Nenda kwa yaliyomo

Dua ya Nane ya Sahifa Sajjadiyya

Kutoka wikishia
Dua ya Nane ya Sahifa Sajjadiyyah
Nakala ya Sahifa al-Sajjadiyah, katika hati ya Naskh ya Abdullah Yazdi, iliyoandikwa katika Sha'ban 1102 AH.
Nakala ya Sahifa al-Sajjadiyah, katika hati ya Naskh ya Abdullah Yazdi, iliyoandikwa katika Sha'ban 1102 AH.
Mtoaji / MwandishiImamu Sajjad (a.s)
LughaKiarabu
Msimulizi / MpokeziMutawakkil ibn Harun
MadaKutafuta kimbilio kwa Mungu kutokana na matendo mapotovu na maadili mabaya.
ChanzoSahifa Sajjadiyah
Tafsiri kwa Lugha yaKifarsi

Dua ya Nane ya Sahifa Sajjadiyya (Kiarabu: الدعاء الثامن من الصحيفة السجادية) ambayo ni miongoni mwa dua zilizopokewa (ma'athur) kutoka kwa Imamu Ali bin Hussein Zainul Abidin (a.s), ni dua maalumu iliyojikita katika kuomba hifadhi ya Mwenye Ezi Mungu dhidi ya kasoro (mbali mbali) za kimaadili na vitendo viovu. Imam Sajjad (a.s) katika maombi haya ameorodhesha maovu kadhaa ambayo yamo katika orodha ya dhambi za kimaadili. Miongoni mwa maovu hayo ni pamoja na; uchoyo (hirs), ghadhabu (khashm), taasubi (ushikiliaji wa itikadi kinyume na misingi ya kimantiki), kusehelea (kujilemaza kwa makusudi) katika kuendelea kutenda dhambi, pamoja na kudanganya watu, ambayo yote yametajwa kuwa ni vyanzo vya maangamizi ya mwanadamu.

Ufafanuzi na uchambuzi wa kina wa dua hii unapatikana katika kazi mbali mbali andishi zilizofanywa na wanazuoni mbali mbali.  Miongoni mwa kazi muhimu zilizokuja kufasiri dua hii ni pamoja na; Diyare Asheghan kazi andishi ya Hussein Ansarian iliyoandikwa kwa lugha ya Kiajemi, na Riyadh as-Salikin kazi andishi ya Sayyid Ali Khan Madani iliyoandikwa kwa lugha ya Kiarabu.

Mafunzo ya Dua ya Nane ya Sahifa Sajjadiyya

Imamu Sajjad (a.s), katika Dua ya Nane, anaomba hifadhi kwa Mungu dhidi ya hali zinazosumbua, kasoro za kimaadili na vitendo visivyokubalika kijamii na kidini. Dua hii inaorodhesha masuala arobaini na manne (44), kila moja likiwa ni kichocheo cha uharibifu wa kibinafsi na kijamii, na hatimaye maangamizi ya kiroho ya mwanadamu.[1] Mafundisho yanayotokana na dua hii,[2] yanajumuisha yafuatayo:

