Hotuba ya Fatima (as) katika mkusanyiko wa wanawake wa Madina
Hotuba ya Fatima (a.s) katika mkusanyiko wa wanawake wa Madina (Kiarabu: خطبة السيدة فاطمة في نساء المدينة) au Hotuba ya Kumtembelea Mgonjwa ni matamshi na hotuba iliyotolewa na Bibi Fatima Zahra (a.s) binti ya Mtume (s.a.w.w) katika hadhara na mkusanyiko wa wanawake wa Madina akilalamikia na kupinga kuporwa na kughusubiwa Ukhalifa. Hotuba hii ambayo aliitoa akiwa mgonjwa kitandani kwa maradhi ambayo ndio yaliyomfanya afe shahidi, inatambuliwa kuwa ina umuhimu mkubwa kutokana na kubainisha hali iliyokuwa ikitawala baada ya kuaga dunia Bwana Mtume (s.a.w.w), indhari kuhusiana na mustakabali wa jamii ya Kiislamu na fasaha na balagha iliyomo ndani yake.
Katika hotuba hii, Bibi Fatima (a.s) sambamba na kutangaza kujibari na kujiweka mbali na waliovunja mapatano na kuwalaumu watu waliofuata hayo, anachora taswira ya kutokuwa kwao waaminifu na anaelezea na kubainisha hali halisi ilivyo, anatabiri mustakabali mbaya wa Waislamu, sifa za serikali ya Alawi, udhaifu wa kifikra na tofauti za maoni ya watu wa Madina, jukumu la watu dhidi ya ufisadi wa serikali na kutoa taswira ya sura ya Saqifa.
Katika hotuba hii, Bibi Fatima anatumia Aya kadhaa za Qur’ani kama hoja ya anayoyasema, zikiwemo Aya ya 80 Surat al-Ma’ida kuhusu matokeo ya kufuata hawaa na matamanio ya nafsi, Aya ya 96 Surat al-A’raf na Aya ya 51 Surat al-Zumar zinazowalaumu wale wasiofuata haki na Aya ya 35 Surat Yunus inayoelezea watu wanaostahili uongozi.
Hotuba ya Bibi Fatima Zahra (a.s) katika kundi la wanawake wa Muhajirina na Ansari imetajwa katika vitabu vya hadithi za Shia na Sunni kwa njia tofauti. hotuba hii pia imeelezewa na watafiti wa kidini katika vitabu vinavyohusiana na maisha ya Bibi Fatima (a.s) na kutolewa maelezo na ufafanuzi wake.
Utambulisho na umuhimu
Hotuba ya Fatima (a.s) katika mkusanyiko wa wanawake wa Madina au Hotuba ya Kumtembelea Mgonjwa ni matamshi na hotuba iliyotolewa na Bibi Fatima Zahra (a.s) binti ya Mtume (s.a.w.w) katika hadhara na mkusanyiko wa wanawake wa Madina. Hotuba hii aliitoa akiwa mgonjwa kitandani kwa maradhi ambayo ndio yaliyomfanya afe shahidi na wanawake hao walikuwa wamekuja kumtembelea kwa ajili ya kumjulia hali na kumtakia ahueni na afya njema. [1] Kuhusiana na idadi ya wanawake waliokuja kumtembelea na kumjulia hali siku hiyo na kwamba, walikuwa ni akina nani hakuna taarifa za uhakika kuhusiana na hili. [2] Hata hivyo imekuja katika kitabu cha Balaghat al-Nisaa [3] na Sherh Nahaj al-Balagha cha Ibn Abil-Hadid [4] kwamba, wanawake wa Muhajirina na Ansari waliokwenda kumjulia hali Bibi Fatima na ambao wametajwa katika kitabu cha Tarikh Ya’qubi ni wake za Mtume (s.a.w.w) na wanawake kadhaa wa Kiqureishi. [5]
Baadhi ya watafiti wanasema kuwa, hotuba ya Bibi Fatima katika hadhara ya wanawake wa Madina ina balagha, fasaha na muhtawa wa kustaajabisha. [6] Kwa mujibu wao ni kuwa, kwa kuzingatia ufahamu na welewa aliokuwa nao Fatima kuhusiana na matukio ya jamii changa ya Kiislamu na kwa ajili ya kuwa na taathira zaidi kwa anaowahutubu, alitumia vitenzi (vitendo) kadhaa vya usemi kama vile vitenzi vya kueleza, vya hisia na ushawishi na kushajiisha katika hotuba hii. [7] Matini na andiko la hotuba hii linaashiria juu ya ufahamu na weledi wa Bibi Fatima kuhusiana na matukio na mambo yaliyokuwa yakitokea katika mji wa Madina. [8]
