Barua ya Imamu Ali (as) Kwa Imamu Hassan (as)

Kutoka wikishia

'Barua ya Imam Ali (as) kwa Imam Hassan' (as) ni barua yenye maudhui ya masuala ya kimaadili ambayo Imam Ali (a.s.) alimwandikia mwanawe Imam Hassan (a.s.) baada ya vita vya Siffin. Barua hii imetathminiwa kuwa ya kina katika kueleza masuala ya kimalezi. Baadhi ya masuala muhimu yaliyozungumziwa katika barua hii ni: Kuelezea hatua za kujijenga na kujiboresha binafsi na thamani za kimaadili, maadili ya kijamii, kulea mtoto na njia yake ya malezi, udharura wa kuzingatia hali ya kiroho na kubainisha vigezo vya mahusiano ya kijamii. Kwa mujibu wa watafiti, barua hii inahusu kanuni, malengo na mbinu ambazo Imam Ali (as) alikuwa akijaribu kuzifikia. Miongoni mwazo ni, kujipamba kwa maadili ya Kimungu, kushikamana maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu, kuzingatia utu na utukufu wa mwanadamu na tofauti za mtu binafsi, kuegemea uadilifu, tafakuri na busara, kutoa waadhi kutoa mifano ya kuigwa na mambo yenye ibra na mafunzo. Kwa kuzingatia baadhi ya vifungu vya barua hii, maudhui ya barua hayawiani na Umaasumu wa Imamu; hata hivyo, katika kujibu madai haya, inasisitizwa kwamba ingawa barua hii inaelekezwa kwa Imam Hassan (a.s.); lakini kimsingi, Imamu alihutubia umma kwa ujumla, na lau Imamu Ali (a.s.) angetaka kumwandikia barua Imamu mwingine maasumu, angeeleza mambo ya ndani na ya kina sana ambayo wengine wasingeyafahamu na hayangekuwa na faida kwao. Wasia huu ni mojawapo ya barua mashuhuri zaidi za Imamu, ambazo, mbali na Nahaj al-Balagha, zimenukuliwa katika vyanzo vilivyotangulia. Kwa mujibu wa nyaraka mbalimbali za simulizi hii na kwa kuzingatia maudhui yake marefu, barua hii inachukuliwa kuwa yenye itibari. Mbali na tafsiri kamili na ufafanuzi wa Nahaj al-Balagha, barua hii pia ina tafsiri na fafanuzi zinazojitegemea, miongoni mwazo ni: Pand Javid, mwandishi: Muhammad Taqi Misbah Yazdi na Hayat Javid, mwandiishi: Sayyid Mohammad Mohsen Hosseini Tehrani.

Utambulisho na Umuhimu

Barua ya Imam Ali (a.s.) kwa Imam Hassan (a.s.) ni mojawapo ya barua zilizonukuliwa katika Nahaj al-Balagha kuhusu suala la maadili.[1], na tabia[2] bali imetambuliwa kuwa ensaiklopidia kamili ya kimalezi.[3] Mohammad Taqi Misbah Yazdi, mmoja wa wafasiri na wafafanuzi wa barua hii, anaamini kwamba pamoja na mafundisho ya juu yaliyomo ndani ya barua hii, Imam Ali (a.s.) pia amezingatia nukta za kisaikolojia na kimalezi katika kueleza yaliyomo.[4]

Kwa mujibu wa nukuu ya Sayyid Radhii katika Nahj al-Balagha, Imam Ali (a.s.) aliandika barua hii aliporudi kutoka katika vita vya Siffin (mwaka 37 Hijria)[5]) na katika "Hadhrin " au "Hadhrein" (eneo la Syria).[6] Ingawa katika Nahaj al-Balagha na vyanzo vingine vingi,[7] wasia huu ulielekezwa kwa Imamu Hassan (a.s.), [8] lakini katika baadhi ya nukuu pia imeelezwa kwamba mlengwa wa barua hii alikuwa Muhammad Hanafia.[9] Kadhalika, kwa mujibu wa yale yaliyotajwa katika vyanzo vingine, sehemu ya barua ya 31 ya Nahaj al-Balagha ilielekezwa kwa Imam Hassan (a.s.) na sehemu nyingine ilielekezwa kwa Muhammad Hanafiya.[10] Kwa mujibu wa baadhi ya watafiti, Imam Ali (as) alikuwa na malengo katika kuandika barua hii na alikuwa akijaribu kuyafikia kupitia mbinu na mtindo fulani.[11] Malengo, misingi, kanuni na mbinu hizi zimeelezwa kama ifuatavyo:

. Malengo: Kuujipamba kwa sifa na maadili ya Kimwenyezi Mungu, kumtambua Mwenyezi Mungu, kujijenga, zuhudi, subra na kushikamana na maamrisho na kumtaja Mwenyezi Mungu.

. Misingi: Utukufu, tofauti za mtu na mtu, uwiano, kutumia akili, kutafakari na kutadabari.

. Mbinu: Kutoa ukumbusho, mawaida, kuja na kigezo, huba, kupata funzo na ibra, toba (kutubia) kujichunga na kujihesabu.[12]

Katika nakala nyingi za Nahajul Balagha, barua hii imewekwa katika orodha ya 31.[13]

Jina la Nakala

Namba ya barua[14]

Al-Mu’jam al-Mufahras, Subhi Saleh, Feidh al-Islam, Khui, Mulla Saleh, Ibn Abil-Hadid, Ibn Maytham, Abduh (barua namba 31)

Mulla Fat’hullah (barua namba 34) Fi Dhilal (barua namba 30)

Je, maudhui ya barua hii yanapingana na umaasumu wa Imam?

Baadhi ya maneno na ibara zilizotumika katika barua ya 31 ya Nahjul Balagha zimetambuliwa kuwa, haziendani na daraja na cheo cha Umaasumu wa Maimamu.[15] Ibn Abi al-Hadid, mmoja wa wafasiri wa Kisunni wa Nahj al-Balagha, anaamini kwamba ibara kama:(Kabla ya maoni yangu na mawazo yangu hayajapungukiwa) inapingana na kuwa Maasumu mwandishi wa barua, yaani Imamu Ali bin Abi Twalib (as), na ibara kama: (kabla ya matamanio na fitina za ulimwengu hazijakushambulia na hivyo kuwa vigumu kuepuka), kwa sababu kwa mujibu wa ibara hizi, fikra na mtazamo wa Imamu Ali ni wenye kubadilika na kadhalika kuna uwezekano hawaa na matamanio ya nafsi yakamuathiri Imamu Hassan (as).[16] Katika kuhalalisha kupingana huku, imesemwa kwamba ingawa barua hii kidhahiri inaelekezwa kwa Imam Hassan, lakini kiuhalisia, mlengwa wa barua hii ni umma kwa ujumla[17] na Imam Ali (as) aliandika barua hii kwa kuzingatia uhusiano wa baba na mwana wa watu wa kawaida; kwa sababu kama Imam Ali (as) angetaka kumwandikia barua Imamu mwingine Maasumu, angeeleza mambo mazito sana ambayo wengine wasingeweza kuyaelewa na kwao yasingekuwa na faida.[18]

Itibari ya Wasia

Kwa mujibu wa Nasser Makarem Shirazi, mmoja wa Marajii Taqlidi wa Kishia ni kuwa, hakuna shaka katika kunasibishwa kwa barua ya 31 ya Nahj al-Balagha kwa Imam Ali (a.s.); kwa sababu kwa upande mmoja, wasia huu una nyaraka mbalimbali, na kwa upande mwingine, maudhui yake ni ndefu kiasi kwamba ni Maasumina pekee ndio wanaoweza kuyaeleza haya.[19] Huu ni mmoja wa wasia maarufu wa Imamu wa kwanza wa Waislamu wa madhehebu ya Shia, ambao wanachuoni wa kabla ya Sayyid Radhi wameunukuu pia [20] wakiwemo:

1. Muhammad bin Ya’qub Kulayni (aliaga dunia: 328 H) katika Kitabu cha al-Rasail[21] na Kafi;[22].

2. Hassan bin Abdalla Askary, mmoja wa Maustadhi wa Sheikh Swaduq katika Kitabu cha al-Zawajir Wal-Mawaidh;[23].

3. Ibn Abdurabbuh, mmoja wa wanazuoni wa Kisunni (aliaga dunia:328 H) katika kitabu cha Al-Iqd al-Faraid;[24]

4. Sheikh Swaduq (aliaga dunia: 381 H) katika kitabu cha Man laYahdhuruh Al-Faqih;[25]

5. Ibn Shu’bah Harrani (mmoja wa Maulamaa wa karne ya 4 H), katika kitabu cha Tuhaf al-Uqul.[26]


Maudhui

Barua ya Imam Ali kwa Imam Hassan ikiwa na mada na maudhui ya maadili.[27] Miongoni mwa mambo yaliyotajwa katika barua hii, tunaweza kuashiria nukta zifuatazo:

• Hatua za kujijenga

• Tabia (akhlaq) na maadili ya kijamii.

• Udharura wa kuzingatia mambo ya kimaanawi.

• Udharura wa kuwa na mtazamo na muelekeo wa Kiakhera.

• Vigezo vya mahusiano ya kijamii.

• Kufanya hima katika kujikusanyia mafungu na masurufu kwa ajili ya Akhera.

• Ishara za rehma ya Mwenyezi Mungu

• Masharti ya kujibiwa dua.

• Udharura wa kukumbuka kifo.

• Kuwatambua waabudu dunia.

• Udharura wa kuangalia mambo kwa uhalisia katika maisha.

• Haki za Marafiki.

• Thamani za Kiakhlaq (kimaadili).

• Nafasi ya mwanamke.[28]


Tarjumi na Maelezo

Mbali na barua ya 31 katika Nahajul Balagha kutarjumiwa na kutolewa sherh (ufafanuzi na maelezo), katika tafsiri, tarjumi na maelezo yaliyoandikwa kwa ukamilifu kuhusu Nahj al-Balagha, kuna maelezo na tafsiri maalumu katika lugha za Kiajemi na Kiarabu ambayo yameandikwa kuhusiana na barua hii. Baadhi yao ni kama ifuatavyo: • Pand Javid (Nasaha za Milele), maelezo kwa lugha ya Kifarsi. Mwandishi: Muhammad Taqi Misbah Yazdi;[29] • Hayat Javid (Maisha ya Milele), mae.ezo ya Kifarsi, Sayyid Muhammad Muhsin Husseini Tehrani;[30] • Farzandam Inchanin Boyad Bud (Mwanangu Alipaswa Kuwa Hivi), mwandishi: Asghar Taherzadeh;[31] • Hekmat va Maishat (Hekima na Maisha), mwandishi: Abdul Karim Sourush;[32]. • Ali va Istimrar Insan (Ali na Kuendelea Mwanadamu), mwandishi: Abdul-Majid Zahadat;[34] • Be Suye Madineh Fazileh, ufafanuzi wa Kifarsi, mwandishi Ali Karimi Johromi.[35] • Amozihaye Tarbiyati Nameh Imam Ali (as) Be Imam Hassan (as)- “Mafunzo ya Kimalezi ya Barua ya Imamu Ali (as) Kwa Imamu Hassan (as), mwandishi Muhammad Yunes Arefi;[36] • Mehrabantarin Nameh (Barua ya Huruma Zaidi), mwandishi: Sayyid Alauddin Musawi Isfahani;[37]. • Aiin Zendegi (Kioo cha Maisha), mwandishi: Sayyid Mahdi Shojaei’[38]. • Tousiyehaye Pedaranew (Nasaha Zenye Hisia za Kibaba), mwandishi: Muhammad Dashti;[39]. • Nama Az Yama, mtarjumi: Fatemeh Karamkhuda Aminiyan na Ali Afrasiyabi;[40] • Be Pesaram (Kwa Mwanangu), mtarjumi: Fatemeh Shahidi;[41] • Nameh Hakimaneh, mtarjumi: Alireza Ali Dost;[42]

Kadhalika angalia: Faharasa ya Maelezo ya Nahajul Balagha na Faharasa ya Tarjumi za Nahajul Balagha.

Andiko la Barua na Tarjumi

Barua ya Imamu Kwa Mwanawe Imamu Hassan (as) Imamu Ali (as) alimuandikia barua hii Hassan bin Ali (as) wakati aliporejea kutoka ardhi ya Hadhirayn katika Vita vya Siffin.

