Abdallah bin Misma' al-Hamdani

Kutoka wikishia

Abdallah bin Misma' al-Hamdani (Kiarabu: عبد الله بن مِسمَع الهَمْداني) (alikuwa hai mwaka 60 Hijria) alikuwa mmoja wa Mashia wa mji wa Kufa ambaye, pamoja na Abdullah bin Wal Taymi, waliwasilisha barua ya kwanza ya Mashia wa Kufa kwa Imamu Hussein (a.s) huko Makka. Kwa mujibu wa riwaya ya Muhammad bin Jarir Tabari (aliyefariki 310 Hijiria), mwanahistoria mashuhuri, katika Tarikh al-Umam wal-Muluk, akimnukuu Abu Mikhnaf mwanahistoria wa Kishia (aliyefariki 157 AH) ni kwamba, baada ya Mashia wa Kufa kusikia habari za kifo cha Muawiya bin Abi Sufyan (15 Rajab 60 Hijria), walikusanyika katika nyumba ya Sulaiman bin Sorad Khuzai mmoja wazee na shakhsia wakubwa wa Kishia na akawaambia kwamba, Hussein amekataa kutoa baia (kiapo cha utii) kwa Yazid, nyinyi ni Shia wa Hussein na baba yake, kama mtamsaidia basi mjulisheni. [1]

Kisha kundi hili likaandika barua kwa Hussein bin Ali (a.s) na kumuita aende katika mji wa Kufa, na kwa mujibu wa Muhammad bin Jarir al-Tabari, Abdullah bin Misma' Hamdani na Abdullah bin Wal waliwasilisha barua hiyo kwa Imamu Hussein (a.s) mnamo tarehe 10 Ramadhani 60 Hijria huko Makka. [2] Mwanahistoria wa Kishia Sheikh Mufidu (aliyefariki 413 H) pia amenukuu riwaya hii katika kitabu cha Al-Irshad na akaandika jina la aliyepeleka ujumbe huo kuwa ni Abdallah bin Misma' Hamdani. [3] Katika kitabu cha Akhbar al-Tawwal cha Ibn Qutaibah Dinawari (aliyefariki mwaka 283 Hijiria), jina lake ni Ubaidullah Ibn Sabi' al-Hamdani. [5]

Rejea

Vyanzo