Hafs bin Suleiman Asadi
Jina Kamili | Hafs bin Suleiman bin Mughirah Asadi |
---|---|
Jina Maarufu | Hafs |
Lakabu/Kunia | Abu Omar |
Jamaa Maarufu | Asim bin Abi al-Najud Kufi |
Tarehe ya Kuzaliwa | 90 Hijria |
Mahali pa Makazi | Kufa, Baghdad na Makka |
Tarehe ya Kufa | 180 Hijria |
Mahala Alipozikwa | Makka |
Walimu | Asim bin Abi al-Najud Kufi |
Wanafunzi | Fadhl bin Yahya Anbari na Amru bin Sabaa |
Nyanja ya Kazi | Mfanyabiashara wa Nguo |
Shughuli | Msomeshaji wa Visomo vya Qur'ani |
Hafs bin Suleiman bin Mughirah Asadi (90-180 Hijria), «Muqri» (msomeshaji wa qiraa za Qur'ani) na mpokezi mashuhuri wa qiraa na kisomo cha Asim bin Abi al-Najud Kufi mmoja wa wasomaji wa viraa (visomo) saba mashuhuri vya Qur’ani. Hafs bin Suleiman bin Mughirah Asadi alijifunza elimu ya qiraa (usomaji) ya Qur'ani kutoka kwa Asim. Wengine wamemwona kuwa mtu mwenye ujuzi zaidi wa wakati wake katika elimu ya qiraa (usomaji Qur’ani). Hafs bin Suleiman bin Mughirah Asadi alieneza na kusambaza visomo vinavyohusishwa na Imam Ali bin Abi Talib (a.s) huko Kufa, Baghdad na Makka. Hivi sasa katika nchi nyingi za Kiislamu, Qur'ani inachapishwa na kusomwa kulingana na qiraa (usomaji) wa Hafs na Asim.
Sheikh Tusi amemtaja na kumuorodhesha Hafs bin Suleiman bin Mughirah Asadi miongoni mwa masahaba wa Imamu Ja’afar Swadiq (a.s). Licha ya kukubali nafasi na daraja yake katika elimu na taaluma ya qiraa, waandishi wa wasifu wamemchukulia Hafs kama mtu dhaifu ambaye hadithi zake hazipaswi kufanyiwa kazi (Matruk al-Hadith). Hata hivyo kwa mujibu wa baadhi ya tafiti, kudhoofika kwa Hafs bin Suleiman bin Mughirah Asadi katika riwaya kunatokana na kufanana kwa jina lake na wapokezi wengine.
Nafasi ya Hafs bin Suleiman bin Mughirah Asadi Katika Elimu ya Qiraa
Hafs bin Suleiman bin Mughira Asadi asili yake ni mtu wa Kufa, Iraq na mtoto wa mke wa Asim bin Abi al-Najud. Hafs ni mmoja wa wasomaji wa viraa (visomo) saba vya Qur’ani.[1] Hafs bin Suleiman bin Mughirah Asadi ametambuliwa kuwa mtu mwenye ujuzi zaidi wa wakati wake katika elimu ya qiraa.[2]
Hafs alieneza na kusambaza visomo vinavyohusishwa na Imam Ali bin Abi Talib (a.s) huko Kufa, Baghdad na Makka.[3] Aina yake ya usomaji (qiraa yake) inatambuliwa kuwa ni mutawatir (iliyoenea sana) na inakubaliwa na Waislamu wote.[4] Katika maeneo mengi ya ardhi za Kiislamu, Qur’ani inachapishwa na kusomwa kwa qiraa hiki.[5] Kwa mujibu wa ripoti nyingi za waandishi wa wasifu wa watu, Hafs bin Suleiman bin Mughirah Asadi alikuwa thiqa (muaminifu) katika qiraa na alikuwa makini mno katika kusajili qiraa ya Asim na alikuwa akisoma kwa umahiri mno.[6]
