Kuficha haki
- Isije kueleweka vibaya na neno kuficha ushahidi
Kuficha haki (Kiarabu: كِتمَان الحقّ) maana yake ni mtu kuficha kitu ambacho hupelekea kufikia uhakika na ukweli.[1] Watafiti wa masuala ya Qur’ani wanasema kuwa, katika kitabu kitakatifu cha Qur’ani kuna Aya 20 ambazo zinazungumzia kuficha.[2] Aya hizi ni mfano na vielelezo vya kuficha haki kwa sababu zinaashiria kuficha maarifa ya dini, kuficha shahada, kuficha imani, kuficha siri na kufiCha neema za Mwenyezi Mungu.[3] Hassan Mustafa, katika kitabu cha Tafsir Rowshan, anafasiri kuficha haki katika istilahi ya Qur’ani kuwa ni kuficha maarifa na itikadi za kidini.[4] Katika Aya ya Kuficha na Aya zingine kama za 146 na 42 za Surat al-Baqarah na vilevile Aya ya 71 ya Surat al-Imran zinabainisha mifano na vielelezo vya kuficha haki.[5]
Kwa mujibu wa tafsiri za Qur’ani za Waislamu wa madhehebu ya Shia ni kwamba, waliokuwa wakificha ukweli na maarifa ya kidini walikuwa wanazuoni wa Ahlul-Kitab[6] ambapo Qur’an inatambulisha nafasi yao kuwa ni duni na imewalaumu na kuwalaani.[7] Kadhalika baadhi ya wafasiri wanaamini kwamba, katika wakati ambao watu wanahitajia mno kufahamu ukweli wa mambo, kunyamaza kimya pia kunahisabiwa kuwa ni kielelezo cha kuficha haki.[8]
Qur'ani katika Aya kama za 106 Surat al-Maidah na 283 ya Surat al-Baqarah zinaashiria kuficha ushahidi,[9] katika Aya ya 28 ya Surat Ghafir kunaashiriwa kuficha imani,[10] katika Aya ya 228 ya Surat al-Baqarah kunaashiriwa kuficha alichoumba Mwenyezi Mungu katika matumbo,[11] na katika Aya ya 37 ya Surat Nisaa kunaashiriwa kuficha neema za Mwenyezi Mungu.[12]
Watafiti wa masuala ya kidini wanaamini kwamba, hatua ya kuficha kitu yenyewe kama yenyewe haina hukumu ya kisheria au kimaadili, bali inakuwa na hukumu mbalimbali kulingana na itibari ya mifano na vielelezo vyake. Kwa maana kwamba, inategemea anachokificha mtu ni nini.[13] Kwa mfano, kuficha siri na aibu za watu na kuficha imani katika maeneo ambayo mtu anahofia kupata madhara (kufanya taqiyyah) ni jambo linalosifiwa kwa upande na mtazamo wa kimaadili,[14] na kwa upande wa mtazamo wa kifikihi ni wajibu au mustahabu.[15] Lakini kuficha haki na uhakika wa dini na vilevile kuficha ushahidi ni jambo linalokemewa kwa mtazamo wa kimaadili[16] na katika sheria kitendo hicho kinatambuliwa kuwa ni haramu.[17]
Rejea
- ↑ Ridhai Isfahani, Tafsir Qur'an Mehr, 1387 S, juz. 2, uk. 59.
- ↑ Muadhini, «Kitman Haq».
- ↑ Hadi, «Kitman Haq Mamduh wa Madhmum (Miiyarha wa Chalesh-ha)», uk. 126; Bigi, Jamal, (Jarm Engari Kitman Shahadat wa Chalesh-hayr on dar Huquq Iran), uk. 151-152.
- ↑ Mustafawi, Tafsir Rqwshan, juz. 4, uk. 268.
- ↑ Bigi, Jamal, «Jarm Engari Kitman Shahadat wa Chalesh-haye on dar Huquq- Iran», uk. 150.
