Nenda kwa yaliyomo

Aljaru Thumma Al-Daru

Kutoka wikishia
Faili:نقاشی الجار ثم الدار.jpg

Al-Jara Thumma Al-Dara (Kiarabu: اَلْجارَ ثُمَّ الدّار) Kauli hii yenye maana ya Kwanza jirani kisha nyumba, imetokana matini ya Hadithi maarufu [1] kutoka kwa Bibi Fatma (a.s). [2] Kwa mujibu wa Riwaya iliyonukuliwa kutoka kwa Imamu Hassan (a.s), ni kwamba; mama yake (Bibi Fatma) alisimama usiku wa Ijumaa kucha hadi alfajiri akimwabudu Mola wake. Akiwa katika Miharabu yake alionekana akiwambea dua waumini wote wake kwa waume huku akiwataja kwa majina yao katika dua zake. Hata hivyo, hakuonekana kujijumuisha yeye mwenye katika dua hiyo. Pale Imamu Hassan alipohoji ni kwa nini hakujiombe dua kama alivyofanya kwa wengine, Bibi Fatma alijibu kwa kusema, Mwanangu! Al-Jara Thumma Al-Dara (اَلْجارَ ثُمَّ الدّار) kwa maana ya kwamba: Jirani kwanza, kisha nyumba. [3] Hadithi hii inatoa somo la kina kuhusiana na umuhimu wa kuwajali wengine kabla ya kujali maslahi binafsi. Pia inaonesha moyo wa ukarimu, huruma, na uwajibikaji kwa jamii, jambo linalosisitiza misingi ya mshikamano na uadilifu wa kijamii katika Uislamu. Msingi huu wa upendo kwa jirani unaimarisha maadili ya kijamii na utu, na hatimae kuleta mafanikio ya pamoja yenye thamani zaidi kuliko mafanikio binafsi.

Sheikh Saduku, katika mlango wa 145 wa kitabu chake Al-‘Ilalu al-Shara'I, amenukuu hadithi mbili zenye misururu tofauti ya wapokezi ambazo zinathibitisha usahihi wa nukuu ya kauli hii isemayo; اَلْجارَ ثُمَّ الدّار (Jirani kwanza, kisha nyumba). Hadithi ya kwanza imenukuliwa kutoka kwa Imamu Hassan (a.s), na ya pili ni ile Hadithi iliyopokewa kutoka kwa Imamu Kadhim (a.s) anayoinukuu kutoka kwa babu zake. Ingawa Hadithi mbili hizi zina misururu tofauti ya wapokezi, ila bado znabali kuwa na madhumuni moja na maana sawa. [4] Sheikh Hur ‘Amili, katika kitabu chake Wasailu al-Shia, ameweka mlango maalumu unaozungumzia jambo hili la kuomba dua kwa ajili ya waumini wengine kabla ya kujiombea mwenyewe, akibainisha kuwa ni kitendo kinachopendekezwa katika Uislamu. Mwanazuoni huyu amezitumia hadithi mbili hizi kama ushahidi wa kuimarisha mtazamo huu, [5] akithibitisha kuwa kitendo hichi kinadhihirisha kuwepo kwa upendo, huruma, na mshikamano ndani ya jamii ya Kiislamu. Hivyo, mtazamo huu unasisitiza umuhimu wa kutafuta kheri za pamoja na kuimarisha udugu wa kidini kwa kutanguliza maslahi ya wengine.

Sayyid Ali Khan Madani, katika kitabu chake cha lugha, ameinukuu sentensi isemayo: “Al-Jar Thumma Al-Dar” samaba na methali nyengine zinayohusiana na umuhimu wa kumtambua na kumjali jirani kabla ya kuamua kuishi mahali fulani au kununua nyumba katika eneo maalumu. [6] Kule Madani kuiitumia Hadithi hii katika muktadha unaohusiana na majirani, unasisitiza uzito ujumbe wa Hadithi hii katika kuonesha umuhimu wa kujenga uhusiano mzuri na majirani bila ya kuzingatia Nafasi zao (za umaskini au utajiri) katika jamii zao. Kwa mujibu wa mafundisho haya, mahusiano ya kijamii yanapaswa kupewa kipaumbele kabla ya masuala binafsi. Katika vitabu vya Hadithi kama vile Al-Kafi na Tuhaf al-Uqul, kuna Riwaya kadhaa za Imam Ali (a.s) akisisitiza msimamo huo huo kuhusiana na umuhimu wa kumjua jirani kabla ya kufanya uamuzi wa kuchagua makazi katika eneo fulani. Kauli za Imamu Ali (a.s) katika suala hili, zinawiana na zile za Bibi Fatima (a.s), [7] jambo linalo onesha kwamba; kuishi katika jamii yenye mshikamano na maelewano ni bora zaidi kuliko kuishi bila kujali utu na maslahi ya pamoja. Mtafiti wa taaluma za Hadithi, Mahdi Mehrizi, amejitahidi kutafiti hali ya mazingira na zama za Hadithi hii, ili kupata welewa halisi wa muktadha wa Hadithi, na hatimae kupata tafsiri sahihi. katika chambuzi zake anaeleza akisema kwamb; wakati mwingine maneno yanayofanana yanaweza kuwa na maana tofauti kulingana na zama pamoja na mazingira tokeo lilipelekea kutamkwa kwa maneno hayo. [8] Pia, imeezwa kwamba; sentensi hii inatumika kwa maana zake mbili katika lugha ya Kifarsi na tamaduni zake, (yaani kwa maana ya kujali majirani na kwa maana ya kutahadhari kabla ya kuchagua mahala pa kuishi). Mwandishi wa kitabu Al-Ikhtisas amenukuu kutoka kwa Al-Awza'i, mwanazuoni mashuhuri wa upande wa Ahlu-Sunnah, ambaye ameitaja hii ya Al-Jar Thumma Al-Dar kama ni moja ya nasaha za Luqman Hakim kwa mwanawe. Jambo linalo onesha umuhimu wa kutanguliza mahusiano ya kijamii na jirani kabla ya kuzingatia manufaa binafsi. [10]

Imelezwa ya kuwa baadhi ya wanazuoni wa elimu ya maadili na washairi maarufu akiwemo Attar Nishaburi na Ghazali, wameinukuu ibara hii maarufu isemayo: Al-Jar Thumma Al-Dar na kuinasibisha na Rabi'a Adawiyya, mtawa maarufu wa Kisufi wa karne ya pili Hijria. [12] Baadhi ya watafiti, kwa kutegemea vyanzo vya Hadithi na maelezo ya Bibi Fatima (a.s), wamekataa dai hili. [13] Wataalamu wa elimu ya tasawwuf wamefafanua wakisema kwamba; tafsiri ya kauli hii ni kumtanguliza na kumweka Mwenye Ezi Mungu mbele kabla ya tamaa ya Pepo, na kumwabudu kwa ikhlasi ya kina bila kujali uwepo wa Pepo hiyo. [14]

Rejea

Vyanzo