Dua ya Ishirini na Saba ya Sahifa Sajjadiyya
Dua ya ishirini na saba ya Sahifa Sajjadiyya: ni miongoni mwa dua zilizonukuliwa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s) kwa ajili ya walinzi wa mipaka ya Kiislamu. Katika dua hii, Imamu Zainu al-Abidina (a.s) anamwomba Mwenye Ezi Mungu kuimarisha mipaka ya Waislamu pamoja na kuwaimarisha walinzi wa mipaka hiyo kwa kuwapa; maarifa, subira, ikhlasi, imani, uchamungu pamoja na kuwapa baraka ya wingi wa idadi. Pia katika dua yake hii, anamwomba Mwenye Ezi Mungu kuwajaalia Waislamu kuwa na ushirikiano wa pamoja katika kuwatetea Waislamu kwa kuwasaidia wapiganaji na walinzi wa mipaka hiyo, pamoja na kuwatunza watu wa familia zao. Imamu Sajjad (a.s) anasisitiza nafasi ya msaada wa ghaibu katika ushindi wa Waislamu dhidi ya washirikina, na anaona kuwa maangamizi ya makafiri ndio msingi wa kujenga jamii ya waumini wanaoamini na kuabudu Mungu mmoja.
Dua ya ishini na nane ya Sahifa Sajjadiyya, ndiyo nuru msingi iliyotumiwa na Sheikh Ja'far Murtada al-Amili, katika kitabu chake Siyasat al-Harb fi Du'a Ahl al-Thughur, chenye kufafanua mbinu za kivita na za kulinda mipaka ya Waislamu. Dua hii imeufafanuzi kwa kina kabisa ndani ya vitabu chambuzi vilivyoshrehesha na kufafanua kitabu cha Sahifa Sajjadiyya, hususan katika lugha ya Kiajemi. Miongoni mwa tafsiri chambuzi kwa lugha ya Kiajemi ni kama vile; Diyare Asheqan, cha Hossein Ansarian na Shuhud wa Shenakht, cha Hassan Mamduhi Kermanshahi. Viilevile kuna tafsiri chambuzi zinazopatikana Kiarabu, miongoni mwazo ni kitabu kiitwacho Riyadhu al-Salikin, kilichoandikwa na Sayyid Ali Khan Madani.
Mafunzo ya Dua ya Ishirini na Nane
Dhamira kuu ya dua ya ishirini na saba ya kitabu cha Sahifa Sajjadiya, inahusiana na kuwaombea dua walinzi na watetezi wa ardhi za Kiislamu daima dawama. Ndani yake, Imamu Sajjad (a.s) anamuomba Mwenye Ezi Mungu awaruzuku walinzi hao kwa kuwapa maarifa, subira, uthabiti, ikhlasi, bajeti isio na mapungufu, mshikamano, uelewano, kuhurumiana, na wingi wa kiidadi.
Kwa na namna anavyobainisha mfasiri wa dua hii Hassan Mamduhi Kermanshahi, ni kwamba; hii ni dua kamilifu iangaziayo pande zote, nayo imesheheni nukta za Tauhidi, akhlaki, na irfani kuhusiana na uwanja wa mapambano. Kadhalika, dua ni yenye kutufunza kanuni na adabu za vita kupitia mfumo uliofumwa kwa njia ya dua. [1] Ja'far Sobhani, mmoja wa Marja'a Taklidi (mujitahid mwenye wafwasi wanaoshikamana na fatwa zake), wa kutoka upande wa madhehebu ya Kishia, anaamini kwamba; fasili ya ibara isemayo "اللَّهُمَّ وَ امْزُجْ مِیاهَهُمْ بِالْوَبَاءِ" (Ewe Mwenye Ezi Mungu yachanganye Maji yao na virusi vya kolera) iliomo duani humo, ni moja wapo ya miujiza ya kiilimu iliyomo ndani ya dua hii; Hii ni kwa kuwa katika zama hizo, hapakuwa na ufahamu kuwa maradhi ya kipindupindu husambaa kwa njia ya maji. [2]
Mafunzo Yaliomo Ndani ya Dua ya Kumi na Nane
· Dua kwa ajili ya kuimarisha mipaka ya Waislamu.
· Umuhimu wa kulinda mipaka na kutetea Uislamu (uzito wa jukumu la ulinzi wa mipaka).
· Dua ya kupata ongezeko la walinzi wa mipaka na kuimarika kwa silaha zao.
· Ombi la kuomba upendo na urafiki kati ya walinzi wa mipaka.
· Ombi la kuwaombea walinzi wa mipaka wapate nguvu, wawe na subra na waokoke kupitia nusura ya Mwenye Ezi Mungu.
· Ombi la kuwaombea walinzi wa mipaka kupata ongezeko la ufahamu na kuboreka kielimu.
· Kuhuisha ukumbusho wa Akhera katika fikra za walinzi wa mipaka ili wasiwakimbie maadui.
· Ombi la kuwaombea walinzi wa mipaka wawe na imani na uchamungu.