Hafs bin Suleiman bin Mughirah Asadi alizaliwa mwaka 90 Hijria.[7] Waandishi wa wasifu wa watu wanasema kuwa, lakabu yake ni Hufais na kuniya yake ni Abu Amr.[8] Imeelezwa kuwa, Hafs bin Suleiman bin Mughirah Asadi alikuwa muuza vitambaa.[9] Kuna nadharia na mitazanmo tofauti kuhusiana na siku wakati alioaga dunia.[10] Lakini baadhi ya watafiti wanasema kuwa, kwa mujibu wa nadharia na mtazamo sahihi na ripoti nyingi za waandishi wa historia, Hafs aliaga dunia mwaka 180 Hijria katika mji mtakatifu wa Makka.[11]
Ufundishaji na Uenezaji wa Qiraa ya Asim

Hafs bin Suleiman bin Mughirah Asadi ni mmoja wa wapokezi wawili mashuhuri wa Asim. Baadhi ya wasomi na wanazuoni wa elimu ya viraa vya Qur’ani wamefadhilisha na kumtanguliza yeye katika elimu ya Qiraa mbele ya Abu Bakr bin Ayyash mpokezi mwingine wa kisomo (qiraa) cha Asim[12] na wamemtambua kuwa msomi na mwenye elimu zaidi miongoni mwa wanafunzi wa Asim.[13]
Ibn Jazari mtaalumu wa hadithi wa Kishia amenukuu kutoka kwa Hafs bin Suleiman bin Mughirah Asadi kwamba, mwalimu wake Asim alimwambia, amemfundisha qiraa na kisomo kile kile ambacho alikichukua kutoka kwa Abdul-Rahman Sulami na Sulami alijifunza kama kilivyo kutoka kwa Imamu Ali bin Abi Talib (a.s).[14]
Kwa mujibu wa ripoti, Hafs bin Suleiman bin Mughirah Asadi alijifunza Qur’an kutoka kwa Asim tangu akiwa mdogo na alifunza Aya tano tano.[15] Baadhi wanasema kuwa, aina hii ya kujifunza Qur’ani ni sababu ya kuwa na ujuzi zaidi katika Qiraa ikilinganishwa na mbinu zingine.[16] Aliwafundisha kisomo cha Qur’ani watu huko Kufa. Kisha akaeleka Baghdad na kujishughulisha na kazi hiyo kwa muda fulani.[17] Katika zama za Harun Rashid pia alielekea Makka na kubakia huko hadi mwishoni mwa umri wake akifundisha watu Qur’ani na mafunzo ya usomaji Qur’ani.[18]
Wanafunzi
Hafs bin Suleiman bin Mughirah Asadi amelea na kufunza wanafunzi katika elimu ya qiraa ambao baadaye waliondokea kuwa wasomi na wanazuoni wa kutegemewa katika zama zao na katika maeneo walioishi. Baadhi ya wanafunzi haowalikuwa wakitoka katika miji mbalimbali na kwenda katika mji mtakatifu wa Makka ili waweze kujifunza elimu ya usomaji Qur’ani kutoka kwa Hafs bin Suleiman bin Mughirah Asadi. Miongoni mwao ni Fadhl bin Yahya Anbari.[19] Wanafunzi wake wengine ni Amru bin Sabah ambaye amekusanya qiraa yake katika kitabu alichoandika.[20] Baadhi ya wanafunzi wengine wa Hafs ni: Othman bin Yama, Ubayd bin Sabah, Hussein bin Muhammad Marwazi na Hubairah bin Hafs.[21] Kila mmoja miongoni mwa wanafunzi wa Hafs bin Suleiman bin Mughirah Asadi waliondokea kuwa wasomi wa kutegemewa katika elimu hiyo.
