Ali Hubbuhu Junna
Ali Hubbuhu Junna (Kiarabu: علي حبه جنة) ni beti za mashairi kuhusiana na daraja na fadhila za Imamu Ali bin Abi Twalib (a.s) ambazo zinanasibishwa na Muhammad bin Idris Shafi’i mmoja wa mafakihi wa moja ya madhehebu nne za Ahlu Sunna. Beti hizi za mashairi zinaashiria kwamba, kumpenda Ali (a.s) ni kinga ya kutoingizwa motoni na kwamba, yeye Imamu Ali (a.s) ndiye mgawaji wa pepo na moto. Sehemu nyingi ya beti hizi mbili za mashairi zinaashiria kwamba, Imamu Ali (a.s) ndiye wasii na mrithi wa haki wa Mtume (s.a.w.w) na kwamba, yeye ndiye kiongozi na Imamu wa watu na majini. Mbali na Shafi’i kumetajwa watu wengine kwamba, walitunga beti hizi mbili za mashairi.
Madhumuni na maana ya beti hizi za mashairi imenukuliwa katika vyanzo vya Kishia na Kisunni. Kadhalika shairi hili au baadhi ya beti zake limetumiwa pia katika beti za mashairi ya washairi wengine. Beti za shairi la “Ali Hubbuhu Junna” zimeandikwa katika Rawdha ya Haram ya Imamu Ali (a.s).
Shairi, tarjuma na maudhui yake
Kumpenda Ali ni kinga (ya kutoingizwa motoni), Mgawaji wa moto na pepo, Wasii wa haki wa Mustafa (Mtume (s.a.w.w)), Imamu (kiongozi) wa watu na majini. [2]
Katika sehemu ya kwanza ya shairi hili, kunaashiriwa kwamba, mapenzi kwa Ali ni kinga. Katika lugha Junna ina maana ya silaha [3] au kinga na ngao [4] ambayo inamzuia na kumhifadhi mtu asidhuriwe. Baadhi wamelitambua neno hili kwamba, ni kila kitu ambacho kinamkinga na kumhifadhi mtu. [5]
Maudhui katika beti ya kwanza yaani kukingwa na moto yaani kutoingizwa motoni kutokana na kumpenda Ali imenukuliwa katika hadithi mbalimbali kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) katika vyanzo vya Kishia [6] na vya Ahlu-Sunna [7]. Hata hivyo jambo hili limebainishwa pia kwa nukuu ya Omar bin al-Khattab [8] na katika baadhi ya vyanzo shairi lenye madhumuni na maana kama hii limenasibishwa na Khalifa wa Pili, (kwa mujibu wa itikadi ya Waislamu wa madhehebu ya Kisunni) Omar bin al-Khattab. [9]
Kutajwa Imamu Ali (as) kuwa ni mgawaji wa moto na pepo pia kumenukuliwa katika hadithi kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) kuhusiana na Imamu Ali [10] na imenukuliwa pia katika mazungumzo yake Imamu Ali (a.s) mwenyewe [11] na Maimamu (a.s). [12] Aidha haya yanapatikana pia katika vyanzo vya Ahlu-Sunna [13] na baadhi kama Ibn Abil-Hadid katika ufafanuzi wake wa Nahaj al-Balagha ameitaja hadithi kuhusiana na maudhui hii kwamba, ni Mustafidh (hadithi ambayo ina mpokezi zaidi ya mmoja lakini haijafikia idadi ya wapokezi wa hadithi ya mutawatir). [14] Inaelezwa kwamba, Ahmad bin Hambal alitetea jambo hili. [15]
- Kadhalika angalia: Hadith Qasim al-Nar Wal-Jannah
Mshairi
Katika vyanzo shairi la “Ali Hubbuhu Junna” limenasibishwa na Muhammad bin Idris Shafi’i, mmoja wa mafakihi wa moja ya madhehebu nne za Ahlu-Sunna (150-204 Hijiria). [16] Aidha kuna watu kama Amir bin Tha’labah [17] au Ammar bin Taghlibah [18] ambaye naye ametajwa kuwa mtunzi wa shairi hili. Kadhalika katika vitabu vingine, beti za mashairi haya zimenukuliwa lakini bila ya kutaja mtunzi wake. [19]
Mashairi yanayofanana
Kuna beti za mashairi pia zilizotungwa ambazo madhumuni yake inafanana na beti hizi za mashairi zinazotaja mapenzi kwa Imamu Ali (a.s) kuwa ni kinga ya motoni na kwamba, yeye ni mgawaji wa moto na pepo. [20]
Madhumuni ya shairi la “Ali Hubbuhu Junna” katika kumsifu Imamu Ali (a.s) ilitumika katika waandishi waliokuja baadaye [24] na baadaye baadhi ya washairi kama Attar Neyshabouri [25] na Mussa bin Ja’far Husseini Taliqani [26] wamenufaika na beti mbili za shairi hili katika mashairi yao.
Mwaka 1376 Hijria Shamsia milango miwili ya dhahabu iliwekwa katika Rawdha ya Imamu Ali (a.s) ambapo ilikuwa imeandikwa shairi la “Ali Hubbuhu Junna”. [27
Rejea
Vyanzo