Ayatullah Makarem Shirazi, mmoja wa Marajii Taqlid, anaichukulia khutba hii kuwa sawa na Hotuba ya Fadak ambayo ina sauti ya ushujaa na lahani ya ghamu na huzuni zaidi. [9] Kulingana naye, ingawa Bibi Fatima alionewa sana na alikuwa mgonjwa kutokana na majeraha yaliyosababishwa na hujuma na shambulio dhidi ya nyumba yake, lakini katika khutba hii, hakusema chochote kuhusu hali yake mwenyewe, na ajenda na mhimili wa maneno yake yote ulikuwa ni unyakuzi na kuporwa ukhalifa, kudhulumiwa Ali (a.s.) na hatari za baadaye za upotofu huu mkubwa, na hii ni hoja na ithbati ya kujisabilia na kujitolea kwake, daraja ya kuridhia kwake na kusalimu amri kwake mbele ya Mwenyezi Mungu. [10] Mazingira ya kutoa hotuba
Mwishoni mwa maisha yake (baada ya kushambuliwa kwa nyumba yake), Fatima aliugua na kubakia kitandani na wanawake wa Muhajirina na Ansari walikwenda kumtembelea na kumjulia hali. [11] Kuhusu msukumo wa wanawake waliokwenda kumzuru, inasemekana kwamba wanaume wa Muhajirina na Ansari kutokana na matukio ya kusikitisha yaliyomtokea Hadhrat Zahra, walijiona kuwa wana masuuliya (wanawajibika); na ni kutokana sababu hiyo, ndio maana waliwatuma wake zao wakamzuru Fatima ili kupunguza mzigo wa dhambi zao. [12] Pia, wengine wanaamini kwamba, nia za kisiasa za kuboresha uhusiano wa familia ya Mtume na mtawala wa wakati huo na kulainisha mazingira ya Madina ndiyo uliokuwa msukumo na sababu ya ziara hii. [13]
Maudhui ya hotuba
Katika hotuba hii, Bibi Fatima (a.s) sambamba na kutangaza kujibari na kujiweka mbali na waliovunja mapatano [15] na kuwalaumu watu waliofuata hayo, anachora taswira ya kutokuwa kwao waaminifu [16] na anaelezea na kubainisha hali halisi ilivyo, anatabiri mustakabali mbaya wa Waislamu, sifa za serikali ya Alawi, udhaifu wa kifikra na tofauti za maoni ya watu wa Madina, jukumu la watu dhidi ya ufisadi wa serikali na kutoa taswira ya sura ya Saqifa. [17] Katika hotuba hii, Bibi Fatima anatumia Aya kadhaa za Qur’ani kama hoja ya anayoyasema, zikiwemo Aya ya 80 ya Surat al-Ma’ida kuhusu matokeo ya kufuata hawaa na matamanio ya nafsi, Aya ya 96 ya Surat a;-A’raf na Aya ya 51 ya Surat al-Zumar zinazowalaumu wale wasiofuata haki naAya ya 35 ya Surat Yunus inayoelezea watu wanaostahili uongozi. [18]
Kuwalaumu watu
Mwanzoni mwa hotuba yake, Bibi Fatima Zahra (a.s) aliwalaumu Muhajirina na Ansari kutokana na kuhadaiwa na kuingia katika mchezo wa mrengo unaotawala [19] na ukimya wao dhidi ya mkondo potofu na kufuatana nao, na anashtakia dhamira zao za chuma katika zama za Mtume (s.a.w.w) ambazo ambazo zimedhoofika katika zama za watawala hawa waliotwaa madaraka baada ya Mtume (s.a.w.w). [20] Bibi Fatima anawashabihisha na panga zilizovunjika na mikuki iliyogawanyika. [21] Kwa mujibu wa Hossein-Ali Montazeri, ushabihishaji huu unaonyesha udhaifu wa kifikra na msambaratiko wa maoni baina ya Waislamu mkabala wa matukio yaliyotokea baada ya kuaga dunia Bwana Mtume (s.a.w.w). [22] Bibi Fatima analichukulia jukumu la kunyakuliwa ukhalifa kuwa ni la Muhajirina na Ansari kwa sababu walifuata mkondo wa mtawala [23] na kwamba aibu yake itabakia kwao milele katika historia. [24]
