Dua ya Tisa ya Sahifa Sajjadiyya
Nakala ya Sahifa al-Sajjadiyah, katika hati ya Naskh ya Abdullah Yazdi, iliyoandikwa katika Sha'ban 1102 AH. | |
Mtoaji / Mwandishi | Imamu Sajjad (a.s) |
---|---|
Lugha | Kiarabu |
Msimulizi / Mpokezi | Mutawakkil ibn Harun |
Mada | Shauku ya kuomba msamaha kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu. |
Chanzo | Sahifa Sajjadiyah |
Tafsiri kwa Lugha ya | Kifarsi |
Dua ya Tisa ya Sahifa al-Sajjadiyya (Kiarabu: الدعاء التاسع من الصحيفة السجادية) ni miongoni mwa dua zilizorithiwa (zilizonukuliwa) kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s), nayo ni dua inajumuisha ndani yake maudhui ya kuomba istighfari na toba kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu. Katika dua hii, Imamu Sajjad (a.s) anamuomba Mola wake ampe msaada wa wa kufanya maamuzi sahihi katika mazingira ya magumu (njia panda), akibainisha kuwa nafsi ya binadamu (al-nafs al-ammara) ina kawaida ya kuelekea kwenye maovu na batili. Aidha, dua hii inagusia dhana ya udhaifu wa kimaumbile wa kila mwanadamu, na hivyo ni muhimu kwa mja kuomba wa Kiungu ili kuzuia mwelekeo na mvutiko wa nafsi (al-nafsu al-ammara) katika kutenda dhambi.
Mafunzo ya Dua ya Tisa
Mada kuu ya Dua ya Tisa ya Sahifatu Sajjadiyya yanahusiana na kuomba msaada kutoka kwa Mungu kwa ajili ya kupata wasaa na taufiki ya kuomba toba kutokana na dhambi mbali mbali, taufiki ya kutenda matendo mema, pamoja na taufiki ya kuacha maovu na matendo yasiyofaa. Mafundisho ya dua hii, yaliyotolewa na Imamu Sajjad (a.s) katika sehemu saba[1] kama yafuatavyo:
- Kuomba taufiki ya kutenda matendo yanayomridhisha Mwenye Ezi Mungu na kuacha yale yanayomghadhibisha, katika hali mbayo mwanadmu huwa katika njia panda kati ya kuchagua radhi au ghadhabu za Mwenye Ezi Mungu.
- Kuomba msaada wa kuchagua hasara ya dunia katika njia panda kati ya kuchagua hasara ya kidunia na hasara ya Akhera.
- Kuomba msaada wa Mungu kwa ajili ya kupata wasaa wa kuomba toba.
- Toka ya mja kutokana na dhambi zake, ni jambo linalopendwa na Mwenye Ezi Mungu, na kung'ang'ania dhambi ni jambo linalomchukiza Allah.
- Nafsi ya mwanadamu, katika njia panda ya haki na batili, kikawaida huwa na tabia ya huchagua batili.
- Msingi wa maumbile ya mwanadamu umejengwa juu ya udhaifu na ulegevu (wa kutokuwa na azma thabiti).
- Kuomba taufiki na himaya ya Kiungu.[2]
- Kuomba upofu wa macho ya moyo wa kutoyaona na kutotamani yale yasiyompendeza na Mwenye Ezi Mungu.[3]
- Kuomba Mungu kufunga njia na kukomea milango ya dhambi na maasi.
