Nenda kwa yaliyomo

Dua ya Kumi na Sita ya Sahifa al-Sajjadiyya

Kutoka wikishia

Dua ya Kumi na Sita ya Sahifa al-Sajjadiyya: ni moja kati ya dua zilizorithiwa (zilizopokewa) kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s), nayo ni dua aliyokuwa akiisoma wakati wa kuomba msamaha na maghufira kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu. Katika dua hii, Imamu Sajjad (a.s) anakisi dhana ya Mungu na sifa Zake, huku akitandaza mapungufu yake mbele ya Mola Wake. Pia ndani yake anatuonesha jinsi ya mtando wa rehema za Mwenye Ezi Mungu ulivyotanda hadi kupindukia ghadhabu Zake, na jinsi Mola wetu alivyo mvumilivu katika kuwahukumu (kuwapindua) waja Wake (kutokana na uasi wao). Katika dua hii, ujinga unatajwa kuwa ndio chanzo cha dhambi, na kwamba njia ya kuepukana na adhabu ya Mungu, ni kumtegemea Yeye pamoja na kutafuta ukaribu Naye (kumuomba msaada) kutumia sifa zake tukufu.

Tafsiri Chambuzi za Dua ya Kuna Sita

Kuna waandishi kadhaa wa lugha mbali mbali mbali waliozamia katika kazi ya uchambuzi na tafsiri ya Dua ya kumi na sita ya Sahifa Sajjadiya. Miongoni mwa tafsiri chambuzi zilizoandikwa kwa lugha ya Kiajemi, ni pamoja na; Diyar-e Ashegan kazi ya Hussein Ansarian, na Shuhud va Shenakht, ambayo kazi ya Hassan Mamduhi Kermanshahi. Aidha, kuna tafsiri ufafanuzi kadhaa zilizoandikwa kwa lugha ya Kiarabu, moja wapo inapatikana katika kitabu kiitacho Riyadhu as-Salikin, kilichoandikwa na Sayyid Ali Khan Madani.

Maudhui makuu ya Dua ya Kumi na Sita ilioko katika Sahifa Sajjadiyya, ni dua ya kuomba msamaha wa dhambi. Ili kujikaribisha na rehema za Mwenye Ezi Mungu, kwanza kabisa Imam Sajjad (a.s), anaanza kwa kuuanika hadharani ule ufukara wa asili n awa kimaumbile alionao mja dhaifu wa Mwenye Ezi Mungu, kisha anaendelea kutaja sifa kamilifu za Mola wake, ikiwemo; sifa ya utoshelevu kamili, fadhila, pamoja na ukarimu wa Mwenye Ezi Mungu. [1] Mafundisho ya Dua ya Kumi na Sita yaliyomo katika ibara 34 za dua hii, [2] yamefafanuliwa katika vipengele vifuatavyo:

·       Tumaini la wenye dhambi katika kutaraji rehema za Mwenye Ezi Mungu.

·       Dhana ya kuomba msaada wa Mungu kwa kurejelea sifa za Kiungu zinazoendana na hali ya uhitaji wa mja ulivyo.

·       Kimbilio la wanyonge la kumkimbilia Mola wao lanalopata msukumo wako kutoka katika hali ya kukumbuka hisani za Mola wao.

·       Kilio cha watenda dhambi kinachojiri kutokana na hofu ya kuogopa adhabu ya Mwenye Ezi Mungu.

·       Mtando wa Rehema na Elimu ya Mwenye Ezi Mungu uliokijumuishi kila kitu katika mtando wako, na kuenea kwenye kila chembe ya uwepo.

·       Fungu na hisa ya viumbe kutoka katika mgao wa neema za Mwenye Ezi Mungu.

·       Utanguliaji wa Rehema za Mwenye Ezi Mungu uliozitangulia Ghadhabu Yake.

·       Utangulji wa ukarimu (utoaji) wa Mwenye Ezi Mungu uliotangulia unyimaji Wake.

·       Kutowepo kwa matarajio ya Mungu ya kutoka malipo na ujira kutokana na neema alizowaneemesha viumbe Wake.

·       Uzingatiaji wa uadilifu katika adhabu za Mwenye Ezi Mungu.

·       Amri ya Mola ya kuomba dua, na wajibu wetu wa kunyenyekea amri zake.

·      Kuungama na kukiri dhambi (kama ni ufunguo wa msamaha).

·      Ujinga ndio chanzo kikuu cha ukiukaji wa amri za Mungu.

·      Kuomba kwa unyeyekevu na kudhihirisha ufukara wa mja mbele ya Mwenye Ezi Mungu.