  • Mlipuko wa tamaa (al-hirs) na uchu (wa kupenda mambo ya kidunia)
  • Ukali au hasira (al-ghadhab)
  • Wivu au uchu wa utawala na husuda (al-hasad)
  • Udhaifu wa uvumilivu (al-sabr) na ukosefu wa subira
  • Uchache wa kuridhika au kuto tosheka (adamu al-qana'a)
  • Tabia mbaya (su'u al-khuluq)
  • Matamanio yaliyopindukia kiasi (al-shahwah)
  • Taasubi au ushabiki usio na msingi wa kimantiki (al-'asabiyyah)
  • Ufuataji wa matamanio ya nafsi (al-hawa)
  • Upinzani dhidi ya mwongozo wa kimaadili na kiroho (al-hidaya)
  • Hali ya kutojitambua au kughafilika kiakili na kiroho (al-ghaflah)
  • Kujiingiza katika mazingira magumu au hatarishi isivyo lazima
  • Ushikiliaji wa batili (al-batil) na kuipa kipaumbele juu ya haki (al-haqq)
  • Kushikilia au kuendeleza utendaji wa dhambi (israar fi al-ithm au al-ma'siyah)
  • Kudharau dhambi na kuonyesha kiburi (al-istikbar) dhidi ya utiifu wa kanuni za kisheria
  • Majivuno ya kitabaka ya matajiri na kudhalilisha wasiojiweza kiuchumi
  • Kupuuza wajibu na haki za walio (wanaohitaji kuwekwa) chini ya usimamizi au uhimili maalumu
  • Kutokuwa na shukrani kwa wema au usaidizi unaopokewa kutoka kwa wengine
  • Kumuunga mkono mkandamizaji (al-dhalim) na kumtelekeza mkandamizwaji (al-madhlum)
  • Kutafuta au kudai kitu fulani ambacho si haki yako kisheria
  • Kuzungumza au kutoa kauli fulani bila ya kuwa na welewa wala maarifa tosha juu ya unachokisema
  • Kuhadaa watu
  • Kujiona au kuwa na majivuno (al-'ujb) ya kitabia, kimatendo au kilugha
  • Kuwa na matarajio yaliyopitiliza mipaka
  • Uovu wa ndani kwa ndani au kuwa na nafsi chafu
  • Kudharau au kutojali makosa madogo madogo (al-saghair) yanayoweza kujilimbikiza
  • Ushawishi au hali ya kutawaliwa na nguvu hasi au nguvu za kishetani (al-Shaitan)
  • Kutotumia rasilimali ya wakati na fursa muhimu
  • Ukandamizaji wa kimamlaka au kiutawala
  • Uchafuzi wa kimaadili na kimwili kwa njia ya ubadhirifu (al-israf) na kutotumia riziki yako kiuangalifu na kwa kiwango kipaswacho
  • Lawama au dhihaka zitokazo kwa wapinzani au maadui
  • Hali ya utegemezi wa kwategemea wanadamu wenza
  • Janga la umaskini na kuishi katika hali ya dhiki ya kiuchumi na kijamii
  • Kifo cha ghafla bila maandalizi ya kiroho na kimatendo
  • Hasara, msiba mkuu binafsi au wa kijamii
  • Bahati mbaya na hatima mbaya
  • Kunyimwa malipo ya kiroho (al-thawab) na kuangukia katika adhabu[3]
  • Kuomba kinga dhidi ya vipengele vyote hivi hasi kupitia rehema za Mwenye Ezi Mungu.

Tafsiri na Maelezo Chambuzi ya Dua ya Nane

Kwa jicho la kitaaluma, Dua ya Nane ya Sahifa Sajjadiya inaakisi kina maarifa ya Kiroho ya Imamu Sajjad (a.s). Kundi kubwa la maandiko mengi chambuzi yalioandikwa kuhusiana na dua hii, yakijumuisha kazi kadhaa za wanazuoni mashuhuri katika lugha mbili ya Kifursi pamoja na Kiarabu. Miongoni mwa tafsiri za Kifursi ni pamoja na; Diare Ashiqaan cha Hussein Ansarian,[4] Shuhud wa Shenakht cha Muhammad Hassan Mamdouhi Kermanshahi,[5] na Sherhe wa Tarjume Sahife Sajjadiyye cha Sayyid Ahmad Fahri.[6] Kwa upande wa pili, pia kuna vitabu kadhaa vya lugha ya Kiarabu vilivyofasiri dua hii. Miongoni mwa vitabu hivi ni pamoja na; Riadhu al-Salihin cha Sayyid Ali Khan Madani,[7] Fi Dhilali Sahifati Al-Sajjadiyya cha Muhammad Jawad Mughniyyah,[8] Riadhu Al-Arifina cha Muhammad ibn Muhammad Darabi,[9] na Aafaqu Al-Ruuh cha Sayyid Muhammad Hussein Fadlallah.[10] Zaidi ya hayo, hata maana za msamiati mahsusi wa maneno ya dua hii, pia nao umewekwa kwenya darubini ya uchambuzi. Jukumu la kazi hii maridadi lilikamilika kupitia mkono wa mwanazuoni ajulikanaye kwa jina la Faidhu Kashani, aliyefafanua msamiatia wa dua hii katika kitabu kiitwacho Taaliiqaat Alaa Al-Sahifati Al-Sajjadiyya.[11]