· Ombi la kuwaombea wapiganaji waisahau dunia yao pale wanapokabiliana na maadui zao.
· Ombi la kuwaombea wakumbuke Pepo na neema zake pale wanapokuwa ndani ya uwanja wa mapambano.
· Neema za Akhera ni bora kuliko tunavyoweza kufikiria.
· Ombi la kumuomba Mola awadhoofish maadui wa Uislamu na kuwafanya wasiwe na nguvu ndani ya uwanja wa mapambano.
· Kuomba mafaninikio ya juhudi za wapiganaji, na matunda yake yawe ni kusimama kwa Tawhidi (Upweke wa Mungu) duniani kote.
· Kuwaombea maadui washindwe katika mipaka yote ya Kiislamu.
· Kuwaombea maadui wa Mungu waangamizwe na kung'olewa kabisa duniani kote.
· Nafasi ya msaada usioonekana (wa ghaibu) katika ushindi wa kuwashinda maadui wa Uislamu.
· Kuangamia kwa wapinzani wa imani ya Kiislamu ndiyo msingi wa kuasisi jamii ya kitauhidi.
· Dua ya kuimarisha hekima na busara za kimkakati kwa Waislamu.
· Dua ya kuviimarisha vikosi vya Kiislamu kupitia nguvu za Malaika.
· Kurejelea nusura ya Kiungu kwa Waislamu katika Vita vya Badr kupitia jeshi la Malaika.
· Dua ya kumuomba Mungo kuwafanya washirikina wapambane wao kwa wao.
· Dua ya kudunisha uwezo wa kimwili na kiakili wa washirikina katika kukabiliana na Waislamu.
· Dua ya kuwanufaisha Mujahidina (wapiganaji wa Kiislamu) na kuwaombea nusura za kighaibu, kama ilivyotokea katika vita vya Badr.
· Dua ya kuomba mghafala na kutojitambua kwa maadui.
· Dua ya kuwaombea heri wapiganaji wa Kiislamu.
· Ufafanuzi wa masharti ya wapiganaji wa Kiislamu (kujitenga na matamanio ya umaarufu na majivuno).
· Dua ya kuomba hatima ya mafanikio na ufanisi.
· Dua ya kupata taufiki ya kufa kishahidi baada ya kupatikana kwa ushindi.
· Ombi la kuomba jaza njema kwa wale wanaosimamia maslahi ya familia za walinzi wa mipaka.
· Thamani ya kuutakia Uislamu maslahi mema na kuwa na azma ya jihadi dhidi ya adui.
· Ombi la thawabu za jihadi kwa wasioshiriki vitani na wale wenye nyudhuru za kisheria.
· Ombi la kuorodheshwa kwa majina ya wasioshiriki Jihadi pamoja na wale wenye nyudhuru kwenye orodha ya Mashahidi, watu wema, na wachamungu.
· Ombi la kumtakia rehma na amani Mtume Muhammad (s.a.w.w), yeye pamoja na Aali zake.
Manufaa na umuhimu wa usaidizi wa raia kwa vikosi vya wapiganaji ni kama ifuatavyo:
· Ushirikishwaji wa umma mzima katika jukumu la kulinda Uislamu.
· Kuimarisha ari ya wapiganaji na kuchochea mtazamo chanya kuhusiana na mustakabali wao.
· Maandalizi ya kiakili na kisaikolojia ya jamii kwa ajili ya ulinzi wa ardhi zao.
· Kudumisha mshikamano na umoja wa kijamii miongoni mwa Waislamu. [3]
Usoma wa Dua ya Ishini na Saba Ndani ya Nyakati za Vita
Baadhi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia huisoma dua hii pindi maadui wa Uislamu wanaposhambulia nchi za Kiislamu au kwashambulia Waislamu wenyewe. Kwa mfano, wakati wa vita vya Israel dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza, makundi ya watu nchini Iran yalichukuwa hatua ya kuisoma dua hii kwa pamoja ili kuwaombea ukombozi watu wa Palestina. [4] Kadhalika, sambamba na vita vya Israel dhidi ya watu wa Gaza na Lebanon katika miaka ya 2023 na 2024, kulishuhudiwa ongezeko la utafutaji (usakaji) wa dua hii mtandaoni. [Inahitaji chanzo]
Tafsiri Chambuzi
Kuna vitabu kadhaa vilivyoandikwa vikitoa uchambuzi na maelezo ya kina kuhusiana na dua ya ishirini na saba. Miongoni mwa vitabu hivyo ni:
· Kitabu "Siyasat al-Harb fi Du'a Ahl al-Thughur" (Sera za Vita katika Dua kwa Watu wa Mpakani) cha mwandishi Ja'far Murtada al-'Amili. Nacho ni kitabu chenye sura kumi na nne zinazofafanua mbinu za kijeshi za kulinda mipaka ya maeneo ya Uislamu. [5] Kitabu hichi kilichapishwa na Kituo cha Kiislamu cha Tafiti (mbali mbali), mnamo mwaka 1428 Hijria. Aidha, tafsiri ya kitabu hchi kwa lugha ya Kifursi (Kiajemii) ilichapishwa na Shirika la Uchapishaji la Ma'aref mnamo mwaka 1394 kulingana na Kalenda ya Jua (Shamsia).
