Aya ya Amana
Aya ya Amana (Kiarabu: آية الأمانة) (Ahzab: 72): Ni Aya inayo zungumzia wajibu (uzito) wa amana ambao Mwenyezi Mungu ameuweka juu shingo ya mwanadamu. Kulingana na Aya hii, kwanza kabisa Mwenye Ezi Mungu aliitaka amana hiyo ichukuliwe mbingu, ardhi, pamoja na milima, lakini vitu hivyo havikukubali kubeba jukumu la amana hiyo. Ila binadamu aliikubali na kuwajibika nayo. Wafasiri wa Kiislamu wamejadili sana kuhusiana na maana hasa ya amana hii, na ni kwa nini mbingu, ardhi, na milima havikuikubali, bali binadamu ndiye aliyekubali kuwajibika nayo.
Kulingana na tafsiri za Kishia, maana ya amana ni Wilaya, yaani kuukubali utawala wa Ahlul-Bayt (a.s) (Maimamu wa Kishia (a.s)), pamoja na uongozi wa bwana Mtume (s.a.w.w). Lakini wafasiri wa Kisunni wameifasiri amana iliyo tajwa katika Aya hiyo, kwa maana ya majukumu ya kidini. Ayatullah Tabatabai anaamini kuwa; amana hiyo ni Wilaya, yaani ni mamlaka ya uongozi wa Mwenyezi Mungu, au kwa lugha nyengine ni Ukhalifa kwa niaba ya Mungu, Ukhalifa ambao ni binadamu pekee anayestahiki kuwa nao miongoni mwa viumbe wa Mwenye Ezi Mungu. Hii ni kwa ni sababu ya kwamba; ni binadamu tu ndiye mwenye uwezo wa kufikia kiwango cha juu cha ukamilifu miongoni mwa viumbe wake.
Umashuhuri wa Aya katika Utamaduni wa Kiislamu
Aya ya 72 ya Sura ya Al-Ahzab imewavutia sana watafsiri wa Kiislamu. Wafasiri wa pande zote mbili za Shia na Sunni, wamejadili kwa kina kuhusu maana ya amana hii, na kwa nini mbingu na ardhi havikukubali kubeba jukumu la amana hii, na badala yake binadamu ndiye aliyekubali kuwajibika nayo. [1] Hata katika hadithi pia kumejadiliwa maana ya amana ilikuja katika Aya hii. Zaidi ya hayo, katika fasihi ya irfani (ya Kisufi), pia kuna wasomi na waandishi kadhaa kama vile; Hafez, Rumi, na Khwaja Abdullah Ansari walio zungumzia jambo hili.
Kwa mfano Hafidh Shirazi amesema:
Maulana Jalalu al-Ddiin Balkhi pia naye amesema:
Khwaja Abdullah Ansari katika mazungumzo yake na Mola wake anasema:
Matini ya Aya na Tafsiri yake
إِنَّا عَرَضْنَا الْأَمَانَةَ عَلَى السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَالْجِبَالِ فَأَبَيْنَ أَنْ يَحْمِلْنَهَا وَأَشْفَقْنَ مِنْهَا وَحَمَلَهَا الْإِنْسَانُ إِنَّهُ كَانَ ظَلُومًا جَهُولًاKwa hakika sisi tumeitangaza amana mbele ya mbingu, ardhi na milima, navyo vikakataa kuwajibika na amana hiyo, na vikaikhofu amana hiyo, na mwanadamu akakubali kuwajibika nayo, kwa hakika yeye ni mjinga aliye dhalimu.
Surat al-Ahzab: 72.
Nini Maana ya Amana?
Swali muhimu lililoko katika vitabu vya tafsiri vya Waislamu ni udadisi juu ya maana ya amana. Kumekuwepo na maoni tofauti yaliyo tolewa na wanazuoni juu ya maana ya neno «amana». Miongoni mwao ni; mamlaka ya utawala na Uimamu wa bwana Mtume (s.a.w.w) pamoja na Maimamu wa Kishia (a.s.), [6] majukumu ya kidini, [7] uongozi wa Kiungu juu ya wanadamu, [8] akili, shahada ya kutamka na kuamini kwamba; hapana Mola isipokuwa Allah, [9] viungo vya mwili [10] na amana za wengine walizotupa kuwahifadhia. [11]
Kulingana na tafsiri za Shia zinazotegemea vyanzo vya Hadithi za Mtume na Maimamu wa Shia (a.s), inaelezwa kwamba; maana ya amana ni mamlaka ya utawala na Uimamu wa Ahlul-Bayt (a.s) pamoja na kuwatii na kuwa na upendo nao. [12] Katika tafsiri za Sunni, imeelezwa ya kwamba; maana ya amana ni majukumu ya kisheria ambayo Allah amemwekea binadamu. [13] Mwandishi wa Kishia wa Tafsiri Tabrasiy pia naye anaunga mkono maoni haya.