·      Mwitikio wa Mwenye Ezi Mungu uliojaa upendo na huruma, kufuatia maombi, vilio, na utegemezi wa waja Wake. [3]

·      Muamala wa Mungu kwa waja wanaotubia (wanaorejea Kwake).

·      Kumwogopa Mungu (Uchaji Mungu).

·      Hisia ya kuhisi aibu mbele ya Mungu kutokana na rimbikizo la dhambi lilimwelemea mwanadamu.

·      Athari za dhambi katika kukosa wasaa na fursa ya kuomba dua.

·      Kukiri sifa ya Mwenye Ezi Mungu ya "As-Sattar" (Mwenye kuficha aibu).

·      Kuthamini neema ya Kiungu ya kuepushwa na fedheha mbele ya umma.

·      Kuelemea kwa nafsi ya mwanadamu kwenye mambo ya shari na ujinga wake juu wake wa kuto elewe lenye kheri naye.

·      Yakini kamili juu ya uwepo wa Janna na Jahannam kama hatima ya mwisho ya huko Akhera. [4]

·      Kuungama dhambi mbele ya Mungu.

·      Pepo ndio mwisho wa kuitikia wito wa Mwenye Ezi Mungu, na moto ndio hatima yaa kuitikia mwito wa Shetani.

·      Sifa ya Mungu ya "Al-Halim" (Mpole/Mvumilivu) katika kuwawajibisha (kuwaadhibu) waja Wake.

·      Kutathmini uzito wa maasi mbele ya mizani ya Kiungu.

·      Msamaha wa dhambi unatokana na fadhila za Mwenye Ezi Mungu, na wala si kwa ustahili walionao waja Wake.

·      Ombi la kuomba kuonjeshwa halawa (ladha) ya maghufira ya Mwenye Ezi Mungu.

·      Ombi la kuomba kuepushwa na adhabu na Moto kupitia msamaha na rehema za Mungu. [5]

·      Tohara na usafi unaopatina kupitia toba.

·      Uhuru kamili wa Mwenye Ezi Mungu wa kufanya alitakalo. [6]

Tafsiri Chambuzi za Dua ya Kumi na Sita

Maana na dhana zilizomo katika Dua ya Kumi na Sita ya Sahifa Sajjadiyya zimekuchunguzwa n kuchambuliwa na kwa lugha ya Kiajemi kupitia wanazuoni mbali mbali waliofasiri dua zilizomo kitabu kitabu Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa kazi hizo ni pamoja na; Diyare Asheqan (Ulimwengu wa Mapenzi), kitabu kilichoandikwa na Hussein Ansarian, [7] Shuhud wa Shenakht (Utambuzi na Welewa wa Kimaarifa), ambacho ni kitabu kilichoandikwa na Mohammad Hassan Mamduhi Kermanshahi, [8] na Sharhe wa Tarjome-ye Sahife Sajjadiyye (Ufafanuzi na Tafasiri ya Sahifa Sajjadiyya), kazi andishi ya Sayyid Ahmad Fahri. [9]

Pia kuna waandishi wengine kadhaa waliandika chambuzi zao kwa lugha ya Kiarabu, miongoni mwao ni kama vile; Sayyid Ali Khan Madani aliyechambua dua hii kitabu chake kiitwacho Riyadh as-Salikin (Bustani za Wasafiri wa Kiroho), [10] Fi dhilali as-Sahifat as-Sajjadiyya (Katika Kivuli cha Sahifa Sajjadiyya), kitabu kilichoandikwa na Mohammad Jawad Mughniyya, [11] Riyadhu al-Arifin (Bustani za Wajuzi wa Haki), cha Muhammad bin Muhammad Darabi, [12] na Afaqi ar-Ruh (Upeo wa Roho) cha Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah. [13] Zaidi ya hayo, pia msimiati misingi wa lugha ya dua hii zimechambuliwa na kurikodiwa ndani ya kitabu vitabu maalumu. Miongoni mwa vitabu hivyo ni pamoja na; Ta'liqat 'ala as-Sahifat as-Sajjadiyya (Maelezo juu ya Sahifa Sajjadiyya), kazi iliofanywa na Faidhu Kashani [14] na cha pili ni kitabu kiitwacho Sharh as-Sahifat as-Sajjadiyya (Ufafanuzi wa Sahifa Sajjadiyya), kilichoandikwa na Izzuddin al-Jazairi. [15]

Matini ya Dua ya Kumi na Sita Pamoja na Tafsiri Yake

وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ إِذَا اسْتَقَالَ مِنْ ذُنُوبِهِ ، أَوْ تَضَرَّعَ فِي طَلَبِ الْعَفْوِ عَنْ عُيُوبِهِ

Na inayofuata ni miongoni mwa dua zake (rehema na amani ziwe juu yake), alizokuwa akiomba kwa ajili kujilinda na kujitakasa na dhambi, huku akimkabili Mola wake kwa unyenyekevu mkubwa katika kutafuta msamaha kutoka na dosari zake.