Kubainisha sababu za kutengwa Imamu Ali (a.s) na Ukhalifa
Katika sehemu ya pili ya hotuba hiyo, Fatima anasema kuwa nia kuu ya kumtenga Imam Ali (a.s) na kutomruhusu aongoze kama Khalifa wa Waislamu baada ya Mtume (s.a.w.w) ilikuwa ni kutosalimu kwake amri, ushujaa wake katika medani za vita dhidi ya maadui wa Uislamu, kuonja ladha ya upanga wake, kutojali kwake kifo, hasira yake katika njia ya Mwenyezi Mungu, na kutopatana kwake na maadui.” [25]
Sifa maalumu za utawala wa Ali (a.s)
Katika sehemu ya hotuba yake, Fatima (a.s) alieleza kwamba kama Ali (a.s) angekuwa mtawala, vipi serikali ingekuwa ni ya watu. Kutenganisha haki na batili na kuizuia serikali isiwe mikononi mwa makafiri waliosalia, huruma ya mtawala na ihsani kwa Waislamu na kutowadhulumu katika njia ya uongofu, kuwanywesha wenye kiu ya haki kutoka kwenye chemchemi ya ukweli, kutoshikamana kwa mtawala na mambo ya kidunia, kumtofautisha muongo na ukweli na kumiminika baraka kwa jamii ya Kiislamu kutokana na kuchunga taqwa na uchamungu ni miongoni mwa dalili na ishara za serikali hiyo. [26]
Wasifu wa watawala maghasibu
Katika sehemu inayofuata ya hotuba yake, Bibi Fatima (a.s) alionyesha kushangazwa kwake na hatua ya Waislamu, ni kwa sababu gani walifuata marafiki wa uongo na kuchagua walinzi wasio na ustahiki, na kwa matumaini gani walifanya uonevu na unyanyasaji mwingi kiasi hiki? [27] Baadhi pia wamesema kwamba, pengine anachomaanisha Bibi Fatima katika sehemu hii ya hotuba yake ni kwamba, kwa hoja gani watu wameacha kiegemeo (tegemeo) chenye nguvu na madhubuti kama Ali na Ahlul-Bayt (a.s) na wakachagua wengine badala yao. [28] Kwa mujibu wa wake ni kuwa, watu wameacha kichwa na kushikamana na mkia na kuwafuata watu wa kawaida na kumuacha msomi na kisha muovu kumfanya kuwa mtenda mema. Fatima anawachukulia kuwa ni wapotovu wanaodhani kuwa ufisadi wao ni mzuri. [29]
Kutabiri mustakabali usio na utulivu
Onyo kuhusu matokeo ya chaguo lisilo sahihi ni sehemu ya mwisho ya maneno ya Fatima katika hotuba yake hii. Anawatahadharisha watu dhidi ya panga zenye kushinda, utawala wa wavamizi madhalimu na wanywaji damu, machafuko yaliyoenea, na serikali dhalimu inayoharibu mali ya Waislamu na kuwatawanya watu wao. [30] Kwa mujibu wa Makarim Shirazi, huenda Fatima anaashiria utawala wa Bani Umayyah na Bani Abbas na watu kama Hajjaj bin Yusuf na matukio kama vile tukio la Harra. [31]
Radiamali ya wanaume wa Muhajirina na Ansari kwa hotuba ya Fatima (a.s)
