Hima elekeni kwenye amali njema

Kutoka wikishia
Kitabu cha Adhana بحی علی خیر العمل kilichoandikwa na Muhammad Alawi moja ya wanazuoni wa Zaidiyyah

Hayya 'Alaa Khair Al-‘Amal (Kiarabu: حي على خير العمل) ni mshororo au kipengele cha Adhana na Iqamah, chenye maana ya "Fanyeni haraka na hima kuelekea kwenye amali bora". Kwa mujibu wa baadhi ya Hadithi, kifungu hichi cha maneno haya kilikuwa ni moja ya mishororo ya wito wa kuswali (Adhana) na Iqamah wakati wa uhai wa bwana Mtume (s.a.w.w), lakini Khalifa wa pili alikiondoa kwenye Adhana ili kuwahimiza watu kufanya jihadi yaani kwa nia ya kutaka kuipa thamani jihadi.

Ibara ya; Haya (Alaa Khair Al-Amal ; حَیَّ عَلی خَیرِ العَمل) bado Mashia wanaendelea kuitumia katika Adhana na Iqamah. Ila Sunni hawaitumii tena ibara hiyo katika wito wa sala (Adhana) zao. Kwa hiyo, Ibara hiyo imegeuka kuwa ni kama nembo na alama ya Mashia duniani. Kwa upande mwingine, (Al-Salaatu Khairٌun mina Al-Naum' ; الصلاةُ خَیرٌ مِنَ النَّوم) katika wito wa sala ya Alfajiri, imekuwa ndiyo nembo na alama ya Masunni. Ibara ya; 'Al-Salatu Khairun Mana Al-Naum', iliongezwa kwenye wito wa sala ya Alfajiri wakati wa zama za Khalifa wa pili, ambapo Mashia wanaihisabu ibara hii kuwa ni uzushi (bid-a).

Hadhi na Nafasi Yake

Maana hasa ya «Hayya 'Alaa Khair Al-Amal' ; {{Arabic|حَیَّ عَلی خَیرِ العَمل» ni; Fanyeni hima na haraka kuikimbilia amali bora na ni moja ya mishororo ya Azan na Iqamah. Sentensi hii ni moja ya tofauti zinazowatofautisha Mashia na Masunni katika wito wa sala zao pamoja na Iqamah. [1] Wakati mwingine mishororo miwili ya Adhana, amabyo ni (Hayya 'Alaa Al-Sala” ; حَیَّ عَلَی الصّلاة) na (Hayya 'Alaa Al-Falaah” ; حی علَی الْفَلاح) huitwa (Hay 'Ala" ; حَیْعَلَه)[2]

Je, «Hayya 'Alaa Khairi Al-'Amal» ni Sehemu ya Adhana?

Mafakihi wa Kishia wanamchukulia ibara ya 'Hayya 'Alaa Khairi Al-'Amal', kuwa ni sehemu na nguzo ya Adha na Iqamah, imbara ambayo husomwa baada ya mshororo wa Adhana usemao; (Hayya 'Alaa Al-Falaah ; حَیَّ عَلَی الفَلاح) yaani (Kimbileni kwenye kufuzu). [3] mafaqihi wa Kisunni hawaifikirii wa kuihisabu ibara hii kuwa nisehemu ya Adhana, seuze tena waitafiti kuwa ni wajibu au si wajibu. Mafaqihi wa Kisunni hata ile ibara ya Adhana yao ya sala ya Alfajiri isemayo; ('Al-Salatu Khairun Mina Al-Naum' ; الصلاة خیر من النوم), yenye maana ya kwamba 'Sala ni bora kuliko usingiza', hawaihisabu huwa ni sehemu au ni nguzo ya Adhani. Bali wao huihisabu ibara hiyo kuwa ni ibara pendekezwa (mustahabbu) tu. ” [4] Kwa mujibu wa mtazamo wa Kisunni, ni makuruhu (ni chukizo) au haipendekezwi kusema (Hayya 'Alaa Khairi Al-'Amal' ; حی علی خیر العمل). katika Adhana. [5]

