Nenda kwa yaliyomo

Haram ya Kadhimayn (as)

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Haram ya Kadhimein)
Haram Takatifu ya Kadhimayn

Haram ya Kadhimayn (Kiarabu: الحرم الكاظمي) au Haram ya Maimamu wawili Kadhim na Jawad (a.s) ni mahali walipozikwa Maimamu wawili Mussa al-Kadhim (Imamu wa saba) na Muhammad Jawad (Imamu wa tisa) wa Waislamu wa madhehebu ya Shia. Haram hii ipo katika kitongoji cha Kadhimayn eneo ambalo kijiografia linapatikana kaskazini mwa Baghdad. Eneo hili takatifu hii leo limegeuka na kuwa sehemu ya kufanya ziara Waislamu hususan wafuasi wa madhehebu ya Shia nchini Iraq na wa kutoka maeneo mbalimbali duniani.

Haram ya Kadhimayn ina eneo la mita za mraba 26,000 na inaundwa sehemu tofauti kama vile uga, rawdha, minara, dharih (eneo la ndani linalolizunguka kaburi) ukumbi na kuba, na ndani yake kumetumumika sanaa mbali mbali kama kazi ya vioo, kazi ya vigae, uchovyaji wa dhahabu na kaligrafia (sanaa ya kuandika vizuri).

Ujenzi wa jengo la kwanza la Maimamu wawili Mussa Kadhim na Muhammad Jawad (a.s) unarejea nyuma kabla ya enzi ya Aali-Bueih. Serikali za Al-Buyeh, Saljukiyan, Al-Jalayr, Safavi na Qajar zilikarabati na kukamilisha Haram hii.

Katika zama za Safavi, kwa amri ya Shah Ismail Safavi, majengo ya Haram yaliharibiwa na jengo jipya likajengwa mahali pake, ambalo lilikuwa likijumuisha kuba na msikiti. Katika zama za Qajar, Farhad Mirza, ami yake Nasser al-Din Shah, alitekeleza hatua kubwa za ujenzi katika Haram hiyo, ambayo ilijumuisha kukarabati ujenzi wa ua.

Haram ya Kadhimayn kutokana na kuwa karibu na Mto Tigris, iliharibiwa na mafuriko katika vipindi tofauti. Pia iliharibiwa katika migogoro na mapigano baina ya Shia na Sunni mwaka 443 Hijiria na mashambulizi ya Wamongolia huko Baghdad.

Hadi katika kipindi cha Safavi, Haram ya Kadhimayn ilikuwa chini ya usimamizi wa Naqib. Sayyid Abdul Karim bin Ahmad Hilli alikuwa mmoja wa watu mashuhuri wa Naqib. Wakati wa zama za Safavi, usimamizi wa Haram hiyo ulikabidhiwa kwa Shaykh al-Islam.

Abdul Hamid Kalidar, Sheikh Abdul Nabi Kazemi na familia yake walikuwa wasiamiaji wa haram hiyo baada ya zama za Safavi. Sasa Haider Hasan al-Shammari ndiye msimamizi wa haram hiyo.

Watu maarufu kama vile Sheikh Mufid, Ibn Qulawayh, Khwaja Nasir al-Din Tusi na Muizz al-Dawla al-Daylami wamezikwa katika haram ya Kadhimayn. Vitabu vya Tarikh al-Imamaym al-Kadhimayn Warawdhatiha al-Sharifa kichoandikwa na Jafar al-Naqdi na Tarikh al-Mashad al-al-Kadhimi kilichoandikwa na Muhammad Hassan Al-Yasin ni miongoni mwa vitabu vilivyoandikwa kuhusu haram ya Kadhimayn.