- Dua ya kupata taufiki ya kutenda mema na kuachana na mabaya.[4]
Tafsiri Fafanuzi za Dua ya Tisa
Maana na ujumbe wa Dua ya Tisa ya Sahifatu Sajjadiyya umechambuliwa na kufafanuliwa kwa kina kabisa na wanazuoni mbalimbali. Katika lugha ya Kiajemi, baadhi ya vitabu mashuhuri vinavyotoa ufafanuzi wa dua hii ni pamoja na: Diyare Asheghan kilichoandikwa na Hussein Ansarian.[5] Shuhud wa Shenakhte cha Muhammad Hassan Mamdouhi Kermanshahi.[6] Sharhe wa Tarjomeh Sahifeh Sajjadiyeh (Tafsiri Chambuzi ya Sahifa Sajjadiyya) kilichoandikwa naSayyid Ahmad Fakhri.[7]
Vilevile, kuna wachambuzi kadhaa wa Kiarabu walioichambua Dua hii kwa lugha ya Kiarabu. Miongoni mwa tafsiri chambuzi za Kiarabu ni: Riyad as-Salikin cha Sayyid Ali Khan Madani.[8] Fi Dhilal as-Sahifat as-Sajjadiyya kilichoandikwa na Muhammad Jawad Mughniyyah.[9] Riyadhu al-Arifin, cha Muhammad bin Muhammad Darabi.[10] Afaq ar-Ruh kilichoandikwa na Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah.[11] Zaidi ya hayo, kuna uchambuzi wa kina wa maneno yaliyotumika katika dua hii, yaani ufafanuzi wa kilugha, unaopatikana katika kitabu kiitwacho Ta'liqat 'ala as-Sahifat as-Sajjadiyya kilichoandikwa na Faidh Kashani.[12]
Matini ya Dua na Tafsiri Yake
وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ فِي الْاِشْتِيَاقِ إِلَي طَلَبِ الْمَغْفِرَةِ مِنْ اللهِ جَلَّ جَلَالُهُ
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ صَيِّرْنَا إِلَى مَحْبُوبِكَ مِنَ التَّوْبَةِ، و أَزِلْنَا عَنْ مَكْرُوهِكَ مِنَ الْإِصْرَارِ
اللَّهُمَّ وَ مَتَى وَقَفْنَا بَيْنَ نَقْصَيْنِ فِي دِينٍ أَوْ دُنْيَا، فَأَوْقِعِ النَّقْصَ بِأَسْرَعِهِمَا فَنَاءً، وَ اجْعَلِ التَّوْبَةَ فِي أَطْوَلِهِمَا بَقَاءً
وَ إِذَا هَمَمْنَا بِهَمَّيْنِ يُرْضِيكَ أَحَدُهُمَا عَنَّا، وَ يُسْخِطُكَ الآْخَرُ عَلَيْنَا، فَمِلْ بِنَا إِلَى مَا يُرْضِيكَ عَنَّا، وَ أَوْهِنْ قُوَّتَنَا عَمَّا يُسْخِطُكَ عَلَيْنَا
وَ لَا تُخَلِّ فِي ذَلِكَ بَيْنَ نُفُوسِنَا وَ اخْتِيَارِهَا، فَإِنَّهَا مُخْتَارَةٌ لِلْبَاطِلِ إِلَّا مَا وَفَّقْتَ، أَمَّارَةٌ بِالسُّوءِ إِلَّا مَا رَحِمْتَ
اللَّهُمَّ وَ إِنَّكَ مِنَ الضُّعْفِ خَلَقْتَنَا، وَ عَلَى الْوَهْنِ بَنَيْتَنَا، وَ مِنْ مَاءٍ مَهِينٍ ابْتَدَأْتَنَا، فَلَا حَوْلَ لَنَا إِلَّا بِقُوَّتِكَ، وَ لَا قُوَّةَ لَنَا إِلَّا بِعَوْنِكَ
اللَّهُمَّ فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اجْعَلْ هَمَسَاتِ قُلُوبِنَا، وَ حَرَكَاتِ أَعْضَائِنَا وَ لَمحَاتِ أَعْيُنِنَا، وَ لَهَجَاتِ أَلْسِنَتِنَا فِي مُوجِبَاتِ ثَوَابِكَ حَتَّى لَا تَفُوتَنَا حَسَنَةٌ نَسْتَحِقُّ بِهَا جَزَاءَكَ، وَ لَا تَبْقَى لَنَا سَيِّئةٌ نَسْتَوْجِبُ بِهَا عِقَابَكَ.
Miongoni mwa barua zake (a.s) kwenda kwa Shuraih bin al-Harith, hakimu wa mji wa Kufa.
Na miongoni mwa dua zake, amani iwe juu yake, ilikuwa ni katika kuonyesha shauku ya kuomba msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu Jalla Jalalu. Dua hii imekuja kwa ibara zisemazo:
Ewe Mwenyezi Mungu, mrehemu Muhammad na Aali zake, na utuelekeze kwenye toba unayoipenda, na utuondoe katika kung'ang'ania (dhambi) unazozikuchukia.
Ewe Mola wete, na pale tunapokabiliwa na kikwazo cha kuchagua kati ya hasara mbili, ya kidini au ya kidunia, basi elekeza (iandamize) hasara hiyo kwenye kipengele chenye (hasara za) muda mfupi zaidi katika kuangamia kwake, na uifanye toba (au mchakato wa kurejea Kwako) uwe katika kile chenye muda mrefu zaidi wa katika kudumu kwake.
Na (Ewe Mola Wetu) pale tunapoazimia kuchagua kati ya mikakati miwili ya kiutendaji (au mambo mawili), huku mojawapo likiwa ni lenye kupelekea ridhaa Yako kwetu sisi, na jengine likiwa ni lenye kusababisha ghadhabu Zako juu yetu, basi tupe mwelekeo (inclination) wa kuelekea kwenye kile kinachowafikiana na ridhaa Yako, na uzidhoofishe nguvu na uwezo wetu ili tusiwezw kutekeleza kile kinachosababisha ghadhabu Zako juu yetu.
