Barua ya Imam Ali (a.s) kwa Ash'ath ibnu Qais
Barua ya Imam Ali (a.s) kwa Ash'ath ibn Qais kutoka kwenye Nahj al-Balagha: Hii ni ile Barua ya Imam Ali (a.s) kwa Ash'ath ibn Qais, mwakilishi na kaimu mtendaji (gavana) wa Othman bin Affan huko Azerbaijan. Hii ni ile barua mashuhuri inayopatikana katika mkusanyiko wa semi hotuba na hekima za Imamu Ali (a.s) zilizoko kwenye kitabu kiitwacho Nahju Al-Balagha. Imamu Ali (a.s) katika barua yake hii, anamkumbusha Ash'ath juu ya matukio muhimu na hatari yaliyojiri wakati huo. Miongoni mwa matukio yaliyohusihwa na barua hii, ni pamoja na kifo cha Othman pamoja na uasi wa Talha na Zubayr. Imamu Ali (a.s) katika barua yake hii, alimtaka Ash'ath kumuunga na kumpa ahadi ya uaminifu (bay'ah) juu yake. [1] Pia, mwishoni mwa barua, Imamu Ali (a.s) anamuonya Ash'ath juu ya kuhifadhi na kuitunza mali ya umma (Baitul Mal). [2] Kwa mujibu wa maoni ya Ayatullahi Makarim Shirazi, mmoja wa wafasiri wa Nahju Al-Balagha, ni kwamba; suala kuu la barua hii ilikuwa ni kusisitiza kwamba nafasi za utawala katika serikali ya Kiislamu ni amana ya Mwenye Ezi Mungu, na hazipaswi kutumiwa kwa maslahi binafsi au kutumia uluwa kwa ajili ya kudhulumu raia. [3] Barua hii iliandikwa na Imamu Ali (a.s) mnamo mwaka wa 36 Baada ya Hijra, na baada ya kumalizika kwa Vita vya Jamal, [4] barua ambayo ilifikisha kwa Ash'ath kupitia Ziyad ibn Marhab al-Hamadani. [5] Wanahistoria kama vile Ibn A'tham Al-Kufi (aliyefariki baada ya mwaka wa 320 Hijiria) katika kitabu chake al-Futuh, na Nasru ibn Muzahim (aliyefariki karne ya 2 Hijiria) katika Waq'at Siffin, ni miongoni mwa wanahistoria waliozungumizia maudhui ya barua hii. Nukuu za wanahistoria hawa ni zenye muiano mkubwa kuhusiana na maudhui ya barua hii, na kuna tofauti ndogo mno katika nukuu zao. [6] Sayyid al-Radi mwandishi wa kitabu cha Nahju Al-Balagha, alinakili sehemu ya mwisho tu ya barua hii katika kitabu cha hicho maarufu. [7] Barua hii ni ya tano katika toleo la Nahju al-Balagha lililohaririwa na Subhi Salih, Faydhu al-Islam, Ibn Mitham, na wahariri wengineo. [8] Wasifu wa Ash'ath ibnu Qais Al-Kindi Ash'ath ibnu Qais (aliyefariki mwaka wa 40 Hijiria) alikuwa ni miongoni mwa watu waliohudhuria uvamizi wa Azerbaijan na kuteuliwa kuwa wakili maalumu na kaimu mtendaji wa nchi hiyo (gavana) kwa amri ya Othman ibn Affan iliyotolewa mnamo mwaka wa 25 Hijiria. [9] Kwa mujibu wa maelezo ya wanahistoria, Ash'ath akiwa katika wadhifa huo, alikuwa akijinyakulia kiasi cha dirham 1,000 kwa mwaka kutoka katika kodi za Azerbaijan kama ni malipo yake kwa idhini ya Othman. [10] Imamu Ali (a.s) hakuwa akifurahishwa wala kurishwa na utendaji wa Ash’ath pamoja na ubadhirifu huo wa mali ya umma, ila hakuamua kumfuvua uongozi mara tu ua kuanza kwa utawala wake. [11] Matukio Baada ya Barua Baada ya Ash'ath kupokea barua ya Imamu Ali (a.s) na kuwasoma barua