Nenda kwa yaliyomo

Barua ya Imamu Ali (a.s) kwa Shuraih

Kutoka wikishia

Barua ya Imamu Ali (a.s) kwa Shuraih: Hii ni barua maalumu ya makemeo ya Imamu Ali (a.s) kwa Shuraih bin Harith, aliyekuwa qadhi wa wakati wa wakati huo mjini Kufa, ambaye ameshutumiwa kwa kununua nyumba kwa bei ghali. Katika barua hii, Imam Ali anamuwaidhi Shuraih na kumkumbusha thamani ya dunia na hisabati ya Siku ya Kiyama. Pia baurua yake hiyo ilitaraji kwamba; Shuraih, ambaye ni afisa wa serikali, ataelewa kuwa mtu kama yeye hatarajiwi kuwa na maisha ya kifahari. Barua hii inahisabiwa kuwa, ni moja ya misingi muhimu ya kanuni za uongozi, ambayo inasisitiza kwamba kiongozi anapaswa kusimamia maafisa wake kwa uamuzi thabiti bila ya kutetereka. Barua hii ni barua ya tatu kutoka kwenye faharasa ya barua zilizomo katika kitabu cha Nahjul Balagha. Pia barua hii inapatikana katika vitabu vingine kadhaa, kitabu kiitwacho Amali kilichoandikwa na Sheikh Saduq, Kitabu cha Arba'in cha Sheikh Bahai. Vile vile barua hii imeripotiwa na baadhi ya vitabu vya wanaislamu wa madhehebu ya Kiunni, kama vile Dastur Ma'alem al-Hikam cha Qadi Quda'i (aliyefariki mnamo mwaka wa 454 Hijiria) na Tadhkiratu al-Khawas cha Sibtu bin Juzi (aliyefariki mwaka 654 Hijiria).

Umuhimu na Nafasi Barua ya Imam Ali (a.s) kwa Shuraih, jaji wa Kufa, inaonekana kama dhibitisho na ryhusa kwa kiongozi wa kidini katika kukabiliana na matumizi mabaya ya madaraka kwa watawala wa serikali. [1] Shuraih, aliyekuwa jaji na kadhi mwenye cheo cha aliyekuwa akikabiliwa na tuhuma za kununua nyumba kwa bei ya kupindukia mipaka, hakubaki salama katika mamlaka ya Amiru Al-lmuuminina, na Imamu Ali (a.s) hakuridhika ununuzi wake huo wa nyumba kwa gharama kubwa, kupitia fedha zitokazo kwenye rasilimali ya umma. [2] Shuraih aliteuliwa na Omar bin Khattab kushika nafasi ya ujaji katika mji wa Kufa ili kushughulikia mizozo ya kijamii katika mji huo. [3] Yeye aliendelea kubaki katika cheo hicho hadi wakati wa ukhalifa wa Othman, na pia aliendelea kushika nafsi hiyo hadi wakati wa uongozi wa Imamu Ali (a.s). [4] Kama ilivyoelezwa katika masimulizi ya kitabu Al-Kafi, pale Imamu Ali (a.s) alipomkabidhi Shuraih jukumu la ukadhi, alimwekea masharti madhubuti yanayomtaka yeye kutofanya maamuzi yoyote yale bila kushirikiana naye kabla ya kufanya maamuzi yake. [5] Kwa maoni ya Ayatullah Makarim Shirazi katika tafsiri yake ya Nahjul Balagha, ni kwamba; uongozi wa Imamu Ali (a.s) ulianza baada tu ya kumaliza kwa kipindi cha ukhalifa wa Othman, ambapo kipindi ambacho hazina ya Baitulmal (ghala au benki ya umma) ilivurugwa na kuchezewa na viongozi wa Kiislamu walijishughulisha na ufisadi na maisha ya anasa. [6] Jambo ambalo lilimfanya Imamu (a.s) kutokukubaliana na hali kama hiyo. Hilo ndilo lililoomfanya yeye kuwapa onyo walioteule wake, na kuwaonya wasiishi maisha ya anasa na kujivunia mambo ya kidunia. [7] Ili kukomesha mwenendo huu, Imamu (a.s) alizidi kuwatetemesha watendaji wake kupitia mawaidha, hotuba na barua zake mbali mbali zinazopatikana katika kitabu kiitwacho Nahjul Balagha. Imamu Ali (a.s) alitumia nyenzo hizi ili kumurika na kuuangaza upotevu na thamani ya dunia na mavuno yake. [8]