Nafasi ya Hadithi
Sheikh Tusi amelitaja jina la «Hafs bin Suleiman Abu Omar Asadi» katika orodha ya masahaba wa Imamu Ja’afar Swadiq (a.s).[22] Kadhalika katika kitabu cha Rijaal Tusi, kuna mtu aliyetajwa kwa jina la «Hafs bin Suleiman» katika orodha ya masahaba wa Imamu Mussa Kadhim (a.s).[23] Sayyid Abul-Qassim Khui kwa kuzingatia kwamba, katika kitabu cha Rijaal Barqi Hafs bin Suleiman bin Sadaqah ametajwa kuwa miongoni mwa masahaba wa Imamu Kadhim (a.s), hajatambua kuwa, watu hawa wawili ni mtu mmoja.[24]
Kwa mujibu wa ripoti ya Shahpasand, katika silsilah Sanad Ahadith (mlolongo wa mapokezi ya hadithi) jina lake wakati mwingine limekuja kwa sura ya Hafs bin Abi Daud na wakati mwingine kwa sura ya Abu Omar Bazzaz.[25]
Licha ya Hafs bin Suleiman Abu Omar Asadi kuwa makini zaidi na mwaminifu katika kusajili kisomo cha Asim,[26] lakini kuna kundi la watu limemtambulisha kuwa mtu dhaifu katika kunukuu hadithi na kwamba, hadithi zake hazipaswi kufanyiwa kazi (Matruk al-Hadith)[27] na hivyo halijamtambua kama mtu thiqa (muaminifu).[28] Ibn Hibban amemtambulisha Hafs kama mtu ambaye alikuwa akitia mkono katika sanadi (mapokezi) na Ibn Kharash amemtambulisha Hafs kuwa mtu mwongo na mwenye kufanya mambo ya bandia.[29]
Mkabala na wao, baadhi ya watafiti wanasema kuwa, sababu ya kutambuliwa Hafs bin Suleiman Abu Omar Asadi kuwa ni dhaifu ni kutokana na jina lake kufanana na watu wengine kadhaa akiwemo Hafs bin Suleiman bin Sadaqah.[30]
Rejea
- ↑ Ibn Jazari, Ghayaat al-Nihayah Fi Tabaqat al-Quraa, 1351 AH, juz. 1, uk. 254; Ibn Jazari, Al-Nashr Fi al-Qira’at al-Ashr, Dar al-Kutub al-Ilmiyyah, juz. 1, uk. 156; Maa’rifat, Al-Tamhid, 1428 AH, juz. 2, uk. 248.
- ↑ Ibn Jazari, Ghayaat al-Nihayah Fi Tabaqat al-Quraa, 1351 AH, juz. 1, uk. 254; Ibn Jazari, Al-Nashr Fi al-Qira’at al-Ashr, Dar al-Kutub al-Ilmiyyah, juz. 1, uk. 156; Maa’rifat, Al-Tamhid, 1428 AH, juz. 2, uk. 248.
- ↑ Ibn Jazari, Ghayaat al-Nihayah Fi Tabaqat al-Quraa, 1351 AH, juz. 1, uk. 254; Maa’rifat, Al-Tamhid Fi Ulumi al-Qur'ani, 1428 AH, juz. 2, uk. 248.
- ↑ Ma’rifat, Al-Tamhid, 1428 AH, juz. 2, uk. 246; Baz, Mabahith Fi Ilmu al-Qiraat Maa Usul Riwayat Hafs, 1425 AH, uk. 81.
- ↑ Habash, Al-Qiraat al-Mutawatir wa A'tharuha Fi Rasmi al-Qur'ani wa al-Ahkami al-Shar'iyyah, 1419 AH, uk. 66; Ismail Muhammad al-Mashhadani, al-Qimat al-Dilaliyat Liqiraat Asim Biriwayat Hafs, 1430 AH, uk. 26.
- ↑ Ma’rifat, Al-Tamhid Fi Ulumi al-Qur'ani, 1428 AH, juz. 2, uk. 248; Dhahabi, Mizan al-Itidal, 1382 AH, juz. 1, uk. 558; Khatib Baghdadi, Tarikh Baghdad, 1417 AH, juz. 9, uk. 64.
- ↑ Hamwi, Muujam al-Udabai, 1414 AH, juz. 3, uk. 1180; Ibn Jazari, Ghayyat al-Nahya Fi Tabaqat al-Quraa, 1429 AH, juz. 1, uk. 385; Ibn Jazari, Al-Nashir Fi al-Qiraat al-Ashar, Misr, juz. 1, uk. 156.
- ↑ Ibn al-Jazari, Ghayyat al-Nihayat Fi Tabaqat al-Quraa, 1429 AH, juz. 1, uk. 385; Ad-Dani, Kitab al-Taysir Fi al-Qira'at al-Sabaa, 1930, uk. 6.