مِنَ الْوَالِدِ الْفَانِ، الْمُقِرِّ لِلزَّمَانِ، الْمُدْبِرِ الْعُمُرِ، الْمُسْتَسْلِمِ لِلدُّنْیا، السَّاكِنِ مَسَاكِنَ الْمَوْتَی، وَالظَّاعِنِ عَنْهَا غَداً; إِلَی الْمَوْلُودِ الْمُؤَمِّلِ مَا لایدْرِكُ، السَّالِكِ سَبِیلَ مَنْ قَدْ هَلَكَ، غَرَضِ الاَْسْقَامِ، وَ رَهِینَةِ الاَْیامِ، وَ رَمِیةِ الْمَصَائِبِ، وَ عَبْدِ الدُّنْیا، وَ تَاجِرِ الْغُرُورِ، وَ غَرِیمِ الْمَنَایا، وَأَسِیرِ الْمَوْتِ، وَحَلِیفِ الْهُمُومِ، وَقَرِینِ الاَْحْزَانِ، وَنُصُبِ الاْفَاتِ، وَصَرِیعِ الشَّهَوَاتِ، وَخَلِیفَةِ الاَْمْوَاتِ.

Barua hii ni kutoka kwa baba (mwenye huruma na mwenye kuguswa na mambo) ambaye maisha yake yanaelekea ukingoni, amekiri juu ya magumu ya zama ( na matatizo yake) kutokana na ukali wa wakati na jua la maisha yake linazama (kwa kutaka au kutotaka), ndiye aliye katika makazi ya watangulizi ambao wamefumba macho kutoka duniani wametulia na wataiacha kesho. Barua hii ni kwa mtoto anayetamani mambo ambayo hayawezi kupatikana kamwe na ambaye amekanyaga njia ambayo wengine wamepitia na kuangamia (na kuufumbia macho ulimwengu), ambaye ndiye mlengwa wa magonjwa na mateka wa zama na nyakati katika msalaba wa mateso, mtumishi wa ulimwengu, mfanyabiashara wa kiburi. Mdaiwa na mateka wa kifo, mshirika wa ghamu, mwenza wa huzuni, shabaha ya maafa na misiba, mshindi wa tamaa na mrithi wa wafu.

أَمَّا بَعْدُ، فَإِنَّ فِیمَا تَبَیَّنْتُ مِنْ إِدْبَارِ الدُّنْیا عَنِّی، وَجُمُوحِ الدَّهْرِ عَلَیَّ، وَإِقْبَالِ الاْخِرَةِ إِلَیَّ، مَا یزَعُنِی عَنْ ذِکْرِ مَنْ سِوَای، وَالاِْهْتِمَامِ بِمَا وَرَائِی، غَیرَ أَنِّی حَیثُ تَفَرَّدَ بی‌دُونَ هُمُومِ النَّاسِ هَمُّ نَفْسِی، فَصَدَفَنِی رَأْیی، وَصَرَفَنِی عَنْ هَوَای، وَصَرَّحَ لِی مَحْضُ أَمْرِی، فَأَفْضَی بی‌إِلَی جِدٍّ لایكُونُ فِیهِ لَعِبٌ، وَصِدْقٍ لایشُوبُهُ كَذِبٌ. وَ وَجَدْتُكَ بَعْضِی، بَلْ وَجَدْتُكَ كُلِّی، حَتَّی كَأَنَّ شَیئاً لَوْ أَصَابَكَ أَصَابَنِی، وَكَأَنَّ الْمَوْتَ لَوْ أَتَاكَ أَتَانِی، فَعَنَانِی مِنْ أَمْرِكَ مَا یعْنِینِی مِنْ أَمْرِ نَفْسِی، فَكَتَبْتُ إِلَیكَ كِتَابِی مُسْتَظْهِراً بِهِ إِنْ أَنَا بَقِیتُ لَكَ أَوْ فَنِیتُ.

Ama baada ya kumhimidi na kumshukuru Mwenyezi Mungu, ufahamu wangu wa kuipa kisogo dunia na kuzishinda zama na akhera kuelekea kwangu, umenizuia nisikumbuke zaidi ya nafsi yangu na kuizingatia dunia na watu wake. Uzingatiaji huu umesababisha kujishughulisha kwangu na nafsi yangu na kunizuia nisifikirie juu ya watu (na kile kilicho mikononi mwao kutoka kwa ulimwengu) na kunizuia na matamanio ya nafsi na jambo hili kunifanya mimi niwe makini (kutokuwa na mzaha) na hakuna utani katika hilo, ukweli umeenea na uwongo haujachanganyika humo. Na kwa sababu nimekupata wewe ni sehemu ya uwepo wangu, bali uwepo wangu wote, ni kana kwamba huzuni inakufikia, inanifikia, na ikiwa kifo kinakuchukua basi kinanichukua pia mimi, ni kwa sababu hii, nilipata uzingatiaji wa kazi yako ni uzingatiaji wa kazi yangu, na ndiyo maana nimekuandikia barua hii ili iwe msaada wako iwe niko hai au la. فَإِنِّی أُوصِیكَ بِتَقْوَی اللهِ أَی بُنَی وَلُزُومِ أَمْرِهِ، وَعِمَارَةِ قَلْبِكَ بِذِکْرِهِ، الاِعْتِصَامِ بِحَبْلِهِ. وَأَی سَبَب أَوْثَقُ مِنْ سَبَب بَینَكَ وَبَینَ اللهِ إِنْ أَنْتَ أَخَذْتَ بِهِ. Mwanangu! Ninakuusia kumcha Mungu wa Mwenyezi Mungu na kushikamana na amri yake, na kuukuza moyo wako na roho yako kwa kumkumbuka Yeye, na kushikilia neema Yake, na ni njia gani inayoweza kuwa salama zaidi kati yako na Mwenyezi Mungu kuliko kamba ya Mwenyezi Mungu ikiwa utashikilia na kutoiachia.

أَحْی قَلْبَكَ بِالْمَوْعِظَةِ، وَأَمِتْهُ بِالزَّهَادَةِ، وَقَوِّهِ بِالْیقِینِ، وَنَوِّرْهُ بِالْحِکْمَةِ، ذَلِّلْهُ بِذِکْرِ الْمَوْتِ، وَقَرِّرْهُ بِالْفَنَاءِ، وَبَصِّرْهُ فَجَائِعَ الدُّنْیا، وَحَذِّرْهُ صَوْلَةَ الدَّهْرِ وَ فُحْشَ تَقَلُّبِ اللَّیالِی وَالاَْیامِ، وَ اعْرِضْ عَلَیهِ أَخْبَارَ الْمَاضِینَ، ذَكِّرْهُ بِمَا أَصَابَ مَنْ كَانَ قَبْلَكَ مِنَ الاَْوَّلِینَ، وَسِرْ فِی دِیارِهِمْ آثَارِهِمْ، فَانْظُرْ فِیمَا فَعَلُوا وَعَمَّا انْتَقَلُوا، وَأَینَ حَلُّوا وَنَزَلُوا! فَإِنَّكَ تَجِدُهُمْ قَدِ انْتَقَلُوا عَنِ الاَْحِبَّةِ، وَحَلُّوا دِیارَ الْغُرْبَةِ، وَكَأَنَّكَ عَنْ قَلِیل قَدْ صِرْتَ كَأَحَدِهِمْ.

(Mwanangu) uhuishe moyo wako kwa mawaidha (nasaha) na fisha (ua) matamanio yako ya nafsi kwa kujinyima moyo (na kutojali fahari ya dunia). Ufanye moyo kuwa na nguvu kwa yakini, na uung'arishe kwa hekima na elimu na uudhalilishe kwa kumbukumbu ya mauti na ulazimishe kukiri kuangamizwa kwa dunia, kwa kuonyesha majanga ya dunia, ufanye moyo wenye kuona na uulinde dhidi ya mashambulizi ya dunia na matukio ya mchana na ubaya wa mzunguko wake wa usiku na mchana. Ifikishie (nafsi yako) habari za waliotangulia na ikumbushe mateso yaliyowapata watu wa kabla yako. Tembelea ardhi na athari zao (zilizoharibiwa) na uone walichokifanya, walikotoka na walikotua. Kila ukiangalia hali zao, utaona kwamba waliacha marafiki zao na kuacha mizigo yao katika nchi ya ugeni. Inaonekana kwamba haitachukua muda mrefu kabla ya kuwa mmoja wao (na utakimbilia kwao kwa mwelekeo huo huo). فَأَصْلِحْ مَثْوَاكَ، وَلاَ تَبِعْ آخِرَتَكَ بِدُنْیاكَ; وَدَعِ الْقَوْلَ فِیمَا لاتَعْرِفُ، الْخِطَابَ فِیمَا لَمْ تُكَلَّفْ. وَأَمْسِکْ عَنْ طَرِیق إِذَا خِفْتَ ضَلاَلَتَهُ، فَإِنَّ الْكَفَّ عِنْدَ حَیرَةِ الضَّلاَلِ خَیرٌ مِنْ رُكُوبِ الاَْهْوَالِ. وَأْمُرْ بِالْمَعْرُوفِ تَكُنْ مِنْ أَهْلِهِ، وَأَنْكِرِ الْمُنْكَرَ بِیدِكَ وَلِسَانِكَ، وَبَاینْ مَنْ فَعَلَهُ بِجُهْدِكَ، وَجَاهِدْ فِی اللهِ حَقَّ جِهَادِهِ، وَلاَ تَأْخُذْكَ فِی اللهِ لَوْمَةُ لاَئِم. وَخُضِ الْغَمَرَاتِ لِلْحَقِّ حَیثُ كَانَ، وَتَفَقَّهْ فِی الدِّینِ، وَعَوِّدْ نَفْسَكَ التَّصَبُّرَ عَلَی الْمَکْرُوهِ، وَنِعْمَ الْخُلُقُ التَّصَبُرُ فِی الْحَقِّ.

Kwa hivyo, tengeneza makazi yako ya baadae na usiuze akhera yako kwa dunia, usizungumze usiyoyajua na usiingilie kisicho wajibu kwako. Usitie mguu katika njia ambayo ndani yake kuna hofu ya kupotea, kwa sababu kujiepusha na upotofu wakati wa kuogopa kupotea ni bora kuliko mtu kujitupa kwenye njia za hatari. Amrisha mema ili uwe sehemu yake, na kanusha maovu kwa mkono wako na ulimi wako, na muepuke kwa nguvu zako zote mtu ambaye anafanya maovu. Fanya jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kama unavyopaswa na unavyoweza kuwa, na kamwe lawama za wanaolaumu zisikuzuie kufanya juhudi katika njia ya Mwenyezi Mungu, zama katika bahari ya shida popote itakapokuwa ili kuufikia ukweli. Bobea katika dini yako (na jifunze ukweli wa dini kwa ukamilifu) na ujizoeshe kustahamili katika kukabiliana na matatizo, kwani kusimama kidete na kuwa na subira katika njia ya haki ni maadili na tabia njema sana. وَأَلْجِئْ نَفْسَكَ فِی أُمُورِكَ كُلِّهَا إِلَی إِلَهِكَ، فَإِنَّكَ تُلْجِئُهَا إِلَی كَهْفٍ حَرِیز، مَانِعٍ عَزِیز. وَأَخْلِصْ فِی الْمَسْأَلَةِ لِرَبِّكَ، فَإِنَّ بِیدِهِ الْعَطَاءَ وَالْحِرْمَانَ، أَکْثِرِ الاِسْتِخَارَةَ، وَتَفَهَّمْ وَصِیتِی، وَلاَ تَذْهَبَنَّ عَنْكَ صَفْحاً، فَإِنَّ خَیرَ الْقَوْلِ مَا نَفَعَ وَاعْلَمْ أَنَّهُ لاخَیرَ فِی عِلْم لاینْفَعُ، وَلاَ ینْتَفَعُ بِعِلْم لایحِقُّ تَعَلُّمُهُ. Jisalimishe kwa Mungu katika kazi zako zote, kwani ukifanya hivyo, umejikabidhi mwenyewe kwenye kimbilio la uhakika na lenye nguvu. Wakati unapoomba dua, muombe Mola wako kwa ikhlasi (tarajia kutoka Kwake na mrejee yeye tu) kwa sababu maghfira na rehema ziko mikononi Mwake, na muombe sana Mwenyezi Mungu akuruzuku kheri na mema. Udiriki na kufahamu vyema wasia wangu na usiuchukulie kirahisi na kijuujuu kwa sababu neno bora ni elimu yenye manufaa, na tambua kwamba, elimu isiyo na faida hakuna kheri ndani yake, na elimu ambayo haistahiki kujifunza haina faida (ni ile ambayo haina faida).