· Kitabu "Marzdarane dar Duaye Emam Sajjad (a.s)" (Walinzi wa Mipaka katika Dua ya Imam Sajjad), kilichoandikwa na Baitullah Bayati Zanjani. Kitabu hiki, chenye jumla ya sura 42, kilichapwa na Shirika la Uchapishaji la Mehr Amirul-Mu'minina mnamo mwaka 1389 (kwa Kalenda ya Jua). [6]
Sambamba na hayo, pia dua hii ianayohusiana na walinzi wa mipaka, imefasiriwa na kufafanuliwa kupitia vitabu vya lugha mbali mbali vilivyofasiri maandiko ya kitabu cha Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa vitabu vilivyotoa tafsiri chambuzi kwa lugha ya Kiajemi, ni pamoja na; Diare Ashiqan, kilichoandikwa na Hussein Ansarian, [7] Shuhud wa Shenakh, kazi ya Muhammad Hasan Mamduhi Kermanshahi [8] na Sherh wa Tarjume Sahife Sajjadiyye, kazi ya Sayyid Ahmad Fahri. [9]
Kwa upande wa lugha ya Kiarabu, kuna waandishi fulani waliofanya jitihada za kufasiri na kuchambua dua hizi adhimu zilizomo katika Sahifa Sajjadiyya. Baadhi ya vitabu zilivyofanya kazi hii kwa lugha ya Kiarabu ni pamoja na; Riadhu al-Salikin, cha Sayyid Ali Khan al-Madani, [10] Fi Dhilal as-Sahifat as-Sajjadiyya, cha Muhammad Jawad Mughniyya, [11] Riyadh al-'Ārifina, kazi ya Muhammad bin Muhammad Darabi, [12] Afaqu Al-Ruuh, kazi ya Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah. [13] Pia kuna kazi andishi za kilugha zilizofanya kwa ajili ya uchambuzi wa ki-isimu wa istilahi zilizotumika katika dua hii. Miongoni mwa kazi hizo ni kama vile; Ta'liqat 'ala as-Sahifat as-Sajjadiyya kazi ya Faidhu Kashani, [14] na Sharhu as-Sahifat al-Sajjadiyya kazi ya Izz al-Din al-Jaza'iri. [15]
Matini na Tafsiri ya Dua ya Ishini na Saba
وَ کانَ مِنْ دُعَائِهِ علیهالسلام لِأَهْلِ الثُّغُورِ
Na miongoni mwa dua zake (rehema na amani zimshukie) ni ile dua aliyokuwa akiwaombea Ahlu ath-Thughur (walinzi wa mpaka). Nayo ni kama ifuatavyo
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ حَصِّنْ ثُغُورَ الْمُسْلِمِینَ بِعِزَّتِک، وَ أَیدْ حُمَاتَهَا بِقُوَّتِک، وَ أَسْبِغْ عَطَایاهُمْ مِنْ جِدَتِک.
Ee Mola, mshushie rehema na amani Muhammad na Aali zake; na uilinde mipaka ya Waislamu kwa uwezo (ukuu) Wako, na waunge mkono wahami (walinzi) wa mipaka hiyo kwa Nguvu Zako, na uwaengezee kipato chao kupitia hazina Yako.
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ کثِّرْ عِدَّتَهُمْ، وَ اشْحَذْ أَسْلِحَتَهُمْ، وَ احْرُسْ حَوْزَتَهُمْ، وَ امْنَعْ حَوْمَتَهُمْ، وَ أَلِّفْ جَمْعَهُمْ، وَ دَبِّرْ أَمْرَهُمْ، وَ وَاتِرْ بَینَ مِیرِهِمْ، وَ تَوَحَّدْ بِکفَایةِ مُؤَنِهِمْ، وَ اعْضُدْهُمْ بِالنَّصْرِ، وَ أَعِنْهُمْ بِالصَّبْرِ، وَ الْطُفْ لَهُمْ فِی الْمَکرِ.
Ewe Mola! Ziteremshe rehema na amani Zako juu ya Muhammad na Aali zake, na ukithirishe idadi ya walinzi wa mipaka hiyo, na uzinoe zana zao (za vita). Imarisha himaya zao ya mipakani humo na uifanye isize kupenyeke. Fuma umoja wao, na uwasimamie katika utekelezaji wa majukumu yao. Wahakikishie ruzuku endelevu, na uwe ni Mwidhinishaji (suluhu pekee) katika haja zao (wakati wa shida zao). Watie nguvu kwa nusra Yako, wasaidie kupitia nguvu za ustahimilivu, na wasaidie waweze kufikiri vizuri na kupanga mambo yao kwa busara.