Mahali na jina

Haram ya Kadhimayn

Haram ya Kadhimayn ni mahali walipozikwa Imam Kadhim (a.s) na Imam Jawad (a.s), Maimamu wa saba na wa tisa wa Waislamu wa madhehebu ya Shia. Imamu Kadhim (a.s.) alizikwa katika makaburi yaliyoanzishwa na Mansoor Abbasi mwaka 149 Hijiria na kujulikana kama makaburi ya Maquraishi. [24] Mtoto wa Mansoor Jafar Akbar alikuwa mtu wa kwanza kuzikwa katika makaburi haya mwaka 150 Hijiria. [25]

Eneo hili kutokana na kunasibishwa na Imamu Kadhim, iliitwa Mash’had al-Imam Musa bin Jafar, na Kadhimiyah. [26] Mnamo mwaka wa 220 AH, mwili wa Muhammad bin Ali (a.s), Imamu wa tisa wa Shia, ulizikwa karibu na kaburi la babu yake Musa bin Jafar. [27] kwa muktadha huo, lilijulikana kama Kadhimiyan (Kadhim Wawili). [28]

Haram ya Kadhimayn inajulikana pia kwa jina la Jawadayn (Jawad wawili). [29] Pia, kutokana na ukaribu wake na Bab al-Tabn, pia ilikuwa ikiitwa "Mashhad ya Bab al-Tabn." [30] Tabn ilikuwa mojawapo ya vitongoji vya Baghdad ambapo kulikuwa na kaburi la Abdullah mwana wa Ahmad bin Hambal. [31]

Historia fupi

Jengo la kwanza kwenye kaburi la Imamu Kadhim (a.s) lilikuwa ni kaburi lililojumuisha chumba na kuba. [32] Rasul Jafarian, mwanahistoria wa Kishia, ameuhusisha ujenzi wa jengo hilo na Ma’mun Abbasi. [33]

Kubomolewa na kundi la Mahambali Baghdad

Haram ya Kadhimayn iliharibiwa katika migogoro ya kidini ya Shia na Sunni. Mnamo mwaka wa 443 Hijiria kundi la Masunni likichochewa na Hanbal wa Baghdad lilishambulia Kadhimayn na kupora mali za haram hiyo sambamba na kuchoma moto dharih (eneo la ndani linalozunguka kaburi) na kuba lake. [37] Kwa mujibu wa Ibn Athir, mwanahistoria wa Kisunni katika karne ya 7, watu hao walikuwa na nia ya kufukua makaburi ya Maimamu wawili na kuhamisha miili yao kwenye kaburi la Ahmad bin Hambal, lakini kutokana na uharibifu walioufanya, hawakuweza kutambua makaburi ya Maimamu hao wawili. [38] Mnamo 450 AH, Arsalan Basasiri alijenga upya kaburi na kuweka sanduku jipya juu ya makaburi na akageuza kuba mbili kuwa kuba moja. [39]

Uhabribifu kutokana na kufurika mto Tigris

Mnamo mwaka wa 569 Hijiria, Haram ya Kadhimayn iliharibiwa na mafuriko ya Tigris. [42] Al-Nasir al-Dinullah Abbasi (622-575 AH), Khalifa wa wakati huo, alifanya matengenezo katika haram hiyo mnamo 575 Hijiria na akajenga vyuma kuzunguka uwanja wake. [43] Hatua yake hii imezingatiwa kuwa ukarabati na ujenzi wa mwisho katika enzi ya Utawala wa Abbas na mkubwa zaidi mwao. [44]

Katika mizozo ya kimadhehebu huko Kadhimayn mnamo 654 AH (miaka miwili kabla ya kuangukia Baghdad mikononi mwa Wamongolia), mali za haram pia ziliporwa. [45]

Katika zama za shambulio la Mongolia

Wamongolia waliiteka na kuidhibiti Baghdad mwaka wa 656 Hijiria. Katika tukio hili, majengo mengi huko Baghdad yaliharibiwa na Haram ya Kadhimayn ikachomwa moto. [48] Hata hivyo baada ya Emir Qaratay kuwasili Baghdad, alimchagua Imad al-Din Omar bin Muhammad Qazvini kama makamu wake. Emad al-Din aliamuru kujengwa upya kwa Msikiti wa Khalifa na Haram. [49] Ata-Malik al-Juwayni, mwandishi wa kitabu cha Jahangushayi Juwayni, alikuwa mtawala wa Baghdad katika miaka ya 657 hadi 681 AH katika kipindi cha Wamongolia. Imesemwa: Alifidia uharibifu uliosababishwa kwenye kaburi hilo na kuirejesha katika hali yake ya zamani. [50] Ibn Batuta, mtalii wa karne ya 8, wakati wa safari yake ya kwenda Baghdad mwaka wa 727 Hijiria, aliripoti kuhusu kaburi la mbao kwenye makaburi ya Maimamu wawili ambapo juu yake kulifunikwa kwa fedha. [51]

