Hadithi al-Wasiyyah
- Tofautisha na Hadithi al-Wisayah
Hadith al-Wasiyyah; (Kiarabu: حديث الوصية) ni hadithi ambayo ndani yake kumezungumziwa Mahdi kumi na wawili ambao wanamrithi Imam Mahdi na kuwa viongozi baada yake. Hadithi hii imekuja katika kitabu cha al-Ghaibah cha Sheikh Tusi. Ahmad al-Hassan, kiongozi wa kundi la Ansar al-Mahdi akitegemea hadithi hiio, anajitambua kama mtoto wa Mahdi kwa kupitia kizazi cha Imam wa Zama na kujiita kuwa ni Mahdi wa kwanza kati ya Mahdi kumi na wawili. Wanazuoni wa Kishia hawakubalianiina nadharia na ufahamu huu wa Ahmad al-Hassan na wanaliona hilo kwamba, ni jambo linalopingana wazi na bayana kabisa na hadithi mashuhuri na sahihi za Mashia.
Baadhi ya watafiti na wahakiki wamefanya uchambuzi na tathmini kuhusiana na sanadi na mapokezi ya hadithi hii pamoja na muhtawa na yaliyomo ndani yake na kuitambua kuwa ni hadithi isiyokubalika; ambapo miongoni mwa waliyoyasema kuhusiana na hadithi hii ni kwamba, sanadi na mapokezi yake ni dhaifu. Kadhalika wamesema, hadithi hii inapinganana na hadithi zinazobainisha wazi idadi ya viongozi baada ya Bwana Mtume (s.a.w.w) kwamba ni kumi na mbili.
Kuitambulisha Hadithi na Yaliyomo Ndani Yake
Hadith al-Wasiyyah, ni hadithi ambayo Sheikh Tusi ameileta katika kitabu chake cha al-Ghaibah akinukuu kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w). [1] Katika hadithi ya al-Wasiyya (wasia) Mtume (s.a.w.w) alimhutubu Imam Ali (a.s) na kubainisha uwepo wa Maimamu kumi na mbili baada yake na majina yao na ndio wale Maimamu kumi na mbili wa Waislamu wa madhehebu ya Shia. Kisha akatoa habari ya uwepo wa Mahdi kumi na wawili ambao ni baada ya kifo cha Imam wa kumi na mbili ambao watakuwa warithi na viongozi. [2] Sehemu ya mwisho ya hadithi inaashiria maudhui hii kama ifuatavyo:
- «Baada yake [Imam wa kumi na mbili) watakuja Mahdi kumi na mbili. Wakati Imam wa kumi na mbili atakapoaga dunia atampa urithi wa uongozi wangu mwanawe ambaye ni mtu wa kwanza wa karibu. Yeye ana majina matatu: Jina lake jingine ni mithili ya jina la baba yangu nalo ni Abdallah na Ahmad; jina lake la tatu ni Mahdi ni wa kwanza katika waumini».[3]
Hadithi hii ni hoja muhimu ya Ahmad al-Hassan, kiongozi wa kundi la Ansar al-Mahdi kwa ajili ya kuthibitisha Mahdi kumi na wawili baada ya Imam wa kumi na mbili. [4] Yeye akitumia hadithi hii amedai kwamba, yeye ndiye Mahdi wa kwanza na mtoto wa Imam wa Zama (a.t.f.s). [5]
Awali ya yote ni kwamba, wanazuoni wa Kishia hawajaitambua hadithi hii kwamba, ina nguvu na mashiko madhubuti na pili hawakukubaliani na mafuhumu na maana hiyo. [6]
Hoja za Ahmad al-Hassan
Ahmad al-Hassan akitumia Hadith al-Wasiyya anasema kuwa, watakuja Mahdi kumi na wawili baada ya Imam Mahdi (a.t.f.s) na kwamba, yeye ni wa kwanza wao. [7] Fauka ya hayo, kwa kuzingatia ibara ya Ibnuh "yaani mwanawe" iliyopo katika hadithi anajitambulisha yeye kama mtoto wa Imam Maadi kwa kupitia kizazi cha Mahdi. [8] Kwa msingi huo, amedai kuwa na nafasi na mchango wake kabla ya kudhihiri na wakati wa utawala wa Imam wa kumi na mbili na baada ya hapo. [9]
Mtazamo wa Maulamaa wa Kishia
Maulamaa na wanazuoni wa Kishia wanasema kuwa, Hadith al-Wasiyya inapingana na hadithi mashuhuri na sahihi. Miongoni mwao ni Tabarsi (mfasiri wa Qur'ani wa karne ya tano Hijria), Irbili (mpokezi wa hadithi wa karne ya saba), Allama Muhammad Baqir Majlis na Hurr al-Amili (mpokezi wa hadithi wa karne ya 11). [10] Aidha Tabarsi na Irbili wamesema, hadithi hizi zinapingana na hadithi sahihi zinazosema kuwa, baada ya Imam Mahdi hakutakuweko tena na dola na utawala mwingine. [11]
Kasoro za Hadithi ya al-Wasiyyah
Baadhi ya kasoro zingine ambazo zimebainishwa na wahakiki na watafiti kuhusiana na hadithi hii ni:
- Hadithi hii ni Khabar Wahid (hadithi ambayo haijathibiti uhakika wake kuwa, ni kutoka kwa Maasumu) na kwamba, hadithi ya namna hii ni habari ya dhana. Kwa msingi huo haiwezekani kuitumia kuthibitisha itikadi. [12]
- Kwa mujibu wa hadithi hii warithi na viongozi wa baada ya Mtume ni 24, na hili ni jambo ambalo linapingana na hadithi sahihi zinazoeleza wazi kwamba, viongozi baada ya Mtume ni kumi na mbili. [13]
- Hadithi hii inapingana na hadithi ambazo zinamtaja na kumtambua Imam Mahdi kuwa ni hitimisho la mawasii. Kadhalika hadithi hii inakinzana na hadithi mbalimbali ambazo zinatoa habari ya raja' (kufufuka na kurejea duniani kundi la watu katika kipindi cha kudhihirii Imam Mahdi). [14]
- Hadithi hii sanadi na mapokezi yake ni dhaifu: Wapokezi wake ni dhaifu na hawambuliki. Kwa hivyo basi haina uwezo wa kupingana na hadithi ambazo ni sahihi. [15]
Rejea
Vyanzo