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ عَرِّفْهُمْ مَا یجْهَلُونَ، وَ عَلِّمْهُمْ مَا لَا یعْلَمُونَ، وَ بَصِّرْهُمْ مَا لَا یُبْصِرُونَ.
Ewe Mola! Ziteremshe rehema na amani yako juu ya Muhammad na Aali zake. Na uwape (walizi hawa) maarifa ya kuelewa yale wasioukuwa na elimu nayo, wafunze yale wasiyoyajua, na uwape mwono wa kuyaona (kuyatambua) yale wasiyokuwa na uoni nayo.
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ أَنْسِهِمْ عِنْدَ لِقَائِهِمُ الْعَدُوَّ ذِکرَ دُنْیاهُمُ الْخَدَّاعَةِ الْغَرُورِ، وَ امْحُ عَنْ قُلُوبِهِمْ خَطَرَاتِ الْمَالِ الْفَتُونِ، وَ اجْعَلِ الْجَنَّةَ نُصْبَ أَعْینِهِمْ، وَ لَوِّحْ مِنْهَا لِأَبْصَارِهِمْ مَا أَعْدَدْتَ فِیهَا مِنْ مَسَاکنِ الْخُلْدِ وَ مَنَازِلِ الْکرَامَةِ وَ الْحُورِ الْحِسَانِ وَ الْأَنْهَارِ الْمُطَّرِدَةِ بِأَنْوَاعِ الْأَشْرِبَةِ وَ الْأَشْجَارِ الْمُتَدَلِّیةِ بِصُنُوفِ الثَّمَرِ حَتَّی لَا یَهُمَّ أَحَدٌ مِنْهُمْ بِالْإِدْبَارِ، وَ لَا یحَدِّثَ نَفْسَهُ عَنْ قِرْنِهِ بِفِرَارٍ.
Ewe Mola! Mbariki Muhammad pamoja na Aali zake. Na pale (walinzi wa mipaka hiyo) wakutanapo na adui (zao), wasahaulishe (kabisa) kumbukumbu ya kukumbuka mapambo yao kidunia yenye hadaa na udanganyifu, na ufute kabisa kutoka katika nyoyo zao fikra ya mali iletayo fitina. Na iweka taswira ya Janna (Pepo) mbele ya macho yao, na uwadhihirishie machoni mwao yale uliyoyaandaa ndani ya makazi hayo ya milele, na mapumzikio matukufu, ikiwa ni pamoja na Hurul-Alhisan (wanawake wa Peponi wenye macho yapendezayo) na sura za kuvutia, mito itiririshayo vinywaji vya aina mbalimbali, miti ya matunda mbalimbali yenye matawi yaliyolemea (yaliyoinama). (Waoneshe neema hizo) ili kusitokee hata mmoja kati yao atakayemgeuzia kisogo adui (yake), wala asiwe na mawazo ya kukwepa na mapambano.
اللَّهُمَّ افْلُلْ بِذَلِک عَدُوَّهُمْ، وَ اقْلِمْ عَنْهُمْ أَظْفَارَهُمْ، وَ فَرِّقْ بَینَهُمْ وَ بَینَ أَسْلِحَتِهِمْ، وَ اخْلَعْ وَثَائِقَ أَفْئِدَتِهِمْ، وَ بَاعِدْ بَینَهُمْ وَ بَینَ أَزْوِدَتِهِمْ، وَ حَیرْهُمْ فِی سُبُلِهِمْ، وَ ضَلِّلْهُمْ عَنْ وَجْهِهِمْ، وَ اقْطَعْ عَنْهُمُ الْمَدَدَ، وَ انْقُصْ مِنْهُمُ الْعَدَدَ، وَ امْلَأْ أَفْئِدَتَهُمُ الرُّعْبَ، وَ اقْبِضْ أَیدِیهُمْ عَنِ الْبَسْطِ، وَ اخْزِمْ أَلْسِنَتَهُمْ عَنِ النُّطْقِ، وَ شَرِّدْ بِهِمْ مَنْ خَلْفَهُمْ وَ نَکّلْ بِهِمْ مَنْ وَرَاءَهُمْ، وَ اقْطَعْ بِخِزْیهِمْ أَطْمَاعَ مَنْ بَعْدَهُمْ.
Ewe Mola! Na wambaratisha maadui zao kupitia hili, na udhoofishe uwezo wa mashambulizi yao. Weka ufa kati yao na zana zao za kijeshi, na fungua vifungo vya azma ya nyoyo yao (samabaratisha azma za nyoyo zao). Weka masafa ya umbali kati yao na rasilimali zao (watenganishe na rasilimali zao), na uwafazaishe katika mikakati yao. Wapotoshe kutoka kwenye muelekeo wao, na uzikatize njia za msaada yao (idhibiti mikono yao). Zijaze kiwewe nyoyo zao na upunguza idadi yao. Zidhibiti ndimi zao zisitamke neno. Watawanye walioko nyuma yao kupitia wapiganaji hao (wa jeshi la Kiislamu), na uwaadhibu ili iwe ni funzo kwa watakaofuata nyuma yao. Katilia mbali matarajio ya vizazi vyao vijavyo baada yao.