Matini ya Dua na Tafsiri Yake

Maandishi
Maandishi na Tafsiri
Tafsiri

وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ فِي الاِسْتِعَاذَةِ مِنَ الْمَكَارِهِ وَ سَيِّيَ الْأَخْلَاقِ وَ مَذَامِّ الْأَفْعَالِ

اللَّهُمَّ إِنيِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَيَجَانِ الْحِرْصِ، وَ سَوْرَةِ الْغَضَبِ، وَ غَلَبَةِ الْحَسَدِ، وَ ضَعْفِ الصَّبْرِ، وَ قِلَّةِ الْقَنَاعَةِ، وَ شَكَاسَةِ الْخُلْقِ، وَ إِلْحَاحِ الشَّهْوَةِ، وَ مَلَكَةِ الْحَمِيَّةِ

وَ مُتَابَعَةِ الْهَوَى، وَ مُخَالَفَةِ الْهُدَى، وَ سِنَةِ الْغَفْلَةِ، وَ تَعَاطِي الْكُلْفَةِ، وَ إِيثَارِ الْبَاطِلِ عَلَى الْحَقِّ، وَ الْإِصْرَارِ عَلَى الْمَأْثَمِ، وَ اسْتِصْغَارِ الْمَعْصِيَةِ، وَ اسْتِكْبَارِ الطَّاعَةِ.

وَ مُبَاهَاةِ الْمُكْثِرِينَ، وَ الْإِزْرَاءِ بِالْمُقِلِّينَ، وَ سُوءِ الْوِلَايَةِ لِمَنْ تَحْتَ أَيْدِينَا، وَ تَرْكِ الشُّكْرِ لِمَنِ اصْطَنَعَ الْعَارِفَةَ عِنْدَنَا. أَوْ أَنْ نَعْضُدَ ظَالِماً، أَوْ نَخْذُلَ مَلْهُوفاً، أَوْ نَرُومَ مَا لَيْسَ لَنَا بِحَقٍّ، أَوْ نَقُولَ فِي الْعِلْمِ بِغَيْرِ عِلْمٍ

وَ نَعُوذُ بِكَ أَنْ نَنْطَوِيَ عَلَى غِشِّ أَحَدٍ، وَ أَنْ نُعْجِبَ بِأَعْمَالِنَا، وَ نَمُدَّ فِي آمَالِنَا

وَ نَعُوذُ بِكَ مِنْ سُوءِ السَّرِيرَةِ، وَ احْتِقَارِ الصَّغِيرَةِ، وَ أَنْ يَسْتَحْوِذَ عَلَيْنَا الشَّيْطَانُ، أَوْ يَنْكُبَنَا الزَّمَانُ، أَوْ يَتَهَضَّمَنَا السُّلْطَانُ.

وَ نَعُوذُ بِكَ مِنْ تَنَاوُلِ الْإِسْرَافِ، وَ مِنْ فِقْدَانِ الْكَفَافِ.

وَ نَعُوذُ بِكَ مِنْ شَمَاتَةِ الْأَعْدَاءِ، وَ مِنَ الْفَقْرِ إِلَى الْأَكْفَاءِ، وَ مِنْ مَعِيشَةٍ فِي شِدَّةٍ، وَ مِيتَةٍ عَلَى غَيْرِ عُدَّةٍ.

وَ نَعُوذُ بِكَ مِنَ الْحَسْرَةِ الْعُظْمَى، وَ الْمُصِيبَةِ الْكُبْرَى، وَ أَشْقَى الشَّقَاءِ، وَ سُوءِ الْمَآبِ، وَ حِرْمَانِ الثَّوَابِ، وَ حُلُولِ الْعِقَابِ.

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ أَعِذْنِي مِنْ كُلِّ ذَلِكَ بِرَحْمَتِكَ وَ جَمِيعَ الْمُؤْمِنِينَ وَ الْمُؤْمِنَاتِ، يَا أَرْحَمَ الرَّاحِمِينَ.

وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ فِي الاِسْتِعَاذَةِ مِنَ الْمَكَارِهِ وَ سَيِّيَ الْأَخْلَاقِ وَ مَذَامِّ الْأَفْعَالِ
Na ilikuwa miongoni mwa dua zake, Rehema na Amani ziwe juu yake, alizokuwa akiomba, ni ile dua aliomba katika kutafuta hifadhi (isti'adha) dhidi ya; mambo yenye kuudhi (yanayochukiza), akhlaki potofu (tabia mbovu), na yale yenye kupelekea lawama. Matini ya dua hii imekuja kama ifuatavyo;
اللَّهُمَّ إِنيِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَيَجَانِ الْحِرْصِ، وَ سَوْرَةِ الْغَضَبِ، وَ غَلَبَةِ الْحَسَدِ، وَ ضَعْفِ الصَّبْرِ، وَ قِلَّةِ الْقَنَاعَةِ، وَ شَكَاسَةِ الْخُلْقِ، وَ إِلْحَاحِ الشَّهْوَةِ، وَ مَلَكَةِ الْحَمِيَّةِ
Ewe Allah, hakika mimi (nimekimbilia Kwako Wewe) nikitafuta hifadhi Kwako dhidi ya mchemko wa tamaa, na mfuriko wa ghadhabu (hasira), na kupinduliwa (kutawaliwa) na hishia za hasadi (husuda), na udhaifu wa kuto kuwa na subira, na uchache wa kukinai, na ukakasi wa akhlaki (tabia mbaya), na shinikizo la shahawa (matamanio), na kumilikiwa na hamasa kali ya kijahiliya (ushabiki usiakubaliana na matiki).
وَ مُتَابَعَةِ الْهَوَى، وَ مُخَالَفَةِ الْهُدَى، وَ سِنَةِ الْغَفْلَةِ، وَ تَعَاطِي الْكُلْفَةِ، وَ إِيثَارِ الْبَاطِلِ عَلَى الْحَقِّ، وَ الْإِصْرَارِ عَلَى الْمَأْثَمِ، وَ اسْتِصْغَارِ الْمَعْصِيَةِ، وَ اسْتِكْبَارِ الطَّاعَةِ.
Na (nakuomba unihifadhi na hisia ya) kufuata matamanio ya nafsi (yangu), na kukhalifu (kupinga na) uongofu (hidaya yako), na kusinzia kwa usingizia wa kughafilika, na kujikalifisha na yasiyo ya lazima, na kupendelea (kuitangulia) batili mbele ya haki, na kusehelea (kujilemaza) katika dhambi, na kudharau (kudogosha) dhambi, na kuitukuza taa (kujiona kuwa ni mtiifu bora)
وَ مُبَاهَاةِ الْمُكْثِرِينَ، وَ الْإِزْرَاءِ بِالْمُقِلِّينَ، وَ سُوءِ الْوِلَايَةِ لِمَنْ تَحْتَ أَيْدِينَا، وَ تَرْكِ الشُّكْرِ لِمَنِ اصْطَنَعَ الْعَارِفَةَ عِنْدَنَا. أَوْ أَنْ نَعْضُدَ ظَالِماً، أَوْ نَخْذُلَ مَلْهُوفاً، أَوْ نَرُومَ مَا لَيْسَ لَنَا بِحَقٍّ، أَوْ نَقُولَ فِي الْعِلْمِ بِغَيْرِ عِلْمٍ
Na naomba (unihaifadhi na) majivuno ya wenye mali (wenye kipato), na kuwadharau wasiojiweza (wenye kipatoa kidogo), na uongozi mbaya wa kuto wajali wale walio chini ya himaya yetu, na kutokuwa na shukurani juu ya yule aliyetutendea wema. Au kumsaidia dhalimu na kumdhalilisha (kumtelekeza) mwenye dhiki anayelilia msaada, au kutafuta (na kutamani) kisicho haki yetu, au kusema jambo tusilokuwa na elimu nalo.
وَ نَعُوذُ بِكَ أَنْ نَنْطَوِيَ عَلَى غِشِّ أَحَدٍ، وَ أَنْ نُعْجِبَ بِأَعْمَالِنَا، وَ نَمُدَّ فِي آمَالِنَا
Na tunatafuta hifadhi Kwako ili tusikunje (nyoyone mwetu) ughushi kwa ajili ya kumhadaa mtu yeyote yule, na tusipendezwe na amali zetu (kwa kudhani kuwa tumetenda amali kubwa au amali bora), na tusijirefushia matarajio (hali ya kwamba hakuna uhakika wa kuyafikia).
