Ihtikaar

Kutoka wikishia

Ihtikaar (Kiarabu: الاحتكار): Neno hili kiasili ni neno la Kiarabu ambalo katika istilahi za kifiqhi humaanisha; tendo la kurimbika na kuficha bidhaa maalumu kwa lengo la kuiuza sokoni kwa bei ya juu zaidi endapo bidhaa hiyo itaadimika. Mafaqihi maarufu wa Kishia wameharamisha tendo la kurimbika bidhaa muhimu, hasa chakula kwa lengo hilo. Bila shaka, baadhi ya mafaqihi wamepanua zaidi wigo wa hukumu hiyo, na wanaamini kwamba ni haramu kurimbika aina yoyote ile ya bidhaa inayohitajika ndani ya jamii.

Falsafa ya kuharamishwa kwake, ni kuzuia mvurugiko wa maisha ya watu na kuleta machafuko ndani ya mfumo wa jamii. Katika sheria za kifiqhi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kuna aina kadhaa ya adhabu dhidi ya kitendo hicho, miongoni mwazo ni; kifungo, malipo ya fidia na kunyimwa huduma za serikali.

Welewa wa dhana

Kurimbika na kuficha ihtikaar (احتکار): Ina maana ya kuficha, kurimbika na kuhifadhi bidhaa adimu sokoni na inayohitajika na wananchi, na kusubiri bei yake iongezeke. [1] Baadhi wameongeza neno “kununua” katika tafsiri dhana ya ihtikaar (احتکار) na kusema kuwa ihtikaar (احتکار); Ni kununua bidhaa na kuificha katika zama za uadimu wake na kuto iweka sokoni kwa ajili ya mauzo, il kuiuza kwa bei ya juu kwa muda ujao. Pia wengine wameifasiri dhana hii kwa kusema kuwa ihtikaar (احتکار): ni kurimbika na kuficha bidhaa katika wakati wa uadimu wake, bila ya kujali ni vipi bidhaa hiyo imepatikana. Yaani tafsiri hii inazingatia suala la kurimbika bila ya kujali mrimbikizaji huyo aimapata vipi bidhaa hiyo, yawezekana mtu huyo akawa ameimiliki bidhaa hiyo kwa kupitia kilimo au biashara. [2] Kifiqhi mwenye kurimbika na kuficha bidhaa kwa lengo lilitjwa hapo juu huitwa Muhtakir (مُحْتکر)

Tathmini ya Ihtikaar

Katika fiqhi suala la Ihtikaar na hukumu zake, hujadiliwa kwenye mlango wa maudhui ya mauzo, [4] sheria, na uchumi. Sheikh Ansari amelielezea suala hili chini ya kichwa kinachozungumzia suala la urimbikizaji na ufichaji wa bidhaa za vyakula. [5] Pia, katika vitavu vyeneye makusanyo ya hadithi za Shia, kuna mlango maalumu wa hadithi zenye mada ya ihtikaar. [6] Katika hadithi, Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliwalaani warimbikizaji. [7]

Sharia

Kuna tofauti baina ya mafaqihi juu ya hukumu ya ihtikaar kuwa je, ni haram au makruhu (haipendezi kisheria) [8] Kwa mujibu wa kile ambacho kimenasibishwa kwa mafaqihi maarufu wa Kishia, ni kwamba; ikiwa hakuna bidhaa za kutosha sokoni na kwamba kurimbika kwa bidhaa hiyo kutasababisha uharibifu kwenye soko la Waislamu, basi tendo hilo litakuwa ni haramu. [9]

Shahidi Shahidu al-Awwal amelihisabu tendo la kurimbika bidha katika biashara za chakula, kuwa ni tendo la makruhu (lenye kuchukiza). [10] Shahidu al-Thani akifafanua uharamu wa jambo hilo katika kitabu Sherhe al-Lum’a, amesema kwamba; urimbikizaji wa bidhaa ni haramu, na uharamu wake unazidi kukolea zaida pale ambapo wanajamii watakuwa ni wahitaji wa bidhaa hiyo. Pia akisisitiza kauli yake, amesema kitabuni humo kwamba; Shahidu al-Awwal ameharamisha kurimbika bidhaa katika kitabu Al-durus. [11] Baadhi ya mafaqihi wamesema kwamba ikiwa mali iliyorimbikwa inahitajika kwa watu na haiwezi kupatikana sokoni, mtawala anaweza kumlazimisha mhifadhi wa bidhaa hiyo kuiuza kwa lazima, [12] ila mtawala hana mamalaka ya kumuainishia bei juu ya bidhaa hiyo katika mauzaji yake. 13

