Karram Allahu Wajhahu

Kutoka wikishia

Karram-Allah-u Wajhahu (Mwenyezi Mungu ameutukuza uso wake). Ni ibara na maneno ya heshima na taadhima ambayo wafuasi wa madhehebu ya Sunni wanayatumia (kila) baada tu ya kutajwa jina la Imam Ali (a.s)! Wafuasi wa Madhehebu ya Sunni hawaitumii ibara hii kwa ajili ya swahaba mwingine yeyote. Wafuasi wa madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s) ambao ni Mashia, badala ya kutumia ibara Karram-Allah-u Wajhahu, wao wanatumia ibara isemayo (Alayhis-Salam). Maulamaa na wazuoni wa madhehebu ya Sunni, wameifanya ibara ya Karram-Allah-u Wajhahu kuwa ni makhsusi kwa ajili ya Imam Ali (as) kwa maana ya kwamba:

‘’Mwenyezi Mungu amemtukuza Imam Ali (a.s) na kumpa heshima’’ kutokana na kwamba wao wanajua kuwa Imam Ali (a.s) hakuwahi katu kusujudia masanamu. Mkabala na hilo, Abdul-Aziz ib Baz, Mufti wa Kiwahabi anaamini kwamba kuifanya sifa ya Karram-Allah-u Wajhahu (Mwenyezi Mungu ameutukuza uso wake) kuwa ni makhsusi kwa Imam Ali (a.s) ni bidaa na uzushi wa Shia.

Hafidh Rajab Bursi, anaamini kwamba; kuifanya sifa ya Karram-Allah-u Wajhahu kuwa ni makhsusi kwa Imam Ali (a.s), kwa mujibu wa madhehebu ya Sunni ni dalili na hoja ya ubora na utukufu wake (a.s) juu ya makhalifa wengine watatu. Baadhi ya wahakiki wa Kishia kwa kuashiria dalili ya kuwa (ibara ya) Karram-Allah-u Wajhahu ni makhsusi kwa Imam Ali (a.s), na kwa kutegemea Aya za Qur’an; Ahadi yangu haitawafikia wenye kudhulumu. (Surat al-Baqarah 124) Kati yao yupo aliye jidhulumu nafsi yake (Surat Faatir 32), wanaamni kwamba makhalifa watatu hawastahiki Uimamu kwani kwa kuzingatia Aya hizi ni kwamba, mtu ambaye amekwisha tenda dhambi ni mwenye kujidhulumu mwenyewe na hivyo ahadi ya Mwenyezi Mungu (Uimamu) haiwezi kumfikia dhalimu.


Maana


Karram-Allah-u Wajhahu ina maana ya kwamba; Mwenyezi Mungu amtukuze na kumkuza yeye [1] hii ni (kuzingatiwa kwamba, kama ibara hii itakuwa ni dua) [2] au Mwenyezi Mungu amemtukuza na kumkuza; kwa kuzingatia sentensi kama ni (yenye kutoa) habari.[3], ni sentensi ya heshima na taadhima ambayo wafuasi wa madhehebu ya Suni wanaitumia na kuitaja kwa wingi baada ya kutajwa jina lmam Ali (a.s) [4]. Ibn Hajar Haytami na Shiblanji ambao miongoni mwa Maulamaa wakubwa wa Kisuni wanaamini kwamba, maana ya sentensi hiyo ni kwamba: Mwenyezi Mungu amemuhifadhi na kumuweka mbali na ibada isiyo ya Mwenyezi Mungu. [5] Katika vitabu vya wafuasi wa madhehebu ya Sunni, wakati mwingine wametumia sentensi na ibara hii kwa Imam Ali (a.s) kwa kusema kwamba! “Karram-Allah-u Wajhahu Filjannah” (Mwenyezi Mungu ametukuza uso wake katika pepo) [6]. Kwa mujibu mapokezi ya Ahmad bin Hanbal mmoja wa mafakihi wanne wa madhehebu ya Suni kuhusiana na riwaya ya bendera ya vita vya Khaybar (al-Rayah), ni kuwa, wakati Mtume mtukufu alipompa Imam Ali (a.s) bendera ya vita vya Khaybar, alitumia ibara isemayo kwamba: Naapa kwa Yule ambaye amemtukuza na kumpa heshima Muhammad [7].


