Hassan Mwalupa
Sheikh Hassan Mwalupa (Kifarsi: حسن مالوپا) (1957-2021 A.D) alikuwa ni Muballighi wa maktab (madhehebu) ya Ahlul-Bayt (a.s) katika eneo la Afrika Mashariki kiasi kwamba umri wake mtukufu na wenye Baraka aliuweka waqfu kwa ajili ya kutarjum vitabu vya kiislaam kwa lugha ya Kiswahili. Kwa hakika kwa kuitarjumi kwake Qur'an tukufu kwa lugha ya Kiswahili aliweka mazingira safi na mazuri ya kuhamisha maarifa safi na ya asili ya Uislamu kwenda kwa watu wazungumzao Kiswahili, na alifanya juhudi za aina yake na za kipekee katika kuwafanya wazungumzaji wa Kiswahili watambue na kufahamu maarifa ya asili ya Uislamu.
Kutarjumi kwake tafsiri ya juzuu 30 ya tafsiri Al-kaashif athari nzuri ya Allamah Mughniya kwa lugha ya Kiswahili ni miongoni mwa huduma zake nzuri alizo zifanya kwa jamii ya Waislamu wa Afrika Mashariki kiasi kwamba tafsiri na tarjama hiyo ilipokelewa kwa kiwango kibubwa kwa wapenda maarifa ya kiislaam.
Mfasiri na mtarjumi huyu mkubwa wa Qur'an tukufu, alikuwa ni miongini mwa watu waliokuwa na mafungamano na Majmaa Ahlul-bayt (a.s), na pamoja na kutarjumi kwake vitabu vingi vya kiislaam kwa lugha ya Kiswahili, pia alikuwa ni miogoni mwa waasisi wa madrasa ya Amiril-muuminiin katika eneo la Matuga na pia alijishughulisha na ufundishaji wa maarifa ya Ahlul-bayt (a.s).
Safari Yake ya Kutafuta Elimu
Sheikh Hassan Mwalupa amezali mnamo tarehe 8 Nov mwaka 1957 A.D katika mji wa Tanga ncini Tanzania. Na masomo yake ya awali aliyapata katika madrasa ya Shamsia na katika miaka hiyo hiyo ya utotoni aliweza kujifunza lugha ya Kiarabu na kuhitimu katika lugha hiyo. Kisha kwa ajili ya kujiendeleza na kupata maarifa zaidi ya kiislaam chini ya usimamizi na uangalizi wa Maulana Sheikh Dhafar Abbas ambae kwa sasa anaishi Uingereza alijiunga na taasisi inayojishughulisha na uenezaji wa dini na tablighi ya kidini ya Bilal katika mji wa Mombasa nchini Kenya. Sheikh Hassan kabla ya kurejea na kurudi Tanzania alishughulika kama mwalimu kwa muda mchache katika mji wa Mackinnon Road katika nchi ya Kenya na kufanikiwa kuoa kwenye mji huo.
Vivyo hivyo alifanya safari ya miaka mitatu katika mji wa Tehran nchini Iran na kuweza kujipatia pia kujifunza masomo ya kihawza kwenye mji huo. Kwa hakiki yeye katika muda alio ishi Tehran aliweza kufahamiana na kuwa na ukaribu na baadhi ya walimu wabobezi wa kihawza kama vile Ayatullah Hadi Al-Mudarrisi na Ayatullah Taqi Mudarrisi.
Allamah Taqi Al-mudarrisiy akiitakidi kwamba ni faida ndogo sana watu wananufaika nayo kutoka kwa Sheikh Hassan Mwalupa na akisema kwamba: hapana budi Sheikh Hasan Mwalupa awe na harakati nyingi zaidi nchini mwake, jambo hilo lilipelekea Sheikh Hassan Mwalupa kurejea kwenye mji wa Mombasa.
Harakati Zake za Kielimu na Kitamaduni Afrika Mashariki
Sheikh Mwalupa, baada ya kurejea Mombasa, akaanza kazi ya kufasiri vitabu vya Kiarabu kwa lugha ya Kiswahili. Na miongoni mwa anwani alizo zifanyika kazi ni kujishughulisha na kazi ya kutarjumi tafsiri adhiim ya Al-miizaan ya Allamah Twabatwabi kiasi kwamba ameweza kukamilisha tarjama ya juzu ya thalathini na kabla ya kufariki kwake alikuwa akijishughulisha na suala la kuchapisha juu ya pili ya tafsiri hiyo. Kwa hakika Shekhe Mwalupa kutokana na usaidizi na ushirikiano na shekhe Abdillah Nassir, waliweza kuanzisha Madrasa ya Amiril-muuminii katika eneo la Matuga na kwa njia hii waliweza kutuma wanafunzi wengi sana nje ya nchi kwa ajili ya kujiendeleza katika kupata maarifa na elimu mbali mbali za kiislaam kiasi kwamba wengi miongoni mwa wanafunzi hao waliweza kujipatia na kufikia daraja tofauti za kielimu, na kwa sasa wanasimamia nafasi mbali mbali kama vile Imamu, Mwalimu na anwani zingine na wanazo harakati mbali mbali katika vituo mbali mbali katika eneo la Afrika Mashariki.
Vile vile kuna kiwango cha takriban wanafunzi 3000 ambao moja kwa moja wamekuwa chini ya usimamizi na uangalizi wa Marhum Shekhe Hasan Mwalupa watu ambao walipata masomo na wanafunzi kutoka kwa shekhe na wanafunzi hao humuangalia shekhe Mwalupa kama mlezi wao na humtaja kama kigezo chema kwao. Sheikh Mwalupa alisimamisha na kuweka semina na daura za mafuzno mafupi nyingi sana aliyaweka kwa ajili ya walimu wa taasisi mbali kiasi kwamba kwa njia hii akilenga kuinua kiwango cha kielimu na kuwaongezea uwezo katika fani zao na pia kukuza uwezo wao katika nyanja hizo.