Kwa mujibu wa Suwaid bin Ghaflah, baada ya wanawake hao kusimulia maneno ya Fatima (a.s) kwa waume zao, kundi miongoni mwao lilikwenda kwa Fatima kumwomba msamaha, na kwa kisingizio kwamba walikuwa wameweka kiapo cha utii kwa Abu Bakr na kisheria hawawezi kuvunja kiapo chao na kwa hivyo wana udhuru wa kutowasaidia Ahlul-Bayt (a.s). Baada ya Bibi Fatima kusikia maneno yao Bibi Fatima Zahra (a.s) alisema: Ondokeni zenu, na msiongee na mimi kwa sababu msamaha wenu ni wa uwongo [32] na nyinyi hamna kisingizio chochote cha kuacha kutetea haki na nyinyi mnabeba dhima ya maafa ambayo yatatokea katika mustakabali. [33]
Vyanzo vya hotuba
Hotuba ya Bibi Fatima katika hadhara na mkusanyiko wa wanawake wa Muhajirina na Ansari imesimuliwa na kunukuliwa na wapokezi Maasumina na wasiokuwa Maasumina katika vitabu vya Shia na Sunni. [34] Hotuba hii imenukuliwa kwa mapokezo kadhaa [35] ambapo miongoni mwayo ni:
- Sheikh Saduq katika kitabu cha Maan al-Akhbar ambapo amenukuu kwa njia mbili. Moja ya njia ya mapokezi yake ni kutoka kwa Imamu Ali (a.s) na nyingine ni kutoka kwa Abdallah bin Hassan bin Hassan kutoka kwa mama yake Fatima binti ya Imamu Hussein. [36]
- Tabari katika kitabu cha Dalail al-Imamah, amenukuu katika hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s) naye amenukuu kutoka kwa babu yake Imamu Sajjad (a.s). [37]
- Ibn Tayfur na Ibn Abil al-Hadid, miongoni mwa Maulamaa wa Ahlu-Sunna katika vitabu vyao vya Balaghaat al-Nisaa [38] na Sharh Nahaj al-Balagha [39] ambapo wamenukuu hotuba hii kutoka kwa Ibn Atiyyah Kufi.
- Ahmad bin Tabarsi pia ameleta hotuba hii katika kitabu chake cha al-Ihtijaj akinukuu kutoka kwa Suwaid bin Ghafla. [40] Allama Hilli anamtambulisha Suwaid kuwa mmoja wa marafiki wa Imamu Ali (as). [41] Allama Majlisi pia ameleta hayo katika kitabu chake cha Bihar al-Anwar akinukuu kitabu cha al-Ihtijaj. [42] Hussein-Ali Montazeri mmoja wa waliotoa sharh (maelezo) na ufafanuzi wa hotuba hii anasema, kuwa Suwaid bin Ghafla mpokezi wa hotuba hii alisilimu katika zama za Bwana Mtume (s.a.w.w) na alikuwa mtu mwenye ikhlasi ambaye wataalamu wa elimu ya hadithi wa Kishia na Kisuni wanamtambua kuwa mtu mwaminifu. [43]
Ufafanuzi
Hotuba ya Bibi Fatima (a.s) katika mkusanyiko wa wanawake wa Madina imefafanuliwa kwa njia ya kujitegemea na katika vitabu vingine.
- Malake Eslam: Kitabu hiki kilichondikwa na Mirza Halil Kamra’i kinafafanua hotuba ya Fadak ya Bibi Fatima na hotuba yake aliyoitoa mbele ya wanawake wa Madina walipokwenda kumtembelea alipokuwa mgonjwa. [44]
- Ranj Nameh Kausar Afarinesh: Kitabu hiki kilichoandikwa na Sayyid Mujtaba Burhani, kinafafanua hotuba ya Fatima aliyoitoa mbele ya wanawake wa Madina.
- Sharh Khutbeh Hazrat Zahra (a.s) wa Majaraye Fadak (Ufafanuzi wa hotuba mbili za fadak na Iyadat): Mwandishi Hussein-Ali Montazeri. [45]
- Zahran Bartarin Banuye Jahan: Mwandishi Naser Makarem Shirazi [46]. Kitabu hiki kinatoa ufafanuzi wa hortuba mbili za Fadak na hotuba mbele ya wanawake wa Madina waliokwenda kumtembelea bibi Fatima alipokuwa mgonjwa.
- Sireh va Simay Raihaneh Payambar: Mwandishi, Ali Karami Faridani. [47. Katika kitabu hiki mwandishi anatoa ufafamnuzi na maelezo kuhusu hotuba za Bibi Fatma sambamba na kufafanuya maisha na fadhila zake.