اللَّهُمَّ عَقِّمْ أَرْحَامَ نِسَائِهِمْ، وَ یبِّسْ أَصْلَابَ رِجَالِهِمْ، وَ اقْطَعْ نَسْلَ دَوَابِّهِمْ وَ أَنْعَامِهِمْ، لَا تَأْذَنْ لِسَمَائِهِمْ فِی قَطْرٍ، وَ لَا لِأَرْضِهِمْ فِی نَبَاتٍ.
Ewe Mola, felisha (tasisha) nguvu za uzazi zilizomo matumboni mwa wanawake wao, na kausha migongo ya wanaume wao. Ukomeshe uzao wa wanyama wao. Usiipe anga yao idhini ya kunyesha mvua, wala ardhi yao (idhini ya) kuotesha mimea.
اللَّهُمَّ وَ قَوِّ بِذَلِک مِحَالَ أَهْلِ الْإِسْلَامِ، وَ حَصِّنْ بِهِ دِیارَهُمْ، وَ ثَمِّرْ بِهِ أَمْوَالَهُمْ، وَ فَرِّغْهُمْ عَنْ مُحَارَبَتِهِمْ لِعِبَادَتِک، وَ عَنْ مُنَابَذَتِهِمْ لِلْخَلْوَةِ بِک حَتَّی لَا یعْبَدَ فِی بِقَاعِ الْأَرْضِ غَیرُک، وَ لَا تُعَفَّرَ لِأَحَدٍ مِنْهُمْ جَبْهَةٌ دُونَک.
Ewe Mola, na kwa njia hiyo, zipe nguvu mbinu za uendeshaji wa Kiislamu, na zihimarishe ngome za miji yao, na uzineemeshe rasilimali zao. Waepushie fikra za vita dhidi ya adui zao, ili fikra zao zijikite kwevye utumishi ibada Yako, na uwatenge na mapambano ili wawe na utulivu wa karibu Nawe kwenye maombi yao. Fanya hivyo ili kusiwe na yeyote yule anayeabudiwa ardhini humu isipokuwa Wewe peke yako, na wala kusitokee mwengine yeyote yule anayewekewa ardhini paji la uso (anayesujudiwa) isipokuwa Wewe tu.
اللَّهُمَّ اغْزُ بِکلِّ نَاحِیةٍ مِنَ الْمُسْلِمِینَ عَلَی مَنْ بِإِزَائِهِمْ مِنَ الْمُشْرِکینَ، وَ أَمْدِدْهُمْ بِمَلَائِکةٍ مِنْ عِنْدِک مُرْدِفِینَ حَتَّی یکشِفُوهُمْ إِلَی مُنْقَطَعِ التُّرَابِ قَتْلًا فِی أَرْضِک وَ أَسْراً، أَوْ یُقِرُّوا بِأَنَّک أَنْتَ اللَّهُ الَّذِی لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ وَحْدَک لَا شَرِیک لَک.
Ewe Mola, waongoze Waislamu nguvu katika kila pembe ya ardhi katika dhidi ya wale washirikina wanaowakabiliana nao. Wadhamini kwa kuwaunga mkono kupitia jeshi la mfululizo wa Malaika kutoka Kwako, (wapigane na maadui hao) wawarudishe nyuma kutoka katika ardhi Yako, wangamiza na kuwateka hadi wawatoe na kuwaweka nje ya upeo wa ardhi. waweze kushuhudia na kukiri kwamba hakika Wewe ndiye Allah, ambaye hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Wewe, wa pekee usiye na mshirika.
اللَّهُمَّ وَ اعْمُمْ بِذَلِک أَعْدَاءَک فِی أَقْطَارِ الْبِلَادِ مِنَ الْهِنْدِ وَ الرُّومِ وَ التُّرْک وَ الْخَزَرِ وَ الْحَبَشِ وَ النُّوبَةِ وَ الزَّنْجِ وَ السَّقَالِبَةِ وَ الدَّیالِمَةِ وَ سَائِرِ أُمَمِ الشِّرْک، الَّذِینَ تَخْفَی أَسْمَاؤُهُمْ وَ صِفَاتُهُمْ، وَ قَدْ أَحْصَیتَهُمْ بِمَعْرِفَتِک، وَ أَشْرَفْتَ عَلَیهِمْ بِقُدْرَتِک.
Ewe Mola! Na uwajumuishe ndani ya hatima hiyo maadui wako wote walioko katika kila pande ya dunia. Wakiwemo wa walioko ardhi ya Wahindi, Warumi, Waturuki, Wakhazari, Wahabeshi, Wanubi, Wazenji, Wasakaliba (karibu na Bulgaria), na Wadaylami (milimani nchini Iran), pamoja na mataifa mengine yote yanayomshirikisha Mungu, ambayo majina na sifa zao zimetufichikia, amabo wamedhibitiwa na hisabu yako kupitia maarifa yako, na ukawatawala (ukawafahamu) kupitia nguvu Zako.
