Mwanzo

Kutoka wikishia
WikiShia
Ensaiklopidia ya Maktaba Ahlul Bayt (a.s.), inayosimamiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (a.s.)
570 Makala / mabadiliko 12,006 kwa Kiswahili

Makala ya Wiki

Kuonekana Mwenyezi Mungu (Kiarabu: رؤية الله) ni maudhui ya kiteolojia (kiitikadi) nayo ni kuhusiana na uwezekano wa kumuona Mwenyezi Mungu kwa macho. Wasomi wa elimu ya teolojia wa madhehebu ya Shia Imamiyyah na wale wa kundi la Mu’tazila wanaamini kwamba, Mwenyezi haonekani kwa macho hapa duniani wala kesho akhera. Mtazamo wao ni kwamba; kumuona Mwenyezi Mungu kwa macho kunalazimu Muumba huyo awe na mwili na umbo, na inafahamika kwa kawaida ya kwamba kila chenye mwili au kiwiliwili kina sehemu maalumu, na kuamini hivyo ni kumwekea mipaka Mwenyezi Mungu, hali ya kuwa ni kinyume na hivyo kwa mujibu wa mantiki na mafundisho ya Uislamu. Hata hivyo mkabala na wao, madhehebu mengi ya kiteolojia ya Ahlu-Sunna kama Ash’ari, Ahlul-Hadithi, al-Mujassamiya, al-Karamiyyah na Salafiyah yenyewe yanaamini kwamba, kuna uwezekano wa kumuona Mwenyezi Mungu.

Read more ...


Je, wajua ...
  • ... Kifo cha Fatima Zahra, binti ya Mtume (s.a.w.w) ni miongoni mwa vifo vilivyo na utata zaidi katika Uislamu na hata kaburi lake halijulikani lilipo?
  • ... Kitendo cha kusengenya kimefananishwa na mtu kula nyama ya nduguye aliyekufa?
  • ... Ramadhani, ndio mwezi pekee jina lake limekuja katika Qur'an?
  • ... Aya ya 7 ya Surat al-Bayyinah ni miongoni mwa Aya ambazo zilizoteremka kuelezea fadhila na ubora wa Ali bin Abi Talib (a.s)?
  • ... Shia ndio madhehebu inayoamini na kuitikadi kuwa Khalifa au Kiongozi baada ya Mtume (s.a.w.w) anapaswa kuchaguliwa na M.mungu kisha kuainishwa na Mtume?
Makala Zilizo Pendekezwa


  • Kukusanya baina ya Sala mbili « Ni namna ya kuzisali sala mbili kwa wakati mmoja kwa sharti ya kuwa sala hizo zinashirikiana katika wakati mmoja, mfano; kusali sala ya Adhuhuri na Alasiri kwa pamoja wakati wa mchana na wakati maaalum unaoruhusiwa kuzisali au kusali sala ya Magharibi na Isha kwa pamoja baada ya kuzama kwa jua na kuingia kwa wakati shirikishi. Kwa upande wa madhehebu ya Shia, wamejuzisha kukusanya baina ya sala mbili kwa mashiko ya Hadithi za Bwana Mtume (s.a.w.w) zinazopatikana katika vitabu vyao na vitabu vya Ahlu-sunna na pia sira ya Maimamu wao (a.s).Ama Ahlu-sunna wao hawakubaliani na suala la kukusanya baina ya sala mbili isipokuwa katika mazingira maalumu tu, kama vile kuwa mgonjwa au safarini.»
  • Kusali kimya kimya «humaanisha kusoma kimya kimya nyiradi au dhikri za swala bila kunyanyua sauti. Dhikri hizo ni kama vile tasbihi nne maarufu za swala zisomwazo badala ya Surat al-Fatiha, Pia Surat al-Fatihah na Surah zisomwazo baada Surat al-Fatihah.»
  • Akhera «Ni ulimwengu baada ya kifo na mauti na ni ulimwengu ujao baada ya maisha ya dunia.»
  • Sadaka za lazima «Ni wajibu wa kimali unaoelezewa katika Uislamu ambao unabeba maudhui mbalimbali kama vile zaka ya mali, zakat al-fitr na kafara.»
  • Ulul-amri «Ina maana ya wenye mamlaka, na hao wenye mamlaka ni watu ambao ni wajibu kuwatii kwa msingi wa Aya ya Ulul-Amr. Istilahi hii imekuja na kuelezwa ndani ya aya ya 59 ya surat al-Nisaa.»
  • Kafara ya swaumu «Ni adhabu ambayo huwekwa kutokana na kubatilisha na kuharibu funga ya mwezi wa Ramadhan, funga ya nadhiri ya muda maalumu na pia kadhwaa au malipo ya funga ya mwezi wa Ramadhan ikiwa itaharibiwa na kubatilishwa baada ya adhana ya adhuhuri, funga ambayo ilikuwa ni wajibu kwa mukallaf (mwenye kuwajibishwa).»
  • Safari ya Kisheria «Ni safari ambayo ndani yake msafiri analazimika kusali sala zake kwa kupunguza (Sala za rakaa nne azisali rakaa mbili) na hapaswi kufunga Swaumu.»
Kategoria Kuu
Jamii inayoitwa Beliefs‎ haikupatikana
Jamii inayoitwa Culture‎ haikupatikana
Jamii inayoitwa Geography‎ haikupatikana
Jamii inayoitwa History‎ haikupatikana
Jamii inayoitwa People‎ haikupatikana
Jamii inayoitwa Politics‎ haikupatikana
Jamii inayoitwa Religion‎ haikupatikana
Jamii inayoitwa Sciences‎ haikupatikana
Jamii inayoitwa Works‎ haikupatikana