Chanzo cha Barua na Muktadha Wake Pale jaji Shuraih, alipokuwa akishikilia nafasi ya ukadhi katika serikalini ya Imam Ali (a.s.), aliamua kununua nyumba kwa bei ghali mno, iliogharimu kiasi cha dinari 80. [9] Baada ya Imam (a.s) kusikia habari hii na kuthibitisha ununuzi huo, aliamua alimtaka Shuraih ahudhurie mbele yake na akamkemea kwa makemeo makali mno, akimtahadharisha kwa kumwambia kwamba: "Kifo kitamkuta kwa haraka bila ya kuchelewa, na kitamtoa na kumng’oa kutoka kwenye nyumba hii." [10] Imamu (a.s) alimshauri Shuraih akimweleza kwamba; ununuzi wa nyumba haupaswi kufanywa kutokana na mali haramu; vinginevyo, atakumbana na hasara kubwa duniani na Akhera. [11] Imam Ali (a.s) alimwandikia Shuraih barua yenye ujembe wa kiroho ndani yake, unaomtaka yeye kuachana na matamanio ya dunia, akisema kwamba; lau kama Shuraih angefahamu maana ya barua hiyo, basi asingejaribu kutumia hata dirhamu moja katika ununuzi wa nyumba hiyo. Kulingana na barua hii, nyumba hiyo ingelimsababishia Shuraih kuingia kwenye mabalaa yatakayo mwongoza yeye kwenye mielekeo minne, nayo ni: kuelekea kwenye majanga, misiba, tamaa ziishiazo kwenye hatima mbaya, na la nne ni kuingia kwenye mapito ya Shetani mwangamizi. Baru hii ilimtambulisha yeye ya kwamba; mlango wa nyumba hiyo unafungukia kwenye uwanja wa shetani (mwelekeo wa nne). Majanga haya ndiyo matunda na faida halisi na changamoto hatari za mnunuzi wa nyumba hiyo. [12] Imamu Ali (a.s) akutumia mifano ya wale waliopindukia mipaka katika dhulma, ambao miili yao tayari imeshaoza huko makaburini mwao, alijaribu kumpa ushauri Shuraih, akimtahadharisha kwa kumwambia kwamba; ajitayarishe kwa ajili ya hesabu ya siku ya Kiyama kuhusiana na majukumu aliyonayo hasa kuhusiana na amana aliyopewa na Waislamu (Baitu Al-Mali). [13] Katika baadhi ya maelezo yaliyoambatanishwa na barua hii katika Nahj al-Balagha, ndani yake kuna nyongeza ya mawaidha khusiana na mambo mengine, kama vile; kutoghafilika pamoja na kuepukana na kiburi, [14] kujihadhari na mapenzi ya dunia, kutotafuta kipato cha dunia kwa njia haramu, na kuepukana na rushwa utoaji wa hukumu za kisheria. [15]

Vyanzo na Ushahidi wa Barua Barua ya Imamu Ali (a.s) kwa Shuraih ni barua maarufu inayopatikana katika kitabu cha Al-Amali cha Sheikh Al-Saduq (aliyefariki mwaka 381 Hijria). [16] Pia barua hii inapatikana katika vyanzo vyengine kadhaa ikiwa na tofauti chache katika matini yake. [17] Miongoni mwa wanazuoni walioinukuu barua hii, huku ikiwa na tofauti chache katika matini yake, ni pamoja na; Sheikh Baha'i (aliyefariki 1031 Hijria) aliyenukuu katika kitabu chake Arba'in, [18] Sibtu ibn Al-Jawzi (aliyefariki mwaka 654 Hijria) aliyeinukuu katika kitabu chake Tadhkiratu al-Khawass, [19] na Al-Qudha'i (aliyefariki mwaka 454 Hijria) aliyeitaja katika kitabu chake Dastur Ma'alim al-Hikam. [20] Hawa ni miongoni mwa wanazuoni walioirekodi barua hii kwa tofauti chache katika matini yake. [21] Barua hii ni barua ya tatu katika faharasa ya baadhi ya nakala za Nahj al-Balagha. [22] Kwa mujibu wa maelezo ya Allama Hassanzade ni kwamba; uhalali wa ushahidi wa barua hii, hauna shaka wala utata wowote ule ndani yake, hii ni kutokana na ukweli kwamba, Sheikh Baha'i aliinukuu barua hii kutoka kwa walimu na wapokezi mashuhuri wa Hadithi wanaoaminika. [23]

