah Sobhani, ukweli kwamba Hadith hii imenukuliwa sana katika vitabu vya Shia na vya Sunni, jambo ambalo linapelekea kuiimarisha kutokana na udhaifu wake, na kunukuliwa kwake katika vitabu tofauti kunajenga imani ya kuiamini na kuitegemea Hadithi hii.[12]

Ni Madhehebu Gani ya Watu Waliyooka?

Kuna ikhtilafu baina ya wanazuoni wa dini mbalimbali kuhusu kubainisha mfano hai wa Madhehebu ya watu waliyookoka. Mara nyingi, kila mmoja miongoni mwa madhehebu ya Kiislamu huyachukulia madhehebu yake kuwa ndio madhehebu ya watu waliyookoka, huku wakiyahisabu madhehebu mengine 72 yaliyobaki kuwa ni madhehebu ya watu waliyoangamia. [13] Jamal Al-Din Razi, mmoja wa wanachuoni wa madhehebu ya Shia Imamiyyah, katika kitabu Tabsiratu Al-'Awaam fi Ma'a rifati Maqaalati Al-Anaam, [14] Ja'far bin Mansur Al-Yaman, mmoja wa wanachuoni wa Ismailia, katika kitabu Saraa-iru wa Asraaru Al-Nutaqaa [15] na Shahristan ambaye ni wa mwanazuoni wa Kisunni katika kitabu cha Al-Milalu wa Al-Nihalu [16] kila mmoja miongoni mwao ameyachukulia madhehebu yake kuwa ni mfano hai wa Madhehebu ya watu wailiookoka.

Kila mmoja miongoni mwa watu wa madhehebu mbali mbali wamejaribu kushikama na moja kati ya nukuu za Hadithi inayobainisha suala umma wa Kiislamu kugawanyika makundi 73 [17], Ili kubainisha mfano hai wa madhehebu ya waliookoka kupitia nukuu hiyo ambayo kwa namna moja au nyenyingi, inavutia upande zaidi kuliko upande mwengine. [18] Kwa mujibu wa utafiti wa Ali Aghanuri ni kwamba; Hadithi hii ina aina 15 tofauit za tafsiri katika nukuu zake kuhusiana na ufafanuzi wa Madhehebu ya waliofuzu, [19] ambapo tafsiri zake nane zinahusiana kundi au wafuasi wa Imam Ali pamoja na Ahlul-Bait (a.s) au Mashia wa Imamu Ali (a.s). [20] Ingawaje kwa mujibu wa maelezo ya Aghanuri, katika baadhi ya nukuu za Hadithi hii hakujatajwa vigezo vya wokovu. [21]

Mtazamo wa Wanazuoni wa Kishia

Katika karne ya nne, Sheikh Sadouq, mwanahadithi mashuhuri wa Shia, katika kitabu Kamal Al-Din wa Tamamu Al-Naimah, akitegemea Hadith ya Thaqlain, amewahisabu wote wanaoshikamana na Qur'ani na Ahlul-Bait wa Mtume (s.a.w.w), kuwa ni miongoni mwa watu wa Madhehebu ya waliookoka. [22] Allamah Majlisi katika kitabu chake Biharu Al-Anwar amenukuu Hadithi kutoka kwa Imam Ali (a.s) ambapo yeye alisema kwamba; Mashia (wafuasi) wangu ndio watu waliookoka. [23] Allamah Hilliy, kwa kutegemea Hadithi kadhaa, amewahisabu Maimamu 12 na wafuasi wao kuwa mifano hai wa kundi la wailiookoka. [24] Allamah Hilliy sababu za kuthibitisha usahihi wa madhehebu ya Shia. [25] Hadithi ya Safina ni moja ya ithibati zinazotumiwa na wale wanaowahisabu wafuasi wa Ahlul-Bait (a.s) kuwa ni ndio watu wa kundi lililookoka. Ithibati hii imeegemea kwenye ibara ilioko katika Hadithi hiyo, ambapo ibara hiyo imeeleza ya kwamba, yoyote yule atakayeshikamana na Ahlul-Bait, basi yeye atakuwa ni miongoni mwa waliookoka. [26]