أَی بُنَیَّ، إِنِّی لَمَّا رَأَیتُنِی قَدْ بَلَغْتُ سِنّاً، وَرَأَیتُنِی أَزْدَادُ وَهْناً، بَادَرْتُ بِوَصِیتِی إِلَیكَ، وَأَوْرَدْتُ خِصَالاً مِنْهَا قَبْلَ أَنْ یعْجَلَ بی‌أَجَلِی دُونَ أَنْ أُفْضِی إِلَیكَ بِمَا فِی نَفْسِی، أَوْ أَنْ أُنْقَصَ فِی رَأْیی كَمَا نُقِصْتُ فِی جِسْمِی، أَوْ یسْبِقَنِی إِلَیكَ بَعْضُ غَلَبَاتِ الْهَوَی وَفِتَنِ الدُّنْیا، فَتَكُونَ كَالصَّعْبِ النَّفُورِ. وَإِنَّمَا قَلْبُ الْحَدَثِ كَالاَْرْضِ الْخَالِیةِ مَا أُلْقِی فِیهَا مِنْ شَیء قَبِلَتْهُ. فَبَادَرْتُكَ بِالاَْدَبِ قَبْلَ أَنْ یقْسُوَ قَلْبُكَ، وَیشْتَغِلَ لُبُّكَ، لِتَسْتَقْبِلَ بِجِدِّ رَأْیكَ مِنَ الاَْمْرِ مَا قَدْ كَفَاكَ أَهْلُ التَّجَارِبِ بُغْیتَهُ وَتَجْرِبَتَهُ، فَتَكُونَ قَدْ كُفِیتَ مَئُونَةَ الطَّلَبِ، وَعُوفِیتَ مِنْ عِلاَجِ التَّجْرِبَةِ، فَأَتَاكَ مِنْ ذَلِكَ مَا قَدْ كُنَّا نَأْتِیهِ، وَاسْتَبَانَ لَكَ مَا رُبَّمَا أَظْلَمَ عَلَینَا مِنْهُ.

Mwanangu! Nilipoona umri unaongezeka na nikaona nguvu zinaniishia niliamua (kukuandikia) wasia huu, nikaweka mambo muhimu kwenye wasia wangu, usije ukafika wakati wa kifo changu nikawa sijaeleza nilichonacho ndani ya moyo, na ndio maana nimefanya hivin kabla ya maoni yangu na mawazo yangu hayajapungukiwa, kama ilivyo katika mwili wangu (kutokana na kupita kwa wakati na umri) na kabla ya matamanio na fitina za ulimwengu hazijakushambulia na hivyo kuwa vigumu kuepuka. Na kwa kuwa moyo wa ujana ni kama ardhi tupu na kila mbegu iliyonyunyiziwa ndani yake itaiota na kuikubali, hivyo kabla ya moyo wako kuwa mgumu na akili yako haijashughulishwa na mambo mengine (nimesema mambo yanayopaswa kusemwa), yote haya ni ili uharakishe katika kuyapokea mambo ya dharura ambayo wanafikra na watu wenye uzoefu wamekufanya usiwe na ulazima wa kuuliza na wamechukua taabu ya kuipima ili usihitaji kuuliza na kutafuta na kujisikia unafuu kutokana na juhudi zaidi. Kwa hiyo, kile ambacho tumepewa kutokana na uzoefu wetu pia kitatolewa kwako (bila jitihada yoyote), na labda sehemu ya kile kilichofichwa kutoka kwetu (pamoja na kupita kwa wakati na uzoefu zaidi) kitakuwa wazi na chenye kueleweka kwako.

أَی بُنَی، إِنِّی وَإِنْ لَمْ أَكُنْ عُمِّرْتُ عُمُرَ مَنْ كَانَ قَبْلِی، فَقَدْ نَظَرْتُ فِی أَعْمَالِهِمْ، فَكَّرْتُ فِی أَخْبَارِهِمْ، وَسِرْتُ فِی آثَارِهِمْ، حَتَّی عُدْتُ كَأَحَدِهِمْ; بَلْ كَأَنِّی بِمَا انْتَهَی إِلَی مِنْ أُمُورِهِمْ قَدْ عُمِّرْتُ مَعَ أَوَّلِهِمْ إِلَی آخِرِهِمْ، فَعَرَفْتُ صَفْوَ ذَلِكَ مِنْ كَدَرِهِ، وَنَفْعَهُ مِنْ ضَرَرِهِ، فَاسْتَخْلَصْتُ لَكَ مِنْ كُلِّ أَمْر نَخِیلَهُ، وَتَوَخَّیتُ لَكَ جَمِیلَهُ، وَصَرَفْتُ عَنْكَ مَجْهُولَهُ، وَرَأَیتُ حَیثُ عَنَانِی مِنْ أَمْرِكَ مَا یعْنِی الْوَالِدَ الشَّفِیقَ، وَأَجْمَعْتُ عَلَیهِ مِنْ أَدَبِكَ أَنْ یكُونَ ذَلِكَ وَأَنْتَ مُقْبِلُ الْعُمُرِ وَمُقْتَبَلُ الدَّهْرِ، ذُو نِیة سَلِیمَة، وَنَفْس صَافِیة. Mwanangu! Ingawa sijaishi muda mrefu kama wale wote walioishi kabla yangu, lakini nilitoa maoni juu ya tabia zao na nilifikiri juu ya habari zao, na nilisafiri katika kazi zao zilizobaki mpaka (kutokana na mafundisho haya) nikawa kama mmoja wao. Ni kana kwamba nimekuwa nao wote tangu mwanzo hadi mwisho kutokana na yale yaliyonifikia kutoka katika historia yao (niliyachunguza yote haya baadaye) na kutenganisha sehemu ya wazi na safi na sehemu ya giza. Niliitambua tena na kujua faida na hasara zake. Kisha nikachukua kutoka kwa kila kitu kilicho bora zaidi kwa ajili yako, na nikakuchagulieni kutoka miongoni mwayo (mabaya na mazuri), na nikaweka mbali na wewe vitu visivyojulikana, na ambavyo baba mwema anamtakia mema mtoto wake, mimi pia nikaona nikusomeshe kwa njia hii na niweke juhudi katika hilo, kwa sababu umri wako unaelekea mbele na siku zako zinaelekea mbele na una nia salama na roho safi. وَأَنْ أَبْتَدِئَكَ بِتَعْلِیمِ كِتَابِ اللهِ عَزَّ وَجَلَّ وَتَأْوِیلِهِ، وَشَرَائِعِ الاِْسْلاَمِ أَحْكَامِهِ، وَحَلاَلِهِ وَحَرَامِهِ، لاأُجَاوِزُ ذَلِكَ بِكَ إِلَی غَیرِهِ. ثُمَّ أَشْفَقْتُ أَنْ یلْتَبِسَ عَلَیكَ مَا اخْتَلَفَ النَّاسُ فِیهِ مِنْ أَهْوَائِهِمْ وَ آرَائِهِمْ مِثْلَ الَّذِی الْتَبَسَ عَلَیهِمْ، فَكَانَ إِحْكَامُ ذَلِكَ عَلَی مَا كَرِهْتُ مِنْ تَنْبِیهِكَ لَهُ أَحَبَّ إِلَی مِنْ إِسْلاَمِكَ إِلَی أَمْر لاآمَنُ عَلَیكَ بِهِ الْهَلَكَةَ، وَرَجَوْتُ أَنْ یوَفِّقَكَ اللهُ فِیهِ لِرُشْدِكَ، وَأَنْ یهْدِیكَ لِقَصْدِكَ فَعَهِدْتُ إِلَیكَ وَصِیتِی هَذِهِ.

Na niliona awali nikufundishe Kitabu cha Mwenyezi Mungu pamoja na tafsiri yake na kanuni zake na hukumu zake na halali yake na haramu, na sikukutuma kwa chochote isipokuwa hicho (ambacho kinaweza kuwa chanzo cha upotofu), basi niliogopa kwamba yale ambayo watu wameshukiwa kutokana na kufuata matamanio na dhana na maoni ya uwongo na wakahitilafiana kuhusu hilo, nawe pia yanaweza kukutia katika shaka. Ni kwa sababu hiyo, niliona ni muhimu kufafanua sehemu hii, ingawa sikutaka kueleza (mashaka) kwa uwazi, lakini kuyataja lilikuwa jambo la kupendeza zaidi kwangu kuliko kukufanya nikusalimishe kwa kitu ambacho siko salama kutokana na uharibifu. Natumaini kwamba Mungu atakupa mafanikio kupitia kukua na wema na kukuongoza kwenye njia inayokufaa, ndiyo maana nikakubainishia wasia wangu huu.

وَاعْلَمْ یا بُنَی أَنَّ أَحَبَّ مَا أَنْتَ آخِذٌ بِهِ إِلَی مِنْ وَصِیتِی تَقْوَی اللهِ الاِقْتِصَارُ عَلَی مَا فَرَضَهُ اللهُ عَلَیكَ، وَالاَْخْذُ بِمَا مَضَی عَلَیهِ الاَْوَّلُونَ مِنْ آبَائِكَ، الصَّالِحُونَ مِنْ أَهْلِ بَیتِكَ، فَإِنَّهُمْ لَمْ یدَعُوا أَنْ نَظَرُوا لاَِنْفُسِهِمْ كَمَا أَنْتَ نَاظِرٌ، وَفَكَّرُوا كَمَا أَنْتَ مُفَكِّرٌ، ثُمَّ رَدَّهُمْ آخِرُ ذَلِكَ إِلَی الاَْخْذِ بِمَا عَرَفُوا، الاِْمْسَاكِ عَمَّا لَمْ یكَلَّفُوا، فَإِنْ أَبَتْ نَفْسُكَ أَنْ تَقْبَلَ ذَلِكَ دُونَ أَنْ تَعْلَمَ كَمَا عَلِمُوا فَلْیكُنْ طَلَبُكَ ذَلِكَ بِتَفَهُّم وَتَعَلُّم، لابِتَوَرُّطِ الشُّبُهَاتِ، وَعُلَقِ الْخُصُومَاتِ. Mwanangu! tambua kwamba jambo linalopendwa zaidi na unalopaswa kushikamana nalo miongoni mwa wasia wangu ni taqwa na uchamungu, na kuridhika na yale ambayo Mwenyezi Mungu ameyaona kuwa ni faradhi na muhimu kwako, na kutembea katika njia ambayo baba zako waliifuata zamani na watu wema kutoka katika familia yako; kwa sababu kama ambavyo wewe unafikiri juu yako, pia walifikiri juu yao, na jinsi unavyofikiri (kwa manufaa yako), wao pia walikuwa wakifikiri hilo (kwa tofauti hii kwamba, wamekuachia upoefu wao kama kumbukumbu). Mwishoni, mawazo na fikra huwaleta mahali ambapo wanachukua kile wanachokijua vizuri na kuacha kile (ambacho hakieleweki na) na ambacho hawajakalifishwa. Iwapo roho na nafsi yako vinasitasita kulikubali na unataka kutochukua hatua mpaka uwe na ufahamu, unapaswa (kuifuata njia hii kupitia njia iliyo sawa na) ombi hili liwe kwa ufahamu, usahihi na kujifunza, na si kwa kutumbukia katika mashaka na kung'ang'ania uadui na chuki.

وَابْدَأْ قَبْلَ نَظَرِكَ فِی ذَلِكَ بِالاِْسْتِعَانَةِ بِإِلَهِكَ، وَالرَّغْبَةِ إِلَیهِ فِی تَوْفِیقِكَ، وَتَرْكِ كُلِّ شَائِبَة أَوْلَجَتْكَ فِی شُبْهَة، أَوْ أَسْلَمَتْكَ إِلَی ضَلاَلَة .فَإِنْ أَیقَنْتَ أَنْ قَدْ صَفَا قَلْبُكَ فَخَشَعَ، وَتَمَّ رَأْیكَ فَاجْتَمَعَ، وَكَانَ هَمُّكَ فِی ذَلِكَ هَمّاً وَاحِداً، فَانْظُرْ فِیمَا فَسَّرْتُ لَكَ، وَإِنْ لَمْ یجْتَمِعْ لَكَ مَا تُحِبُّ مِنْ نَفْسِكَ، وَفَرَاغِ نَظَرِكَ وَفِکْرِكَ، فَاعْلَمْ أَنَّكَ إِنَّمَا تَخْبِطُ الْعَشْوَاءَ، وَتَتَوَرَّطُ الظَّلْمَاءَ. وَلَیسَ طَالِبُ الدِّینِ مَنْ خَبَطَ أَوْ خَلَطَ وَالاِْمْسَاكُ عَنْ ذَلِكَ أَمْثَلُ.