اللَّهُمَّ يَا مَنْ بِرَحْمَتِهِ يَسْتَغيثُ الْمُذْنِبُونَ

Ewe Mola wangu, ambaye huruma zake (Zako) ndio tegemeo (pekee) kinachotegemewa na waasi katika kuomba wokovu.

وَ يَا مَنْ إِلَى ذِكْرِ إِحْسَانِهِ يَفْزَعُ الْمُضْطَرُّونَ

Na Ewe ambaye, tafakuri ya kutafakari katika hisani yake isiyo na mipaka, ndiyo ngao iyayotegemewa (inayokimbiliwa) na wenye shida.

وَ يَا مَنْ لِخِيفَتِهِ يَنْتَحِبُ الْخَاطِئُونَ

Na Ewe ambaye wakosaji huomboleza (hulia) kutoka na waoga wa kumkhofu Yeye.

يَا أُنْسَ كُلِّ مُسْتَوْحِشٍ غَرِيبٍ ، وَ يَا فَرَجَ كُلِّ مَكْرُوبٍ كَئِيبٍ ، وَ يَا غَوْثَ كُلِّ مَخْذُولٍ فَرِيدٍ ، وَ يَا عَضُدَ كُلِّ مُحْتَاجٍ طَرِيدٍ

Ewe Liwazo la kila mkiwa aliye tengwa, na Ewe Ukombozi wa kila mwenye dhiki na sononeko, na Ewe Nusura ya kila aliyedhalilishwa na kusalia pekee, na Ewe Nguzo ya kila fukara (mhitaji) aliyetengwa.

أَنْتَ الَّذِي وَسِعْتَ كُلَّ شَيْ‌ءٍ رَحْمَةً وَ عِلْماً

Wewe ndiye Yule ambaye ujuzi na rehema zake zimeenea na kutanda juu ya kila kitu.

وَ أَنْتَ الَّذِي جَعَلْتَ لِكُلِّ مَخْلُوقٍ فِي نِعَمِكَ سَهْماً

Nawe ndiwe uliyemjaalia kila mmoja (kati ya viumbe Wako) fungu lake miongoni mwa fadhila zako.

وَ أَنْتَ الَّذِي عَفْوُهُ أَعْلَى مِنْ عِقَابِهِ

Na Wewe ndiye ambaye huruma Zake zinashinda (zimepindukia) adhabu Yake.

وَ أَنْتَ الَّذِي تَسْعَى رَحْمَتُهُ أَمَامَ غَضَبِهِ .

Na ni Wewe ambaye daima rehema Zake ziko mbele ya ghadhabu Zake.

وَ أَنْتَ الَّذِي عَطَاؤُهُ أَكْثَرُ مِنْ مَنْعِهِ .

Na Wewe ndiye ambaye utoaji wako umepitiliza (umepindukia) unyimaji wako.

وَ أَنْتَ الَّذِي اتَّسَعَ الْخَلَائِقُ كُلُّهُمْ فِي وُسْعِهِ .

Na ni Wewe ambaye ukunjufu Wako umevienea na kuvijumuisha viumbe vyote (ndani yake).

وَ أَنْتَ الَّذِي لَا يَرْغَبُ فِي جَزَاءِ مَنْ أَعْطَاهُ .

Nawe Ndiwe ambaye huna shauku ya kupokea fidia (ujira) kutoka kwa yule uliyemruzuku.

وَ أَنْتَ الَّذِي لَا يُفْرِطُ فِي عِقَابِ مَنْ عَصَاهُ .

Nawe ndiwe Ambaye hapitilizi mipaka (kuliko inavyostahili) katika kumuadhabu yule aliyemkosea.

وَ أَنَا ، يَا إِلَهِي ، عَبْدُكَ الَّذِي أَمَرْتَهُ بِالدُّعَاءِ فَقَالَ لَبَّيْكَ وَ سَعْدَيْكَ ، هَا أَنَا ذَا ، يَا رَبِّ ، مَطْرُوحٌ بَيْنَ يَدَيْكَ .