اللَّهُمَّ اشْغَلِ الْمُشْرِکینَ بِالْمُشْرِکینَ عَنْ تَنَاوُلِ أَطْرَافِ الْمُسْلِمِینَ، وَ خُذْهُمْ بِالنَّقْصِ عَنْ تَنَقُّصِهِمْ، وَ ثَبِّطْهُمْ بِالْفُرْقَةِ عَنِ الاحْتِشَادِ عَلَیهِمْ.
Ewe Mola! Washughulishe washirikina na vya kupigana wao kwa wao, ili wasiwe na fikra za kushambulia mipaka ya Waislamu. Na wapunguzie nguvu (idadi) zao ili wasiweze kupunguza (uwezo na idadi ya) Waislamu. Na wadhibiti kwa kuwatia migawanyiko (mifarakano), ili wasiweze kukusanyika pamoja dhidi yao (dhidi ya Waislamu).
اللَّهُمَّ أَخْلِ قُلُوبَهُمْ مِنَ الْأَمَنَةِ، وَ أَبْدَانَهُمْ مِنَ الْقُوَّةِ، وَ أَذْهِلْ قُلُوبَهُمْ عَنِ الِاحْتِیالِ، وَ أَوْهِنْ أَرْکانَهُمْ عَنْ مُنَازَلَةِ الرِّجَالِ، وَ جَبِّنْهُمْ عَنْ مُقَارَعَةِ الْأَبْطَالِ، وَ ابْعَثْ عَلَیهِمْ جُنْداً مِنْ مَلَائِکتِک بِبَأْسٍ مِنْ بَأْسِک کفِعْلِک یوْمَ بَدْرٍ، تَقْطَعُ بِهِ دَابِرَهُمْ وَ تَحْصُدُ بِهِ شَوْکتَهُمْ، وَ تُفَرِّقُ بِهِ عَدَدَهُمْ.
Ewe Mola! Zipokonye nyoyo zao utulivu iliomo ndani yake, na (un’ngoe) nguvu zilizomo viwiliwilini mwao. Zipumbaze akili zao dhidi ya kubuni njama (fulani), na idhoofishe mihimili yao ishindwe kukabiliana na wapambanaji (wa Kiislamu). Watie woga ili wasiweze kupambana na vigogo hivyo. Na watumie dhidi yao kikosi cha Malaika wako vyenye ukali utokanao na ukali Wako mkuu, kama ilivyokuwa katika tukio la Siku ya Badr. (Watumie jeshi lako hilo la Malaika) ili ukate kabisa mzizi wao wa fitna, uyafyagigie (uyafute) makali yao na ufarakanishe idadi yao, kupitia jeshi hilo.
اللَّهُمَّ وَ امْزُجْ مِیاهَهُمْ بِالْوَبَاءِ، وَ أَطْعِمَتَهُمْ بِالْأَدْوَاءِ، وَ ارْمِ بِلَادَهُمْ بِالْخُسُوفِ، وَ أَلِحَّ عَلَیهَا بِالْقُذُوفِ، وَ افْرَعْهَا بِالْمُحُولِ، وَ اجْعَلْ مِیرَهُمْ فِی أَحَصِّ أَرْضِک وَ أَبْعَدِهَا عَنْهُمْ، وَ امْنَعْ حُصُونَهَا مِنْهُمْ، أَصِبْهُمْ بِالْجُوعِ الْمُقِیمِ وَ السُّقْمِ الْأَلِیمِ.
Ewe Mola! Changanya vyanzo vyao vya maji yao na magonjwa ya miripuko (kipindupindu), na viharibu vyakula vyao (mazao yao) kwa maradhi mbali mbali. Ishambulie miji mijini yao mipasuko ya ardhi, na uifuatilizie mfululizo wa makombora ya maangamizi. Ikabili kwa ukame wa kutisha, na ujaalia riziki yao iwe katika ardhi tasa iliyo mbali mno nao. Vifanye vituo vyao vya ulinzi wao visiwe na kinga kwao, na uwakabili na njaa isiyokoma na maradhi yenye maumivu kupita budi.
اللَّهُمَّ وَ أَیّمَا غَازٍ غَزَاهُمْ مِنْ أَهْلِ مِلَّتِک، أَوْ مُجَاهِدٍ جَاهَدَهُمْ مِنْ أَتْبَاعِ سُنَّتِک لِیکونَ دِینُک الْأَعْلَی وَ حِزْبُک الْأَقْوَی وَ حَظُّک الْأَوْفَی فَلَقِّهِ الْیسْرَ، وَ هَیئْ لَهُ الْأَمْرَ، وَ تَوَلَّهُ بِالنُّجْحِ، وَ تَخَیرْ لَهُ الْأَصْحَابَ، وَ اسْتَقْوِ لَهُ، الظَّهْرَ، وَ أَسْبِغْ عَلَیهِ فِی النَّفَقَةِ، وَ مَتِّعْهُ بِالنَّشَاطِ، وَ أَطْفِ عَنْهُ حَرَارَةَ الشَّوْقِ، وَ أَجِرْهُ مِنْ غَمِّ الْوَحْشَةِ، وَ أَنْسِهِ ذِکرَ الْأَهْلِ وَ الْوَلَدِ.
