Kitendo cha wizi

Kutoka wikishia

Kitendo cha Wizi (Kiarabu: السرقة) katika welewa wa kidini na kijamii, kinatambuliwa kama ni kitendo cha kunyakua mali ya mtu mwingine kwa njia ya siri. [1] Wizi katika Uislamu umeharamishwa wazi kabisa, na kuorodheshwa miongoni mwa dhambi makubwa. [2] Athari za wizi zilizotajwa katika vyanzo vya Hadithi ni pamoja na; kutoweka kwa amani ya kiuchumi katika jamii, kuzuka kwa mizozo, kuongezeka kwa mauaji, na kupungua kwa hamasa za kufanya biashara. [3] Wanazuoni wa sheria za Kiislamu wanaeleza kuwa; mwizi anakabiliwa na dhima ya kurudisha mali aliyoiba kwa mmiliki wake, [4] hali mali hiyo ikiwa katika hali yake ile ile ya mwazo, au kurudusha mali ifananayo na mali hiyo. [5] Ila kama mmiliki wa mali hiyo atakuwa amesha fariki, basi mali hiyo itapaswa kurudishwa kwa warithi wake. Na endapo mmiliki wa mali hiyo atakuwa hana warithi, mali hiyo itatakiwa kupelekwa kwa Imamu (a.s), au kwa viongozi wa Kiislamu wa wakati huo. [6]

Katika sheria za Kiislamu (fiq’hi), adhabu ya wizi ni kukatwa vidole vya mkono wakemwizi. Adhabu hii imetokana na Aya ya Qur'an inayosema: «...وَالسَّارِقُ وَالسَّارِقَةُ فَاقْطَعُوا أَیدِیهُمَا» "Na mwizi mwanamume na mwizi mwanamke, ikateni...". [7] Kwa hiyo kulingana na Aya hiyo mafaqihi wanaamini kwamba; adhabu halisi ya mwizi ni kukatwa viganja vya mkono wake. [8] Hata hivyo, wanazuoni wa fiqhi wameweka masharti maalum ili kuweza kutimizwa kwa adhabu hiyo. [9] Na iwapo masharti hayo yatakuwa hayakutimia, basi mwizi huyo itabidi ahukumiwe kwa adhabu ya ta'zir, ambayo ni adhabu nyinginezo zisizo kinyume na ile ya kukatwa kwa mkono wake. [10] Miongoni mwa masharti ya kutekeleza adhabu ya kukata mkono (hadd ya wizi) ni Kuvunja hirz. Hirz ni eneo au aina ya ulizni wa kutosha kwa ajili ya kuhifadhi mali fulani, kama vile kufuli au ukuta maalumu. Hivyo basi ili mwizi aweze kukabiliwa na adhabu ya kukatwa vidole vya mkono wake, ni lazima awe amevunja au kuchupa katika eneo hilo na na kuiba mali iliomo ndani yake, [11] huku mwenye mali akiwa hana habari ya jambo hilo. [12] Kwa mujibu wa maelezo ya wanazuoni ni kwamba; hirzi ni kile kitu ambacho kwa kawaida kinatambuliwa kuwa ni kizuizi kinachoweza kuhifaadhi mali ya mtu fulani. [13] Kulingana na imani ya Sheikh Tabarsi, hirz ni kitu ambacho kinaweza kumzuia mtu asiweze kuingia katika eneo fulani au kinachomzuia asiweze kuchukua mali bila ya ruhusa ya mmiliki wake. [14]

Kwa mujibu wa wanazuoni wa fiqhi, kuna utofauti muhimu katika kutekeleza hadd (adhabu asilia) ya wizi kulingana na aina ya ulinzi wa mali (hirz) na jinsi ya wizi unavyofanyika. Katika baadhi ya hali fulani, haiwezekani mwizi kutekelezewa adhabu ya kukata vidole vyake. Hii ni kwa sababu lake la wizi haliku ambatana na kuvunja hirz, ambayo ni sharti muhimu katika utekelezaji wa adhabu hiyo.

  • Wizi wa Mfukoni na Ubadhirifu

Wanazuoni wanasema kwamba watu kama wanyang'anyi kwa njia ya ukwapuaji[15] na wale wanaofanya ubadhirifu (wanachukua mali waziwazi bila ya kuvunja eneo la ulinzi wa mali), [16] hawastahili adhabu ya kukata mikono. [17] Bali watu kama hawa, hupewa adhibu ya ta'zir, ambayo ni adhabu nyinginezo zisizohusisha na kukata kwa mkono yao. [18] Hii ni kwa sababu wao hawakuvunja hirz kwa namna iliyo ainishwa kisheria.

  • Wizi wa Mfuko ya Ndani ya Nje

Ikiwa wizi ataiba mali kutoka katika mfukoni wa ndani ya nguo ya mtu fulani, yeye huhisabiwa sawa na yule ailiyeiba kwa kuvunja hirz, kwa sababu mfuko wa ndani kiasili unaonekana sawa na hirzi. Hivyo, adhabu yake itakuwa ni kukata vidole vya mkono wake. [19]

Hata hivyo, kama mwizi fulani ataiba mali kutoka kwenye mfuko wa nje ya nguo, ambao ni mfuko ulio wazi au rahisi kupatikana, mwizi huyo hatahisabiwa kuwa amevunja hirz. Kwa hiyo, yeye atakabiliwa na adhabu ya ta'zir badala ya adhabu kali ya kukatwa mkono wake. [20]

  • Maoni ya Imam Khomeini

Kwa mujibu wa maoni ya Imamu Khomeini, kama jamii inatambua kwamba; kuchukua mali kutoka katika mfuko wa nje ni sawa na kuvunja hirz, hali hii inaweza kusababisha kutekelezwa kwa hadd ya wizi, yaani kukatwa vidole vya mkono wa mwizi huyo.[21]

Kwa mujibu wa wanazuoni wa fiqhi, adhabu ya wizi kupitia mtandao wa intaneti inategemea kama wizi huo umekidhi masharti yaliyowekwa kwa ajili ya kutekelezwa kwa hadd (adhabu) ya wizi, kama ilivyoainishwa katika sheria za Kiislamu. Masharti muhimu yanayoangaliwa ni pamoja na kuvunja hirz (ulinzi wa mali) na kuchukua mali kwa siri bila idhini ya mmiliki wake. [22]

Rejea

Vyanzo