Na (Ewe Mola Wetu) katika hilo (jambo/mambo hayo), usiziachie nafsi zetu kuwa na hiari ya maamuzi juu ya mambo hayo; kwani hakika nafsi huchagua (hupendezwa na yale ya) batili, isipokuwa zile Ulizozijaalia taufiki (kuongoka), na huamrisha sana maovu, isipokuwa zile Ulizozirehemu.
Ewe Mola wetu, na kwa hakika (ni yakini kwamba), Wewe umetuumba tukiwa na asili ya udhaifu, na umezijenga khulka zetu (maumbile yetu) juu ya msingi wa uhafifu (udhaifu), na umetuumba kutokana na majimaji yasiyo na hadhi. Basi hakuna nguvu yoyote ile yenye uwezo wa kubadilisha hali wala mamlaka yoyote (Ulimwenguni), na Wala sisis hatuna nguvu ya utendaji (wa jambo lolote lile) isipokuwa kwa msaada Wako.
Basi, Ewe Mola wetu Mlezi, tunakusihi umrehemu na umbariki Muhammad, pamoja na Aali zake watoharifu. Na tunakuomba uijaalie minong'ono ya siri iliyofichama ndani ya nyoyo zetu, miondoko na harakati zote za viungo vyetu, kila mtupo (mwangazo) wa macho yetu, na kila tamko liponyokalo kutoka kwenye ndimi zetu, (vyote kwa pamoja) viwe ni chemchemi (na chimbuko) la thawabu Zako zisizo na kikomo. Ili kusiwe na chembe hata moja ya wema itakayotuepuka ambayo kwayo tungetarajia kupata malipo Yako matukufu, na wala isisalie ndani yetu hata chembe ya dhambi ambayo kwayo tungeliwajibikiwa na mateso (adhabu) Yako.
Rejea
- ↑ Tarjume wa Sherh Duaye Nahom Sahife Sajjadiyeh, Tovuti ya Erfan.
- ↑ Matini ya Dua
- ↑ Matini ya Dua
- ↑ Ansarian, Diyar Ashiqan, 1372 S, juz. 5, uk. 21-74.
- ↑ Ansarian, Diyar Ashiqan, 1372 S, juz. 5, uk. 21-74.
- ↑ Mamduhi, Kitab Shuhud wa Shanakhte, 1388 S, juz. 1, uk. 451-464.
- ↑ Fihri, Sherh wa Tafsir Sahifa Sajjadiyah, 1388 S, juz. 1, uk. 499-515.
- ↑ Madani Shirazi, Riyadh al-Salikin, 1435 AH, juz. 2, uk. 401-423.
- ↑ Mughniyah, Fi Dhilal al-Sahifa, 1428 AH, uk. 153-159.
- ↑ Darabi, Riyadh al-Arifin, 1379 AH, uk. 133-136.
- ↑ Fadhlullah, Afaq al-Ruh, 1420 AH, juz. 1, uk. 261-273.
- ↑ Faidh Kashani, Taaliqat Ala al-Sahaifa al-Sajadiyeh, 1407 AH, uk. 34.
Vyanzo
- Ansarian, Hussein, Diyar Asheqan, Tafsir Jamii Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Payam Azadi, 1374.
- Khalji, Muhammad Taqi, Asrar al-Khamushan, Qom, Parto Khorshid, 1383 S.
- Darabi, Muhammad bin Muhammad, Riyadh al-Arifin Fi Sherh Sahifa Sajjadiyah, Muhaqiq Hussein Dargahi, Tehran, Nashr Us-wah, 1379.
- Fadhlullah, Sayyid Muhammad Hussein, A'faq al-Ruh, Beirut, Dar al-Malik, 1420 AH.
- Fahri, Sayyid Ahmad, Sherh wa Tarjume Sahifa Sajjadiyeh, Tehran, Us-wah, 1388 S.
- Faidh Kashani, Muhammad bin Murtaza, Taaliqat Ala Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Muasase al-Bahth wa al-Tahqiqat al-Thaqafiyah, 1407 AH.
- Mughniyeh, Muhammad Jawad, Fi Dhilal al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Qom, Dar al-Kitab al-Islami, 1428 AH.
- Madani Shirazi, Sayyid Ali Khan, Riyadh al-Salikiin Fi Sherh Sahifa Sayyid al-Sajidin, Qom, Muasase al-Nashr al-Islami, 1435 AH.
- Mamduhi Kermanshahi, Hassan, Shuhud wa Shenakhte: Tarjume wa Sherh Sahifa al-Sajjadiyyah, Ba Muqadime Ayatullah Jawadi Amuli, Qom, Bostan Kitab, 1385 S.