Ewe Mola! Basi, mjaalie wepesi mpiganaji yeyote yule aliye shujaa miongoni mwa wafuasi wa mila Yako anayepambana nao, au mpambanaji kutoka kwa wafuasi wa mwenendo Wako anayesimama vikali dhidi yao, wanaosimama kwa ajiili ya kuikweza dini Yako, kuliimarisha kundi Lako, na kuboresha ukamilifu wa nafasi Yako. Mrahisishie jambo lake, na umhakikishie ushindi wake. Mchagulie wasaidizi na marafiki (wema). Muimarishie nguvu za uti wa mgongo wake, na umpe rizki ya kutosha. Mjaze uchangamfu wa mwili, na uzime ndani yake ushawashi wa matamanio (ya kidunia). Mkinge na huzuni ya upweke, na umsahaulishe mawazo ya familia na watoto.
وَ أْثُرْ لَهُ حُسْنَ النِّیةِ، وَ تَوَلَّهُ بِالْعَافِیةِ، وَ أَصْحِبْهُ السَّلَامَةَ، وَ أَعْفِهِ مِنَ الْجُبْنِ، وَ أَلْهِمْهُ الْجُرْأَةَ، وَ ارْزُقْهُ الشِّدَّةَ، وَ أَیدْهُ بِالنُّصْرَةِ، وَ عَلِّمْهُ السِّیرَ وَ السُّنَنَ، وَ سَدِّدْهُ فِی الْحُکمِ، وَ اعْزِلْ عَنْهُ الرِّیاءَ، وَ خَلِّصْهُ مِنَ السُّمْعَةِ، وَ اجْعَلْ فِکرَهُ وَ ذِکرَهُ وَ ظَعْنَهُ وَ إِقَامَتَهُ، فِیک وَ لَک.
Na mteulie dhamira njema, mstawishie anya yake, na uandamizie amani. Mkinge dhidi ya woga, na mpandikizie msimamo (wa maamuzi). Mruzuku ukakamavu, na andamana naye kwa kumpa nusra. Mwelimishe njia na mikakati ya sheria, na mthibitishe kwenye hukumu iliyo sahihi. Mweke mbali na unafiki, na mtakase kutokana na hamu ya kusifika (umaarufu). Hakikisha kuwa fikra zake, utajo wake, uhamaji, na uhamiaji wake, vyote viwe vimejikita Kwako na ni kwa ajili Yako.
فَإِذَا صَافَّ عَدُوَّک وَ عَدُوَّهُ فَقَلِّلْهُمْ فِی عَینِهِ، وَ صَغِّرْ شَأْنَهُمْ فِی قَلْبِهِ، وَ أَدِلْ لَهُ مِنْهُمْ، وَ لَا تُدِلْهُمْ مِنْهُ، فَإِنْ خَتَمْتَ لَهُ بِالسَّعَادَةِ، وَ قَضَیتَ لَهُ بِالشَّهَادَةِ فَبَعْدَ أَنْ یجْتَاحَ عَدُوَّک بِالْقَتْلِ، وَ بَعْدَ أَنْ یجْهَدَ بِهِمُ الْأَسْرُ، وَ بَعْدَ أَنْ تَأْمَنَ أَطْرَافُ الْمُسْلِمِینَ، وَ بَعْدَ أَنْ یوَلِّی عَدُوُّک مُدْبِرِینَ.
Na pindi wanapojipanga safu maadui Zako na maadui zake, basi dunisha (dogosha) idadi ya maadui hao machoni mwake, na uudhalilishe umuhimu (uzito) wao moyoni mwake. Igeuza zamu ya ushindi iwe kwake yeye, na wala usiufanya mwelekeo wa hatima ya zamu hiyo kuwa dhidi yake. Na iwapo utamhitimishia kwa saada (mafanikio ya mwisho), na ukamhukumia shahada (kifo cha ushahidi), basi fanya jambo hilo liwe ni baada ya kuwateketeza na kuaangamiza maadui Zako, na iwe ni baada ya kuwachosha kuwatekaji nyara, na baada ya mipaka ya Waislamu kupata amani, na baada ya adui Zako kugeuza migongo yao katika hali ya kushindwa.