(Pamoja na hayo) kabla ya kupiga hatua katika mambo haya kupitia weledi na ufahamu, muombe msaada Mungu wako ili akupe tawfiki na akuonyeshe raghba na akuepushe na jambo lolote ambalo linakutia katika utata na shaka au kukusalimisha katika upotofu. Utakapokuwa na yakini kwamba moyo wako na nafsi yako vimetakaswa, inyenyekee haki, na maoni yako yameunganishwa ukamilifu na yamejikita katika hilo, na uamuzi wako umekuwa uamuzi mmoja (na umeacha kila kitu kingine), katika hali hii, fuata niliyokueleza (katika wasia huu), kuwa makini (ili upate matokeo yanayofaa) na ikiwa hujakipata unachokipenda katika muktadha huu (kutoka katika masharti niliyosema), na haukupata wakati wa faragha na haujapatikana utayari wa mawazo, kwa hivyo tambua kwamba, unapiga hatua katika njia ambayo mithili ya ngamia ambaye macho yake ni dhaifu, unaelekea shimoni na unatumbukizwa gizani, na yule ambaye amenasa katika kosa na mkanganyiko wa haki na batili hawezi kuwa mtafutaji wa dini na kwa hili ni bora ikiwa hautaingia katika hatua hii. فَتَفَهَّمْ یا بُنَی وَصِیتِی، وَاعْلَمْ أَنَّ مَالِكَ الْمَوْتِ هُوَ مَالِكُ الْحَیاةِ، وَأَنَّ الْخَالِقَ هُوَ الْمُمِیتُ، وَأَنَّ الْمُفْنِی هُوَ الْمُعِیدُ، وَأَنَّ الْمُبْتَلِی هُوَ الْمُعَافِی، وَأَنَّ الدُّنْیا لَمْ تَكُنْ لِتَسْتَقِرَّ إِلاَّ عَلَی مَا جَعَلَهَا اللهُ عَلَیهِ مِنَ النَّعْمَاءِ، وَالاِْبْتِلاَءِ، وَالْجَزَاءِ فِی الْمَعَادِ، أَوْ مَا شَاءَ مِمَّا لاتَعْلَمُ، فَإِنْ أَشْكَلَ عَلَیكَ شَیءٌ مِنْ ذَلِكَ فَاحْمِلْهُ عَلَی جَهَالَتِكَ، فَإِنَّكَ أَوَّلُ مَا خُلِقْتَ بِهِ جَاهِلاً ثُمَّ عُلِّمْتَ، وَمَا أَکْثَرَ مَا تَجْهَلُ مِنَ الاَْمْرِ، یتَحَیرُ فِیهِ رَأْیكَ، وَیضِلُّ فِیهِ بَصَرُكَ ثُمَّ تُبْصِرُهُ بَعْدَ ذَلِكَ! فَاعْتَصِمْ بِالَّذِی خَلَقَكَ وَرَزَقَكَ وَسَوَّاكَ، وَلْیكُنْ لَهُ تَعَبُّدُكَ، وَإِلَیهِ رَغْبَتُكَ، وَمِنْهُ شَفَقَتُكَ.

Mwanangu! Kuwa makini katika kuelewa wasia wangu. Tambua kwamba, Mwenye kumiliki mauti ndiye mmiliki wa uzima, na Muumbaji ndiye mwenye kufisha, na mwenye kufisha ndiye Mwenye kuirejesha dunia, na mwenye kutoa maradhi ndiye Mwenye kuponyesha, na dunia haibakii ikiwa imesimama isipokuwa kama Mungu alivyoiweka; kuna wakati kuna neema, wakati fulani shida na hatimaye malipo Siku ya Kiyama au aliyoyataka wewe huyajui (ya adhabu za dunia) na kama itakuwia vigumu kuelewa mambo haya (na matukio ya dunia), lijaalie kuwa ni kutokana na ujinga wako. Kwa sababu ulikuwa mjinga na jahili mwanzoni mwa kuumbwa kwako, kisha ukawa na ujuzi na ufahamu, na kuna mambo mengi ambayo bado huyajui, na akili yako inachanganyikiwa na macho yako yanafanya makosa ndani yake; lakini baada ya muda utaiona (na utajua hekima yake). Kwa hivyo shikamana na aliyekuumba na akakupa riziki na akaratibisha(kuwa wenye nidhamu) uumbaji wako na muabudu yeye peke yake, na huba na raghba yako iwe kwa ajili yake tu na muogope yeye tu.

وَاعْلَمْ یا بُنَی أَنَّ أَحَداً لَمْ یُنْبِئْ عَنِ اللهِ سُبْحَانَهُ كَمَا أَنْبَأَ عَنْهُ الرَّسُولُ(صلی الله علیه وآله)فَارْضَ بِهِ رَائِداً، وَإِلَی النَّجَاةِ قَائِداً، فَإِنِّی لَمْ آلُكَ نَصِیحَةً. وَإِنَّكَ لَنْ تَبْلُغَ فِی النَّظَرِ لِنَفْسِكَ وَإِنِ اجْتَهَدْتَ مَبْلَغَ نَظَرِی لَكَ.

Mwanangu! Fahamu kwamba hakuna aliyejulisha juu ya Mwenyezi Mungu kama Mtume wa Uislamu (saww) (na hakuna aliebainisha maamrisho ya Mwenyezi Mungu kama yeye), basi mkubali kuwa kiongozi wako na mchague awe kiongozi wako katika njia ya wokovu na ukweli. Kwa hakika mimi sijatembea hata kidogo katika ushauri wowote kuhusu wewe, na haijalishi ni kiasi gani unajaribu kujua faida na manufaa yako mwenyewe, hutafikia vile nilivyotambua kukuhusu. وَاعْلَمْ یا بُنَی أَنَّهُ لَوْ كَانَ لِرَبِّكَ شَرِیکٌ لاََتَتْكَ رُسُلُهُ، وَلَرَأَیتَ آثَارَ مُلْكِهِ سُلْطَانِهِ، وَلَعَرَفْتَ أَفْعَالَهُ وَصِفَاتِهِ، وَلَكِنَّهُ إِلَهٌ وَاحِدٌ كَمَا وَصَفَ نَفْسَهُ، لایضَادُّهُ فِی مُلْكِهِ أَحَدٌ، وَلاَ یزُولُ أَبَداً وَلَمْ یزَلْ. أَوَّلٌ قَبْلَ الاَْشْیاءِ بِلاَ أَوَّلِیة، وَآخِرٌ بَعْدَ الاَْشْیاءِ بِلاَ نِهَایة. عَظُمَ عَنْ أَنْ تَثْبُتَ رُبُوبِیتُهُ بِإِحَاطَةِ قَلْب أَوْ بَصَر. فَإِذَا عَرَفْتَ ذَلِكَ فَافْعَلْ كَمَا ینْبَغِی لِمِثْلِكَ أَنْ یفْعَلَهُ فِی صِغَرِ خَطَرِهِ، وَقِلَّةِ مَقْدِرَتِهِ، وَكَثْرَةِ عَجْزِهِ، و عَظِیمِ حَاجَتِهِ إِلَی رَبِّهِ، فِی طَلَبِ طَاعَتِهِ، وَالْخَشْیةِ مِنْ عُقُوبَتِهِ، وَالشَّفَقَةِ مِنْ سُخْطِهِ: فَإِنَّهُ لَمْ یأْمُرْكَ إِلاَّ بِحَسَن، وَلَمْ ینْهَكَ إِلاَّ عَنْ قَبِیح. Mwanangu! Jua kwamba lau Mola wako Mlezi angekuwa na mshirika, wangekujia Mitume Wake na ungeona athari za milki Yake na uwezo wake na ungejua matendo yake na sifa zake. Lakini Yeye ndiye Mungu pekee kwani amejieleza Mwenyewe kwa sifa hii. Hakuna anayempinga katika milki yake, na katu hatatoweka na amekuwa hivyo daima. Yeye ndiye kichwa cha mnyororo wa maisha bila ya kuwa na mwanzo na yeye ndiye wa mwisho wao bila ya kuwa na mwisho. Ni mkubwa mno kwa Uola wake kuzungukwa na mawazo au jicho. Sasa kwa kuwa umeujua ukweli huu, jaribu kutenda unavyostahiki katika suala la udogo wa utu na heshima na nguvu ndogo na ongezeko la unyonge wako na haja kubwa kwa Mola wako. Jaribu kumtii, jihadhari na adhabu zake, na uogope hasira yake, kwa sababu yeye amekuamrisha tu kufanya mema na hakukukatazeni kufanya chochote isipokuwa baya na lisilofaa. یا بُنَی إِنِّی قَدْ أَنْبَأْتُكَ عَنِ الدُّنْیا وَحَالِهَا، وَزَوَالِهَا وَانْتِقَالِهَا، وَأَنْبَأْتُكَ عَنِ الاْخِرَةِ وَمَا أُعِدَّ لاَِهْلِهَا فِیهَا، وَضَرَبْتُ لَكَ فِیهِمَا الاَْمْثَالَ، لِتَعْتَبِرَ بِهَا وَتَحْذُوَ عَلَیهَا. إِنَّمَا مَثَلُ مَنْ خَبَرَ الدُّنْیا كَمَثَلِ قَوْم سَفْر نَبَا بِهِمْ مَنْزِلٌ جَدِیبٌ، فَأَمُّوا مَنْزِلاً خَصِیباً وَجَنَاباً مَرِیعاً، فَاحْتَمَلُوا وَعْثَاءَ الطَّرِیقِ، وَفِرَاقَ الصَّدِیقِ، خُشُونَةَ السَّفَرِ، وَجُشُوبَةَ المَطْعَمِ، لِیأْتُوا سَعَةَ دَارِهِمْ، وَمَنْزِلَ قَرَارِهِمْ، فَلَیسَ یجِدُونَ لِشَیءٍ مِنْ ذَلِكَ أَلَماً، وَلاَ یرَوْنَ نَفَقَةً فِیهِ مَغْرَماً. وَلاَ شَیءَ أَحَبُّ إِلَیهِمْ مِمَّا قَرَّبَهُمْ مِنْ مَنْزِلِهِمْ، وَأَدْنَاهُمْ مِنْ مَحَلَّتِهِمْ. Mwanganu! Nimekufahamisha dunia na hali zake na kudorora kwake na kubadilika kwake, na nikakupa habari ya Akhera na yale ambayo yametayarishwa kwa ajili ya watu wake ndani yake, na nikakupa mifano katika yote mawili ili ujifunze kutoka kwayo na utembee na kupiga hatua katika njia sahihi. Wale ambao wameijaribu dunia vizuri (wanajua kwamba wao) ni kama wasafiri walioingia kwenye makazi yasiyo na maji na yasiyokaliwa na watu (ambayo hayafai kuishi na kukaa), kwa hiyo wameamua kuelekea kwenye nyumba yenye neema nyingi na eneo la raha (kwa ajili ya kuishi). Kwa muktadha huo, (ili wao wafike katika nyumba hiyo) walistahimili taabu za barabara na wakakubali kutenganishwa na marafiki na wakakubali utumiaji mabavu na ugumu wa safari na chakula kisichopendeza (kwa nyoyo na nafsi zao), ili wapige hatua kuelekea katika nyumba kubwa na makao ya utulivu. Ni wa sababu hiyo, hawasikii uchungu na mateso yoyote kutokana na usumbufu wowote ule, na hawaoni gharama wanazolipa katika njia hii kuwa ni hasara, na hakuna kitu wanachopenda zaidi kuliko kuwaleta karibu na nyumba yao na mahali pao pa utulivu. (Lakini) watu ambao wameghurika na kuhadaika na dunia ni kama wasafiri waliokaa katika nyumba yenye neema nyingi, kisha wanapewa habari kwamba inabidi wahamie kwenye nyumba kavu isiyo na neema, (ni wazi kuwa) kwao hili ni jambo lisilofurahisha kabisa na ni msiba mzito zaidi kuliko kutengana na kile walichokuwa ndani yake na ni kufanya harakati kuelekea upande ambao ndani yake hakuna mchakato na hatima mbele. یا بُنَیَّ، اِجْعَلْ نَفْسَكَ مِیزَاناً فِیمَا بَینَكَ وَبَینَ غَیرِكَ، فَأَحْبِبْ لِغَیرِكَ مَا تُحِبُّ لِنَفْسِكَ، وَاکْرَهْ لَهُ مَا تَکْرَهُ لَهَا، وَلاَ تَظْلِمْ كَمَا لاتُحِبُّ أَنْ تُظْلَمَ، وَأَحْسِنْ كَمَا تُحِبُّ أَنْ یحْسَنَ إِلَیكَ، وَاسْتَقْبِحْ مِنْ نَفْسِكَ مَا تَسْتَقْبِحُهُ مِنْ غَیرِكَ، وَارْضَ مِنَ النَّاسِ بِمَا تَرْضَاهُ لَهُمْ مِنْ نَفْسِكَ، وَلاَ تَقُلْ مَا لاتَعْلَمُ، وَإِنْ قَلَّ مَا تَعْلَمُ وَلاَ تَقُلْ مَا لاتُحِبُّ أَنْ یقَالَ لَكَ. (Mwanangu!) Jua kwamba kujiona, kujikweza na kiburi ni kinyume cha ukweli na kufikiri sahihi na ni janga la akili, basi fanya uwezavyo ili upate maisha (na toa kile unachochuma katika njia ya Mwenyezi Mungu na) kuwa mhifadhi wa wengine. Unapoongoka kwenye njia iliyonyooka (kwa neema ya Mwenyezi Mungu) (usisahau kumshukuru Mungu na) kuwa mnyenyekevu kabisa na kunyenyekea mbele ya Mola wako.