- ↑ Tabrasi, Majma' al-Bayan, jld. 1, uk. 442.
- ↑ Muadhini, «Kitman Haq».
- ↑ Makarim Shirazi, Tafsir Nemuneh, juz. 1, uk. 550.
- ↑ Bigi, Jamal, «Jarm Engari Kitman Shahadat wa Chalesh-haye on dar Huquq- Iran», uk. 151.
- ↑ Muadhini, «Kitman Haq».
- ↑ Risheyabi Madee Katm, Tovuti ya Tanzil.
- ↑ Risheyabi Made-e Katm, Tovuti ya Tanzil.
- ↑ Hadi, «Kitman Haq Mamduh wa Madhmum (Miiyarha wa Chalesh-ha)», uk. 124.
- ↑ Hadi, «Kitman Haq Mamduh wa Madhmum (Miiyarha wa Chalesh-ha)», uk. 126.
- ↑ Tayyib, Atyab al-Bayan, juz. 2, uk. 266; Shahid Awal, al-Qawaid wa al-Fawaid, juz. 2, uk. 157; Muasase Dairat al-Ma'arif Fiqh Islami bar Madhhab Ahlul-bait (a.s), Farhange Fiqh Mutabiq Madhhab Ahlul-bait (a.s), juz. 1, uk. 591.
- ↑ Hadi, «Kitman Haq Mamduh wa Madhmum (Miiyarha wa Chalesh-ha)», uk. 138.
- ↑ Shahid Thani, Masalik al-Afham, juz. 14, uk. 263.
Vyanzo
- Risheyabi Made-e Katm. Tanzil. Tovuti ya tanzil.ir, Tarekh buzdad: 9 Aban 1402 S.
- Bigi, Jamal. (Jarm Engari Kitman Shahadat wa Chalesh-hayr on dar Huquq Iran). Dofasliname Āmuzehaye Huquq Keifari, juz. 14, 1396 S.
- Hadi As-ghar. «Kitman Haq Mamduh wa Madhmum (Miiyarha wa Chalesh-ha)». Fasliname Akhlak, Sale Hashtom, juz. 30, Tabistun, 1397 S.
- Makarim Shirazi, Nashir. Tafsir Nemuneh. Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiah, Chapa ya kwanza, 1371 S.
- Muasasat Dairah al-Ma'arif Fiqh Islami bar Madhhab Ahlul-bait (a.s). Farhange Fiqh Mutabiq Madhab Ahlul-bait (a.s). Muasasat Dairah al-Ma'arif Fiqh Islami bar Madhhab Ahlul-bait (a.s), Chapa ya kwanza, 1426 HS.
- Mustafawi, Hassan. Tafsir-e Rowshan. Tehran: Markaz Nashr Kitab, Chapa ya kwanza, 1380 S.
- Muadhini, Muhammad. Kitman Ha. Bank Makalat Ulum Insani Pazhuhe, 1393 HS.
- Ridhai Isfahani, Muhammad Ali. Tafsir Mehr. Qom: Pazhuhesh-hae Tafsir wa Ulum Qur'an, Chapa ya kwanza, 1378 S.
- Shahid Awal, Muhammad. al-Qawaid wa al-Fawaid. Qom: Maktabat al-Mufid, Chapa ya kwanza, 1400 HS.
- Shahid Thani, Zainuddin bin Ali. Masalik al-Afham ila Tanqih Sharai' al-Islam. Qom: Muasasat al-Ma'arif al-Islamiya Chapa ya kwanza, 1413 HS.
- Tabrasi, Fadhl bin Hassan. Majma' al-Bayan fi Tafsir al-Quran. Tehran: Markaz Nashri Khusru, Chapa ya tatu, 1372 S.
- Tayyib, Abdul Hussein. Atyab al-Bayan fi Tafsir al-Qur'an. Tehran: Nashri Islam, Chapa ya pili, 1369 S.