Nenda kwa yaliyomo

Abraha

Kutoka wikishia

Abraha au Abraha al-Ashram (Kiarabu: أبرهة أو أبرهة الأشرم) alikuwa mfalme wa Yemen na kamanda wa (jeshi la) watu wa tembo (As'hab al-Fil) ambaye alikusanya jeshi la kuelekea Makka kwa ajili ya kuibomoa Kaaba. Hata hivyo alishindwa vibaya na ndege waliokuwa makundi kwa makundi na waliokuwa wakitupa mawe ya udongo wa motoni. Kutokana na majeraha makubwa aliyoyapa Abraha katika tukio hilo, baadaye aliaga dunia huko Yemen.

Abraha alikuwa mfuasi wa dini ya Ukristo na mtawala wa Yemen. Sababu na msukumo wa yeye kutaka kubomoa Kaaba ni kuvunjiwa heshima na mmoja wa Yemen kanisa alilokuwa amejenga ili kuzuia watu wasiende Makka na badala yake waelekee huko Yemen. Kupanua satwa na ushawishi wa Ukristo na kudhamini maslahi ya Roma na Uhabeshi (Ethiopia ya leo) pia yanahesabiwa kuwa yalikuwa miongoni mwa malengo ya Abraha ya kushambuliai Makka ili kubomoa nyumba ya Mwenyezi Mungu al-Kaaba.

Utambulisho

Abraha alikuwa mtu wa Habasha (Uhabeshi).[1] Alikuwa akiishi katika karne ya 6 Miladia, takribani katika mwaka aliozaliwa Mtume (s.a.w.w).[2] Abraha aliwashinda Wayamen na kuwa mfalme wa eneo hilo.[3]

Abraha alifahamika kwa jina la Ashram (mwenye pua na mdomo wenye shimo) kutokana na majeraha aliyokuwa amepata katika vita.[4] Pamoja na hayo, katika Dalail al-Nubuwwah jina lake limesajiliwa kuwa ni "Abraha ibn Ashram".[5] Inaelezwa kuwa, Ashram halikuwa jina la baba yake.[6] Jina la baba yake limetajwa katika Mu'jam al-Buldan kuwa ni Sabah.[7]

Kadhalika Abraha alikuwa akiitwa kwa majina kama Abu Taksum,[8] Sahib al-Fil (mtu au mwenye tembo)[9] na Abraha Habashi.[10]

Kupeleka Jeshi Makka

Makala Asili: As'hab al-Fil
Mchoro Wenye Kuakisi As-hab al-fil, mchoraji Isfandiyan Ahmadie

Abraha akiwa na jeshi ambalo lilitanguliwa na tembo alianza safari kuelekea Makka ili akabomoe Kaaba.[11] Kwa mujibu wa Aya za Qur'an Tukufu walijitokeza ndege kutoka angani na kulishambulia jeshi la Abraha kwa mawe.[12] Baada ya jeshi la Abraha kushindwa lilirejea Yemen.[13] Abraha alikuwa amejeruhiwa na baada ya kurejeshwa Yemen akiwa na majeraha aliaga dunia huko Yemen.[14]

Mkasa na tukio la watu wa tembo la kuangamizwa jeshi lao kwa ndege waliokuwa makundi kwa makundi (Ababil) na waliokuwa wakitupa mawe ya udongo wa motoni (Sijjil) limeelezewa katika Qur’an Tukufu katika Surat al-Fil.[15]

Sababu ya Kutaka Kubomoa Kaaba

Abraha alikuwa mfuasi wa dini ya Ukristo[16] na akiwa na lengo la kuzuia safari za Waarabu wa Yemen kuelekea Makka, alijenga kanisa kubwa katika mji wa Sana'a na akalipamba vizuri kwa dhahabu na vito vya thamani na kuwalazimisha Wayemen wafanye ziara katika kanisa hilo.[17] Kanisa hilo lilikuwa likijulikana kwa jina la Qilis[18] na lilijengwa ili kuwazuia Waarabu wasisafiri kuelekea Makka.[19] Hata hivyo mmoja wa Wayamen alilivunjia heshima kanisa hilo. Ni kutokana na sababu hiyo, Abraha akaapa kwamba, ataiangamiza Kaaba.[20] Pamoja na hayo kumetajwa sababu nyingine za msukumo wa Abraha wa kutaka kubomoa Kaaba kwamba, ni kupanua satwa na ushawishi wa Ukristo katika maeneo ya magharibi na kusini mwa Peninsula ya Uarabuni (Saudi Arabia) na vilevile kudhamini maslahi ya kisiasa na kiuchumi ya Roma na Uhabeshi.[21]