وَاعْلَمْ أَنَّ أَمَامَكَ طَرِیقاً ذَا مَسَافَةٍ بَعِیدَة، وَمَشَقَّة شَدِیدَة، وَأَنَّهُ لاغِنَی بِكَ فِیهِ عَنْ حُسْنِ الاِرْتِیادِ، وَقَدْرِ بَلاَغِكَ مِنَ الزَّادِ، مَعَ خِفَّةِ الظَّهْرِ، فَلاَ تَحْمِلَنَّ عَلَی ظَهْرِكَ فَوْقَ طَاقَتِكَ، فَیكُونَ ثِقْلُ ذَلِكَ وَبَالاً عَلَیكَ، وَإِذَا وَجَدْتَ مِنْ أَهْلِ الْفَاقَةِ مَنْ یحْمِلُ لَكَ زَادَکْ إِلَی یوْمِ الْقِیامَةِ، فَیوَافِیكَ بِهِ غَداً حَیثُ تَحْتَاجُ إِلَیهِ فَاغْتَنِمْهُ وَحَمِّلْهُ إِیاهُ، وَأَکْثِرْ مِنْ تَزْوِیدِهِ وَأَنْتَ قَادِرٌ عَلَیهِ، فَلَعَلَّكَ تَطْلُبُهُ فَلاَ تَجِدُهُ وَاغْتَنِمْ مَنِ اسْتَقْرَضَكَ فِی حَالِ غِنَاكَ، لِیجْعَلَ قَضَاءَهُ لَكَ فِی یوْمِ عُسْرَتِكَ. (Mtoto wangu!) tambua kwamba, mbele yako kuna njia ndefu na ngumu. Katika njia hii (iliyojaa hofu na hatari), bila shaka unahitaji bidii nyingi na mizigo (ya mahitaji) ya kutosha kukufikisha (uendako) kituoni kwako, zaidi ya hayo, lazima uwe na uzito mwepesi kwenye njia hii (ili uweze kufikia makusidio yako (uendako), kwa hivyo usijiwekee majukumu mali ya dunia katika mabega yako kuliko uwezo wako, kwani uzito wake utakuwa chanzo cha shida na mashaka kwako. Kila unapompata mhitaji ambaye anaweza kubeba mali yako kwa ajili ya Siku ya Kiyama na kukurudishia kesho unapohitaji, lichukulie hilo kuwa ni fursa na ghanima na (fanya haraka iwezekanavyo) na zaidi, kuweka mzigo huo katika mabega yake, kwani yumkini siku moja ukamtafuta mtu kama huyo na usimpate. (Pia) tumia fursa ya kumkopesha mtu anayetaka mkono hali ya kuwa wewe ni tajiri na mhitaji akakulipa kwa ajili ya siku yako ya dhiki na umasikini na lihesabu hilo kama ni gahina na neema!

وَاعْلَمْ أَنَّ أَمَامَكَ عَقَبَةً كَئُوداً، الْمُخِفُّ فِیهَا أَحْسَنُ حَالاً مِنَ الْمُثْقِلِ، وَالْمُبْطِئُ عَلَیهَا أَقْبَحُ حَالاً مِنَ الْمُسْرِعِ، وَأَنَّ مَهْبِطَكَ بِهَا لامَحَالَةَ إِمَّا عَلَی جَنَّة أَوْ عَلَی نَار، فَارْتَدْ لِنَفْسِكَ قَبْلَ نُزُولِكَ، وَوَطِّئِ الْمَنْزِلَ قَبْلَ حُلُولِكَ، «فَلَیسَ بَعْدَ الْمَوْتِ مُسْتَعْتَبٌ»، وَلاَ إِلَی الدُّنْیا مُنْصَرَفٌ. (Mwanangu!) tambua kwamba, mbele yako kuna njia ngumu, ambapo mwepesi hali yake ni bora kuliko mzito, na mwenye mwendo wa polepole ana hali mbaya zaidi kuliko mwenye kasi, na (jua kwamba) kushuka kwako baada ya kuvuka kwa hakika ni peponi au motoni. Hivyo basi kabla ya kuingia huko jiandalie vifaa muhimu na uandae makazi yako kabla ya kushuka, kwa sababu baada ya kifo hakuna njia ya kuomba msamaha na hakuna na njia ya kurudi ulimwengu (na kurekebisha au kufidia yaliyopita).

وَاعْلَمْ أَنَّ الَّذِی بِیدِهِ خَزَائِنُ السَّمَاوَاتِ وَالاَْرْضِ قَدْ أَذِنَ لَكَ فِی الدُّعَاءِ، تَكَفَّلَ لَكَ بِالاِْجَابَةِ، وَأَمَرَكَ أَنْ تَسْأَلَهُ لِیعْطِیكَ، وَتَسْتَرْحِمَهُ لِیرْحَمَكَ، وَلَمْ یجْعَلْ بَینَكَ وَبَینَهُ مَنْ یحْجُبُكَ عَنْهُ، وَلَمْ یلْجِئْكَ إِلَی مَنْ یشْفَعُ لَكَ إِلَیهِ، وَلَمْ یمْنَعْكَ إِنْ أَسَأْتَ مِنَ التَّوْبَةِ، وَلَمْ یعَاجِلْكَ بِالنِّقْمَةِ، وَلَمْ یُعَیِّرْكَ بِالاِْنَابَةِ، وَلَمْ یفْضَحْكَ حَیثُ الْفَضِیحَةُ بِكَ أَوْلَی، وَلَمْ یُشَدِّدْ عَلَیكَ فِی قَبُولِ الاِْنَابَةِ، وَلَمْ یُنَاقِشْكَ بِالْجَرِیمَةِ وَلَمْ یُؤْیسْكَ مِنَ الرَّحْمَةِ، بَلْ جَعَلَ نُزُوعَكَ عَنِ الذَّنْبِ حَسَنَةً، وَحَسَبَ سَیَّئَتَكَ وَاحِدَةً، وَحَسَبَ حَسَنَتَكَ عَشْراً، وَفَتَحَ لَكَ بَابَ الْمَتَابِ، وَبَابَ الاِسْتِعْتَابِ،

(Mtoto wangu!) fahamu kwamba yule ambaye ana hazina za mbingu na ardhi mkononi mwake, amekupa ruhusa ya kuomba dua na amekuhakikishia kujibu takwa hilo, akakuamrisha kumuomba ili akupe na omba rehma kutoka Kwake ili ujumuishwe katika rehema Zake. Mwenyezi Mungu hakumuweka mtu baina yako na nafsi yake ili awe pazia lako mbele yake, na wala hakukulazimisha kutafuta hifadhi kwa muombezi, na Mwenyezi Mungu hakukuzuia kutubu ukifanya uovu (na amekufungulia milango yake). Hakukuharakishia adhabu yako (na akaichelewesha kwa sababu ya kuwa utatubu), wala Yeye kamwe hakulaumu kwa kutubia na kurejea Kwake (kama vile walipizaji kisasi wanavyowaweka watu waliotubu kwenye safu ya lawama) na hata pale unapostahiki fedheham hakukufedhehesha na kukuumbua (kama watu wenye mawazo finyu wanavyoanza mara moja kuumbua na kuwafichua wakosaji) na wala hakuwa mgumu kwako katika kukubali toba (kama ilivyo kawaida kwa watu wenye fikra fupi) na wala hakuwa umakini na kuchunguza kwa undani mno katika kuhesabu makosa yako (badala yake amepita kirahisi). Hakuna wakati ambao alikukatisha tamaa na rehema yake (ijapokuwa dhambi yako ni nzito na kubwa), bali amekufanya kurudi kwako kutoka katika dhambi kuwa ni jambo zuri (na muhimu zaidi) anaihesabu dhambi yako kuwa ni moja na analihesabu jema lako moja mara kumi na ameacha wazi daima kwako mlango wa toba, marejeo na msamaha kwako ili kila umwitapo asikie wito wako.

فَإِذَا نَادَیتَهُ سَمِعَ نِدَاكَ، وَإِذَا نَاجَیتَهُ عَلِمَ نَجْوَاكَ، فَأَفْضَیتَ إِلَیهِ بِحَاجَتِكَ، وَأَبْثَثْتَهُ ذَاتَ نَفْسِكَ، وَشَكَوْتَ إِلَیهِ هُمُومَكَ، اسْتَکْشَفْتَهُ كُرُوبَكَ، وَاسْتَعَنْتَهُ عَلَی أُمُورِكَ، وَسَأَلْتَهُ مِنْ خَزَائِنِ رَحْمَتِهِ مَا لایقْدِرُ عَلَی إِعْطَائِهِ غَیرُهُ، مِنْ زِیادَةِ الاَْعْمَارِ، وَصِحَّةِ الاَْبْدَانِ، سَعَةِ الاَْرْزَاقِ. ثُمَّ جَعَلَ فِی یدَیكَ مَفَاتِیحَ خَزَائِنِهِ بِمَا أَذِنَ لَكَ فِیهِ مِنْ مَسْأَلَتِهِ، فَمَتَی شِئْتَ اسْتَفْتَحْتَ بِالدُّعَاءِ أَبْوَابَ نِعْمَتِهِ، وَاسْتَمْطَرْتَ شَآبِیبَ رَحْمَتِهِ Basi utakapomuita anasikia mwito wako na unaponong’ona, yeye anajua, kwa hivyo peleka mahitaji yako Kwake na kujionyesha kama uko mbele Yake, mshirikishe katika ghamu na huzuni yako na umwombe atatue shida na uchungu wako, na utafute msaada kutoka Kwake katika kazi yako, unaweza kuomba kutoka katika hazina za rehema Yake kwa vitu ambavyo hakuna mtu isipokuwa yeye anayeweza kukupa, kama vile kuongezeka kwa umri, afya ya mwili na upana wa riziki. Kisha Mwenyezi Mungu ameweka funguo za hazina Yake mikononi mwako kwa kibali alichokupa cha kumuomba, hivyo kila unapotaka, unaweza kufungua milango ya baraka za Mungu kwa njia ya maombi na mvua ya rehma Zake itanyesha.