Andiko la hotuba kamili
وَ قَالَ سُوَیْدُ بْنُ غَفَلَةَ لَمَّا مَرِضَتْ فَاطِمَةُ س الْمَرْضَةَ الَّتِی تُوُفِّیَتْ فِیهَا دَخَلَتْ عَلَیْهَا نِسَاءُ الْمُهَاجِرِینَ وَ الْأَنْصَارِ یَعُدْنَهَا فَقُلْنَ لَهَا کَیْفَ أَصْبَحْتِ مِنْ عِلَّتِکِ یَا ابْنَةَ رَسُولِ اللهِ فَحَمِدَتِ اللهَ وَ صَلَّتْ عَلَی أَبِیهَا
ثُمَّ قَالَتْ أَصْبَحْتُ وَ اللهِ عَائِفَةً لِدُنْیَاکُنَّ قَالِیَةً لِرِجَالِکُنَّ لَفَظْتُهُمْ بَعْدَ أَنْ عَجَمْتُهُمْ وَ سَئِمْتُهُمْ بَعْدَ أَنْ سَبَرْتُهُمْ فَقُبْحاً لِفُلُولِ الْحَدِّ وَ اللَّعِبِ بَعْدَ الْجِدِّ وَ قَرْعِ الصَّفَاةِ وَ صَدْعِ الْقَنَاةِ وَ خَتْلِ الْآرَاءِ وَ زَلَلِ الْأَهْوَاءِ وَ بِئْسَ ما قَدَّمَتْ لَهُمْ أَنْفُسُهُمْ أَنْ سَخِطَ اللهُ عَلَیْهِمْ وَ فِی الْعَذابِ هُمْ خالِدُونَ
لَا جَرَمَ لَقَدْ قَلَّدْتُهْم رِبْقَتَهَا وَ حَمَّلْتُهُمْ أَوْقَتَهَا وَ شَنَنْتُ عَلَیْهِمْ غَارَاتِهَا فَجَدْعاً وَ عَقْراً وَ بُعْداً لِلْقَوْمِ الظَّالِمِینَ وَیْحَهُمْ أَنَّی زَعْزَعُوهَا عَنْ رَوَاسِی الرِّسَالَةِ وَ قَوَاعِدِ النُّبُوَّةِ وَ الدَّلَالَةِ وَ مَهْبِطِ الرُّوحِ الْأَمِینِ وَ الطَّبِینِ بِأُمُورِ الدُّنْیَا وَ الدِّینِ أَلا ذلِکَ هُوَ الْخُسْرانُ الْمُبِینُ
وَ مَا الَّذِی نَقَمُوا مِنْ أَبِی الْحَسَنِ ع نَقَمُوا وَ اللهُ مِنْهُ نَکِیرَ سَیْفِهِ وَ قِلَّةَ مُبَالاتِهِ لِحَتْفِهِ وَ شِدَّةَ وَطْأَتِهِ وَ نَکَالَ وَقْعَتِهِ وَ تَنَمُّرَهُ فِی ذَاتِ اللهِ وَ تَاللهِ لَوْ مَالُوا عَنِ الْمَحَجَّةِ اللَّائِحَةِ وَ زَالُوا عَنْ قَبُولِ الْحُجَّةِ الْوَاضِحَةِ لَرَدَّهُم إِلَیْهَا وَ حَمَلَهُمْ عَلَیْهَا وَ لَسَارَ بِهِمْ سَیْراً سُجُحاً لَا یَکْلُمُ حشاشه [خِشَاشُهُ] وَ لَا یَکِلُّ سَائِرُهُ وَ لَا یَمَلُّ رَاکِبُهُ وَ لَأَوْرَدَهُمْ مَنْهَلًا نَمِیراً صَافِیاً رَوِیّاً تَطْفَحُ ضَفَّتَاهُ وَ لَا یَتَرَنَّقُ جَانِبَاهُ وَ لَأَصْدَرَهُمْ بِطَاناً
وَ نَصَحَ لَهُمْ سِرّاً وَ إِعْلَاناً وَ لَمْ یَکُنْ یَتَحَلَّی مِنَ الدُّنْیَا بِطَائِلٍ وَ لَا یَحْظَی مِنْهَا بِنَائِلٍ غَیْرَ رَیِّ النَّاهِلِ وَ شُبْعَةِ الْکَافِلِ وَ لَبَانَ لَهُمُ الزَّاهِدُ مِنَ الرَّاغِبِ وَ الصَّادِقُ مِنَ الْکَاذِبِ وَ لَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُری آمَنُوا وَ اتَّقَوْا لَفَتَحْنا عَلَیْهِمْ بَرَکاتٍ مِنَ السَّماءِ وَ الْأَرْضِ وَ لکِنْ کَذَّبُوا فَأَخَذْناهُمْ بِما کانُوا یَکْسِبُونَ وَ الَّذِینَ ظَلَمُوا مِنْ هؤُلاءِ سَیُصِیبُهُمْ سَیِّئاتُ ما کَسَبُوا وَ ما هُمْ بِمُعْجِزِینَ