Katika zama za Jalayir

Wakati wa utawala wa Al-Jalayr, miji ya Baghdad na Kadhimayn iliathiriwa na maji kutokana na kufurika maji katika mto Tigris na hivyo Haram ya Kadhimayn ikaharibiwa. [52] Sultan Uwais Jalayri (757-777 AH) alitengeneza na kukarabati Haram hiyo. Kwa amri yake, kukawekwa masanduku mawili kwenye makaburi ya Maimamu hao wawili. [53] Vile vile alijenga makuba mawili na minara miwili na kupamba kaburi hilo kwa vigae ambavyo juu yake viliandikwa surah za Qur'an. [54] Mnamo mwaka wa 776 AH, kufurika Mto Tigris kulisababisha uharibifu wa haram hiyo, ambapo Sultan Uways alifanya tena ukarakati mara hii kwa juhudi za waziri wake na kukajengwa maeneo ya malazi kwa ajili ya wafanyaziara. [55]

Zama za Safavi

Wakati wa enzi ya Safavi, Haram ya Kadhimayn ilikaratatiwa. Shah Ismail aliiteka Baghdad mwaka wa 914 A.H. Baada ya muda fulani, aliamuru kubomoa majengo yote ya haram na badala yake kujenga jengo, ambalo lilijumuisha ukumbi, uwanja, msikiti kwa upande wa kaskazini na makuba mawili na minara miwili. [56] Kadhalika Shah Ismail alitengeneza masanduku mawili ya fedha kwa ajili ya makaburi mawili ya Maimamu hao wawili. [57]

Katika zama za Qajar

Katika zama za utawala wa Qajar, kwa msaada wa Agha Muhammad Khan Qajar (1212-1193 AH), kulitengenezwa makuba mawili, ukumbi wa kusini ambao ulikuwa na njia ya juu kwa kaburi la Kadhim (a.s.), ambayo yalifunika na sakafu ya Haram ilifunikwa kwa marumaru. [66] Mnamo mwaka wa 1221 AH, Fath Ali Shah Qajar (1250-1212 AH) alifanya upya kazi ya vioo, kuweka marumaru kwenye ukumbi na minara ya dhahabu katika Haram ya Kadhimayn. [67] Mnamo mwaka wa 1282 AH, Abdul Hussein Tehrani, aliyejulikana kama Sheikh Al-Iraqiyyin, wakili wa Mirza Khan Amir Kabir, alitoa theluthi moja ya urithi wa Amir Kabir, na kufanya matengenezo katika haram. [68]

Naser al-Din Shah (1313-1264 AH) alibadilisha dharih ya shaba mwaka 11283 Hijria na kuweka dharih ya zama za Safavi kama ambavyo alipamba kwa vioo na mapambano ya dhahabu. [69] Farhad Mirza ami yake Nasser al-Din Shah alijadidisha jengo la Haram. [70] Alinunua nyumba za karibu na Haram na kuongeza kwenye ua. Pia aliweka saa mbili, moja juu ya ukumbi wa ndani wa milango mitatu ya kusini na moja juu ya ukumbi wa ndani wa milango mitatu ya mashariki. [71]

Baada ya utawala wa Saddam

Wakati wa utawala wa Chama cha Baath cha Iraq, hakukuwa na shughuli za ujenzi katika haram ya Kadhimayn. Baada ya kuanguka kwa chama hiki, miradi mbalimbali ya maendeleo na upanuzi wa haram ilifanywa na Kamati ya Ukarabati wa maeneo Matakatifu. Ukarabati huo ulihusisha maeneo mbalimbali kama milango, kuba, minara, masanduku ya Maimamu hao wawili, ujenzi wa milango ya kuingilia, upachipakaji wa milango mipya, ushonaji wa kitu cha kufunika dharih, ukarakati na uhuishaji wa msikiti wa kihistoria wa Safavi jirani na Haram na kadhalika ni miongoni mwa kazi zilizofanywa na Kamati ya Ukarabati wa Maeneo Matakatifu. [72] Kazi zingine zilikuwa ni kubadilisha dharih na kujenga kumbi mbili za Sahib al-Zaman na Imamu Ali (as). [73]