hiyo mbele ya wafuasi wake, kwa nia ya kusikiliza maoni yao, wafwasi wake walimtaka amuunge mkono Imam Ali (a.s) na amkubali kama ni kiongozi wake. Lakini Ash'ath alisema kwamba yeye anaogopa kufanya hivyo, kwani iwapo atamuunga mkono Ali (a.s), atamlazimisha kurudisha mali aliyopora kutoka Azerbaijan, ilhali kama ataamua kumfuata Muawiyah, basi hakuna kitu chochote kile atakachotakiwa kurudisha. [12] Hata hivyo, baada ya kulaumiwa na wenzake, aliachana mawazo hayo hayo, na hatimae akakubaliana na Imamu Ali (a.s). [13] Kwa mujibu wa watafiti, Ash'ath alihamia Kufa, na Imamu (a.s) naye akampigia hisabu ya mali alizpora na kumnyang'anya mali hizo na kuzirudisha kwenye Baitul Mal, kisha kumvua uongozi aliokuwa nao. [14] Matini ya Barua kwa Kiarabu أَمَّا بَعْدُ فَلَوْ لَا هَنَاتٌ كُنَّ فِيكَ كُنْتَ الْمُقَدَّمَ فِي هَذَا الْأَمْرِ قَبْلَ النَّاسِ وَ لَعَلَّ أَمْرَكَ يَحْمِلُ بَعْضُهُ بَعْضاً إِنِ اتَّقَيْتَ اللَّهَ ثُمَّ إِنَّهُ كَانَ مِنْ بَيْعَةِ النَّاسِ إِيَّايَ مَا قَدْ بَلَغَكَ وَ كَانَ طَلْحَةُ وَ الزُّبَيْرُ مِمَّنْ بَايَعَانِي ثُمَّ نَقَضَا بَيْعَتِي عَلَى غَيْرِ حَدَثٍ وَ أَخْرَجَا أُمَّ الْمُؤْمِنِينَ وَ سَارَا إِلَى الْبَصْرَةِ فَسِرْتُ إِلَيْهِمَا فَالْتَقَيْنَا فَدَعَوْتُهُمْ إِلَى أَنْ يَرْجِعُوا فِيمَا خَرَجُوا مِنْهُ فَأَبَوْا فَأَبْلَغْتُ فِي الدُّعَاءِ وَ أَحْسَنْتُ فِي الْبَقِيَّةِ وَ إِنَّ عَمَلَكَ لَيْسَ لَكَ بِطُعْمَةٍ وَ لَكِنَّهُ أَمَانَةٌ وَ فِي يَدَيْكَ مَالٌ مِنْ مَالِ اللَّهِ وَ أَنْتَ مِنْ خُزَّانِ اللَّهِ عَلَيْهِ حَتَّى تُسَلِّمَهُ إِلَيَّ وَ لَعَلِّي أَلَّا أَكُونَ شَرَّ وُلَاتِكَ لَكَ إِنِ اسْتَقَمْتَ وَ لا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّهِ Tafsiri kwa Kiswahili Ama baad (ama baada ya hayo), elewa ya kwamba; lau kama si kasoro chache zilizojitokeza kutoka kwako, basi wewe ungalikuwa ndiye wa kwanza kupewa nafasi katika jambo hili (yaani kuongoza) kabla ya watu wote. Ila huenda ukafanya mambo yatakayo kukomboa na kufunika makosa iwapo utakuwa ni mcha Mungu. Pia bila shaka, tayari utakuwa umeshapata habari za watu kunipa bai’a (kunikubali kama ni kiongozi). Talha na Zubair walikuwa miongoni mwa wale walionipa bai’a, kisha wakaiivunja bai’a yao bila ya sababu yoyote halali. Wakamtoa Ummu Al-Muuminia nyumbani kwake na kuelekea Basra. Nami nikafuatilia safari yao hadi tukakutana na kukabiliana. Niliwanasihi warejee katika haki waliyoachana nayo, lakini wakakataa. Nilifanya juhudi kubwa katika kuwalingania huku nikitumia njia bora za hisani katika yaliyobaki. Bila shaka, kazi yako si tongo au fursa ya kujinufaisha, bali ni amana. Na mikononi mwako mna mali za Mwenye Ezi Mungu, nawe ni miongoni mwa wahifadhi na walinzi wa mali hiyo mpaka urudishe hesabu yake kwangu mimi. Huenda mimi nisiwe mtawala mbaya zaidi kwako ikiwa utasimama kwenye mstari wa haki. Na hakuna nguvu ila kwa uwezo wa Mwenye Ezi Mungu (walaa haula walaa quwwatan illa Billahi). [15]