أَلَا هَلُمَّ فَاسْمَعْ وَ مَا عِشْتَ أَرَاکَ الدَّهْرَ عَجَباً- وَ إِنْ تَعْجَبْ فَعَجَبٌ قَوْلُهُمْ لَیْتَ شِعْرِی إِلَی أَیِّ سِنَادٍ اسْتَنَدُوا وَ إِلَی أَیِّ عِمَادٍ اعْتَمَدُوا وَ بِأَیَّةِ عُرْوَةٍ تَمَسَّکُوا وَ عَلَی أَیَّةِ ذُرِّیَّةٍ أَقْدَمُوا وَ احْتَنَکُوا لَبِئْسَ الْمَوْلی وَ لَبِئْسَ الْعَشِیرُ وَ بِئْسَ لِلظَّالِمِینَ بَدَلًا اسْتَبْدَلُوا وَ اللهِ الذَّنَابَی بِالْقَوَادِمِ وَ الْعَجُزَ بِالْکَاهِلِ فَرَغْماً لِمَعَاطِسِ قَوْمٍ یَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ یُحْسِنُونَ صُنْعاً ... أَلا إِنَّهُمْ هُمُ الْمُفْسِدُونَ وَ لکِنْ لا یَشْعُرُونَ- وَیْحَهُمْ أَ فَمَنْ یَهْدِی إِلَی الْحَقِّ أَحَقُّ أَنْ یُتَّبَعَ أَمَّنْ لا یَهِدِّی إِلَّا أَنْ یُهْدی فَما لَکُمْ کَیْفَ تَحْکُمُونَ
أَمَا لَعَمْرِی لَقَدْ لَقِحَتْ فَنَظِرَةٌ رَیْثَمَا تُنْتَجُ ثُمَّ احْتَلَبُوا مِلْءَ الْقَعْبِ دَماً عَبِیطاً وَ ذُعَافاً مُبِیداً هُنَالِکَ یَخْسَرُ الْمُبْطِلُونَ وَ یُعْرَفُ الْبَاطِلُونَ غِبَّ مَا أُسِّسَ الْأَوَّلُونَ ثُمَّ طِیبُوا عَنْ دُنْیَاکُمْ أَنْفُساً وَ اطْمَأَنُّوا لِلْفِتْنَةِ جَاشاً وَ أَبْشِرُوا بِسَیْفٍ صَارِمٍ وَ سَطْوَةِ مُعْتَدٍ غَاشِمٍ وَ بِهَرْجٍ شَامِلٍ وَ اسْتِبْدَادٍ مِنَ الظَّالِمِینَ یَدَعُ فَیْئَکُمْ زَهِیداً وَ جَمْعَکُمْ حَصِیداً فَیَا حَسْرَتَی لَکُمْ وَ أَنَّی بِکُمْ وَ قَدْ عَمِیَتْ عَلَیْکُمْ أَ نُلْزِمُکُمُوها وَ أَنْتُمْ لَها کارِهُونَ
قَالَ سُوَیْدُ بْنُ غَفَلَةَ فَأَعَادَتِ النِّسَاءُ قَوْلَهَا ع عَلَی رِجَالِهِنَّ فَجَاءَ إِلَیْهَا قَوْمٌ مِنَ الْمُهَاجِرِینَ وَ الْأَنْصَارِ مُعْتَذِرِینَ وَ قَالُوا یَا سَیِّدَةَ النِّسَاءِ لَوْ کَانَ أَبُو الْحَسَنِ ذَکَرَ لَنَا هَذَا الْأَمْرَ قَبْلَ أَنْ یُبْرَمَ الْعَهْدُ وَ یُحْکَمَ الْعَقْدُ لَمَا عَدَلْنَا عَنْهُ إِلَی غَیْرِهِ فَقَالَتْ ع إِلَیْکُمْ عَنِّی فَلَا عُذْرَ بَعْدَ تَعْذِیرِکُمْ وَ لَا أَمْرَ بَعْدَ تَقْصِیرِکُمْ.[۴۸]
Tarjuma ya hotuba