- ↑ Ad-Dani, Kitab al-Taysir Fi al-Qiraat al-Sabaa, 1930, uk. 6; Ibn Hajar Asqalani, Kitab Tahdhib al-Tahdhib, 1325 AH, juz. 2, uk. 364.
- ↑ Shahpasand, «Pezhuhesh Darbareye Wadhiat Hafs ibn Suleiman Qari», uk. 124.
- ↑ Shahpasand, «Pezhuhesh Darbareye Wadhiat Hafs ibn Suleiman Qari», uk. 124; Ibn al-Jazari, Ghayyat al-Nahiyyah Fi Tabaqat al-Quraa, 1429 AH, juz. 1, uk. 386; Hamwi, Muujam al-Udabai, 1414 AH, juz. 3, uk. 1180.
- ↑ Ad-Dani, Kitab Al-Taysir Fi al-Qira’at al-Saba’a, 1930, uk. 6; Ibn Jazari, Ghayat al-Nihayah Fi Tabaqat al-Quraa, 1429 AH, juz. 1, uk. 386.
- ↑ Ibn Jazri, An-Nashr Fi al-Qira’at al-‘Ashr, Misri, Juz. 1, uk. 156.
- ↑ Ibn Jazri, Ghayaat al-Nihaya Fi Tabaqat al-Qur'ati, 1351 AH, juz. 1, uk. 348.
- ↑ Shahpasand, «Pezhuhesh Darbareye Waz-iyat Hafs ibn Suleiman Qari», uk. 127.
- ↑ Shahpasand, «Pezhuhesh Darbareye Waz-iyat Hafs ibn Suleiman Qari», uk. 127.
- ↑ Shahpasand, «Pezhuhesh Darbareye Waz-iyat Hafs ibn Suleiman Qari», uk. 128.
- ↑ Shahpasand, «Pezhuhesh Darbareye Waz-iyat Hafs ibn Suleiman Qari», uk. 128.
- ↑ Shahpasand, «Pezhuhesh Darbareye Waz-iyat Hafs ibn Suleiman Qari», uk. 128.
- ↑ Shahpasand, «Pezhuhesh Darbareye Waz-iyat Hafs ibn Suleiman Qari», uk. 128.
- ↑ Shahpasand, «Pezhuhesh Darbareye Waz-iyat Hafs ibn Suleiman Qari», uk. 128.
- ↑ Tusi, Rijal Tusi, 1427 AH, UK. 189.
- ↑ Tusi, Rijal Tusi, 1427 AH, UK. 335.
- ↑ KhUi, Mu'jam Rijal al-Hadith, 1372. Juz. 7, uk. 149.
- ↑ Shahpasand, «Pezhuhesh Darbareye Waz-iyat Hafs ibn Suleiman Qari», uk. 123.
- ↑ Tazama: Maarifat, Al-Tamhid Fi Ulum al-Qur'an, 1428 AH, juz. 2, uk. 248; Dhahabi, Mizan al-I'tdal, 1382 AH, juz. 1, uk. 558; Khatib Baghdadi, Tarikh Baghdad, 1417 AH, juz. 9, uk. 64.
- ↑ Tazama: Dhahabi, Mizan al-I'tidal, 1382 AH, juz. 1, uk. 558; Dhahabi, Maarifat al-Quraa al-Kibar, 1417 AH, juz. 1, uk. 84; Ibn al-Jazri, Ghayyat al-Nihayyah Fi al-Tabaqat al-Qura’a, 1351 AH, juz. 1, uk. 254; Ad-Dani, al-Taysir Fi Al-Qiraat al-Sabaa, 1404 AH, uk. 6; Ibn al-Badhish, Al-Iqnaa Fi al-Qiraat al-Sabaa, Dar al-Sahaba Litturath, uk. 34.
- ↑ Tazama: Khatib Baghdadi, Tarikh Baghdad, 1417 AH, juz. 9, uk. 64; Khui, Al-Bayan Fi Tafsiri al-Qur'an, Daru Zahra, uk. 131.
- ↑ Halabi, Al-Kashf al-Hathith Amman Zamaa Biwadhii al-Hadithi, 1984, uk. 154.
- ↑ Shahpasand, «Pezhuhesh Darbareye Waz-iyat Hafs ibn Suleiman Qari», uk. 122.