Wasimamiaji na waendeshaji wa Haram

Katika karne ya 5 Hijria, Kadhimayn ilikuwa ni katika vitongoji vya Baghdad. Baada likawa eneo linalojitegemea na likawa likainishwa naqib (tasisii maalumu ya usimiamaiji wa masuala ya masharifu na maeneo ya waqf). Moja ya yaliyokuwa majukumu ya naqivban ni uendeshajki wa masuala ya Haram. [99] Katika kitabu Tarikh al-Mashhad al-Kadhimi, kumetajwa walezi na wasimamizi 27 au viongozi wa Kadhimayn ambapo miongioni mwao yumu Sayyid Abdul-Karim bin Ahmad Hilli (648-693) mmoja wa wanazuoni wa familia ya Tawus. Ibn Jafar al-Qayyim, Abu Talib Alavi, Ali bin Ali, anayejulikana kama Fakhir Alavi (aliyekufa karibu 569 AH) na Najm al-Din Ali bin Mousawi ambao ni wanazuoni wa karne ya 7 walikuwa miongoni mwa viongozi wa Kadhimayn. [100]

Waliozikwa katika Haram

Makala asili: Faharasa ya waliozikwa katika Haram ya Kadhimayn
Ramani ya Haram ya Kadhimayn ikionyesha makaburi ya Sheikh Mufid, Ibn Quwlawy na Khaaje Nasiru al-Din al-Tusi.

Watu wengi wamezikwa katika Haram ya Kadhimayn ambapo, miongoni mwao kuna shakhsia wasomi na watu wa kisiasa. [106] Katika kitabu Tarikh al-Mash’had al-Kadhimi, wametajwa zaidi ya watu thelathini ambao wamezikwa katika Haram ya Kadhimayn katika zama za utawala wa Bani Abbas. Miongoni mwao ni Abu Abdullah Muhammad Amin, Khalifa wa sita wa Bani Abbas, Zubaydah, mke wa Harun Abbasi, na Ibn Qulawayh (aliyefariki 368 AH), mwanachuoni wa Kishia. [107]

Baada ya kipindi cha Abbas, idadi ya watu waliozikwa kwenye kaburi hilo iliongezeka. [108] Baadhi ya waliozikwa katika Haram ya Kadhimayn ni:

Monografia

Kuhusiana na Haram ya Kadhimayn kumeandikwa vitabu na athari za kujitegemea. Miongoni mwa vitabu hivyo ni kitabu cha Tarikh al-Mash’had al-Kadhimi, mwandishi Muhammad Hassan al-Yassin (aliaga dunia 1372 Hijria. Mwandishi wa hiki anachambua historia ya Haram ya Kadhimayn katika zama za Bani Abbas, Aali-Bueih, Saljukian, Mongolia, Safavi, Othmania na Qajar. [116] Aidha sehemu ya kitabu hiki inabainisha hali ya Haram hiyo. [117]

Vitabu vya Tarikh al-Imamaym al-Kadhimayn Wa Rawdhatiha al-Sharifa kichoandikwa na Jafar al-Naqdi (aliaga dunia 1370 Hijria) [119] na Tarikh al-Mashad al-al-Kadhimi kilichoandikwa na Mustafa Javad. [120]