Kwa mujibu wa Hadithi, katika zama za Mtume (s.a.w.w), ibbara ya Hayya 'Alaa Khairi Al-'Amal ilikuwa ni sehemu na ni nguzo. [6] Pia kuna ripoti kwamba baadhi ya masahaba kama vile Abdullah Ibn Umar, [7] Bilal Habashi [ 8] na Abu Mahzuura [9] walikuwa wakiisoma na kuitumia ibara hii walipokuwa wakiadhini.

Kuondolewa Kwake katika Adhana

Wakati wa utawala wa Umar bin Khattab, kwa amri yake, Hayya 'Alaa Khairi Al-'Amal iliondolewa kwenye wito wa sala (Adhana). [10] Kwa mujibu kauli ya Sheikh Swaduq, akimnukuu Ibn Abbas, ambapo alisema ya kwamba; Lengo la khalifa wa pili lilikuwa ni kuwazuia watu wasiipe mgongo amali ya Jihadi kwa kisingizio cha kuwa sala ndiyo amali bora zaidi. [11] Katika riwaya ya Imamu Kadhim (a.s), sababu ya kweli na iliyofichika kuhusiana na sababu hasa ya Khalifa huyo kuifuta ibara hiyo; Ni kuwazuia watu wasiwaelekee Maimamu watoharifu (a.s) na kushikamana nayo. Ingawaje dhahiri yake imedaiwa kuwa yeye alikhofu watu kuikimbia Jihadi. Msingi tegemezi wa maelezo ya Hadithi hii, unatokana na Hadithi ya Imamu Swadiq (a.s), alipokuwa akijibu swali aliloulizwa kuhusiana na maana ya ('Hayya 'Alaa Khairi Al-'Amal' ; حی علی خیرالعمل) naye akajibu kwa kusema; Maana yake ni kushikamana na (Wilaya), yaani kushikamana na Maimamu watoharifu. [13]

Nembo ya Adhana ya Shia

Hayya 'Alaa Khairi Al-'Amal (حی علی خیر العمل) imekuwa ni moja ya alama na nembo za Shia. Kwa hiyo, katika serikali za Kishia, ilikuwa ni kawaida ibara hiyo kusomwa katika Adhana. Lakini watawala wa Kisunni waliiondoa Hayya 'Alaa Khairi Al-'Amal ; (حی علی خیر العمل) kwenye wito wa sala (kwenye Adhana).