Kutawala Yemen

Abraha alikuwa kamanda wa moja ya majeshi ambayo mtawala wa Uhabeshi aliyatuma Yemen ili yakaitwaie na kuidhibiti ardhi hiyo.[22] Jeshi jingine lilikuwa chini ya kamanda aliyejulikana kwa jina la Ariat.[23] Kwa mujibu wa baadhi ya nukuu ni kuwa, ni jeshi moja lililotumwa huko Yemen na lilikuwa chini ya Kamanda Ariat, na Abraha alikuwa miongoni mwa wanajeshi wa jeshi la Ariyat.[24]

Baada ya Yemen kukombolewa na jeshi la Uhabeshi[25] kukaibuka vita baina ya Abraha na Ariat. Abraha alimshinda Ariat na akawa mtawala wa Yemen.[26]

Kwa mujibu wa ripoti ya Mas'oudi, mtawala wa Uhabeshi alichukizwa mno na kitendo cha kuuawa Ariat na hivyo alichukua uamuzi wa kumshambulia Abraha ili amuangamize.[27] Hata hivyo Abraha alimtumia mtawala wa Uhabeshi zawadi zikiwa zimeambatana na barua ambamo ndani yake aliomba msamaha na kutangaza utii na uaminiifu wake kwa mfalme wa Uhabeshi.[28] Naye mfalme wa Uhabeshi akamsamehe.[29]

Rejea

  1. Maqrizi, Imta' al-Asma', juz. 4, uk. 68
  2. Bargenisi, Abraha, juz. 2, uk. 563
  3. Maqdisi, al-Bad'u wa al-Tarikh, Bursa'id, juz. 2, uk. 185
  4. Tabari, Tarikh al-Umam wa al-Muluk, juz. 2, uk. 129
  5. Baihaqi, Dalail al-Nubuwah, juz. 1, uk. 117
  6. Bargenisi, Abraha, juz. 2, uk. 563
  7. Yaqut Hamawi, Mujam al-Buldan, juz. 2, uk. 53
  8. Dhahabi , Tarikh al-Islam, juz. 1, uk. 164
  9. Sam'ani, al-Ansab, juz. 5, uk. 200
  10. Muqrizi, Imta' al-Asma', juz. 4, uk. 68
  11. Makarim Syirazi, Tafsir Nemuneh, juz. 27, uk. 335
  12. Tazama: Surat al-Fil
  13. Makarim Syirazi, Tafsir Nemuneh, juz. 27, uk. 335
  14. Ibnu Qutaibah, al-Ma'arif, uk. 638
  15. Surat al-Fil: 1-5
  16. Jawad Ali, al-Mufashshal fi Tarikh al-Arab Qabla al-Islam, juz. 6, uk. 184
  17. Baladhuri, Ansab al-Ashraf, juz. 1, uk. 67
  18. Ibnu al-Kalbi, al-Ashnam, uk. 46-47.
  19. Ibnu Kathir, al-Bidayah wa al-Nihayah, juz. 2, uk. 170.
  20. Baladhuri, Ansab al-Ashraf, juz. 1, uk. 67.
  21. Bargenisi, Abraha, juz. 2, uk. 569.
  22. Ibnu Kathir, al-Bidayah wa al-Nihayah, juz. 6, uk. 306
  23. Ibnu Kathir, al-Bidayah wa al-Nihayah, juz. 6, uk. 306
  24. Tabari, Tarikh al-Umam wa al-Muluk, juz. 2, uk. 125
  25. Yaqubi, Tarikh al-Yaqubi, juz. 1, uk. 200
  26. Ibnu Hisham, al-Sirah al-Nabawiyah, juz. 1, juz. 41
  27. Mas'udi, Muruj al-Dhahab, juz. 2, uk. 52
  28. Muqadas, Al-badiu wa Tarikh, Bursaid, juz. 3, uk. 185.
  29. Ibnu Hisham, al-Sirah al-Nabawiyah, juz. 1, uk. 42.