Matini ya Barua Kiarabu na Tafsiri yake من کتاب له(ع) لشريح بن الحارث قاضيه Miongoni mwa barua zake (a.s) kwenda kwa Shuraih bin al-Harith, hakimu wa mji wa Kufa. رُوِيَ أَنَّ شُرَيْحَ بْنَ الْحَارِثِ قَاضِيَ أَمِيرِالْمُؤْمِنِينَ (علیه السلام) اشْتَرَى عَلَى عَهْدِهِ دَاراً بِثَمَانِينَ دِينَاراً فَبَلَغَهُ ذَلِكَ، فَاسْتَدْعَى شُرَيْحاً، Imesimuliwa kwamba Shuraih bin al-Harith, hakimu mteule wa zama za Amir al-Mu'minin (a.s), alinunua nyumba katika zama za utawala wa Amir al-Mu'minin, nyumba ambayo ilimgharimu kiasi cha dinari themanini. Habari hiyo ikamfikia Imamu Ali (a.s), hivyo akamwita Shuraih na kuhudhurisha mbele yake. وَ قَالَ لَهُ: بَلَغَنِي أَنَّكَ ابْتَعْتَ دَاراً بِثَمَانِينَ دِينَاراً وَ كَتَبْتَ لَهَا كِتَاباً وَ أَشْهَدْتَ فِيهِ شُهُوداً فَقَالَ لَهُ شُرَيْحٌ قَدْ كَانَ ذَلِكَ يَا أَمِيرَالْمُؤْمِنِينَ(ع) Alipofika mbele yake alimwambia: "Nimepata habari ya kwamba; umenunua nyumba kwa dinari themanini, na ukaandika waraka wa kujimilikisha na kushuhudisha mashahidi katika umiliki huo?" Shuraih akamwambia: "Ni kweli nemefanya hivyo, Ee Amir al-Mu'minina.

قَالَ فَنَظَرَ إِلَيْهِ نَظَرَ الْمُغْضَبِ ثُمَّ قَالَ لَهُ: يَا شُرَيْحُ أَمَا إِنَّهُ سَيَأْتِيكَ مَنْ لَا يَنْظُرُ فِي كِتَابِكَ وَ لَا يَسْأَلُكَ عَنْ بَيِّنَتِكَ، حَتَّى يُخْرِجَكَ مِنْهَا شَاخِصاً وَ يُسْلِمَكَ إِلَى قَبْرِكَ خَالِصاً. Msimulizi anasema; Hapo Imamu Ali (a.s) kamtazama kwa mtazamo wa hasira, kisha akamwambia: "Ewe Shuraih! Hakika muda si mrefu atakujia yule (Malaika wa mauti) ambaye hatakuwa na haja ya kutazama waraka wako, wala hakuuliza juu ya ushahidi wako, na hakuacha mpaka akutoe kutoka nyumbani humo ukiwa uchi na akukabidhishe kaburi kwako ukiwa mikono mitupu.

فَانْظُرْ يَا شُرَيْحُ لَا تَكُونُ ابْتَعْتَ هَذِهِ الدَّارَ مِنْ غَيْرِ مَالِكَ أَوْ نَقَدْتَ الثَّمَنَ مِنْ غَيْرِ حَلَالِكَ؛ فَإِذَا أَنْتَ قَدْ خَسِرْتَ دَارَ الدُّنْيَا وَ دَارَ الْآخِرَةِ Basi kuwa makini, ewe Shuraih! Usiwe umenunua nyumba hii kutoka kwa asiyekuwa mmiliki wake, au umelipa thamani yake kutoka kwa kisichokuwa halali yako; Kwani katika hali hiyo, utakuwa umekula khasara duniani na Akhera.

أَمَا إِنَّكَ لَوْ كُنْتَ أَتَيْتَنِي عِنْدَ شِرَائِكَ مَا اشْتَرَيْتَ لَكَتَبْتُ لَكَ كِتَاباً عَلَى هَذِهِ النُّسْخَةِ، فَلَمْ تَرْغَبْ فِي شِرَاءِ هَذِهِ الدَّارِ [بِالدِّرْهَمِ] بِدِرْهَمٍ فَمَا فَوْقُ. Bila shaka, lau ungenijia wakati wa manunuzi yako ya hicho ulichokinunua, basi ningekuandikia hati yenye nasaha kama hizi, hivyo usingetamani kununua nyumba hii kwa dirhamu moja, seuze zaidi ya dirhamu moja.

وَ النُّسْخَةُ هَذِهِ هَذَا مَا اشْتَرَى عَبْدٌ ذَلِيلٌ مِنْ مَيِّتٍ قَدْ أُزْعِجَ لِلرَّحِيلِ اشْتَرَى مِنْهُ دَاراً مِنْ دَارِ الْغُرُورِ مِنْ جَانِبِ الْفَانِينَ وَ خِطَّةِ الْهَالِكِينَ Na hati hii ni kwamba; Hichi ndicho alichonunua mja dhalili kutoka kwa maiti ambaye tayari ameshaharakishwa kwa ajili safari (mauti), amenunua kutoka kwake nyumba miongoni mwa nyumba danganyifu, kutoka kwa wale wanaotoweka na wanaofariki.

