Hizbu (Qur’an)
Hizbu (Kiarabu: حزب (قرآن)) ni moja ya vifungu na migawanyo ya Qur’an. [1] Kila juzuu ya Qur’an hugawanywa katika hizbu kadhaa. [2] Katika baadhi ya Qur’an kila juzuu hugawiwa vifungu viwili. [3] Hivyo basi iwapo kila juzuu itagawiwa vifungu viwili, jumla kutakuwa na hizbu 60 za Qur'an. [4] Baadhi wamegawanywa kila juzuu hizbu nne ambapo kwa mgawanyo huu Qur’an itakuwa na hizbu 120. [5] Kadhalika kila hizbu inagawanywa mara nne ambapo kila sehemu yake inajulikana kwa jina la robo. Kwa maana kwamba, hizbu ina robo nne. [6] Ugawanyaji huu umefanyika kwa mujibu wa Aya. [7] Kwa mujibu wa hadithi ambazo baadhi zimenukuliwa katika vyanzo vya ahlu-Sunna, imenukuliwa kutoka kwa Omar bin al-Khattab ya kwamba, istilahi ya hizbu ilikuweko katika zama za Mtume (s.a.w.w) na katika mazungumzo yake na Waislamu walikuwa wakisoma hizbu moja kila siku. Hata hivyo katika hadithi hii hakujaashiriwa kiwango na kiasi cha hizbu. [8]
Katika baadhi ya nchi kama Iran, kila hizbu huchapishwa kando na majimui ya machapisho haya ya Qur’an inafahamika kwa jina la Qur’an ya mgawanyiko mara 120. Nakala na chapa za namna hii hutumika katika shughuli na visomo vya khitma. [9] Hata hivyo, Sayyid Muhammad Hussein Tehrani (aliaga dunia: 1416 Hijria) alikuwa akipinga kugaiwa Qur’ani katika khitma kwa sura ya juzuu juzuu. Alikuwa akitambua ada hii kwamba, ilienea katika zama za Yazid bin Muawiya na alikuwa akiamini kwamba, katika khitma ni lazima Qur’ani kamili itumike. [10]
Lengo la kugawanywa Qur’an juzuu juu au hizbu hizbu limetambuliwa kuwa ni kumshajiisha msomaji kusoma zaidi [11] na urahisi wa kuhifadhi [12] na kufundishia pia. [13] Wazo la kugawa Qur’an katika sura ya juzuu na hizbu linanasibishwa na Maamun mtawala wa Bani Abbas (aliaga dunia: 218 Hijiria); ingawa baadhi wamelinasibisha hilo na Hajjaj bin Yusuf al-Thaqafi (aliaga dunia: 95 Hijria). [14] Miongoni mwa mapunfuzfu yaliyotajwa ya kuigawa Qur’an katika mtindo wa juzuu na hizbu ni kumalizika kisomo katikati ya maneno au kuanza kisomo baina ya maudhui. [15]
Mwandishi wa kitabu cha al-Ziyadah Wal-Ihsan fi ulumi al-Qur’an ni kuwa, masahaba wa Mtume (s.a.w.w) wakiwa na lengo kuhitimisha Qur’an katika wiki moja, waliigawa katika sehemu saba ambapo kila sehemu moja walikuwa wakiita kuwa ni hizbu moja. [16] Ugawanyaji huu ulikuwa ukifanyika kwa mujibu wa sura. [17] Kwa mujibu wa aina hii ya ugawaji, hizbu ya kwanza ilikuwa ikijumuisha sura tatu za awali za Qur’an (ukiacha Surat al-Fatiha). Hizbu ya pili ilikuwa na sura tano zilizofuata, hizbu ya tatu Sura saba zilizofuata, hizbu ya nne ilikuwa na sura tisa zilizofuata, hizbu ya tano sura 11 zilizofuata, hizbu ya sita sura 13 zilizofuata na hizbu ya saba ambayo walikuwa wakiita ‘Hizb Mufassal” ilikuwa ikunda sura zilizobakia (kuanzia Suraf Qaaf mpaka mwisho wa Qur’an). [18] Ugawaji wa sehemu saba nyingine umenukuliwa pia na masahaba. [19] Kwa mnasaba huu inaelezwa kuwa, kila sehemu ya Qur’an ambayo mtu anajilazimisha kuisoma, inaitwa hizbu. [20]
Rejea
Vyanzo