Makhsusi Kwa Imam Ali (a.s)


Kwa kuzingatia kauli ya Ibn Kathir na Ibni Hajar Haytami, miongoni mwa Maulamaa wakubwa wa madhehebu ya Kisuni ni kwamba; ibara ya Karram-Allah-u Wajhahu ni yenye kutumiwa kwa wingi na wafuasi wa madhahebu ya Suni kwa kuinasibisha kuwa ni makhsusi kwa Imam Ali (a.s). Wao kwa ajili ya makhalifa akiwemo na Imam Ali (a.s) na mwaswahaba wengine, huwa wanatumia ibara isemayo; radhiallah anhu (Mwenyezi amuwiye radhi), ama ibara ya Karram-Allah-u Wajhahu huitumia makhsusi kwa Imam Ali tu na hawaitumii kwa makhalifa watatu na maswahaba wengine katu [8]. Ahmad bin Muhammad Khafaji na Muhammad bin Ahmad Safarini ambao ni katika Maulamaa kwa madhehebu ya Hanafi, nao pia wamesema bayana kwamba, ibara ya (Karram-Allah-u Wajhahu) imeenea na inatumika baina ya wafuasi wa madhehebu ya Suni.[9] Katika vitabu imeandikwa kwamba, katika karne 15 Hijria pia! ibara hii (Karram-Allah-u Wajhahu) Mwenyezi Mungu ameutukuza uso wake, ilikuwa ni makhsusi kwa Imam Ali (a.s) tu. [10]


Sababu ya Kuwa Makhsusi kwa Ali (as)


Maulamaa wa madhehebu ya Kisuni wametaja sababu za ibara ya: Karram-Allah-u Wajhahu kuwa makhsusi kwa Imam Ali (a.s) kwamba ni: • Ni kutokusujudia masanamu: Ibn Hajar Haytami na Mu’min Shiblanji wanaamini kwamba dalili ya ibara Karram-Allah-u Wajhahu kuwa makhsusi kwa Imam Ali (a.s) ni kwamba yeye (Imam) hakuwahi kusujudia masanamu katu [11]. Ibn Hajar anaamini kwamba Abu Bakr bin Quhafa anashirikiana na Imam Ali (a.s) katika kutokusujudia masanamu, kwa utofauti wa kwamba; kutokusujudia masanamu kwa Ali (a.s) kunakubalika na (Waislamu) wote [12] (ambapo ni kinyume na Abu Bakr bin Quhafa). Hali kadhalika Haytami katika kujibu (na kuivunja hoja) ya watu waliosema kwamba, maswahaba wengine kama Abdullah bin Abbas na Abdullah bin Omar pia hawakusujudia masanama anasema kwamba: Wale wamezaliwa baada ya kuangamizwa na kwisha kwa shirk, kwa sababbu hii hawawezi kuwa sawa na watu ambao waliozaliwa wakati wa (watu) kuomba na kuabudu masanamu, lakini hawakuabudu masanamu. • Heshima na taadhima kwa Mtume (s.a.w.w) kabla ya kuzaliwa: Kwa kuzingatia kauli ya Jalal Al-Din Dawani, mwanateolojia na mwanafalsafa wa Kiislamu ni kuwa: Wakati Fatma bint Asad (mama wa Imam Ali a.s) alipokuwa mjamzito, kila alipokuwa akimuona Mtume Muhammad (a.s.w.w), alikuwa akinyanyuka na kusimama bila hiyari (kama alikuwa ameketi) kwa ajili ya heshima na taadhima kwa Mtume mtukufu, na mtoto ( ambae ni Imam Ali a.s) aliyekuwa tumboni kwake alikuwa anacheza au kutikisika jambo ambalo lilikuwa likimfanya (bint Asad) afahamu kuwa ni lazima asimame. Kwa kuzingatia kauli ya Dawani ni kwamba; Maulama wengi wa madhehebu ya Sunni wanaamini kwamba, sababu ya ibara ya Karram-Allah-u Wajhahu kuwa makhsusi kwa ajili ya Imam Ali (a.s) tu (bila ya mwingine yeyote katika maswahaba) inarejea katika kisa na tukio hili. [14]