Suwayd bin Ghafla amesema: “Fatima alipougua na akafa shahidi kwa maradhi hayo, wanawake wa Muhajirina na Ansari walikuja kumzuru ambapo walipofika walimsalimia na kumwambia: “Ewe binti ya Mtume wa Mwenyezi Mungu vipi hali ya maradhi yako na uko nayo vipi? Bibi Fatima alimshukuru Mungu na kumswali baba yake. Kisha akasema: Najisikia kuchukizwa sana na ulimwengu wenu na ninachukia waume zenu! Nilipima hali zao na sikufurahishwa sana na walichofanya na niliwaweka kando. Kwa sababu wao ni wepesi kama ubapa (wa panga) ulio na kutu na kama mkuki uliogawanywa vipande viwili, nao ni wamiliki wa mawazo meusi na yasiyofaa. Ni mabaya kiasi gani yaliyotangulizwa na nafasi zao, hakika hasira za Mwenyezi Mungu ziko pamoja nao na wako kwenye moto na watabakia humo milele.
Kutokana na kutokuwa na budi, kamba ya mambo na wajibu imewekwa shingoni mwao, nikawaachia mzigo na jukumu la kazi, na nikawatwisha aibu ya kuua haki. Laana ya milele iwe juu ya hawa watenda maovu, wawe mbali na rehema ya haki madhalimu hawa, ole wao! Kwa nini hawakuzingatia haki katika kitovu chake? Na kwa njia hii, wakawa mbali na ukhalifa na misingi ya utume na wakautoa kutoka kwenye nyumba ambayo Jibril aliteremka na kuupeleka kwenye nyumba nyingine na wakauondoa katika uwezo wa wafanyakazi wa dini na ulimwengu! Kwa hakika, huko ni kuhasirika pakubwa.
Ni nini kiliwafanya wapate makosa na mapungufu kwa Ali (as)? Walisema kosa lake; ni wa sababu upanga wake haukujua mtu wake wala asiye katika wao (mgeni na ajinabi), jasiri na mwoga. Waligundua kwamba hajali kifo. Waliona jinsi anavyowakimbilia na kuwatupa kwenye bonde la uharibifu na kuwaacha wengine kwa adhabu na mfano kwa wengine. Mjuzi wa kitabu cha Mwenyezi Mungu, na hasira yake ilikuwa katika njia ya kumpendeza Mwenyezi Mungu. Naapa kwa Mwenyezi Mungu, lau wasingekataa kupokea hoja na dalili zilizo wazi na bayana kupitia njia ya ukweli iliyo wazi na inayoonekana, wangeongoka na kuongozwa na kuzuiwa kuingia kwenye upotofu na kupotea. Naapa kwa Mwenyezi Mungu, lau waume zenu hawangeiacha mikono ya Ali wakati yeye hayuko katika udhibiti wa mambo, na wangemkabidhi mipango ya kazi kama alivyokabidhiwa na Mtume, basi angeisimamia kwa wepesi na angelimfikisha ngamia huyu mahali pake kwa salama, kiasi kwamba mwendo wa ngamia huyu usingekuwa wa mateso na mchungu. Ali angewaongoza kwenye kisima kisafi na kilichojaa maji, ambapo maji yalitiririka na katu hayakuwahi kuwa na rangi ya uadui.