Kulingana na maoni ya Sayyid Muhammad Hussain Tabatabai mwandishi wa Tafseer al-Mizan ni kwamba; maana halisi ya amnaa hiyo, ni uongozi mkamilifu ulio wekwa juu ya shingo ya mwanadamu, yaani Ukhalifa wa kuitawala ardhi, hii ni kotokana na kwamba yeye ndiye kiumbe pekee mwenye uwezo wa kufikia cheo hicho kupitia itikadi kamili na amali njema, na kwamba hakuna kiumbe mwengine yeyote yule awezaye kuifikia daraja hiyo. [15]
Tabatabi akisisitiza imani hiyo, amenukuu Hadithi kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s), ambayo kwa mujibu wake ni kwamba; Maana ya amana ni Mamlaka ya Utawala wa Ali bin Abi Talib kutoka nasaha ya imamu Swadiq (a.s). Yeye akifafanua Hadithi hiyo amesema kwamba; uongozi wa Ahlul-Bayt ni mwendelezo wa Uongozi huo mkamilifu aliowajibishwa na mwanadamu katika Aya hiyo. [17]
A
Moja ya maswali ambayo wafasiri wanajiuliza kuhusiana na Aya ya amana, ni maana halisi ya kuitangaza amana na nini kusudio la amana kwa ajili ya mbingu, ardhi na milima? Kuna mawazo tofauti kuhusiana na suala hili, baadhi ya wafasiri wameelemea kwenye maana dhahiri ya kilugha, na wengine wameelea kwenye batini. Maana hizo ni kama ifuatavyo:
Maana Dhahiri ya Kilugha
Kulingana na moja ya Hadithi ambayo imekuwa ikirejelewa katika tafsiri za Shia zitegemeazo msingi wa Hadithi, ni kwamba; Mungu alisema kuziambia mbingu, ardhi na milima ya kwamba, Muhammad na Ahlul-Bayt wake ni marafiki zangu, wawakilishi wangu, na viongozi wangu juu ya watu. Hakuna kiumbe chochote kinachopendwa zaidi nami kuliko wao, na uongozi wao ni amana yangu miongoni mwa viumbe vyangu. Basi ni yupi anayetaka kuwajibika juu ya kubeba uongozi huu – ukiachana na wao nilio wachagua? Viumbe wate wasio kuwa waliogopa na kukhofia kukubali jukumu hili lenye umuhimu mkubwa kama huo. [18]
Katika baadhi ya tafsiri za Sunni pia imeelezwa kwamba; Mwenye Ezi Mungu aliziuliza mbingu, ardhi, na milima akaviambia; Jee hivi mnaweza kutimiza majukumu haya ya kidini? Navyo vilijibu kuuliza ni nini fungu lao watakalo pata katika kutimiza majukumu hayo. Mwenye Ezi Mungu akasema; Mtalipwa thawabu iwapo mtaweza kwenda sawa na njia hiyo, lakini mtakapoelekea upotovuni, basi malipo yenu itakuwa ni adhabu. Vitu hivyo vikaamua kukataa majukumu hayo kwa sababu vilikhofia visingeweza kutii sheria hizo, lakini binadamu akakubali kubeba jukumu hilo. [19]
Maana Batini (Maana ya Kimajazi)
Allama Tabatabi anasema kuwa; Maana ya kauli isemaye: Tumeikabidhi (tumeitangaza) amana hii mbele ya mbingu, ardhi na milima inamaanisha mlinganisho wa kulinganisha uwezo wa binadamu na mbinguni, ardhi na milimani. Na maana yake ni kwamba, licha ya ukubwa wa vitu hivyo, havikuwa na uwezo wa kukubali amana ya Mungu (yaani utawala (Ukhalifa) wake), na ni binadamu tu ndiye aliyekuwa na wa kukubali na kubeba utawala wa Kiungu juu yake na kuwa na uwezo wa kufikia daraja za juu kabisa za ukamilifu. [20]
Kwa mujibu wa maoni ya Alusi, ambaye ni mmoja miongoni mwa wanazuoni wa Sunni, ni kwamba; Katika Aya hii, Mungu ametumia lugha ya tamthilia na amefanya hivyo ili kuonyesha umuhimu wa amana ya mbinguni (ya Mungu), yaani majukumu ya kidini na ugumu wake. Pia yaonesha kwamba; binadamu ameikubali amana hiyo kwa hiari yake; na kama vile mbingu, ardhi na milima vilivyo amua kukataa kubeba jukumu hilo, yeye pia angekuwa na uwezo wa kulikataa jukumu hilo. Kulingana mawazo ya Alusi, Mwenye Ezi Mungu katika Aya hii, amedhamiria kuonesha umuhimu mkubwa wa amana ya mbinguni kupitia ligha hii ya kimifano, na amesema ya kwamba; kutimiza majukumu ya sheria ni jambo muhimu mno, kiasi ya kwamba, licha ya nguvu za mbingu, ardhi na milima, lau zingelikuwa na akili welewa wa kufahamu mambao, basi katu zisingekubali kubeba jukumu hilo. [21]