Vyanzo

  • Balādhurī, Aḥmad b. Yaḥyā al-. Ansāb al-ashrāf. Edited by Suhayl Zakār & Riyāḍ al-Ziriklī. 1st edition. Beirut: Dār al-Fikr, 1417 AH.
  • Bayhaqī, Aḥmad b. al-Ḥusayn al-. Dalāʾil al-nubuwwa wa maʿrifat aḥwāl ṣāḥib al-sharīʿa. Edited by ʿAbd al-Muʿṭī al-Qalʿajī. 1st edition. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1405 AH.
  • Bargnīsī, Kāzim. "Abraha", dāʾirat al-maʿārif buzurg-i Islāmī. volume 2. Tehran: Markaz-i Dāʾirat al-maʿārif buzurg-i Islāmī, 1368 Sh.
  • Dhahabī, Muḥammad b. al-Aḥmad al-. Tārīkh al-Islām. Edited by ʿUmar ʿAbd al-Salām al-Tadmurī. 2nd edition. Beirut: Dār al-Kitāb al-ʿArabī, 1409 AH.
  • Ibn Kalbī, Hishām b. Muḥammad. Al-Aṣnām. Tehran:Nashr-i Nu, 1364 Sh.
  • Ibn Qutayba al-Dīnawarī, ʿAbd Allāh b. Muslim . Al-Maʿārif. Edited by Tharwat ʿAkkāsha. Cairo: al-Hayʾat al-Misrīyya al-ʿĀmma li l-Kitāb, 1992 CE.
  • Ibn Kathīr al-Dimashqī, Ismāʿīl b. ʿUmar. Al-Bidāya wa l-nihāya. Beirut: Dār al-Fikr, 1407 AH-1986.
  • Ibn Hishām, ʿAbd al-Malik. Al-Sīra al-nabawīyya. Edited by Muṣṭafā al-Saqā, Ibrāhīm Ābyārī and ʿAbd al-Ḥafīz Shalbī. 1st edition. Beirut: Dār al-Maʿrifa, [n.d].
  • Jawād ʿAlī. Al-Mufaṣṣal fī tārīkh al-ʿarab qabl al-Islām. [n.p]: Dār al-Sāqī, 2001.
  • Masʿūdī, ʿAlī b. al-Ḥusayn al-. Murūj al-dhahab wa maʿadin al-jawhar. Edited by Asʿad Dāghir. 2nd edition. Qom: Dār al-Hijra, 1409 AH.
  • Maqdisī, Muṭahhar b. Ṭāhir. Al-Bidaʾ wa tārīkh. Port Said: Maktabat al-Thaqāfa al-Dīnīyya, [n.d].
  • Maqrizī, Aḥmad b. ʿAlī. Imtāʿ al-asmāʾ. Edited by Muḥammad ʿAbd al-Ḥamīd al-Namīsī. 1st edition. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmiyya, 1420 AH.
  • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tafsīr-i nimūna. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1374 Sh.
  • Samʿānī, ʿAbd al-Karīm b. Muḥammad. al-. Al-Ansāb. Edited by ʿAbd al-Raḥmān b. Yaḥyā al-Muʿallimī al-Yamānī. 1st edition. Hyderabad: Majlis Dāʾirat al-Maʿārif al-ʿUthmānīyya, 1382 AH/1962.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-.Tārīkh al-umam wa l-mulūk. Edited by Muḥammad Abu l-faḍl Ibrāhīm. 2nd edition. Beirut: Dar al-Turāth, 1387 AH.
  • Yāqūt al-Ḥamawī. Muʿjam al-buldān. 2nd edition. Beirut: Dār Ṣādir, 1995.
  • Yaʿqūbī, Aḥmad b. Abī Yaʿqūb al-. Tārīkh al-Yaʿqūbī. 1st edition. Beirut: Dār Ṣādir, [n.p].