Falsafa ya kuharamishwa kwa ihtikaar (urimbikizaji wa bidhaa), ni kuzuia mvurugika wa mfumo na machafuko ugumu wa maisha kwa wanajamii. [14]

Hukumu ya uharamu au umakruhu wa urimbikizaji wa bidhaa iliyo tolewa na mafaqihi wa Kishia, imeegemea kwenye Hadith za Mtume (s.a.w.w), Imam Swadiq (a.s), [ 15] na amri ya Imam Ali (a.s) kwa Malik Ashtar inahusu uzuiaji wa urimbikizaji wa bidhaa [16]. [17] Katika moja ya Hadithi hizo, [Maelezo 1] limetumika neno makruhu' ndani yake [18], baadhi ya mafaqihi wamelifasiri neno hili kwa maana na ya jambo lisilopendekezwa 19] Na wengine wakalifasiri kwa maana na haramu. [20]

Ni bidhaa gani zilizopigwa marufuku kuzirimbika?

Kuna bidhaa maalumu zilizojadiliwa katika Hadithi kuhusiana na uharamu wa kurimbika bishaa, nazo ni; ngano, shayiri, tende, zabibu na mafuta. 21 Kwa hivyo, kulingana na maelezo ya Alama Majlisi ni kwamba; mtazamo maarufu miongoni mwa wanazuoni wa Shia, ni kuwa uharamu wa kurimbika bidhaa, havuki zaidi bidhaa hizo zilizohusihwa ndani ya Hadithi, na hawakuvijumisha vitu au bidhaa nyingine katika hukumu hiyo, kwa hiyo mafaqihi wa Kishia hawakuinyumbua hukumu hiyo zaidi ya hapo. [22] Baadhi pia wameongeza bidhaa ua chumvi kwenye orodha hiyo. [23] Hata hivyo, katika baadhi ya Hadithi, urimbikizaji wa aina yoyote ile ya chakula umepigwa marufuku, [24] na baadhi ya wanavyuoni wa Kishia wanaona kuwa, hukumu hiyo haiwezekani kujumuisha aina zote zile za chakula. [25] Kwa upande wa pili kuna wanazouoni wengine wa Kishia walioingiza ndani ya hukumu hiyo mahitaji yote ya umma, kama vile; chakula, nguo na makazi. Tegemeo na ithibati za kundi hili la mwisho, ni baadhi ya kanuni za kifiqhi kama vile; kanuni ya Laa Dharar na kanuni ya Laa Haraj. Kwa kuwa kanuni hizi ni kanuni zinazopinga ukandamizaji, na kwa upande mwengine; Kuna Hadithi zilizozungumzia sababu ya uharamu wa ihtikaarkwamba ni ukandamizaji. Hivyo basi kwa kuwa aina zote za urimbikizaji, iwe nguo, chakula na vinginevyo ni miongoni mwa mifano hai ya ukandamizaji, hivyo basi, aina zote hizo zitaingia katika hukumu ya uharamu. [26]

Adhabu na kanuni za kisheria

Hakuna hukumu ya wazi juu ya adhabu ya mwenye kurimbika bidhaa katika Aya na Hadithi. Kwa hivyo, baadhi ya wanazuoni, kwa kurejelea barua ya Imam Ali kwa Malik Ashtar, wamesema kuwa adhabu ya mrimbikizaji bidhaa ni ta’aziir, nayo ni adhabu inayokadiriwa na kadhi wa Kiislamu kwa kadri ya kumpa somo ili aachane na tabia hiyo. [27]

Kwa mtazamo wa sheria za kiraia pia, suala la urimbikizaji linachukuliwa kuwa ni kosa la jinai, na hata katika sheria za kiraia za Iran, kuna adhabu maalumu zimewekwa kwa ajili ya warimbikizaji bidhaa. [28] Katika Sheria ya Bajeti ya Ziada ya Mwaka 1317 ya Iran (iliyopitishwa tarehe 29 Februari 1316 Shamsia), kuna adhabu maalumu kuhusiana na suala hilo, miongoni mwazo ni kama vile; kifungo na kulipa fidia zilizoainishwa kwa ajili yake. Katika Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kuna adhabu zilizoorodheshwa ndani yake, ikiwemo adhabu ya kutengwa na huduma za umma kwa wanao jaribu kurimbikiza bidhaa maghalani mwao. [29]

Maelezo

  1. فَإِنَّهُ يُكْرَهُ أَنْ يَحْتَكِرَ الطَّعَام‏