فَلاَ یقَنِّطَنَّكَ إِبْطَاءُ إِجَابَتِهِ، فَإِنَّ الْعَطِیةَ عَلَی قَدْرِ النِّیةِ، وَرُبَّمَا أُخِّرَتْ عَنْكَ الاِْجَابَةُ، لِیكُونَ ذَلِكَ أَعْظَمَ لاَِجْرِ السَّائِلِ، وَأَجْزَلَ لِعَطَاءِ الاْمِلِ. وَرُبَّمَا سَأَلْتَ الشَّیءَ فَلاَ تُؤْتَاهُ، وَأُوتِیتَ خَیراً مِنْهُ عَاجِلاً أَوْ آجِلاً، أَوْ صُرِفَ عَنْكَ لِمَا هُوَ خَیرٌ لَكَ، فَلَرُبَّ أَمْر قَدْ طَلَبْتَهُ فِیهِ هَلاَكُ دِینِكَ لَوْ أُوتِیتَهُ، فَلْتَكُنْ مَسْأَلَتُكَ فِیمَا یَبْقَی لَكَ جَمَالُهُ، وَینْفَی عَنْكَ وَبَالُهُ; فَالْمَالُ لایبْقَی لَكَ وَلاَ تَبْقَی لَه. Na kuchelewa kujibiwa maombi yako kusikukatishe tamaa, kwa sababu ataa na utoaji wa Mola ni kwa kiwango cha nia na makusudio ya (waja); kuna wakati jibu la maombi hucheleweshwa ili ujira na thawabu za mwombaji ziongezeke na ataa (zawadi) ya wanaotaka iongezeke na wakati mwingine unamwomba Mungu kitu na hakupi, huku akikupa kilicho bora zaidi katika muda mfupi au kwa muda mrefu au kugeuka kuwa kitu ambacho ni bora kwako kuliko hicho. Wakati fulani unamwomba Mungu kitu ambacho ukikipata kitaharibu dini yako (na Mungu atakuzuilia na kukupa kilicho bora kuliko hicho), hivyo ombi lako kutoka kwa Mungu daima liwe ni jambo litakalobaki kuwa zuri kwako. Mwache akuache (na ujue kuwa utajiri wa dunia hauko hivi) utajiri hautabaki kwako na hutabaki kwa ajili mali pia!

وَاعْلَمْ یا بُنَی أَنَّكَ إِنَّمَا خُلِقْتَ لِلاْخِرَةِ لالِلدُّنْیا، وَلِلْفَنَاءِ لالِلْبَقَاءِ، وَلِلْمَوْتِ لالِلْحَیاةِ، وَأَنَّكَ فِی قُلْعَة وَدَارِ بُلْغَة، وَطَرِیقٍ إِلَی الاْخِرَةِ، وَأَنَّكَ طَرِیدُ الْمَوْتِ الَّذِی لاینْجُو مِنْهُ هَارِبُهُ، وَلاَ یفُوتُهُ طَالِبُهُ، وَلاَ بُدَّ أَنَّهُ مُدْرِكُهُ، فَكُنْ مِنْهُ عَلَی حَذَرِ أَنْ یدْرِكَكَ وَأَنْتَ عَلَی حَال سَیئَة، قَدْ كُنْتَ تُحَدِّثُ نَفْسَكَ مِنْهَا بِالتَّوْبَةِ، فَیحُولَ بَینَكَ وَبَینَ ذَلِكَ، فَإِذَا أَنْتَ قَدْ أَهْلَکْتَ نَفْسَكَ. (Mwanangu!) Jua kwamba umeumbwa kwa ajili ya akhera, si kwa ajili ya dunia hii, kwa ajili ya kwisha (kuangamia), si kwa ajili ya kuishi (duniani), kwa ajili ya kifo, si kwa ajili ya uhai (katika dunia hii). Wewe upo katika makao ambayo wakati wowote yumkini ukahama, upo sehemu ambayo unapaswa kupakia mizigo na kukusanya masurufu na njia ya akhera ni yako. Na (ujue) unasukumwa na mauti (na mauti yanakuwinda na hatimaye yatakupata), kifo kile kile ambacho hakuna akikimbiaye atakayeokolewa kutoka humo, na hakitampoteza yeyote kinachomtafuta, na hatimaye kitamkamata. Kwa hiyo, ogopa kwamba mauti yasikupate ukiwa katika hali mbaya (hali ya dhambi) ikiwa ulikuwa unajisemea kabla ya kifo kwamba, utatubu; lakini kifo kinasimama kati yako na toba, na hapa ndipo umejitupa kwenye uharibifu. یا بُنَیَّ أَکْثِرْ مِنْ ذِکْرِ الْمَوْتِ، وَذِکْرِ مَا تَهْجُمُ عَلَیهِ، وَتُفْضِی بَعْدَ الْمَوْتِ إِلَیهِ، حَتَّی یأْتِیكَ وَقَدْ أَخَذْتَ مِنْهُ حِذْرَكَ، وَشَدَدْتَ لَهُ أَزْرَكَ، وَلاَ یأْتِیكَ بَغْتَةً فَیبْهَرَكَ. Mwanangu! Kumbuka sana mauti na kumbuka unaloliendea na utakalokuwa nalo baada ya kufa kwa namna ambayo wakati wowote kifo kitakapokujia, uwe umejiandaa kwa kila hali, na jifunge mshipi wa moyo mkabala wake, yasije yakakujia ghafla na kukushinda. وَإِیاكَ أَنْ تَغْتَرَّ بِمَا تَرَی مِنْ إِخْلاَدِ أَهْلِ الدُّنْیا إِلَیهَا، وَتَكَالُبِهِمْ عَلَیهَا، فَقَدْ نَبَّأَكَ اللهُ عَنْهَا، وَنَعَتْ هِی لَكَ عَنْ نَفْسِهَا، وَتَكَشَّفَتْ لَكَ عَنْ مَسَاوِیهَا Na jihadhari mno, mshikamano wa watu wa kidunia na shauku kubwa ya dunia na tamaa yao ya pupa juu ya dunia yasije yakakuhadaa na kukufanya upate kiburi, kwa sababu Mwenyezi Mungu amekujulisha hali ya dunia na dunia yenyewe imekujulisha juu maangamizo yake na kuporomoka kwake na mabaya yake.

فَإِنَّمَا أَهْلُهَا كِلاَبٌ عَاوِیةٌ، وَسِبَاعٌ ضَارِیةٌ، یَهِرُّ بَعْضُهَا عَلَی بَعْض، وَیأْكُلُ عَزِیزُهَا ذَلِیلَهَا، وَیقْهَرُ كَبِیرُهَا صَغِیرَهَا. نَعَمٌ مُعَقَّلَةٌ، وَأُخْرَی مُهْمَلَةٌ، قَدْ أَضَلَّتْ عُقُولَهَا، رَكِبَتْ مَجْهُولَهَا. سُرُوحُ عَاهَة بِوَاد وَعْث، لَیسَ لَهَا رَاع یقِیمُهَا، وَلاَ مُسِیمٌ یسِیمُهَا. Kwa hakika watu wake (wanaoabudu dunia) ni sawa na mbwa wanaobweka mfululizo (na kupiga kelele ili kuchukua chambo) au wanyama wanaotafuta kuraruana, kuunguruma na kuzomeana, wenye nguvu hula wanyonge na wakubwa huwashinda wadogo, Au ni kama ng'ombe ambao mikono na miguu yao imefungwa (na wenye kiburi) (na wao ni watumwa wao) na kundi jingine ni kama wanyama walioachwa jangwani (matamanio) waliopoteza akili zao (na wakapotea njia sahihi) na katika njia zisizojulikana. zimechukuliwa. Wao ni kama wanyama walioachwa katika bonde lililojaa mabalaa na wametanga-tanga katika nchi kavu, bila mchungaji wa kuwaongoza katika njia ifaayo, na hakuna wa kuwaongoza kwenye malisho yanayofaa.

سَلَكَتْ بِهِمُ الدُّنْیا طَرِیقَ الْعَمَی وَأَخَذَتْ بِأَبْصَارِهِمْ عَنْ مَنَارِ الْهُدَی، فَتَاهُوا فِی حَیرَتِهَا، وَغَرِقُوا فِی نِعْمَتِهَا وَاتَّخَذُوهَا رَبّاً، فَلَعِبَتْ بِهِمْ لَعِبُوا بِهَا، وَنَسُوا مَا وَرَاءَهَا. Ulimwengu umewaongoza kwenye njia ya upofu na kuyageuza macho yao yasione dalili za uongofu, matokeo yake wanatangatanga katika bonde la maajabu na kuzama katika neema na fahari za dunia, wameichagua dunia kuwa ni kitu choa cha kuabudu, na dunia pia imewafanya mchezo na pia wamefurahia kushughulishwa na kucheza na dunia na kusahau yaliyo nyuma yake.

رُوَیداً یُسْفِرُ الظَّلاَمُ، كَأَنْ قَدْ وَرَدَتِ الاَْظْعَانُ، یُوشِكُ مَنْ أَسْرَعَ أَنْ یلْحَقَ! وَاعْلَمْ یا بُنَی أَنَّ مَنْ كَانَتْ مَطِیَّتُهُ اللَّیلَ وَالنَّهَارَ، فَإِنَّهُ یُسَارُ بِهِ وَإِنْ كَانَ وَاقِفاً، وَیقْطَعُ الْمَسَافَةَ وَإِنْ كَانَ مُقِیماً وَادِعاً. Tulia (na ungoje kidogo) kwani hivi karibuni giza litaondolewa (na ukweli utadhihirika) kana kwamba wasafiri hawa wamefika nyumbani (na waone mwisho wa maisha kwa macho yao.) Anayesonga haraka yuko karibu na marudio (kifo). Mwanangu, jua kwamba yule ambaye mchanganyiko wake ni usiku na mchana, anachukuliwa na anasonga ingawa amesimama, na anakata masafa, ingawa inaonekana amesimama na kupumzika.

وَاعْلَمْ یقِیناً أَنَّكَ لَنْ تَبْلُغَ أَمَلَكَ، وَلَنْ تَعْدُوَ أَجَلَكَ، وَأَنَّكَ فِی سَبِیلِ مَنْ كَانَ قَبْلَكَ. فَخَفِّضْ فِی الطَّلَبِ. وَأَجْمِلْ فِی الْمُکْتَسَبِ، فَإِنَّهُ رُبَّ طَلَبٍ قَدْ جَرَّ إِلَی حَرَب، فَلَیسَ كُلُّ طَالِبٍ بِمَرْزُوق، وَلاَ كُلُّ مُجْمِلٍ بِمَحْرُوم. Na fahamu kwa yakini kwamba hutafikia yote unayoyatamani na (pia jua) hutavuka mpaka wako (na hutaishi muda mrefu zaidi ya ilivyoamrishwa) na uko kwenye njia sawa na walivyokuwa watangulizi wako (walikwenda na pia utaenda)) Sasa hali iko hivyo, usifanye mambo kupita kiasi katika kupata dunia na kuwa na kiasi katika biashara, kwa sababu imeonekana kwamba jitihada nyingi (katika njia ya dunia) huongoza kwenye maangamizi (fauka ya hayo), sio kila jitihada inashia kupata riziki na si kila mtu wa wastani amenyimwa.

أَکْرِمْ نَفْسَكَ عَنْ كُلِّ دَنِیَّة وَإِنْ سَاقَتْكَ إِلَی الرَّغَائِبِ، فَإِنَّكَ لَنْ تَعْتَاضَ بِمَا تَبْذُلُ مِنْ نَفْسِكَ عِوَضاً. وَلاَ تَكُنْ عَبْدَ غَیرِكَ وَقَدْ جَعَلَكَ اللهُ حُرّاً. وَمَا خَیرُ خَیرٍ لایُنَالُ إِلاَّ بِشَرّ، وَیسْر لاینَالُ إِلاَّ بِعُسْر. Ikirimu na kuiheshimu nafsi yako kunako tabia yoyote ya unyonge (na uwe mtukufu zaidi kuliko kujiingiza katika unyonge), hata kama tabia ya unyonge inakuongoza kwenye matamanio yako, kwa sababu huwezi kamwe kustahili kile unachopoteza katika tabia yako kwa njia hii usiwe mtumwa wa wengine, Mungu alikuumba huru. Jema ambalo halipatikani isipokuwa kwa ubaya si jema, na utulivu ambao haupatikani isipokuwa kwa dhiki kubwa sio utulivu.