Ee Mungu wangu, Nami, ni yule mja Wako uliyemwamuru kuomba dua (kukuomba Wewe), naye akajibu kwa kusema: 'Naitika wito Wako na nina furaha ya kuwa chini ya amri Yako.' Basi mimi ndiye huyu hapa, Ewe Bwana wangu, nimejitupa (nimejisalimisha) mikononi Mwako.

أَنَا الَّذِي أَوْقَرَتِ الْخَطَايَا ظَهْرَهُ ، وَ أَنَا الَّذِي أَفْنَتِ الذُّنُوبُ عُمُرَهُ ، وَ أَنَا الَّذِي بِجَهْلِهِ عَصَاكَ ، وَ لَمْ تَكُنْ أَهْلًا مِنْهُ لِذَاكَ .

Nami ndiye yule mja ambaye dhambi zimeulemea mgongo wake, nami ndiye ambaye madhambi yake yamefutilia mbali (yameukunja) umri wake, na mimi ndiye aliyekuasi kwa ujinga wake, na wala Wewe hukustahili (hukustahiki) kufanyiwa hivyo.

هَلْ أَنْتَ ، يَا إِلَهِي ، رَاحِمٌ مَنْ دَعَاكَ فَأُبْلِغَ فِي الدُّعَاءِ أَمْ أَنْتَ غَافِرٌ لِمَنْ بَكَاكَ فَأُسْرِعَ فِي الْبُكاء أَمْ أَنْتَ مُتَجَاوِزٌ عَمَّنْ عَفَّرَ لَكَ وَجْهَهُ تَذَلُّلًا أَمْ أَنْتَ مُغْنٍ مَنْ شَكَا اِلَيْكَ ، فَقْرَهُ تَوَكُّلاً

Je, Ee Mungu wangu, hivi Wewe ni Mrehemevu wa yule anayekuomba na akafikia ukomo (upeo) wa dua (katika maombi yake)? Au unamsamehe yule anayekulilia na akaharakisha katika kulia (kilio chake)? Au unayafumbia macho (unaachana na) makosa ya yule anayekuinamia huku uso wake ukiwa juu ya ardhi kwa unyenyekevu wake? Au unamtajirisha yule anayekuelezea ufakiri wake huku akikukutegemea Wewe?

إِلَهِي لَا تُخَيِّبْ مَنْ لَا يَجِدُ مُعْطِياً غَيْرَكَ ، وَ لَا تَخْذُلْ مَنْ لَا يَسْتَغْنِي عَنْكَ بِأَحَدٍ دُونَكَ .

Ewe Mola wangu, usivunje matumaini ya yule asiyekuwa na mneneemeshaji ghairi Yako, na usimdhalilishe (usimnyime) yule asiyepata usiyejitosheleza (asiyetegemea) kwa mwengine yeyote asiyekuwa Wewe.

إِلَهِي فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ ، وَ لَا تُعْرِضْ عَنِّي وَ قَدْ أَقْبَلْتُ عَلَيْكَ ، وَ لَا تَحْرِمْنِي وَ قَدْ رَغِبْتُ إِلَيْكَ ، وَ لَا تَجْبَهْنِي بِالرَّدِّ وَ قَدِ انْتَصَبْتُ بَيْنَ يَدَيْكَ .

Ee Mola wangu, basi mshushie rehema Muhammad na Aali zake. Na wala Usinigezie uso, hali nikiwa nimekuelekea Wewe; na wala usininyime, hali shauku yangu ikiwa iko Kwako, na usinikabili kwa kunikataa (mkatao) huku mimi nikiwa nimejiegemeza mikononi Mwako.

أَنْتَ الَّذِي وَصَفْتَ نَفْسَكَ بِالرَّحْمَةِ ، فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ ، وَ ارْحَمْنِي ، وَ أَنْتَ الَّذِي سَمَّيْتَ نَفْسَكَ بِالْعَفْوِ فَاعْفِ عَنّي

Wewe ndiye uliyejitambulisha kwa Sifa ya Urehemevu, hivyo basi, mbariki Muhammad na Aali zake, na unihurumie. Na Wewe ndiye uliyejiita Msamehevu, bais (nakuomba) unisamehe.

قَدْ تَرَى يَا إِلَهِي ، فَيْضَ دَمْعِي مِنْ خِيفَتِكَ ، وَ وَجِيبَ قَلْبِي مِنْ خَشْيَتِكَ ، وَ انْتِقَاضَ جَوَارِحِي مِنْ هَيْبَتِكَ

Ee Mola wangu, bila shaka unaona mafuriko ya machozi yangu kwa ajili ya hofu Yako, na mapigo ya moyo wangu kutokana (uchaji) kukucha Wewe, na mtetemeko wa viungo vyangu kutokana na (tishio la) haiba Yako.