اللَّهُمَّ وَ أَیّمَا مُسْلِمٍ خَلَفَ غَازِیاً أَوْ مُرَابِطاً فِی دَارِهِ، أَوْ تَعَهَّدَ خَالِفِیهِ فِی غَیبَتِهِ، أَوْ أَعَانَهُ بِطَائِفَةٍ مِنْ مَالِهِ، أَوْ أَمَدَّهُ بِعِتَادٍ، أَوْ شَحَذَهُ عَلَی جِهَادٍ، أَوْ أَتْبَعَهُ فِی وَجْهِهِ دَعْوَةً، أَوْ رَعَی لَهُ مِنْ وَرَائِهِ حُرْمَةً، فَآجِرْ لَهُ مِثْلَ أَجْرِهِ وَزْناً بِوَزْنٍ وَ مِثْلًا بِمِثْلٍ، وَ عَوِّضْهُ مِنْ فِعْلِهِ عِوَضاً حَاضِراً یتَعَجَّلُ بِهِ نَفْعَ مَا قَدَّمَ وَ سُرُورَ مَا أَتَی بِهِ، إِلَی أَنْ ینْتَهِی بِهِ الْوَقْتُ إِلَی مَا أَجْرَیتَ لَهُ مِنْ فَضْلِک، وَ أَعْدَدْتَ لَهُ مِنْ کرَامَتِک.
Ewe Mola! Toa thawabu na malipo sawa na kiwango cha mpiganaji, na kwa uzani uleule, kwa Mwislamu yeyote yule anayegharamia masuala ya kaya za wapiganaji au walindaji mipaka ya Waislamu, au yule anayefadhili na kusimamia familia za mmoja wa katika kipindi cha kutokuwepo kwake, au akamsaidia kifedha kutoka katika sehemu ya mali yake, au akampa rasilimali za kivita, au akachochea hima yake ya kushiriki Jihadi, au akamuunga mkono kwa dua njema, au akahifadhi hadhi yake wakati wa kutokuwepo kwake. Na umlipe kwa amali yake hiyo malipo yake bila kuchelewa (tokea duniani), ili apokee (aanze kuonja) matunda ya kazi yake bila kuchelewa, na afurahie manufaa ya kazi aliyoitanguliza; (aendelee na neema hizo) hadi pale uhai wake utakapomailizika, na kuanza kupokea yale malipo uliyomwandalia kwa hisani Yako na uliyomtayarishia kwa ukarimu Wako.
اللَّهُمَّ وَ أَیّمَا مُسْلِمٍ أَهَمَّهُ أَمْرُ الْإِسْلَامِ، وَ أَحْزَنَهُ تَحَزُّبُ أَهْلِ الشِّرْک عَلَیهِمْ فَنَوَی غَزْواً، أَوْ هَمَّ بِجِهَادٍ فَقَعَدَ بِهِ ضَعْفٌ، أَوْ أَبْطَأَتْ بِهِ فَاقَةٌ، أَوْ أَخَّرَهُ عَنْهُ حَادِثٌ، أَوْ عَرَضَ لَهُ دُونَ إِرَادَتِهِ مَانِعٌ فَاکتُبِ اسْمَهُ فِی الْعَابِدِینَ، وَ أَوْجِبْ لَهُ ثَوَابَ الْمُجَاهِدِینَ، وَ اجْعَلْهُ فِی نِظَامِ الشُّهَدَاءِ وَ الصَّالِحِینَ.
Ee Mola! Liweke kwenye orodhha ya wanaoabudu jina Mwislamu yeyote yule anayejali na kuguswa na hali ya Uislamu, na anahuzunishwa na mkusanyiko wa washirikina dhidi ya Waislamu, na hivyo akatia nia ya kupigana vita au kujiunga na mapambano (dhidi yao); ila akafelishwa na udhaifu aliokuwa nao, au umasikini wake ukawa ni kizingiti kwake, au akacheleweshwa na tukio fulani, au akakwazwa na kikwazo fulani bila ya kukusudia.
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ عَبْدِک وَ رَسُولِک وَ آلِ مُحَمَّدٍ، صَلَاةً عَالِیةً عَلَی الصَّلَوَاتِ، مُشْرِفَةً فَوْقَ التَّحِیاتِ، صَلَاةً لَا ینْتَهِی أَمَدُهَا، وَ لَا ینْقَطِعُ عَدَدُهَا کأَتَمِّ مَا مَضَی مِنْ صَلَوَاتِک عَلَی أَحَدٍ مِنْ أَوْلِیائِک، إِنَّک الْمَنَّانُ الْحَمِیدُ الْمُبْدِئُ الْمُعِیدُ الْفَعَّالُ لِمَا تُرِیدُ.
Ee Mungu! Mbariki Muhammad, ambaye ni mtumishi wako na mtume wako, yeye pamoja na Aali zake. Ziwe ni baraka bora zaidi kuliko baraka nyingine zote, na zenye mchanuo mkubwa zaidi kuliko zote. Ziwe ni Baraka zisizo na kikomo cha nyakati zake wala idadi yake. Ziwe ndiyo kamilifu zaidi juu ya zile baraka Zako kwa mwengine yeyote yule miongoni mwa Wateule Wako. Hakika, wewe ni Mpaji, Msifiwa, Mwanzilishi, Mrejeshaji, na Mtendaji chochote kile akitakacho.