وَإِیاكَ أَنْ تُوجِفَ بِكَ مَطَایا الطَّمَعِ، فَتُورِدَكَ مَنَاهِلَ الْهَلَكَةِ. وَإِنِ اسْتَطَعْتَ أَلاَّ یكُونَ بَینَكَ وَبَینَ اللهِ ذُو نِعْمَة فَافْعَلْ، فَإِنَّكَ مُدْرِکٌ قَسْمَكَ، وَآخِذٌ سَهْمَكَ، وَإِنَّ الْیسِیرَ مِنَ اللهِ سُبْحَانَهُ أَعْظَمُ وَأَکْرَمُ مِنَ الْكَثِیرِ مِنْ خَلْقِهِ وَإِنْ كَانَ كُلٌّ مِنْهُ. Jiepushe na fitna za tamaa zisije zikakuchukua haraka na kukutupa kwenye midomo ya maangamizo, na ukiweza hakikisha kusiwe na kiunganishi baina yako na Mola wako Mwenye neema, kwa sababu wewe utapata fungu lako na utaomba fungu lako na kiasi kidogo kinachokujia kutoka kwa Mungu kina thamani zaidi kuliko kiasi kikubwa kitokacho katika kiumbe wake, ingawa neema zote (hata zile zinazotokana na kiumbe) zinatoka kwa Mungu.

وَتَلاَفِیكَ مَا فَرَطَ مِنْ صَمْتِكَ أَیسَرُ مِنْ إِدْرَاكِكَ مَا فَاتَ مِنْ مَنْطِقِكَ، وَحِفْظُ مَا فِی الْوِعَاءِ بِشَدِّ الْوِكَاءِ، وَحِفْظُ مَا فِی یدَیكَ أَحَبُّ إِلَیَّ مِنْ طَلَبِ مَا فِی یدَی غَیرِكَ. (Ewe mwanangu!) Ni rahisi kufidia ulichopoteza kutokana na ukimya wako kuliko kufidia kilichopotea kutokana na kuongea, na kukiweka kilichomo ndani ya chombo inawezekana kwa kufunga mdomo kwa nguvu, na kukihifadhi kile ulichonacho ni jambo linalopendwa zaidi na mimi kuliko kuomba kitu ambacho kiko mikononi mwa mtu mwingine.

وَمَرَارَةُ الْیأْسِ خَیرٌ مِنَ الطَّلَبِ إِلَی النَّاسِ، وَالْحِرْفَةُ مَعَ الْعِفَّةِ خَیرٌ مِنَ الْغِنَی مَعَ الْفُجُورِ، وَالْمَرْءُ أَحْفَظُ لِسِرِّهِ، وَرُبَّ سَاعٍ فِیمَا یَضُرُّهُ! Uchungu wa kukata tamaa (kwa sabababu ya kilichomo mikononi mwa watu) ni bora kuliko kunyoosha mkono ili kuwaomba, na kipato kidogo kinachombatana na usafi na uadilifu ni bora kuliko mali nyingi inayoambata na upotovu na dhambi, na mtu anajua siri zake (kuliko mtu mwingine) na kuna watu wengi wanaofanya kazi kwa hasara yao wenyewe.

مَنْ أَکْثَرَ أَهْجَرَ، وَمَنْ تَفَكَّرَ أَبْصَرَ. قَارِنْ أَهْلَ الْخَیرِ تَكُنْ مِنْهُمْ، وَبَاینْ أَهْلَ الشَّرِّ تَبِنْ عَنْهُمْ، Mtu anayeongea sana husema maneno mengi yasiyo na maana. Yeyote anayetumia mawazo yake huona ukweli na kuchagua njia sahihi. Jikurubishe na watu wema na wenye kufanya kheri ili ujitenge na kujiepusha na watu waovu na watenda shari.

بِئْسَ الطَّعَامُ الْحَرَامُ! وَظُلْمُ الضَّعِیفِ أَفْحَشُ الظُّلْمِ! إِذَا كَانَ الرِّفْقُ خُرْقاً كَانَ الْخُرْقُ رِفْقاً. Vyakula vibaya zaidi ni vyakula haramu na dhulma dhidi ya wanyonge ni ukandamizaji mbaya zaidi. Ambapo ulaini na uvumilivu husababisha utumiaji mabavu, utazingatiwa kuwa utumiaji mabavu wa uvumilivu. رُبَّمَا كَانَ الدَّوَاءُ دَاءً، وَالدَّاءُ دَوَاءً، وَرُبَّمَا نَصَحَ غَیرُ النَّاصِحِ، وَغَشَّ الْمُسْتَنْصَحُ. Inawezekana dawa zikasababisha maradhi, na yawezekana magonjwa yakawa ni dawa ya binadamu, wakati mwingine wasiopewa mawaidha wanatoa nasaha, na yule ambaye ni mtu wa kutoa nasaha na anatakiwa kutoa nasaha hufanya khiana. وَإِیاكَ وَالاِتِّكَالَ عَلَی الْمُنَی فَإِنَّهَا بَضَائِعُ النَّوْكَی وَالْعَقْلُ حِفْظُ التَّجَارِبِ، وَخَیرُ مَا جَرَّبْتَ مَا وَعَظَكَ. بَادِرِ الْفُرْصَةَ قَبْلَ أَنْ تَكُونَ غُصَّةً. لَیسَ كُلُّ طَالِب یصِیبُ، وَلاَ كُلُّ غَائِب یئُوبُ. Jihadhari na kutegemea ndoto (matumaini) ambazo ni mtaji wa wajinga. Hekima ni hifadhi ya uzoefu, na uzoefu wako bora ni ule unaokuwaidhi, tumia fursa kabla ya kupotea na kuwa chanzo cha huzuni. Sio kila mtu anayetafuta kitu anapata kile anachotaka, na sio kila mtu anayejificha kutoka kwa macho hurejea. مِنَ الْفَسَادِ إِضَاعَةُ الزَّادِ، وَمَفْسَدَةُ الْمَعَادِ. وَلِكُلِّ أَمْر عَاقِبَةٌ، سَوْفَ یأْتِیكَ مَا قُدِّرَ لَكَ. التَّاجِرُ مُخَاطِرٌ، وَرُبَّ یسِیر أَنْمَی مِنْ كَثِیر! لاخَیرَ فِی مُعِین مَهِین، وَلاَ فِی صَدِیق ظَنِین. سَاهِلِ الدَّهْرَ مَا ذَلَّ لَكَ قَعُودُهُ، وَلاَ تُخَاطِرْ بِشَیء رَجَاءَ أَکْثَرَ مِنْهُ، وَإِیاكَ أَنْ تَجْمَحَ بِكَ مَطِیُّةُ اللَّجَاجِ. Kuharibu riziki ni aina fulani ya ufisadi na sababu ya ufisadi wa kufufuliwa. Kila kitu kina mwisho (na unapaswa kuwa mwangalifu kuhusu mwisho wake.) Kile ambacho umekadiriwa kitakufikia hivi karibuni. Kila mfanyabiashara hujitia katika hatari. (Siku zote usitafute ongezeko kwa sababu) huenda mtaji mdogo ukawa na baraka kuliko mtaji mkubwa na ukuaji wake ni mkubwa zaidi. Hakuna kheri katika kusaidia kazi mbaya, wala hakuna faida yoyote kwa rafiki aliyetuhumiwa madhali maisha unayo nufaika nayo kwa wepesi na usiwahi kuhatarisha neema (baraka) uliyo nayo ili kupata zaidi. Jihadhari na kupanda juu ya ukaidi wako ambao utakufanya uwe maskini.

اِحْمِلْ نَفْسَكَ مِنْ أَخِیكَ عِنْدَ صَرْمِهِ عَلَی الصِّلَةِ، وَعِنْدَ صُدُودِهِ عَلَی اللَّطَفِ وَالْمُقَارَبَةِ، وَعِنْدَ جُمُودِهِ عَلَی الْبَذْلِ، وَعِنْدَ تَبَاعُدِهِ عَلَی الدُّنُوِّ، وَعِنْدَ شِدَّتِهِ عَلَی اللِّینِ، وَعِنْدَ جُرْمِهِ عَلَی الْعُذْرِ، حَتَّی كَأَنَّكَ لَهُ عَبْدٌ، وَكَأَنَّهُ ذُو نِعْمَة عَلَیكَ وَإِیاكَ أَنْ تَضَعَ ذَلِكَ فِی غَیرِ مَوْضِعِهِ، أَوْ أَنْ تَفْعَلَهُ بِغَیرِ أَهْلِهِ. (Mwanangu!) mbele ya ndugu yako wa kidini (jilazimishe mambo haya:) Uhusiano unapokatika kutoka kwake, wewe anzisha uhusiano na wakati ana hasira na kuwa mbali na wewe (anapojitenga) wewe mkaribie, toa mkabala na ubakhili wake, kuwa karibu naye anapokuwa mbali, kuwa mpole anapokuwa mkali, na ukubali udhuru wake anapofanya uhalifu, kana kwamba wewe ni mja wake na yeye ndiye mwenye neema zako. Lakini uwe mwangalifu usiifanye kazi hii au kuitumia kwa mtu asiye na sifa. لاَ تَتَّخِذَنَّ عَدُوَّ صَدِیقِكَ صَدِیقاً فَتُعَادِی صَدِیقَكَ، وَامْحَضْ أَخَاكَ النَّصِیحَةَ، حَسَنَةً كَانَتْ أَوْ قَبِیحَةً، وَتَجَرَّعِ الْغَیظَ فَإِنِّی لَمْ أَرَ جُرْعَةً أَحْلَی مِنْهَا عَاقِبَةً، وَلاَ أَلَذَّ مَغَبَّةً. وَلِنْ لِمَنْ غَالَظَكَ، فَإِنَّهُ یوشِكُ أَنْ یلِینَ لَكَ، وَخُذْ عَلَی عَدُوِّكَ بِالْفَضْلِ فَإِنَّهُ أَحْلَی الظَّفَرَینِ. وَإِنْ أَرَدْتَ قَطِیعَةَ أَخِیكَ فَاسْتَبْقِ لَهُ مِنْ نَفْسِكَ بَقِیةً یرْجِعُ إِلَیهَا إِنْ بَدَا لَهُ ذَلِكَ یوْماً مَا. وَمَنْ ظَنَّ بِكَ خَیراً فَصَدِّقْ ظَنَّهُ. Kamwe usimchukulie adui wa rafiki yako kama rafiki, kwa sababu kwa kufanya hivi umeanzisha adui kwa rafiki yako. Andaa ushauri wako wa ikhlasi kwa ajili ya ndugu yako, ikiwa ni mzuri na wa kupendeza au mbaya na wa kufadhaisha. Meza hasira yako funda kwa funda, kwani sijawahi kuona funda tamu na la kufurahisha zaidi kuliko hilo. Kuwa mpole na mtu anayekutendea kwa jeuri na kwa matumaini kwamba, hivi karibuni atakua laini. Mtendee adui yako kwa neema na ukarimu na katika hali hii umechagua ushindi mtamu zaidi kati ya aina mbili za ushindi (ushindi kupitia jeuri na ushindi kupitia upendo). Ikiwa unataka kukata mfungamano wa udugu na urafiki, acha mahali pa upatanisho ili akitaka kurudi siku moja aweze. Yeyote anayefikiria vizuri juu yako, sadikisha maoni yake na vitendo vyako. وَلاَ تُضِیعَنَّ حَقَّ أَخِیكَ اتِّكَالاً عَلَی مَا بَینَكَ وَبَینَهُ، فَإِنَّهُ لَیسَ لَكَ بِأَخ مَنْ أَضَعْتَ حَقَّهُ. وَلاَ یكُنْ أَهْلُكَ أَشْقَی الْخَلْقِ بِكَ، وَلاَ تَرْغَبَنَّ فِیمَنْ زَهِدَ عَنْكَ، وَلاَ یكُونَنَّ أَخُوكَ أَقْوَی عَلَی قَطِیعَتِكَ مِنْكَ عَلَی صِلَتِهِ، وَلاَ تَكُونَنَّ عَلَی الاِْسَاءَةِ أَقْوَی مِنْكَ عَلَی الاِْحْسَانِ. وَلاَ یکْبُرَنَّ عَلَیكَ ظُلْمُ مَنْ ظَلَمَكَ، فَإِنَّهُ یسْعَی فِی مَضَرَّتِهِ وَنَفْعِكَ، وَلَیسَ جَزَاءُ مَنْ سَرَّكَ أَنْ تَسُوءَهُ. Usipoteze kamwe uaminifu wa urafiki na umoja kati yako na ndugu yako; kwa sababu mtu ambaye unapoteza haki yake hatakuwa ndugu yako. Familia yako haipaswi kuwa watu wasio na bahati zaidi na huzuni zaidi mbele yako. Usionyeshe kupendezwa na mtu ambaye hupendezwi naye (anayepuuza na kudharau) na ndugu yako asiwe na nguvu zaidi katika kukata kiungo cha udugu kuliko wewe katika kuunganisha udugu, na wala asiwe na nguvu zaidi katika kutenda ubaya kuliko wewe katika kutenda wema. Na dhulma ya mtu anayekudhulumu isikugharimu kamwe, kwa sababu anajaribu kujidhuru mwenyewe na kukunufaisha (hufanya mzigo wa dhambi yake kuwa mzito na kukuzidishia malipo) na bila shaka malipo ya mtu ambaye anayekufurahisha sio kumtendea ubaya. وَاعْلَمْ یا بُنَی أَنَّ الرِّزْقَ رِزْقَانِ: رِزْقٌ تَطْلُبُهُ، وَرِزْقٌ یطْلُبُكَ، فَإِنْ أَنْتَ لَمْ تَأْتِهِ أَتَاكَ. Mwanangu! Jua kwamba "riziki" ni za aina mbili: Aina moja ni kuamka kuitafuta (na unapaswa kuinuka) na aina nyingine ni kwamba itakujia hata usipoifuata, itakujia na kukufuata. مَا أَقْبَحَ الْخُضُوعَ عِنْدَ الْحَاجَةِ، وَالْجَفَاءَ عِنْدَ الْغِنَی. إِنَّمَا لَكَ مِنْ دُنْیاكَ، مَا أَصْلَحْتَ بِهِ مَثْوَاكَ، وَإِنْ كُنْتَ جَازِعاً عَلَی مَا تَفَلَّتَ مِنْ یدَیكَ، فَاجْزَعْ عَلَی كُلِّ مَا لَمْ یصِلْ إِلَیكَ. Ni ubaya ulioje kunyenyekea (kwa wengine) wakati wa shida na kupuuza na kufanya ukandamizaji wakati wa kutokuwa na shida na kuwa na uwezo, dunia itakuwa yako tu pale utakapoitengeneza na kuifanya kuwa nyumba yako huko Akhera na ikiwa utahuzunika kwa jambo fulani ambalo hujalipata na kukosa utulivu basi kosa furaha kwa kila jambo ambalo halijakufikia (hujalipata). اِسْتَدِلَّ عَلَی مَا لَمْ یكُنْ بِمَا قَدْ كَانَ، فَإِنَّ الاُْمُورَ أَشْبَاهٌ; وَلاَ تَكُونَنَّ مِمَّنْ لاتَنْفَعُهُ الْعِظَةُ إِلاَّ إِذَا بَالَغْتَ فِی إِیلاَمِهِ، فَإِنَّ الْعَاقِلَ یتَّعِظُ بِالاْدَابِ الْبَهَائِمَ لاتَتَّعِظُ إِلاَّ بِالضَّرْبِ. Toa hoja kwa kile kilichotokea huko nyuma, juu ya kile ambacho hakikutokea; kwa sababu mambo ya dunia yanafanana. Usiwe katika watu ambao mawaidha yao hayawanufaishi ila pale unapong'ang'ania kukemea; kwa sababu wenye hekima hupokea ushauri kwa mawaidha na adabu; lakini wenye miguu minne (wanyama) hawachukui mawaidha ila kwa kupigwa.