Kwanini
Kulingana na mfasiri mkuu ajulikanaye kwa jina laTabatabai, ni kwamba; Mwenyezi Mungu amemtaja mwanadamu kwa sifa ya udhalimu na ujinga ili kuonyesha kuwa mwanadamu anaweza kujidhulumu mwenyewe endapo hatozingatia umuhimu wa amana hiyo na asitambue kuwa adhabu kubwa inamsubiri kutokana na kuto wajibika na amana hiyo. Lakini maana ya msemo huu si kwamba watu wote wana sifa kama hizo; badala yake inamaanisha kuwa; mwanadamu ana uwezo wa kufikia daraja za kielimu na uadilifu, kama vile pia alivyo kuwa na uwezo wa kuwa na udhalimu na ujinga. [22] Hili pia ndio moja miongoni mwa maana zilizo orodheshwa na Fakhruddin Razi mfasiri wa Sunni, kuhusiana na maana ya Aya hii. [23]
Kwa mujibu wa tafsiri na welewa wa Alusi ambaye ni mfasiri wa Kisunni, ni kwamba; Kutajwa kwa udhalimu na ujinga wa mwanadamu katika Aya hiyo, kunamaanisha kuwa, watu wengi hawawezi kutimiza amana hii na kutenda wajibu wao wa kidini. Hii ndiyo sababu ya Aya hiyo kufuatiwa na tangazo lisemalo kwamba; Mwenyezi Mungu atawaadhibu wanafiki na washirikina na atakubali toba za waumini. [24]
Vyanzo
- Ālūsī, Maḥmūd b. ʿAbd Allāh al-. Rūḥ al-maʿānī fī tafsīr al-Qurʾān al-ʿaẓīm. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1372 AH.
- Abū l-Futūḥ al-Rāzī, Ḥusayn b. 'Alī. Rawḍ al-Jinān wa Rawḥ al-Janān fī Tafsīr al-Qurʾān. Qom: 1404 AH.
- ʿAlāʾ al-dawla simnānī, Aḥmad. Al-ʿUrwa li ahl al-khalwa wa al-jalwa. Tehran: 1362 SH.
- ʿĀmilī, Ibrahim. Tafsir ʿĀmilī. Mashhad: 1363 SH.
- Baḥrānī, Hāshim b. Sulaymān al-. Al-Burhān fī tafsīr al-Qurʾān. Tehran: Bunyād-i Biʿthat, 1416 AH.
- Fakhr al-Rāzī, Muḥammad b. al-ʿUmar al-. Al-Tafsīr al-Kabīr. Beirut: 1405 AH.
- Ghazālī, Muḥammad. Mukashifat al-qulub. Beirut: 1402 AH.
- Ḥaydar Āmulī, Jāmiʿ al-asrār. By the efforts of Henry Corbin and Uthman Ismāʿil Yaḥyā, Tehran: 1368 SH.
- Ḥuwayzī, ʿAbd ʿAlī b. al-Jumʿa al-. Tafsīr nūr al-thaqalayn. Edited by Hāshim Rasūlī. Qom: 1385 AH.
- Ibn Arabī, Muḥammad. Aḥkām al-Qurʾān. By the efforts of ʿAlī Muḥammad Bajāwī, Beirut: 1387 AH.
- Ibn Arabī, Muḥyiddīn. Futūḥat al-makkīyya. By the efforts of Uthman Yaḥyā. Cairo: 1392 AH.
- Istarābādī, ʿAlī. Taʿwil al-āyāt al-zāhira. Qom: 1409 AH.
- Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Beirut: 1403 AH.
- Mawlawī. Mathnawī maʿnawī. By the efforts of Nicholson. Tehran: 1363 SH.
- Maybudī, Aḥmad b. Muḥammad. Kashf al-asrār. Tehran: 1357 SH.
- Nasafī, ʿIzz al-Dīn. Al-Insān al-kāmil. By the efforts of Mari Juan mole. Tehran: 1403 AH.
- Sulṭān ʾAlīshāh. Bayān al-saʾāda fī maqāmāt al-ʾibāda. Tehran: Dānishgāh-i Tehrān, 1344 Sh.
- Ṭabāṭabāʾī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: 1394 AH.
- Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Majmaʿ al-bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: 1408 AH.
- Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Tafsīr-i Ṭabarī. [n.p].
- Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Majmaʿ al-bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Tehran: Farāhānī, 1360 Sh.
- Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Tafsīr-i jawāmiʾ al-jāmiʾ.
- Ṭabāṭabāʾī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Translated by Sayyid Muḥammad Bāqir Mūsawī. Qom: Intishārāt-i Islāmī, 1363 Sh.