Vyanzo
- Ibn al-Bādhish, Aḥmad bin ʿAlī. Al-Iqnāʿ fī al-qirāʾāt al-sabʿ. Dār al-ṣaḥāba li-turāth, [n.p], [n.d].
- Ibn al-Jazarī, Muḥammad b. Muḥammad. Al-Nashr fī al-qirāʾāt al-ʿashr. Beirut: Dar al-Kutub al-'Ilmiyya, [n.d].
- Ibn al-Jazarī, Muḥammad b. Muḥammad. Ghāyat al-nihāya fī ṭabaqāt al-qurrā. Maktaba Ibn Taymīyya, [n.p], 1351 AH.
- Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, Aḥmad b. ʿAlī. Tahdhīb al-tahdhīb. Beirut: Dār al-ṣādir 1325 AH.
- Bāz, Muḥammad b. ʿAbbās. Mabāḥith fī ʿIlm al-qirāʾāt maʿ bayān usūl riwāyāt Ḥafṣ. Misri: Dār al-kalima, 1425 AH.
- Dānī, ʿUthmān b. Saʿīd al-. Al-Taysīr fī al-qirāʾāt al-sabʿ. Beirut: Dār al-Kitāb al-ʿArabī, 1404 AH.
- Dāraquṭnī, ʿAlī b. ʿUmar. Al-Kitāb al-ḍuʿafāʾ wa al-matrūkīn. Beirut: [n.p], 1406 AH.
- Dhahabī, Shams al-Dīn Muḥammad. Maʿrifat al-qurrāʾ al-Kibār ʿalā ṭabaqāt wa al-aʿsār. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1417 AH.
- Dhahabī, Muḥammad b. al-Aḥmad al-. Mīzān al-iʿtidāl. Beirut: Dār al-Maʿrifa li-ṭibaʿat wa al-Nashr, 1382 AH.
- Ḥabash, Muḥammad. Al-Qirāʾāt al-mutawātira wa atharuhā fī al-rasm al-qurʾānī wa al-aḥkām al-sharʿiyya. Damascus: Dār al-Fikr, 1419 AH.
- Ḥalabī, Burhān al-Dīn. Al-Kashf al-ḥathīth ʿamman rumiya bi waḍʿ al-ḥadīth. Mhariri: Ṣubḥī Samirāʾī. Baghdad: [n.p], 1984 CE.
- Ḥamawī, Shahāb al-Dīn Yāqūt b. ʿAbd Allāh al-. Muʿjam al-udabāʾ. Mhariri: Iḥsān ʿAbbās. Beirut: Dār al-Maghrib al-Islāmī, 1414 AH.
- Ismāʿīl Muḥammad al-Mashhadānī, Muḥammad. Al-Qīma al-dalālīya li qirāʾa ʿĀṣim bi riwāyat Ḥafṣ. Irāq: Markaz al-Buhūth wa al-dirāsāt al-Islāmiya, 1430 AH.
- Khaṭīb Baghdādī, Aḥmad b. ʿAlī. Tārīkh Baghdād. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1417 AH.
- Khoeī, Abū l-Qāsim. Al-Bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Dār al-Zahrāʾ, 1430 AH.
- Khoeī, Sayyid Abū l-Qāsim al-. Muʿjam rijāl al-ḥadīth. Qom: Muʾassisat al-Khuī al-Islāmīyya, 1372 Sh.
- Maʿrifat, Muḥammad Hādī. Al-Tamhīd fī ʿulūm al-Qurʾān. Qom: Muʾassisa-yi Farhangī Intishārātī-yi al-Tamhīd, 1428 AH.
- Shāhpasand, Ilāha. Pazhūheshī darbāra-yi waḍʿīyyat-i Ḥafṣ b. Sulaymān-i Qārī. Faṣlnāma-yi ʿUlūm-i Ḥadīth 21-1 (1395 Sh).
- Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥaasn al-. Al-Rijāl al-Ṭūsī. Mhariri: Muḥammad Ṣādiq Āl-i Baḥr al-ʿUlūm. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī affiliated to Jāmiʿa-yi Mudarrisīn-i Ḥawza-yi ʿIlmīyya-yi Qom, 1427 AH.