كُلُّ ذَلِكَ حَيَاءٌ مِنْكَ لِسُوءِ عَمَلِي ، وَ لِذَاكَ خَمَدَ صَوْتِي عَنِ الْجَأْرِ إِلَيْكَ ، وَ كَلَّ لِسَانِي عَنْ مُنَاجَاتِكَ .

Yote hayo yanatokana na haya niliyonayo kutokana na ubaya wa matendo yangu; na ndiyo maana sauti yangu imedhoofika na kuzimika katika (hali hii ya) kukulalamikia, na ulimi wangu umekuwa butu katika kukuomba (katika kufikisha lalama zake Kwako).

يَا إِلَهِي فَلَكَ الْحَمْدُ فَكَمْ مِنْ عَائِبَةٍ سَتَرْتَهَا عَلَيَّ فَلَمْ تَفْضَحْنِي ، وَ كَمْ مِنْ ذَنْبٍ غَطَّيْتَهُ عَلَيَّ فَلَمْ تَشْهَرْنِي ، وَ كَمْ مِنْ شَائِبَةٍ أَلْمَمْتُ بِهَا فَلَمْ تَهْتِكْ عَنِّي سِتْرَهَا ، وَ لَمْ تُقَلِّدْنِي مَكْرُوهَ شَنَارِهَا ، وَ لَمْ تُبْدِ سَوْءَاتِهَا لِمَنْ يَلْتَمِسُ مَعَايِبِي مِنْ جِيرَتِي ، وَ حَسَدَةِ نِعْمَتِكَ عِنْدِي

Ee Mola wangu, sifa (zote adhimu) ni Zako! Jee ni aibu ngapi ulizonisitiri nazo bila ya hukunifedhehi; na ni hatia ngapi ulizozifinikia (ulizozifunika) na wala hukunitangazia nazo; na ni madoa mangapi niliyojichafua nayo, nawe hukufunua pazia (lako) nililositirika nalo kutokana na madoa hayo, wala hukunivika mkufu wa fedheha zake (shingoni mwangu), wala hukudhihirisha maovu yake mbele ya wenye kunapekua mapungufu yangu miongoni mwa jirani zangu, na mbele ya wale mahasidi wa fadhila Zako kwangu.

فَمَنْ أَجْهَلُ مِنِّي ، يَا إِلَهِي ، بِرُشْدِهِ وَ مَنْ أَغْفَلُ مِنِّي عَنْ حَظِّهِ وَ مَنْ أَبْعَدُ مِنِّي مِنِ اسْتِصْلَاحِ نَفْسِهِ حِينَ أُنْفِقُ مَا أَجْرَيْتَ عَلَيَّ مِنْ رِزْقِكَ فِيما نَهَيْتَنِي عَنْهُ مِنْ مَعْصِيَتِكَ وَ مَنْ أَبْعَدُ غَوْراً فِي الْبَاطِلِ ، وَ أَشَدُّ إِقْدَاماً عَلَي السُّوءِ مِنِّي حِينَ أَقِفُ بَيْنَ دَعْوَتِكَ وَ دَعْوَةِ الشَّيْطَانِ فَأَتَّبِعُ دَعْوَتَهُ عَلَي غَيْرِ عَميً مِنِّي فِي مَعْرِفَةٍ بِهِ وَ لَا نِسْيَانٍ مِنْ حِفْظِي لَهُ

Ewe Mola wangu! Ni nani basi aliye mjinga zaidi yangu, katika kuelewa mwelekeo wa ustawi wake (maslahi ya nafsi yake)? Na ni nani aliyeghafilika zaidi kuliko mimi juu ya hadhi na fungu lake? Na ni nani aliyejitenga zaidi na jitihada za kuijenga nafsi yake, pale ninapozitumia neema zako zote katika kutenda yale uliyonikataza miongoni mmwa maasi ya kukuasi Wewe? Na ni nani aliyetumbukia kwa kina kikubwa zaidi katika batili, na (ni nani) mwenye kasi zaidi katika kuukumbatia uovu kuliko mimi, pale ninaposimama katika njia panda kati ya mwito wako na mwito wa Shetani, kisha nikafuata mwito wake, (jambao ambalo) sikulifanya kwa kutokana na ujinga wangu wa kutomjua, na wala si kwa usahau wa akili (kumbukumbu) yangu kuhudisiana naye.