Rejea

Vyanzo

  • Āl Yāsīn, Muḥammad Ḥasan. Tārīkh al-Mashhad al-Kāẓimī. Al-amānat al-ʿĀmma li-l-ʿAtabt al-Kāẓimīyya al-Muqaddasa, 1435 AH/2014.
  • Amīnī Hirawī, Amīr Ṣadr al-Dīn Ibrāhīm. Futūḥāt-i Shāhī tārikh-i Ṣafawī az āghāz tā 920 Qamarī. Edited by Muḥammad Riḍā Nāṣirī. Tehran: Intishārāt-i Anjuman-i Āthār wa Mafākhir-i farhangī, 1383 Sh.
  • Anṣārī Qummī, Nāṣir al-Dīn. Kitābnāma-yi Imām Kāzim ʿalayhi al-salām. Kungira-yi Jahānī Imām Riḍā (a), 1370 Sh.
  • ʿAlawī, Aḥmad. Rāhnamā-yi musawwar-i safar-i ziyāratī-yi Irāq. Qom: Maʿrūf, 1389 Sh.
  • Būdāq Munshī Qazwīnī. Jawāhir al-Akhbār. Tehran: Mīrāth-i Maktūb, 1378 Sh.
  • Fayḍ Qummī, Mīrzā ʿAbbās. Tārīkh-i Kāẓimayn wa Baghdād. Qom: [n.p], 1327 Sh.
  • Ḥamawī, Yāqūt b. ʿAbd Allāh al-. Muʿjam al-buldān. Beirut: Dār al-Ṣādir, 1995.
  • Ḥusaynī Jalālī, Muḥammad Ḥusayn. Mazārāt Ahl al-Bayt wa tārīkhuhā. 3rd edition. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī, 1415 AH.
  • Ibn al-Athīr al-Jazarī, ʿAlī b. Abī l-Karam. Al-Kāmil fī l-tārīkh. Beirut: Dār Ṣādir, 1385 AH-1965.
  • Ibn ʿAnba, Aḥmad b. ʿAlī b. Ḥusayn b. ʿAlī. ʿUmdat al-ṭālib fi ansāb Āl Abī Ṭālib. Qom: Anṣārīyān, 1417 Ah.
  • Ibn Fuwaṭī, ʿAbd al-Razzāq b. Aḥmad. Al-ḥawādith al-jāmiʿa fī miʾat al-sābiʿa. Beirut: Dar al-Kutub al-ʿIlmiyya, [n.d].
  • Iʿtimād al-Salṭana, Muḥammad Ḥasan Khān. Rūznāma-yi khāṭirāt. Tehran: Intishārāt-i Amīr Kabīr, 1377 Sh.
  • Īdram, Ḥasan. Sīmā-yi Kāẓimayn. Tehran: Mashʿar, 1387 Sh.
  • Īzadī, Ḥusayn. Tārīkhcha-yi ḥaram-i Kāẓimayn.
  • Jaʿfarīyān, Rasūl. Aṭlas-i Shīʿa. Tehran: Intishārāt-i Sāzmān-i Jughrāfīyāyī-yi Nīrūhā-yi Musallaḥ, 1391 SH.
  • Khalīlī, Jaʿfar. Mawsūʿa al-ʿatabāt al-Muqaddasa. 2nd edition. Beirut: Muʾassisa al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1987.
  • Khaṭīb Baghdādī, Aḥmad b. ʿAlī. Tārīkh-i Baghdād. Edited by Musṭafā ʿAbd al-Qādir ʿAṭā. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1417 AH.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Irshād fī maʿrifat ḥujaj Allāh ʿalā l-ʿibād. Qom: Kungira-yi Shaykh al-Mufīd, 1413 AH.
  • Mīlānī, Muḥammad. Rāhnamā-yi ʿAtabāt ālīyāt. Mashhad: Nashr-i Muḥibb, 1377Sh.
  • Mūsawī Zanjānī, Sayyid Ibrāhīm. Jawlat fī al-Amākin al-Muqaddasa. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, [n.d].
  • Qazwīnī, Abu l-Ḥasan. Fawāʾid al-Ṣafawiyya. Tehran: Muʾassisa-yi Muṭāliʿat wa Taḥqīqāt-i Farhangī, 1367 Sh.
  • Qazwīnī Rāzī, ʿAbd al-Jalīl. Al-Naqḍ. Tehran: Anjuman-i Āthār-i Millī, 1358 Sh.
  • Qummī, Shaykh ʿAbbās. Muntahā l-āmāl. Edited by Naṣir Bāqirī Bīdhindī. 1st edition. Qom: Intishārāt-i Dalīl, 1379 Sh.
  • Shūshtarī, Nūr Allāh al-Ḥusaynī al-. Majālis al-muʾminīn. Tehran: Islāmiyya, 1377 Sh.