Kupinga Mawahabi Sifa Hiyo Kuwa Makhasusi Kwa Imam Ali (a.s)


Mahdi Farmaniyan, mtafiti na mhakiki wa madhehebu za Kiislamu anasema kwamba; Mawahabi wamezuia kusema ibara ya Karram-Allah-u Wajhahu wakati wa kutajwa Imam Ali (a.s) [15] na kwa kulingana na mapokezi ya Qasim Uf ni kwamba; Ibn Taymiyah katika vitabu vyake vingi (palipotajwa) Imam Ali (a.s) hajatumia ibara ya Karram-Allah-u Wajhahu.[16] Abdul-Aziz bin Baz, Mufti wa Kiwahabi anaamini kwamba; kutumia ibara ya Karram-Allah-u Wajhahu kwa ajili ya Imam Ali (a.s) ni hila [17] na bidaa ya Shia (madhehebu ya Ahlul-Bayt a.s).[18] Muhammad Swalih Al-Munajjid ambaye ni miongoni mwa wanafunzi wa ibn Baz, anaamini kwamba! Mwanzo Mashia waliitumia ibara hii kwa ajili ya Imam Ali (a.s) kisha waandishi wasiojua (wajinga) wakawaiga na kuwafuata.[19] Hata hivyo wao hawakutaja chanzo na chimbuko la madai yao haya.[20] Kwa kuzingatia kauli ya mwanafasihi Darruh Sufi, alimu wa Kishia wa karne ya 13 Hijria ni kwamba: Mashia walikuwa wakitumia ibara zifuatazo kwa ajili ya Imam Ali (a.s): Alayhi salaam, Salamullah alayhi au Swalawatullah alayh [21]. Muhammad A’sif Mohseni alimu wa Kishia wa Afghanistani anaamini kwamba, kutumia ibara ya Karram-Allah-u Wajhahu kwa ajili ya Imam Ali (a.s) ni makhsusi kwa Maulamaa wa Kisuni.[22]


Hoja ya Ubora na Utukufu wa Imam Ali (a.s)


Hafidh Rajab Bursi, mpokezi wa hadithi ambaye ni alimu wa Kishia wa karne ya 6 Hijria anaamini kuwa, ibara ya Karram-Allah-u Wajhahu ni makhsusi kwa Imam Ali (a.s) kupitia wafuasi wa Madhehebu ya Suni na hii ni dalili na hoja ya heshima na utukufu wake juu ya maswahaba wengine.[23] Muhammad Thaqafi Tehrani anaamini kwamba, kuwa kwake makhsusi kwa Imam Ali (a.s) ni dalili kwamba miongoni mwa makhalifa ni Imam Ali tu ndiye ambaye hakusujudia masanamu. Alimu huyu kutokana na ukweli huu amechukua natija ya kwamba, baina ya makhalifa wote ni Imam Ali tu ndiye anayestahiki Uimamu (na ukhalifa) baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) [24]. Sayyid Muhammad Jawad Husseini Jalali ambaye pia ni mtafiti na mhakiki wa Kishia, baada ya kuashiria na kuonyesha dalili na hoja ya ibara ya Karram-Allah-u Wajhahu kuwa ni makhsusi kwa Imam Ali (a.s), kwa kutegemea Aya zifuatazo: Ahadi yangu haitawafikia wenye kudhulumu. [25] Kati yao yupo aliye jidhulumu nafsi yake. [26], anaamini kwamba makhalifa watatu (Abu Bakr, Omar na Othman) hawakuwa na ustahiki wa Uimamu (Imamah). Kwani kwa mujibu wa Aya zilizotajwa hapo juu ni kwamba, mtu ambaye amefanya dhambi ni mwenye kijidhulumu nafsi yake na ahadi ya Mwenyezi Mungu (yaani Uimamu) haiwezi kumfikia [27].