وَ نَعُوذُ بِكَ مِنْ سُوءِ السَّرِيرَةِ، وَ احْتِقَارِ الصَّغِيرَةِ، وَ أَنْ يَسْتَحْوِذَ عَلَيْنَا الشَّيْطَانُ، أَوْ يَنْكُبَنَا الزَّمَانُ، أَوْ يَتَهَضَّمَنَا السُّلْطَانُ.
Na tunatafuta hifadhi Kwako dhidi ya uovu wa nia za siri (dhamira mbaya nyoyoni), na kudharau (kupuuza) dhambi ndogo, na (tunakuomba utuhifadhi na) kutawaliwa na Shetani, au kuangamizwa na masaibu (matukio) ya zama, au kukandamizwa na kunyanyaswa na Sultani (kiongozi au mtawala).
وَ نَعُوذُ بِكَ مِنْ تَنَاوُلِ الْإِسْرَافِ، وَ مِنْ فِقْدَانِ الْكَفَافِ.
Na tunajilina na hifadhi Yako dhidi ya kujihusisha na israfu (au ufisadi na ubadhirifu mbali mbali), na (tunaomba hifadhi Yako) dhidi ya mapungufu ya riziki (ili tuwe na kiwango tosha cha kujikimu).
وَ نَعُوذُ بِكَ مِنْ شَمَاتَةِ الْأَعْدَاءِ، وَ مِنَ الْفَقْرِ إِلَى الْأَكْفَاءِ، وَ مِنْ مَعِيشَةٍ فِي شِدَّةٍ، وَ مِيتَةٍ عَلَى غَيْرِ عُدَّةٍ.
Na tunakimbilia hifadhi Yako dhidi ya udhalili wa kudhahikiwa na kechekwa na wapinzani wetu, tunakimbilia hifadhi Yako ili tutoke kwenye ufakiri wetu na tuelekee kwenye hali ya kujitosheleza, na tunakimbilia hifadhi Yako dhidi ya unyonge wa uhitaji, na tunakimbilia hifadhi Yako dhidi ya kuikabili safari ya mwisho (mauti) bila ya kuwa na maandalizi ya kiroho na matendo mema kwa ajili ya maisha yajayo.
وَ نَعُوذُ بِكَ مِنَ الْحَسْرَةِ الْعُظْمَى، وَ الْمُصِيبَةِ الْكُبْرَى، وَ أَشْقَى الشَّقَاءِ، وَ سُوءِ الْمَآبِ، وَ حِرْمَانِ الثَّوَابِ، وَ حُلُولِ الْعِقَابِ.
Na tunakimbilia himaya Yako dhidi ya majuto yasiyo na kifani, na tunakimbilia hifadhi Yako dhidi ya janga kuu (linalovunja na kuangamiza matumaini), na tunakimbilia hifadhi Yako dhidi ya kuingia kwenye kipeo cha udhalili na uovu usiokuwa na kifani, na tunakimbilia hifadhi Yako dhidi ya hatima mbaya kabisa (katika makao ya milele), na tunakimbilia hifadhi Yako dhidi ya kunyimwa baraka na malipo ya wema yanayotarajiwa, na tunakimbilia hifadhi Yako dhidi ya kukumbwa na adhabu isiyoepukika.
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ أَعِذْنِي مِنْ كُلِّ ذَلِكَ بِرَحْمَتِكَ وَ جَمِيعَ الْمُؤْمِنِينَ وَ الْمُؤْمِنَاتِ، يَا أَرْحَمَ الرَّاحِمِينَ.
Ewe Mola wetu, mshushie baraka Zako Muhammad, (kielelezo na kitovu cha ukamilifu), pamoja na Aali zake watoharifu. Na (ninakuomba) kwa rehema zako zisizo na kifani, uniepushe mimi na jamii nzima ya waliojisalimisha Kwako kwa imani thabiti – wake kwa waume – dhidi ya athari zote mbaya (za yale nilizozitaja katika dua hii). Ewe Chanzo cha Rehema zote, (Ambaye rehema Zako zinakifunika na kutanda juu ya kila kitu).

