Aba Saleh

Kutoka wikishia
Pete ya Haqiq iliyoandikwa Aba Saleh

Aba Saleh (Kiarabu: أبا صالح) ni kuniya ya Imam Mahdi (a.t.f.s) ambayo ilianza kutumika karne ya 11 Hijiria ikimuashiria mtukufu huyo. Neno hili na maneno yanayoshabihana nalo, «Saleh» na «Ba Saleh» yametumika katika hadithi kadhaa ambapo inausiwa kwamba, kama umepotea njia basi ita «Saleh», «Aba Saleh» au «Ya Ba Saleh» ili kuomba msaada. Lakini katika hadithi hizi hakujatajwa kama hizi ni katika kuniya na lakabu za Imam wa Zama na wataalamu wa elimu ya hadithi na wafafanuzi wake pia hawajazitambua kuwa ni kuniya za Imamu Mahdi.

Aba Saleh, Kuniya Inayo Nasibishwa kwa Imamu wa Zama

Aba Saleh ni kuniya mashuhuri ambayo inatumiwa kwa ajili ya Imamu Mahdi (a.t.f.s).[1] Kuniya hii haijatajwa katika hadithi na maandiko ya kale ya historia kwa ajili ya Imamu wa Zama,[2] isipokuwa katika vitabu vilivyokuja baadaye ambapo baadhi walimwita Imam wa Zama kwa wito wa Aba Saleh. Kwa mfano Mirza Hussein Nouri, mmoja wa Maulamaa wa Kishia wa karne ya 13 na 14 Hijiria ameandika, wazungumzaji wa lugha ya Kiarabu wanamtaja Imam Mahdi katika maombolezo na mashairi kwa jina la Aba Saleh.[3]

Historia ya Matumizi

Kwa mujibu wa kitabu cha Insaiklopidia ya Imam Mahdi, kuniya ya «Aba Saleh» ilianza kutumika kwa ajili ya Imam Mahdi kuanzia karne ya 11 Hijria na hakuna ripoti ya matumizi ya istilahi hii kuhusiana na Imam Mahdi kabla ya karne ya 11 Hijiria.[4]

Allama Majlisi (1110-1037) akinukuu hekaya kutoka kwa baba yake anasema, Bwana mmoja aliyejulikana kwa jina la Amir Is’haq Asterabad alipotea njia alipokuwa akielekea Makka na kwa kusema «Ya Saleh» au «Ya Aba Saleh Arshiduna» (Ewe Saleh au Ewe Aba Saleh, tuonyeshe njia), alimpata mtu ambaye alimsaidia na kumfikisha Makka ambapo anadhani kwamba, mtu huyo alikuwa ni Imam Mahdi (a.t.f.s).[5] Muhaddith Nouri pia amesema kuna uwezekano, matumizi ya kuniya ya Aba Saleh kwa ajili ya Imamu Mahdi yamechukuliwa katika hekaya na simulizi ya kupotea bwana mmoja katika njia ya kuelekea Hija ambapo kwa kusema, «Ya Aba Sale» aliokoka.[6]

Imekuja katika Iinsaiklopidia ya Imamu Mahdi kwamba, hakuna sababu ya kunasibishwa «Aba Saleh» na Imamu Mahdi (a.t.f.s) na kile ambacho kimepelekea kuenea kunasibishwa kwa lakabu hii na Imamu Mahdi, ni hekaya ambayo haina hoja ya maana hii.[7]

Matumizi ya Neno «Aba Saleh» Katika Hadithi

Bendera yenye nembo ya Aba Saleh Al-Mahdi katika Msikiti wa Jamkaran

Katika baadhi ya hadithi zilizopokewa na Waislamu wa madhehebu ya Shia maneno «Ba Saleh» na «Aba Saleh» yametumika; lakini hakuna mwanazuoni yeyote wa hadithi na mfafanuzi wa hadithi ambaye ameona kuwa makusudio ya maneno haya ni Imamu Mahdi. Kwa mfano imekuja katika hadithi iliyonukuliwa na Ahmad bin Muhammad bin Khalid Barqi (200-274 au 280) kutoka kwa Imam Swadiq (a.s) kwamba: Kila mara unapopotea njia, ita «Ya Saleh» au «Ba Saleh Arshidana Tariq Yarhamukuma llah» (Ewe Saleh, au Ewe Ba Saleh, tuonyesheni njia Allah akurehemuni).[8]

