Bab Hitta

Kutoka wikishia
Mlango wa Yerusalemu, unaojulikana kama Bab Hatta.

Bab Hatta (Kiarabu: باب حطة) ni mlango kutoka Yerusalemu, unaojulikana kwa jina la Bab Hatta. Ni mlango ambao Waisraeli walipaswa kuupitia baada ya kutangatanga katika nchi ya Tiye. Walipoingia katika nchi takatifu, iliwabidi kupita katika mlango huu kwa kusema neno «Hatah» ili kusamehewa dhambi zao. Wafasiri wengi wamechukulia Bab Hatta kama moja ya milango ya Jerusalemu huko Palestina. Katika Hadithi za Shia na Sunni, Imam Ali (a.s) na Ahlul-Bayt (a.s) wanalinganishwa na mlango huu

Amri kwa Waisraeli

Kwa mujibu wa aya za Qur'ani, wana wa Israeli walipokuwa wakienda kuingia katika mojawapo ya miji ya Ardhi Takatifu, iliwabidi waingie kupitia mlango maalum kwa amri ya Mwenye ezi Mungu na kutamka neno «Hatta». [2] Wafasiri wengi [3] hata wafasiri waliokiita kijiji hicho mji wa «Jeriha» [4] wamewafikiana na kunukuu kuwa «Al-Bab» yaani mlango ni moja ya milango ya Jerusalemu.[5]

Neno Hatah maana yake ni kuteremsha cheo, kuondoa mzigo wa wajibu au dhambi kutoka kwenye mabega ya mtu.[6]

Mfano wa Ahlul-Bayt kwa Bab Hatta

Katika vyanzo vya Kishia, Ahlul-Bayt (a.s) wamelinganishwa na Bab Hatta, imeelezwa katika riwaya kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba:

Yeyote anayeshika dini yangu na akafuata njia yangu na akafuata Sunnah zangu ni lazima aamini utukufu wa maimamu wa Ahlul-Bayt wangu juu ya mataifa yote. Mfano wao miongoni mwa taifa hili ni kama «Bab Hatta» miongoni mwa Waisraeli.[7]

Pia kuna riwaya kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) iliyonukuliwa na Abu Saeed Khodri katika vyanzo vya Ahlu-Sunnah wa Al-Jama’a:

Mfano wa Ahlul-Bayt wangu miongoni mwenu ni kama mfano wa Bab Hatta katika Wana wa Israili, atakayeingia humo atasamehewa.[8]

Wamesema kuhusu mfano huu: Kama vile Sura ya Hatah ilivyokuwa kipimo cha imani kwa Waisraeli, Hadhrat Ali (a.s) na Ahlul-Bayt (a.s) pia ni kipimo cha imani ya Umma wa Mtume Muhammad (s.a.w.w). [9] Kwa sababu Ahlul-Bayt (a.s) ni mlango ambao yeyote miongoni mwa Wana wa Israili hukimbilia, husamehewa madhambi yake, na atakayejikinga kwa Ahlul-Bayt wa Mtume (a.s) ataokolewa. .[10]

Rejea

Vyanzo