وَ أَنَا حِينَئِذٍ مُوقِنٌ بِأَنَّ مُنْتَهَى دَعْوَتِكَ إِلَى الْجَنَّةِ ، وَ مُنْتَهَى دَعْوَتِهِ إِلَي النَّارِ .

Na wakati wote huo (huyafanya yote haya) hali nikiwa na welewa kamili (nikiwa na yakini) kwamba; hatima ya kufuata mwongozo wako ni (kuingia) Peponi, na hatima ya kufuata mwongozo wake (yeye) ni (kuingia) motoni.

سُبْحَانَكَ مَا أَعْجَبَ مَا أَشْهَدُ بِهِ عَلَى نَفْسِي ، وَ أُعَدِّدُهُ مِنْ مَكْتُومِ أَمْرِي

Umetukuka Ee Mungu! Ni cha ajabu mno kile ninachokishuhudia juu ya nafsi yangu, na kukihesabu (na kile ninacho kihisabu) miongoni mwa (yale) mambo yangu yaliyositirika (yaliofichika).

وَ أَعْجَبُ مِنْ ذَلِكَ أَنَاتُكَ عَنِّي ، وَ إِبْطَاؤُكَ عَنْ مُعَاجَلَتِي ، وَ لَيْسَ ذَلِكَ مِنْ كَرَمِي عَلَيْكَ ، بَلْ تَأَنِّياً مِنْكَ لِي ، وَ تَفَضُّلًا مِنْكَ عَلَيَّ لِأَنْ أَرْتَدِعَ عَنْ مَعْصِيَتِكَ الْمُسْخِطَةِ ، وَ أُقْلِعَ عَنْ سَيِّئَاتِيَ الْمخْلِقَةِ ، وَ لِأَنَّ عَفْوَكَ عَنِّي أَحَبُّ إِلَيْكَ مِنْ عُقُوبَتِي

Na cha kustaajabisha zaidi ya hili ni ustahamilivu wako kwangu kunihusu, na uchelewesha wako wa kuto niharakishia adhabu (kwa kunipatiliza). Na hili halitokani na thamani yangu yoyote ile mbele Yako, bali ni kutokana na subra zako juu yangu, na ni hisani zako kwangu. Lengo ni kunipa fursa, ili niachane na ukaidi unaosababisha ghadhabu Zako, na niitenge nafsi yangu na maovu yanayochakaza utu (yenye kuhilikisha). Hii ni kwa sababu, msamaha Wako kwangu ndiyo jambo linalopendeza zaidi mbele yako kuliko adhabu Yako dhidi yangu.

بَلْ أَنَا ، يَا إِلَهِي ، أَكْثَرُ ذُنُوباً ، وَ أَقْبَحُ آثَاراً ، وَ أَشْنَعُ أَفْعَالًا ، وَ أَشَدُّ فِي الْبَاطِلِ تَهَوُّراً ، وَ أَضْعَفُ عِنْدَ طَاعَتِكَ تَيَقُّظاً ، وَ أَقَلُّ لِوَعِيدِكَ انْتِبَاهاً وَ ارْتِقَاباً مِنْ أَنْ أُحْصِيَ لَكَ عُيُوبِي ، أَوْ أَقْدِرَ عَلَي ذِكْرِ ذُنُوبِي .

Ewe Mola wangu! Bali mimi, ni mwingi zaidi wa dhambi, na ni mwenye athari mbaya zaidi, pia ndiye mwenye matendo mabaya zaidi. Ni mwenye upapiaji mkubwa zaidi wa kuzama kwenye batili, (mimi ndiye) dhaifu zaidi wa kuamka kwa ajili ya taa yako, na mchache zaidi wa kuzingatia thahadhari zako (maonyo yako ya adhabu) na kujitathmini (kujifuatilia). Kiasa ya kwamba sina uwezo kukuhisabia aibu zangu, au pia sina uwezo wa kutaja dhambi zangu.

وَ إِنَّمَا أُوَبِّخُ بِهَذَا نَفْسِي طَمَعاً فِي رَأْفَتِكَ الَّتِي بِهَا صَلَاحُ أَمْرِ الْمُذْنِبِينَ ، وَ رَجَاءً لِرَحْمَتِكَ الَّتِي بِهَا فَكَاكُ رِقَابِ الْخَاطِئِينَ .

Na kwa hakika, ninaikemea vikali nafsi yangu (kutokana na hayo), kwa shauku (tamaa) ya kupata huruma Zako (adhimu) ambayo ni nyenzo (njia) inayopelekea marekebisho ya hali za waasi (matenda dhambi), na nina (tamaa) matumaini ya kupata rehema Zako ambazo funguo za kuwapa uhuru watenda dhambi (walioko ndani ya magereza ya dhambi).