Na ilikuwa miongoni mwa dua zake, Rehema na Amani ziwe juu yake, alizokuwa akiomba, ni ile dua aliomba katika kutafuta hifadhi (isti'adha) dhidi ya; mambo yenye kuudhi (yanayochukiza), akhlaki potofu (tabia mbovu), na yale yenye kupelekea lawama. Matini ya dua hii imekuja kama ifuatavyo;

Ewe Allah, hakika mimi (nimekimbilia Kwako Wewe) nikitafuta hifadhi Kwako dhidi ya mchemko wa tamaa, na mfuriko wa ghadhabu (hasira), na kupinduliwa (kutawaliwa) na hishia za hasadi (husuda), na udhaifu wa kuto kuwa na subira, na uchache wa kukinai, na ukakasi wa akhlaki (tabia mbaya), na shinikizo la shahawa (matamanio), na kumilikiwa na hamasa kali ya kijahiliya (ushabiki usiakubaliana na matiki).

Na (nakuomba unihifadhi na hisia ya) kufuata matamanio ya nafsi (yangu), na kukhalifu (kupinga na) uongofu (hidaya yako), na kusinzia kwa usingizia wa kughafilika, na kujikalifisha na yasiyo ya lazima, na kupendelea (kuitangulia) batili mbele ya haki, na kusehelea (kujilemaza) katika dhambi, na kudharau (kudogosha) dhambi, na kuitukuza taa (kujiona kuwa ni mtiifu bora)

Na naomba (unihaifadhi na) majivuno ya wenye mali (wenye kipato), na kuwadharau wasiojiweza (wenye kipatoa kidogo), na uongozi mbaya wa kuto wajali wale walio chini ya himaya yetu, na kutokuwa na shukurani juu ya yule aliyetutendea wema. Au kumsaidia dhalimu na kumdhalilisha (kumtelekeza) mwenye dhiki anayelilia msaada, au kutafuta (na kutamani) kisicho haki yetu, au kusema jambo tusilokuwa na elimu nalo.

Na tunatafuta hifadhi Kwako ili tusikunje (nyoyone mwetu) ughushi kwa ajili ya kumhadaa mtu yeyote yule, na tusipendezwe na amali zetu (kwa kudhani kuwa tumetenda amali kubwa au amali bora), na tusijirefushia matarajio (hali ya kwamba hakuna uhakika wa kuyafikia).

Na tunatafuta hifadhi Kwako dhidi ya uovu wa nia za siri (dhamira mbaya nyoyoni), na kudharau (kupuuza) dhambi ndogo, na (tunakuomba utuhifadhi na) kutawaliwa na Shetani, au kuangamizwa na masaibu (matukio) ya zama, au kukandamizwa na kunyanyaswa na Sultani (kiongozi au mtawala).

Na tunajilina na hifadhi Yako dhidi ya kujihusisha na israfu (au ufisadi na ubadhirifu mbali mbali), na (tunaomba hifadhi Yako) dhidi ya mapungufu ya riziki (ili tuwe na kiwango tosha cha kujikimu).

Na tunakimbilia hifadhi Yako dhidi ya udhalili wa kudhahikiwa na kechekwa na wapinzani wetu, tunakimbilia hifadhi Yako ili tutoke kwenye ufakiri wetu na tuelekee kwenye hali ya kujitosheleza, na tunakimbilia hifadhi Yako dhidi ya unyonge wa uhitaji, na tunakimbilia hifadhi Yako dhidi ya kuikabili safari ya mwisho (mauti) bila ya kuwa na maandalizi ya kiroho na matendo mema kwa ajili ya maisha yajayo.