Ali anawapendelea kheri na wema kwa siri na wazi kwa ajili yao. Lau angekaa kwenye kiti cha uongozi, kamwe hangejinufaisha na mali ya hazina ya dola kwa ajili yake, na asingechukua kutoka kwa wingi na mali ya dunia isipokuwa kiasi cha mahitaji, ambacho huzima kiu na chakula ambacho kinakata njaa. (Wakati huo) mtu mchamungu angetambulika kutokana na kiu ya uharibifu wa dunia, na mkweli angetofautishwa na mwongo, katika hali hii, milango ya baraka za mbinguni na duniani ingefunguliwa kwa ajili yao, na hivi karibuni Mwenyezi Mungu atawaadhibu kwa amali na matendo yao. Kwa sababu: “Na lau kuwa watu wa miji wangeli amini na wakamchamngu, kwa yakini tungeli wafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi. Lakini walikanusha basi tukawapatiliza kwa sababu ya yale waliyo kuwa wakiyachuma. Na wale walio dhulumu miongoni mwa hawa utawasibu uovu wa waliyo yachuma vile vile. Nao si wenye kushinda.”
Njooni! na msikilize! Ni aina gani ya zama ambazo umri huficha na ni michezo gani inafunua moja baada ya nyingine. Laiti ningejua wametegemea makazi hifadhi gani? Na wameunga mkono safu gani? Na ni kamba gani walishikamana nayo? Na ni nasaba gani walitangulia na kushinda? Inashangaza! wamechagua uongozi mbaya na kuchagua marafiki wabaya, na waovu [waliomtii Shetani badala ya Mungu] ni mbadala gani mbaya walioufanya. Wameweka mkia kwenye bawa badala ya manyoya makubwa, wamekabidhi kichwa na kuchukua mkia. Wametumbuikia katika madhila "waliodhani kuwa walifanya jambo jema kwa vitendo hivi, tambueni kwamba, wao ni wafisadi, lakini wao wenyewe hawajui." Ole wao! Basi, je, anaye stahiki kufuatwa ni yule Mwenye kuongoa kwendea Haki au asiye ongoa ila aongozwe yeye? Basi nyinyi mna nini? Mnahukumu namna gani?
Lakini anaapa kwa roho yangu (maisha yangu) kwamba, mbegu ya hii imefungwa. [Na ngamia wa fitna hii atazaa hivi karibuni] Subirini mpaka ufisadi huu uenee katika mwili wa umma wa Kiislamu. Baada ya hapa, kamueni katika chuchu za ngamia ambapo kutatoka damu na sumu ambayo ni angamizi. “Hapa ndipo watapata hasara wale wanaofuata njia ya batili” na Waislamu watakaofuata watajua hali ya Waislamu ilikuwaje mwanzoni mwa Uislamu. Moyo wenu utatulizwa na fitina. Bishara kwenu kwa panga zilizochomolewa na zenye ncha kali, na shambulio kali la dhalimu, na mkanganyiko wa mambo ya kila mtu na kujiona kuwa waadilifu kwa madhalimu! Watakupeni ngawira kidogo na mshahara. Nao wataufukuza umati wenu kwa panga zao. Na hamtavuna ila matunda ya majuto. Kazi yenu itafikia wapi? Wakati "ukweli wa mambo umefichwa kwenu. Je, nikulazimisheni kufanya kitu ambacho mnachukia?"
Suwaid bin Ghafla anasema: Wanawake waliokuwepo kwenye mkusanyiko huo waliwafikishia waume zao maneno ya Fatima (as). Baada ya hapo, kundi la wazee na shakhsia wakubwa wa Muhajirina na Ansari walikwenda kwa Fatima Zahra (as) na kumwambia: Ewe kiongozi wa wanawake ulimwenguni! Lau Abu al-Hassan (a.s.) angetuambia ukweli kabla hatujafanya na kufunga agano madhubuti na imara na yule mwingine (Abu Bakr), tusingempa kisogo na kutamani mwingine. Bibi Fatima (as) akasema: Nilikuwa na jukumu la kueleza ukweli (ilikuwa ni ushauri kutoka kwangu kwa ajili yenu), nimekamilisha hoja kwenu. Udhuru wenu sio kisingizio kinachokubalika na kinachofaa, na kosa na upungufu wenu unatambuliwa na hakuna kisingizio au uhalali unaweza kufikirika baada ya hapo. [49]
Rejea
Vyanzo