Kadhalika Sheikh Saduq (305-381 Hijiria) amenukuu kukiwa na tofauti kidogo:«Ya Saleh» au «Ya ABa Saleh Arshiduna Tariq Yarhamukum llah» (Ewe Saleh, au Ewe Aba Saleh, tuonyesheni njia Allah akurehemuni).[9] Kisha ananukuu hadithi nyingine ambayo kwa mujibu wake: Sehemu ya bara imekabidhiwa kwa «Saleh» na sehemu ya baharini imekabidhiwa kwa «Hamza».[10]

Imeelezwa kwamba, si Shekhe Saduq na wala mfafanuzi yeyote yule wa kitabu cha Man La Yahdhuruh al-Faqih aliyeitabakisha lakabu iliyotajwa kwa Imamu Mahdi (a.t.f.s).[11] Kadhalika katika hadithi iliyonukuliwa katika kitabu cha Mahasin kilichoandikwa na Barqi ameitambulisha Saleh kuwa ni jini ambaye ana jukumu la kuwasaidia watu walipotea njia.[12]

Rejea

  1. Reyshahri, Daneshnameh Imamu Mahdi, juz. 2, uk. 322.
  2. Reyshahri, Daneshnameh Imamu Mahdi, juz. 2, uk. 322.
  3. Nuri, Jannatu al-Ma'wa, uk. 136; Nuri, Najm al-Thaqab, uk. 45
  4. Reyshahri, Daneshnameh Imamu Mahdi, juz. 2, uk. 322.
  5. Majlisi, Bihar al-Anwar, juz. 52, uk. 175-176
  6. Nuri, Najm al-Thaqib, uk. 571
  7. Reyshahri, Daneshnameh Imamu Mahdi, juz. 2, uk. 322.
  8. Al-Barqi, al-Mahasin, juz. 2, uk. 362-363
  9. Saduq, Man Laa Yahdhuruh al-Faqih, juz. 2, uk. 298
  10. Saduq, Man Laa Yahdhuruh al-Faqih, juz. 2, uk. 298
  11. Reyshahri, Danehsnameh Imamu Mahdi, juz. 2, uk. 322
  12. Al-Barqi, al-Mahasin, juz. 2, uk. 380

Vyanzo

  • Al-Barqi, Ahmad bin Muhammad bin Khalid, al-Mahasin, Tasihih Muhadith Armawi, Qom: Dar al-Kutub al-Islamiyah, 1371 H
  • Reyshahri, Muhammad Muhammadi Niku dkk, Daneshnameh Imam Mahdi bar Payeh Quran, Hadith wa Tarikh , Qom: Intisharat Dar al-Hadith, 1393 H.S.
  • Majlisi, Muhammad Baqir, Bihar al-Anwar al-Jami'ah lildurar Akhbar al-Aimmah al-Athar, Beirut: Dar Ihya al-Turath al-'Arabi, Toleo nambari II, 1403 H
  • Nuri, Mirza Hussein, Jannatu al-Ma'wa fi Dzikri Man Faza bi Liqa' al-Jannah, Markaz al-Dirasat al-Takhasusiyah fi al-Imam al-Mahdi (a.j.t.f), Qom: Muasasse al-Sayyidah al-Ma'shumah (a.s), 1327 H
  • Nuri, Mirza Hussein. Najm al-Thaqib, Qom: Intisharat Masjid Jamkaran, 1410 H.
  • Shaduq, Muhammad bin Ali, Man Laa Yahdhuruh al-Faqih, Qom: Jami'ah Mudarrisin, Toleo nambari II, 1413 H