Kwa hakika Sheikh Mwalupa katika maisha yake pia aliendelea na harakati za kurekodi vipindi vya televisheni kwa ajili ya Kanali ya Televisheni ya IBN Afrika (IBN TV Afrika) na katika kipindi cha kuenea ugonjwa wa Covid 19 (virusi vya Korona) aliendelea na masomo ya online (kwa njia ya mawasiliano ya intaneti) katika taasisi ya kitablighi ya Bilal Muslim Mission katika nchi ya Kenya.
Ushirikiano Wake na Taasisi ya Al-Itrah ya Dar es salaam
Sheikh Mwalupa, alikuwa na ratiba ya tarjuma na ufasiri wa vitabu kwa kushirikia na taasisi ya Al-Itrah ya mjini Dar es salaam (mji mkuu wa kibishara wa Tanzania) kiasi kwamba kila mwezi aliainisha siku kumi na kusafiri kuelekea kwenye mji huo kwa ajli ya kukamilisha na kuendelea na kazi ya kukamilisha ratiba hiyo na kuhakisha mpango huo unakamilika na kujiridhisha juu ya maendeleo ya mpango huo. Na mipango asili (project) aliyokuwa nayo kwa kushirikiana na taasisi ya Al-itrah ni kama zifuatazo:
- Kutarjumi tafsiri ya Al-kashaaf ya Allamah Muhammad Mughniyah yenye mijeledi 30 kwa lugha ya kiswahili, na tarjama hii ni tarjama ambayo iliwavutia wengi na wengi kuisifia na maimamu wengi wa Jamaa wa misikiti mbalimbali ya Afrika wamekuwa wakifaidika na kunukuu kutoka kwenye tafsiri hii. Na katika utangulizi wa kitabu hiki amendika kama ifuatavyo: (Mzungumziwa na mlengwa wangu wa asili na wa kwanza katika kitabu hiki, ni kizazi kipya pia vijana, kizazi ambacho kimeathirika na kuathiriwa na Aidiolojia za kimagharibi kama vile Capitalism (Ubepari), Socialism (Ujamaa) na Demokrasia ya kisasa. Kwa mtizamo wa Shekhe Mwalupa vijana wa Kiislamu wa Afrika kwa kiwango kikubwa ni wenye kuhitajia ufahamu mpya wa Uislaam ili waweze kukabiliana na fikra ngeni ambazo huwafikia na kutawanywa kupitia vitabu mbali mbali vya Kkiingereza, majarida, Televisheni na redio.
- Tarjuma ya Qur'an tukufu kwa lugha ya Kiswahili. Kwa mujibu wa tangazo la taasisi ya Kiislamu ya Al-itrah, tarjama hii ya Kiswahili ya Qur'an tukufu inaweza kutumika kwa ajili ya makundi yenye urimri bali tofauti na inaweza kuwafaidi makundi yote ya umri na inarahisisha na kufanya wepesi katika kujifunza aya za Qur'an. Na nakala au chapa hii, imepangiliwa kiasi kwamba matini ya aya zimewekwa upande wa kulia na tarjama yake kwa lugha ya Kiswahili imeweka katika ukurasa ulio mkababala wake. Sheikh Mwalupa amesema kuhusiana na tarjama ya Qur'an:(Mtarjumi wa Qur'an si tu kwamba anapaswa kuwa mbobezi kwenye lugha ya Kiarabu na elimu za Kiislamu, vilevile mtarjumi haipaswi kujielekeza na kutosheka tu na suala la kufahamu Wahyi na maneno ya Mwenyezi Mungu, bali hapana budi kuzihisi kwa dhati na kwa moyo wake Nyanja zote za Qur'an).
- Mpango (project) ya uandishi wa tafsiri ya Qur'an tukufu ni miongoni mwa harakati zingine za shekhe Mwalupa akishirikiana na taasisi ya Al-itrah.
- Marehemu Mwalupa, alikuwa ni msahihishaji wa vitabu vingi vya kidini vilivyo tarjumiwa na kufasiriwa kwa lugha ya Kiswahili na kusambazwa. Kwa hakika yeye pia aliweza kutarjumi Makala mbili za Ayatullah Haadi Mudarrisi na Ayatullah Muhammad Taqi Mudarrisi kwa lugha ya Kiswahili.
Tabia na Maadili Yake
Alikuwa ni mnyenyekevu, Mkweli, mpambanaji na mtu asie choka na mwenye nidhamu, hizi ni miongoni mwa sifa barizi alizokuwanazo shekhe Hasana Mwalupa. Yeye katika kueneza madhehebu ya Ahlul-baiti (a.s) katika eneo la Afrika mashariki alikuwa ni mwenye nafasi na mchango mkubwa na wa msingi na katika njia hii hakuacha kufanya juhudi zozote kuhakikisha jambo hilo linatimia.
Kufariki Kwake
Mwishowe, Sheikh Hassan Mwalupa aliaga dunia na kuitika wito wa Mola wake mnamo siku ya juma pili tarehe 25 July mwaka 2021 A.D katika mji wa Mombasa nchini Kenya na kuzikwa katika siku iliyo fuatia katika mji wa Matuga kijiji cha Kwala. Na kufuatia kifo chake shakhsiya mbalimbali na taasisi mbali mbali za kimadhehebu walituma salam mbali mbali za rambirambi na za maombolezo na kutoa mkono wa pole na salam za rambi rambi kwa kumpoteza Marhumu huyo adhiim.
Rejea
Vyanzo