وَ تَجْمَعُ هَذِهِ الدَّارَ حُدُودٌ أَرْبَعَةٌ الْحَدُّ الْأَوَّلُ يَنْتَهِي إِلَى دَوَاعِي الْآفَاتِ وَ الْحَدُّ الثَّانِي يَنْتَهِي إِلَى دَوَاعِي الْمُصِيبَاتِ وَ الْحَدُّ الثَّالِثُ يَنْتَهِي إِلَى الْهَوَى الْمُرْدِي وَ الْحَدُّ الرَّابِعُ يَنْتَهِي إِلَى الشَّيْطَانِ الْمُغْوِي وَ فِيهِ يُشْرَعُ بَابُ هَذِهِ الدَّارِ Na nyumba hii imekushana ndani yake mipaka minne: Mpaka wa kwanza unaishia kwenye vichocheo vya majanga, na mpaka wa pili unaishia kwenye vichocheo vya misiba, na mpaka wa tatu unaishia kwenye tamaa iangamizayo, na mpaka wa nne unaishia kwenye mamlaka ya Shetani adanganyaye, na huo ndiwo mlango mlango wa kuingilia nyumba hii. اشْتَرَى هَذَا الْمُغْتَرُّ بِالْأَمَلِ مِنْ هَذَا الْمُزْعَجِ بِالْأَجَلِ هَذِهِ الدَّارَ بِالْخُرُوجِ مِنْ عِزِّ الْقَنَاعَةِ وَ الدُّخُولِ فِي ذُلِّ الطَّلَبِ وَ الضَّرَاعَةِ فَمَا أَدْرَكَ هَذَا الْمُشْتَرِي فِيمَا اشْتَرَى مِنْهُ مِنْ دَرَكٍ فَعَلَى مُبَلْبِلِ أَجْسَامِ الْمُلُوكِ وَ سَالِبِ نُفُوسِ الْجَبَابِرَةِ وَ مُزِيلِ مُلْكِ الْفَرَاعِنَةِ مِثْلِ كِسْرَى وَ قَيْصَرَ وَ تُبَّعٍ وَ حِمْيَرَ Mdanganwa huyu aliyedanganywa na matumaini, amenunua nyumba hii kutoka kwa yule aliyeharakiswha kuielekea ajali (kifo), ameinunua kwa thamani ya kutoka katika heshima ya kutosheka (kuridhika) na kuingia katika udhalili (unyonge) wa kuomba na kunyenyekea. Basi chochote kile kitakachomsibu mnunuzi huyu kutokana na kile alichonunua kutoka kwa muuzaji huyo, basi ni kazi ya yule anayetikisa miili ya wafalme, na kunyakua roho za majabari, na kuondoa ufalme wa mafarao, kama vile Kisra, Kaisari, Tubba', na Himyar.

وَ مَنْ جَمَعَ الْمَالَ عَلَى الْمَالِ فَأَكْثَرَ وَ مَنْ بَنَى وَ شَيَّدَ وَ زَخْرَفَ وَ نَجَّدَ وَ ادَّخَرَ وَ اعْتَقَدَ وَ نَظَرَ بِزَعْمِهِ لِلْوَلَدِ إِشْخَاصُهُمْ جَمِيعاً إِلَى مَوْقِفِ الْعَرْضِ وَ الْحِسَابِ وَ مَوْضِعِ الثَّوَابِ وَ الْعِقَاب Na yeyote yule aliyekusanya mali juu ya mali kupita kiasi, na yeyote yule aliyejenga na akainua na kuimarisha kisha akapamba kwa mapambo ya nje na ya ndani, na akahifadhi (akarimbika) na kuamini (akajenga matumaini) na akajenga mtazamo wa kuwekeza, kwa madai yake, kwa ajili ya mtoto (au watoto wake), Malaika wa mauti amewaondoa wote na kuwaongoza kwenye uwanja wa kuonyeshwa na kuhisabiwa, na (kuwahudhurisha) mahali pa thawabu na adhabu.

إِذَا وَقَعَ الْأَمْرُ بِفَصْلِ الْقَضَاءِ «وَ خَسِرَ هُنالِكَ الْمُبْطِلُونَ

Pale itakapotoka amri ya kuhitimishwa kwa hukumu, "Na huo nido wakati watakapokula kahasara wale wanaotenda batili.

شَهِدَ عَلَى ذَلِكَ الْعَقْلُ إِذَا خَرَجَ مِنْ أَسْرِ الْهَوَى وَ سَلِمَ مِنْ عَلَائِقِ الدُّنْيَا Akili inathibitisha hayo, pale akili hiyo itakapokuwa imejiondoa katika kifungo cha tamaa na kuwa huru kutokana na pingamizi za kidunia.