Na tunakimbilia himaya Yako dhidi ya majuto yasiyo na kifani, na tunakimbilia hifadhi Yako dhidi ya janga kuu (linalovunja na kuangamiza matumaini), na tunakimbilia hifadhi Yako dhidi ya kuingia kwenye kipeo cha udhalili na uovu usiokuwa na kifani, na tunakimbilia hifadhi Yako dhidi ya hatima mbaya kabisa (katika makao ya milele), na tunakimbilia hifadhi Yako dhidi ya kunyimwa baraka na malipo ya wema yanayotarajiwa, na tunakimbilia hifadhi Yako dhidi ya kukumbwa na adhabu isiyoepukika.

Ewe Mola wetu, mshushie baraka Zako Muhammad, (kielelezo na kitovu cha ukamilifu), pamoja na Aali zake watoharifu. Na (ninakuomba) kwa rehema zako zisizo na kifani, uniepushe mimi na jamii nzima ya waliojisalimisha Kwako kwa imani thabiti – wake kwa waume – dhidi ya athari zote mbaya (za yale nilizozitaja katika dua hii). Ewe Chanzo cha Rehema zote, (Ambaye rehema Zako zinakifunika na kutanda juu ya kila kitu).

🌞
🔄

Rejea

  1. Ansarian, Diyar Ashiqan, 1371 S, juz. 4, uk. 225.
  2. Tarjume wa Sherh Duaye Hashtom Sahife Sajjadiyeh, Tovuti ya Erfan.
  3. Ansarian, Diyar Ashiqan, 1371 S, juz. 4, uk. 225-419; Mamduhi, Shuhud va Shanakhte, 1385 S, juz. 1, uk. 435-450.
  4. Ansarian, Diyar Ashiqan, 1371 S, juz. 4, uk. 225-419.
  5. Mamduhi, Kitab Shuhud va Shanakhte, 1388 S, juz. 1, uk. 435-450
  6. Fihri, Sherh waTafsir Sahifa Sajjadiyah, 1388 S, juz. 1, uk. 415-495.
  7. Madani Shirazi, Riadh al-Salikin, 1435 AH, juz. 2, uk. 325-400.
  8. Mughniyyah, Fi Dhilal al-Sahifa, 1428 AH, uk. 141-153.
  9. Darabi, Riadh al-Arifin, 1379, uk. 127-132.
  10. Fadhlullah, Afaq al-Ruh, 1420 AH, Juz. 1, uk. 259-199.
  11. Faidh Kashani, Taaliqat Ala al-Sahaifa al-Sajadiyeh, 1407 AH, uk. 33-34.

Vyanzo

  • Ansarian, Hussein, Diyar Asheqan, Tafsir Jamii Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Payam Azadi, 1374.
  • Khalji, Muhammad Taqi, Asrar al-Khamushan, Qom, Parto Khorshid, 1383 S.
  • Darabi, Muhammad bin Muhammad, Riyadh al-Arifin Fi Sherh Sahifa Sajjadiyah, Muhaqiq Hussein Dargahi, Tehran, Nashr Us-wah, 1379.
  • Fadhlullah, Sayyid Muhammad Hussein, A'faq al-Ruh, Beirut, Dar al-Malik, 1420 AH.
  • Fahri, Sayyid Ahmad, Sherh wa Tarjume Sahifa Sajjadiyeh, Tehran, Us-wah, 1388 S.
  • Faidh Kashani, Muhammad bin Murtaza, Taaliqat Ala Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Muasase al-Bahth wa al-Tahqiqat al-Thaqafiyah, 1407 AH.
  • Mughniyeh, Muhammad Jawad, Fi Dhilal al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Qom, Dar al-Kitab al-Islami, 1428 AH.
  • Madani Shirazi, Sayyid Ali Khan, Riyadh al-Salikiin Fi Sherh Sahifa Sayyid al-Sajidin, Qom, Muasase al-Nashr al-Islami, 1435 AH.
  • Mamduhi Kermanshahi, Hassan, Shuhud wa Shenakhte: Tarjume wa Sherh Sahifa al-Sajjadiyyah, Ba Muqadime Ayatullah Jawadi Amuli, Qom, Bostan Kitab, 1385 S.