  • Mnamo mwaka wa 169 Hijiria, pale Mashia walipouteka mji wa Madina wakati wa msimamo wa Hussein bin Ali (Shahidi Fakh), walimlazimisha muadhini katika Adhana ya sala ya Alfajiri kusema Hayya 'Alaa Khair Al-‘Amal ; (حی علی خیر العمل). Gavana wa Madina alikimbia baada ya kuisikia Adhana hiyo. [14]
  • Wakati wa zama za Nasser Atrush (aliyefariki mwaka 304 Hijiria), kauli mbiu ya Mashia ilikuwa ni kusema "Hai Ali Khair al-Alam" katika Adhana na kutumia bendera nyeupe. [15]
  • Wakati wa utawala wa Fatiyyah (Ulioanzia mwaka 297 hadi 567 Hijiria) huko Misri, walitu ibara ya Hai 'Alaa Khairi Al-'Amal katika Adhana zao. [16] Mnamo mwaka wa 359 Hijiria, kwa mara ya kwanza kabisa nchini Misri, ibara ya Hayya 'Alaa Khairi 'Al-'Amal ilisikika katika Adhana ya msikiti wa Ibnu Tutun. [17] Baada ya Salahu Al-Din Ayyubi kuuteka mji wa Misri, aliiondoa ibara hiyo kwenye Adhana. [18]
  • Wakati wa utawala wa Aal-Buweih (Aali Buweihi) (uliotawala kuanzia mwaka 322 hadi 448 Hijiria), Hayya 'Alaa Khairi 'Al-'Amal ilikuwa ni miongoni mwa mishororo ya Adhana za utawala huo. Baada ya utawala wa Seljuqiyaan kushika hatamu za serikali, waliuondoa mshororo huo katika vipengele vya Adhana. [19]
  • Mnamo mwaka 441 Hijiria, kulikuwa na mzozo wa kimadhehebu katika kitongoji cha Karkh huko Baghdad. Mashia walikuwa wakiitumia ibara ya Hayya 'Alaa Khairi Al-'Amal' katika Adhana zao [20] Mnamo mwaka wa 448 Hijiria, kwa amri ya mtawala wa wakati huo, ikaondolewa ibara ya 'Hayya Alaa Khairi Al-'Amal' katika Adhana na kaongezwa Al-Salatu Khairun Mina Al-Naum kwenye sala ya Al-fajiri. [21]
  • Baada ya Muhammad Ghiathu Al-Diin anayejulikana kwa jina la 'Uljaito' (aliyeishi baina ya mwaka 680 na 716 Hijirira) kuingia katika madhehebu ya Shia nchini Iran, kupitia amri yake; 'Alaa Khairi Al-'Amal' iliwekwa rasmi kwenye Adhana za sala. [22]

Nembo na Alama ya Adhana ya Kisunni

Kinyume na ibara ya 'Hayya Alaa Khairi Al-'Amal' ambayo ni nembo ya Adhana ya Kishia, ibara ya 'Al-Salat Khairun Mina Al-Naum' au “Tawheeb” ni ishara na nembo ya Adhana ya Masunni. [23] Kwa mujibu mtazamo wa Shia Imaamiyyah na Zaidiyyah, 'Tathwiib' yenye maana ya ibara ya kuongeza 'Al-Salat Khairun Mina Al-Naum' katika Adhana ni uzushi (Bid-'ah). [24] kwa sababu kauli na vitendo vya Masahaba si uthibitisho wala hoja ya kusimamisha misingi na nyenendo za kidini. Bali kauli, matendo na taqriri ya Maasumu (Mtume au Imamu (a.s), ndio msingi na ithibati za kusimamisha misingi na nyenendo za kidini. [25]

Maana ya amali njema (خیر العمل)

Katika baadhi ya Hadithi, amali njema (خیر العمل), imefasiriwa kuwa ni sala [26], lakini kwa mujibu wa baadhi ya Hadithi nyingine, maana ya amali njema, imeelezwa kwa ni; (Wilaya) kushikama [27] au kumfanyia wema bibi Fatima pamoja na watoto wake (a.s). [28]

Orodha ya Vitabu na Maandiko

kuna mengi yalioandikwa kuhusu ibara ya Hayya 'Alaa Khairi Al-'Amal: baadhi yake ni kama ifuatavyo:

  • Al-Aadhanu Hayya 'Alaa Khairi Al-'Amal «الاذان بحیّ علی خیر العمل» cha Muhammad bin Ali bin Hassan Alawi (aliyezaliwa mwaka 445 na kufariki 367 Hijiria), naye ni mmoja wa wanazuoni wa madhehebu ya Zaidiyyah: Kitabu hichi, kimekusanya ndani yake riwaya kuhusiana na ibara ya "Hayya 'Alaa Khairi Al-'Amal" kuwa sehemu ya adhana au la. Zaidiyyah, kama sambamba na Imaamiyyah wanaihisabu ibara ya "Hayya 'Alaa Khairi Al-'Amal" kuwa ni sehemu na nguzo ya Adhana [29]. Kitabu hichi kimetafitiwa na Mohammad Yahya Salem Azzan, mtafiti wa Zaydiyyah, na kimechapishwa na Badr Al-Alami na Al-Thaqafi Centre huko Sana'a, mwaka 1418 Hjiria sawa na1997 Miladia.
  • Hayya 'Alaa Khairi Al-'Amal Baina Al-Shari'ati wa Al-Ibtada'i «حی علی خیر العمل بین الشریعة و الابتداع» kilichoandikwa na Mohammad Salem Azan. Kitabu hichi chenye kurasa themanini kilichapishwa huko Yemen mwaka wa 1419 Hijiria. [30]
  • Juz-iyyatu Hayya 'Alaa Khairi Al-'Amal Fi Al-Aadhan «جزئیة حی علی خیر العمل فی الاذان» kilichoandikwa na Abdul Al-Mir Soltani, Chapa ya Majma Jihani Ahlu Al-Bait (a.s)
  • Al-Aadhan Baina Al-Asaalati wa Al-Tahrifi Hayya Alaa Khairi Al-'Amal Al-Shari'atu Al--Shi'aariyyah kilichoandikwa na Sayyid Ali Shahrishtani
  • Hayya 'Alaa Khairi Al-'Amal, Masaa-ili Al-Shar-'iyyah Baina Al-Sunnati wa Al-Bi-d'ah, kilichoandikwa na Sayyid Muhammad Mahdi Khorsan. [31]

Maudhui Yanayo Husiana

Rejea

Vyanzo

  • Abū l-Faraj al-Iṣfahānī, ʿAlī b. al-Ḥusayn. Maqātil al-ṭālibīyyīn. Edited by Sayyid Aḥmad Ṣaqar. Beirut: Dār al-Maʿrifa, [n.d].
  • Dhahabī, Muḥammad b. Aḥmad al-. Tārīkh al-Islām wa wafayāt al-mashāhīr wa l-aʿlām. Edited by ʿUmar ʿAbd al-Salām Tadmurī. Second edition. Beirut: Dār al-Kitāb al-ʿArabī, 1413 AH.
  • Ibn Athīr, ʿAlī b. Muḥammad. Al-Kāmil fī l-tārīkh. Beirut: Dār al-Ṣādir, 1965.
  • Ibn Kathīr, Ismāʿīl b. ʿUmar. Al-Bidāya wa l-nihāya. Beirut: Dār al-Fikr, 1986.
  • Ibn Khaldūn, ʿAbd al-Raḥmān b. Muḥammad. Dīwan al-mubtadaʾ wa l-khabar. Edited by Khalīl al-Shaḥāda. Second edition. Beirut: Dār al-Fikr, 1408 AH.
  • Mālik b. Anas. Al-Muwaṭṭaʾ. Edited by ʿAbd al-Wahhāb ʿAbd al-Laṭīf. Second edition. [n.p], al-Maktaba al-ʿIlmīyya, [n.d].
  • Maqdisī, Muḥammad b. Aḥmad al-. Aḥsan al-taqāsīm fī maʿrifat al-aqālīm. Translated to Farsi by ʿAlī Naqī Munzawī. Tehran: Shirkat-i Muʾallifān wa Mutarjimān-i Iran, 1361 Sh.
  • Qāshānī, ʿAbd Allāh b. Muḥammad. Tārīkh Oljaito. Edited by Mahīn Hambalī. Tehran: Bungāh-i Tarjuma wa Nashr, 1348 Sh.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. ʿIlal al-sharāʾiʿ. Qom: Intishārāt-i Dāwarī, 1385 Sh.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Maʿānī l-akhbār. Beirut: Dār al-Maʿrifa, 1399 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Man lā yaḥḍuruh al-faqīh. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1413 AH.
  • Sayyid Murtaḍā, ʿAlī b. al-Ḥusayn. Al-Intiṣār fī infirādāt al-imāmīyya. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1415 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Tahdhīb al-aḥkām. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1407 AH.