Nenda kwa yaliyomo

Allahumma Il'an Qatalata Amiril al-Muuminina

Kutoka wikishia

Allahumma Il'an Qatalata Amirul al-Muuminina (Kiarabu: اللهم العَن قَتَلَةَ أمير المؤمنين) Ni ibara itokanayo na lugha ya Kiarabu, ambayo inamwomba Mwenye Ezi Mungu kuwalaani wauaji wa Ali bin Abi Talib (a.s). Ibara hii yafasirika Kiswahili kwa ibara isemayo: “Ewe Allah, walaani wauaji wa Amir al-Mu’minina”. Chanzo hasa cha ibara hii kinatoka kwenye vipengele vya maombi yaombwayo wakati wa kumzuru Imamu Ali (a.s).[1] Sheikh Abbas Qummiy ameiorodhesha ibara hii katika mlango wa amali zitendwazo ndani ya usiku wa kuamkia mwezi 19 Ramadhani, na akaidhinisha kusomwa ibara hii mara 100 ndani ya usiku huo.[2]

Kwa mujibu wa Ayatollah Khamenei ni kwamba; neno “qatalata” «قتلة» lina maana wauaji zaidi ya mmoja, kwa hiyo mbali na Ibn Muljam ambaye alimpiga Ali (a.s) kwa upanga, pia ibara hii inawaingiza na kuwapa hukumu moja, wale wote waliohusika na kusababisha tukio hilo; ikiwa ni pamoja na wale waliosababisha Ali bin Abi Talib kupitisha makubaliano ya kusimamisha vita kwenye uwanja wa Siffin. Jambo ambalo lilimweka madarakani Muawiya. Hivyo basi laana hii inawalenga wale wote waiojenga msingi wa dhulma dhidi yake, ambao kiuhasilia ndio chanzo kilichopelekea kifo chake.[3] Muhsin Qiraati, mwanazuoni wa Kiislamu na mfasiri wa Qur’ani wa madhehebu ya Shia, pia ameelezea kwamba; neno “qatalata” «قتلة» linamaanisha mkondo, fikra, na kundi ambalo Ibnu Muljam al-Muradi alikuwa ndiye mwakilishi wake.[4] Pia katika kazi zake nyengine za kimaandishi, amesema kwamba neno “qatalata” «قتلة» limetumika katika kuwajumuisha wale wote walioridhia mauaji ya Imam Ali (a.s).[5]

Kulingana na jibu lililotolewa na Mirza Javad Tabrizi, aliyo yatoa kuhusiana na maswali yanayo fungamana na Sala ni kwamba; hakuna tatizo mtu kuisoma dua hii katika qunuti ya Sala yake au katika sijda.[6]

Rejea

  1. Ibnu Qauluyeh, Kamil al-Ziyarat, 1356 S, uk. 44.
  2. Qummiy, Kuliyat Mafatih al-Jinan, 1384 S, Amali Makhsus Shab-haye Qadr, uk. 366.
  3. Bayanat Dar Khutbehaye Namaz Jum-e Tehran, 21 Mehr 1385 S.
  4. «Shab Qadr», Markaz Farhangy Darsa-haye Az Qur'an.
  5. «Thabit Hameye Amali Insan Dar Duniya», Markaz Farhangy Darsa-haye Az Qur'an.
  6. Tabrizi, Taaliqat Bar Sirat al-Najat, 1433 H, juz. 2, uk. 609.

Vyanzo

  • Bayanat Dar Khutbehaye Namaz Jum-e Tehran, 21 Mehr 1385 S. Paygah Itilai Resani Daftar Hifdh wa Nashr Athar Ayatullah al-Udhma Khamenei, Murur Khabar 14 Farvardin 1403 S.
  • Tabrizi, Mirza-Jawad, Taaliqat Bar Sirat al-Najat Fi Aj-wibat al-Istiftaat, Dar al-Sidiqat al-Shahidat, Qom, 1433 H.
  • «Thabit Hameye Amali Insan Dar Duniya», Markaz Farhangy Darsa-haye Az Qur'an, Tarikh Bakhsh, 16 Urdibehesht 1400 S, Tarikh Bazdid: 13 Farvadin 1403 S.
  • «Shab Qadr», Markaz Farhangy Darsa-haye Az Qur'an, 15 Urdibehesht 1367 S, Tarikh Bazdad: 13 Farvardin 1403 S.
  • Qummiy, Sheikh Abas, Kuliyat Mafatih al-Jinan, Qom, Matbuat Dini, 1384 S.