Hata hivyo, Sunni, wakitegemea Hadith nyingine, wanachukulia madhehebu ya watu wliookoka kuwa ni gurupu au kundi la Wailamu walio wengi zaidi [27], kwa lugha nyengine ni Masunni [28] au wengiau wafuasi wa Makhalifa wema (Khulafau Al-Rashidina). [29]

Pia, kuna nukuu juu ya Hadithi ya Iftiraq, ambayo kwa mujibu wake madhehebu yote ya Kiislamu ni miongoni mwa watu wa kundi la waliookoka, isipokuwa wazushi tu, wao hawataoka. [30] Baadhi ya watafiti wa kidini kwa kuzingatia ulazima wa kufikiria upya na kutathmini kiakili na kimantiki zaidi Hadithi ya Iftiraq. Kwa mtazamo wao; Ni vigumu kuweza kutoa hukumu isemayo kundi moja tu miongoni mwa makundi kadhaa, ndilo kundi lililookoka. Hasa ukizingatia ya kwamba, kuna aina ya dini tofauti kama vili Uislamu Uyahudi, Ukiristo n.k, na kila moja kati yao ina madhehebu na makundi mengine tofauti. Kwa hiyo tukisema tuhesabu makundi na madhehebu ya dini mbali mbali, tutakuta tumepata zaidi ya idani ya makundi 73. Hivyo basi, akili salama yenye mwamko wa kimatiki haiwezi kutoa huku ya kuangamia watu wote wa dini mbali mabli na kudai kuwa kundi fulani tu ndilo kundi la watu waliookoka. [31]Baadhi Wengine wamedai ya kwamba, kundi la waliookoka ni kundi la kila Aliyeshikamana kiroho na Ahlul-Bait (a.s), hata kama atakuwa hana madhehebu au jina maalumu.

Orodha ya Vitabu

Kuna maandishi na vitabu kadhaa vilivyoandikwa kuhusiana na Kundi la Waliookoka. Agha Bozorge Tehrani ameorodhesha baadhi ya kazi zilizofanywa na wanazuoni mbali mbali wa Kishia kuhusiana na mada hii katika kitabu chake Al-Dhari'a, navyo ni: [32]

  • Al-Sawarimu Al-Madhiyyah fi Al-Firqati Al-Najiah, cha Sayyid Muhammad Mehdi Husseini Qazwini Hiliy: [33] Katika kitabu hichi, imethibitishwa kwamba; Madhehebu ya Shia wa Maimamu, ndilo kundi la watu waliookoka. [34] Kitabu hichi kina takriban beti 25,000 za ushairi ndani yake. [35] Wanachuoni wa Kishia wamekisifu sana kitabu hichi, [36] na Allamah Majlesi amekihisabu kuwa ni miongoni mwa vitabu bora vilivyoandikwa juu ya mada hii. Kitabu hichi pia kinaitwa "Al-Sawaram Al-Madhiah Liraddi Al-Firqati Al-Hadiyah wa Tahqiiq Al-Firqati Al-Najiah". [38]
  • Ithbati Al-Firqai Al-Najia, cha Muhammad Hasan Shariatmadar Estra-abadiy (aliyefariki mwaka 1318 Hijiria), mwandishi katika kazi yake hii amefanya juhudi kubwa katika kubainisha madhehebu ya waliookoka na madhehebu mengine 72 yaliobakia.
  • Al-Firqatu Al-Najia, cha Ibrahim bin Suleiman Qatiifiy (aliyefariki mwaka 950 Hijiria), Risalatu Al-Usuliyyah Fi Ithbati Madh-habi Al-Firqati Al-Najia, cha Sheikh Jafar Kaashif Al-Ghitaa, Ithbatu Al-Firqati Al-Najia wa Annahum Al-Shia Al-Imaamiyyah, cha Seyyed Hossein bin Ali bin Abi Talib Hosseiniy Hamdani na kitabu chengine kilichoandikwa katika uwanja huu, ni Ithbatu Al-Firqati Al-Najia, kilichoandikwa na Khaaje Nasiru Al-Din Tusi.

Masuala yanayofungamana

Rejea

Vyanzo