اللَّهُمَّ وَ هَذِهِ رَقَبَتِي قَدْ أَرَقَّتْهَا الذُّنُوبُ ، فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ ، وَ أَعْتِقْهَا بِعَفْوِكَ ، وَ هَذَا ظَهْرِي قَدْ أَثْقَلَتْهُ الْخَطَايَا ، فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ ، وَ خَفِّفْ عَنْهُ بِمَنِّكَ    

Ewe Mola wangu! Na hii (ndiyo) shingo (nafsi) yangu ambayo madhambi (yangu) yameitia utumwani, basi mswalie Mtume Muhammad na Aali zake, na uiachie huru kupitia msamaha Wako. Na huu (ndiwo) mgongo wangu ambao tayari umeshaelemewa na makosa (yangu), basi mswalie Mtume Muhammad na Aali zake, na uupunguze mzigo (huu) ulioko juu yake kwa hisani Zako.

يَا إِلَهِي لَوْ بَكَيْتُ إِلَيْكَ حَتَّى تَسْقُطَ أَشْفَارُ عَيْنَيَّ ، وَ انْتَحَبْتُ حَتَّى يَنْقَطِعَ صَوْتِي ، وَ قُمْتُ لَكَ حَتَّى تَتَنَشَّرَ قَدَمَايَ ، وَ رَكَعْتُ لَكَ حَتَّى يَنْخَلِعَ صُلْبِي ، وَ سَجَدْتُ لَكَ حَتَّى تَتَفَقَّأَ حَدَقَتَايَ ، وَ أَكَلْتُ تُرَابَ الْأَرْضِ طُولَ عُمْرِي ، وَ شَرِبْتُ مَاءَ الرَّمَادِ آخِرَ دَهْرِي ، وَ ذَكَرْتُكَ فِي خِلَالِ ذَلِكَ حَتَّى يَكِلَّ لِسَانِي ، ثُمَّ لَمْ أَرْفَعْ طَرْفِي إِلَى آفَاقِ السَّمَاءِ اسْتِحْيَاءً مِنْكَ مَا اسْتَوْجَبْتُ بِذَلِكَ مَحْوَ سَيِّئَةٍ وَاحِدَةٍ مِنْ سَيِّئَاتِي .    

Yaa Ilahi (Ewe Mola wangu)! Lau ningekulilia Wewe hadi kope zangu zikaanguka, na nikaomboleza kwa nadama hadi sauti yangu ikakatika, na nikakusimamia Wewe katika Swala (yangu) hadi miguu yangu ikavimba, na nikakurukuia Wewe hadi uti wangu wa mgongo ukavunjika, na nikakusujudia Wewe hadi mboni za macho yangu zikatoka, na nikala udongo wa ardhi umri wangu wote, na nikanywa maji ya majivu hadi mwisho wa maisha yangu, na nikakufanyia dhikri katika yote hayo hadi ulimi wangu ukachoka, kisha nisiinue macho yangu kuelekea mbinguni kwa haya zangu mbele Yako, yote hayo, yasingepelekea nisistahiki kufutiwa hata dhambi moja miongoni mwa dhambi zangu.

وَ إِنْ كُنْتَ تَغْفِرُ لِي حِينَ أَسْتَوْجِبُ مَغْفِرَتَكَ ، وَ تَعْفُو عَنِّي حِينَ أَسْتَحِقُّ عَفْوَكَ فَإِنَّ ذَلِكَ غَيْرُ وَاجِبٍ لِي بِاسْتِحْقَاقٍ ، وَ لَا أَنَا أَهْلٌ لَهُ بِاسْتِيجَابٍ ، إِذْ كَانَ جَزَائِي مِنْكَ فِي أَوَّلِ مَا عَصَيْتُكَ النَّارَ ، فَإِنْ تُعَذِّبْنِي فَأَنْتَ غَيْرُ ظَالِمٍ لِي .      

Na hata kama, unaponipa Maghufira Yako pale ninapostahiki msamaha Wako, na kunipa Afua (msamaha) Yako pale ninapostahili msamaha Wako, bila shaka jambo hilo haliniwajibikii mimi kutokana kustahiki kwangu, wala mimi si stahili hilo, kutokana na kuwajibikiwa kwangu na jambo hilo. Kwani kutokana na uasi wangu wa awali dhidi Yako, jazaa yangu kutoka Kwako ilikuwa ni Moto wa Jahannam. Kwa hiyo hata kama utaniadhibu, bila shaka hutakuwa ni mwenye kunidhulumu.