اِطْرَحْ عَنْكَ وَارِدَاتِ الْهُمُومِ بِعَزَائِمِ الصَّبْرِ وَحُسْنِ الْیقِینِ. مَنْ تَرَكَ الْقَصْدَ جَارَ، وَالصَّاحِبُ مُنَاسِبٌ، وَالصَّدِیقُ مَنْ صَدَقَ غَیبُهُ. الْهَوَی شَرِیكُ الْعَمَی وَ رُبَّ بَعِید أَقْرَبُ مِنْ قَرِیب، وَقَرِیب أَبْعَدُ مِنْ بَعِید، وَالْغَرِیبُ مَنْ لَمْ یكُنْ لَهُ حَبِیبٌ. Epuka mashambulizi ya ghamu na huzuni kwa nguvu ya subira na yakini nzuri. Mwenye kuacha wastani hukengeuka kutoka kwenye njia iliyo sawa, (na jua) rafiki na sahiba (mzuri) ni kama jamaa na ndugu wa mtu. Rafiki ni yule anayetimiza haki ya urafiki pasipo kuwepo mtu. Muabudu matamanio ni mshirika na mwenza wa upofu. Huenda wale wa mbali wakawa karibu na ndugu wa mtu wakawa mbali zaidi. Mgeni ni mtu ambaye hana rafiki. نْ تَعَدَّی الْحَقَّ ضَاقَ مَذْهَبُهُ، وَمَنِ اقْتَصَرَ عَلَی قَدْرِهِ كَانَ أَبْقَی لَهُ. وَأَوْثَقُ سَبَب أَخَذْتَ، بِهِ سَبَبٌ بَینَكَ وَبَینَ اللهِ سُبْحَانَهُ. وَمَنْ لَمْ یبَالِكَ فَهُوَ عَدُوُّكَ. قَدْ یكُونُ الْیأْسُ إِدْرَاکاً، إِذَا كَانَ الطَّمَعُ هَلاَکاً. Mtu anayekanyaga haki atakuwa kwenye shida. Na mwenye kuridhika na thamani yake atakuwa imara zaidi. Chombo cha uhakika unachoweza kunyakua ni kuanzisha uhusiano kati yako na Mungu wako. Asiyejali (kazi na haki zako) ni adui yako. Wakati mwingine kukata tamaa ni njia ya kufikia lengo, ambapo pupa husababisha uharibifu. لَیسَ كُلُّ عَوْرَة تَظْهَرُ، وَلاَ كُلُّ فُرْصَة تُصَابُ، وَرُبَّمَا أَخْطَأَ الْبَصِیرُ قَصْدَهُ، وَأَصَابَ الاَْعْمَی رُشْدَهُ. أَخِّرِ الشَّرَّ فَإِنَّكَ إِذَا شِئْتَ تَعَجَّلْتَهُ، وَقَطِیعَةُ الْجَاهِلِ تَعْدِلُ صِلَةَ الْعَاقِلِ. Sio hivyo kwamba kila kasoro iliyofichwa ifunuliwe. Na si kila fursa ni ya kutumika. Wakati mwingine mtu mwenye kuona hukosea na kipofu hufika katika kituo (palipokusudiwa). Chelewesha kufanya ubaya (na usikimbilie) kwa sababu unaweza kuufanya wakati wowote unapotaka. Kuachana na mjinga ni sawa na kuungana na mwenye akili na busara. مَنْ أَمِنَ الزَّمَانَ خَانَهُ، وَمَنْ أَعْظَمَهُ أَهَانَهُ. لَیسَ كُلُّ مَنْ رَمَی أَصَابَ. إِذَا تَغَیرَ السُّلْطَانُ تَغَیرَ الزَّمَانُ. سَلْ عَنِ الرَّفِیقِ قَبْلَ الطَّرِیقِ، وَعَنِ الْجَارِ قَبْلَ الدَّارِ. إِیاكَ أَنْ تَذْكُرَ مِنَ الْكَلاَمِ مَا یكُونُ مُضْحِکاً، وَإِنْ حَكَیتَ ذَلِكَ عَنْ غَیرِكَ. Yule anayejiona yuko salama kutokana na matukio ya wakati, basi zama na wakati utamsaliti na anayeona kuwa ni mkubwa utamdhalilisha. Sio kila risasi inafikia na kulenga shabaha. Kila mtawala anapobadilika, nyakati nazo hubadilika. Kabla ya kuamua kusafiri, angalia ni nani msafiri mwenzako na kabla ya kuchagua nyumba, angalia jirani yako ni nani? Epuka kusema maneno ya kuchekesha (na yasiyo na maana), hata kama unanukuu kutoka kwa mtu mwingine. وَإِیاكَ وَمُشَاوَرَةَ النِّسَاءِ فَإِنَّ رَأْیهُنَّ إِلَی أَفْنٍ، وَعَزْمَهُنَّ إِلَی وَهْنٍ. وَاکْفُفْ عَلَیهِنَّ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ بِحِجَابِكَ إِیاهُنَّ، فَإِنَّ شِدَّةَ الْحِجَابِ أَبْقَی عَلَیهِنَّ، وَلَیسَ خُرُوجُهُنَّ بِأَشَدَّ مِنْ إِدْخَالِكَ مَنْ لایوثَقُ بِهِ عَلَیهِنَّ، وَإِنِ اسْتَطَعْتَ أَلاَّ یعْرِفْنَ غَیرَكَ فَافْعَلْ. وَلاَ تُمَلِّكِ الْمَرْأَةَ مِنْ أَمْرِهَا مَا جَاوَزَ نَفْسَهَا، فَإِنَّ الْمَرْأَةَ رَیحَانَةٌ، لَیسَتْ بِقَهْرَمَانَة. وَلاَ تَعْدُ بِكَرَامَتِهَا نَفْسَهَا، وَلاَ تُطْمِعْهَا فِی أَنْ تَشْفَعَ لِغَیرِهَا. وَإِیاكَ وَالتَّغَایرَ فِی غَیرِ مَوْضِعِ غَیرَة، فَإِنَّ ذَلِكَ یدْعُو الصَّحِیحَةَ إِلَی السَّقَمِ وَالْبَرِیئَةَ إِلَی الرِّیبِ. Epuka kushauriana na wanawake (waliopungukiwa na hekima) kwa sababu hukumu yao ni pungufu na uamuzi wao ni dhaifu, na kupitia hijabu, wazuie kuwaona wanaume ajinabi, kwa sababu kusisitiza hijabu kutawafanya kuwa salama na safi zaidi. (Usiwaruhusu watu wasioaminika ndani yako kwa sababu) kutoka kwao sio kubaya zaidi kuliko kuwaruhusu watu wasio wa kuaminika waingie. Fanya hivyo, ukiweza ili wasimjue asiyekuwa wewe (watu wa kigeni). Usimpe mwanamke zaidi ya kazi yake mwenyewe, kwa sababu yeye ni kama tawi la maua, si shujaa na bwana wa kusimamia mambo (mnyapara). Kwa ajili ya heshima yake, usimheshimu mwingine (ajinabi) na uweke heshima yake kiasi kwamba asifikiriei kuwaombea wengine (ajinabi). Uwe mwangalifu usionyeshe bidii mahali ambapo haupaswi kuwa na bidii (na kazi yako itasababisha tuhuma zisizo za haki) kwa sababu bidii hii isiyofaa na tuhuma za uwongo humpeleka mwanamke msafi (kimaadili) kwenye uchafu, na asiye na hatia kwenye uchafu. وَاجْعَلْ لِكُلِّ إِنْسَان مِنْ خَدَمِكَ عَمَلاً تَأْخُذُهُ بِهِ، فَإِنَّهُ أَحْرَی أَلاَّ یتَوَاكَلُوا فِی خِدْمَتِكَ وَأَکْرِمْ. عَشِیرَتَكَ، فَإِنَّهُمْ جَنَاحُكَ الَّذِی بِهِ تَطِیرُ، وَأَصْلُكَ الَّذِی إِلَیهِ تَصِیرُ، وَیدُكَ الَّتِی بِهَا تَصُولُ. (Mwanangu!) Weka kazi fulani kwa kila mmoja wa watumishi wako ambayo unamwajibisha; kwa sababu hii itawafanya wasiachiane kazi zako wenyewe kwa wenyewe (na kutokwepa mzigo wa wajibu. Heshima kabila, ndugu na jamaa zako, kwani wao ni kama mbawa kupityia kwao unaweza kupaaa na wao ni mzizi na asili ambayo inarejea kwao na nguvu unazomshambulia nazo (adui).

اِسْتَوْدِعِ اللهَ دِینَكَ وَدُنْیاكَ، وَاسْأَلْهُ خَیرَ الْقَضَاءِ لَكَ فِی الْعَاجِلَةِ وَالاْجِلَةِ، وَالدُّنْیا وَالاْخِرَةِ، وَالسَّلاَمُ. Itegemee dini yako na dunia yako kwa Mwenyezi Mungu na muombe hatima njema ya leo, kesho, dunia na akhera, na amani iwe juu yako.