إِلَهِي فَإِذْ قَدْ تَغَمَّدْتَنِي بِسِتْرِكَ فَلَمْ تَفْضَحْنِي ، وَ تَأَنَّيْتَنِي بِكَرَمِكَ فَلَمْ تُعَاجِلْنِي ، وَ حَلُمْتَ عَنِّي بِتَفَضُّلِكَ فَلَمْ تُغَيِّرْ نِعْمَتَكَ عَلَيَّ ، وَ لَمْ تُكَدِّرْ مَعْرُوفَكَ عِنْدِي ، فَارْحَمْ طُولَ تَضَرُّعِي وَ شِدَّةَ مَسْكَنَتِي ، وَ سُوءَ مَوْقِفِي .      

Mola wangu! Kwa kuwa umenifunika (umenistiri) kwa sitara yako, wala hukunifedhehesha kwa kuyaweka hadharani madhambi yangu, na ukanivumilia kwa ukarimu wako, na wala hukuniharakishia (adhabu Yako). Na ulinichukulia (ulinistahamilia) kwa fadhila zako, na hukuniondolea (hukuninyima) neema zako, wala hukuutia dosari wema Wako juu yangu. Basi, rehemu urefu wa kilio changu, ukubwa wa dhiki yangu, pamoja na hali yangu ya kusikitisha (au ubaya wa hadhi yangu).

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ ، وَ قِنِي مِنَ الْمَعَاصِي ، وَ اسْتَعْمِلْنِي بِالطَّاعَةِ ، وَ ارْزُقْنِي حُسْنَ الْإِنَابَةِ ، وَ طَهِّرْنِي بِالتَّوْبَةِ ، وَ أَيِّدْنِي بِالْعِصْمَةِ ، وَ اسْتَصْلِحْنِي بِالْعَافِيَةِ ، وَ أَذِقْنِي حَلَاوَةَ الْمَغْفِرَةِ ، وَ اجْعَلْنِي طَلِيقَ عَفْوِكَ ، وَ عَتِيقَ رَحْمَتِكَ ، وَ اكْتُبْ لِي أَمَاناً مِنْ سُخْطِكَ ، وَ بَشِّرْنِي بِذَلِكَ فِي الْعَاجِلِ دُونَ الآْجِلِ . بُشْرَى أَعْرِفُهَا ، وَ عَرِّفْنِي فِيهِ عَلَامَةً أَتَبَيَّنُهَا .    

Ewe Mola wangu, mswalie Muhammad na Aali zake. Na unikinge na maasi, na unitumikishe katika taa (nifanye niwe ni mtiifu Kwako). Na uniruzuku toba ya kweli (nipe taufiki njema ya kurudi Kwako). Na unitoharishe kwa Tawba. Na unipe nguvu ya Isma (hifadhi dhidi ya dhambi). Na uboreshe maisha yangu kwa kunipa afya njema. Na unionjeshe ladha ya Maghfira. Na unijaalie niwe huru kupitia msamaha Wako, na niliyekombolewa kwa huruma (rehema) Zako. Na uniandikie amani ili niwe mbali na ghadhabu Zako (nipe usalama dhidi ya hasira yako). Na unibashirie hayo duniani kabla ya Akhera (na unipatie bishara hiyo mapema hapa duniani kabla ya Akhera), nayo iwe ni bishara ya wazi mbele yangu, na unioneshe alama itakayoniwezesha kutambua hilo.

إِنَّ ذَلِكَ لَا يَضِيقُ عَلَيْكَ فِي وُسْعِكَ ، وَ لَا يَتَكَأَّدُكَ فِي قُدْرَتِكَ ، وَ لَا يَتَصَعَّدُكَ فِي أَنَاتِكَ ، وَ لَا يَؤُودُكَ فِي جَزِيلِ هِبَاتِكَ الَّتِي دَلَّتْ عَلَيْهَا آيَاتُكَ ، إِنَّكَ تَفْعَلُ مَا تَشَاءُ ، وَ تَحْكُمُ مَا تُرِيدُ ، إِنَّكَ عَلَى كُلِّ شَيْ‌ءٍ قَدِيرٌ .

Hakika, haya hayakupi shida (hayakukwazi) ndani ya uwezo Wako adhimu, wala hayakusumbui ndani ya nguvu Zako. Wala wala hayakuchoshi katika utoaji wa vipawa Vyako (fadhila Zako) ambavyo vimethibitishwa na alama zako (madhihiriko Yako). Hakika wewe hunafanya ulitakalo, na hunaamua ulipendalo. Bila shaka Wewe una Mweza wa kila jambo.