Mazungumzo Kati ya Mungu na Nabi Musa (a.s)

Kutoka wikishia

Mazungumzo Kati ya Mungu na Nabii Mussa (a.s) (Kiarabu:تَكلِيم الله لموسى (ع)): ni yale mazungumzo yaliokuwa yakijiri baina ya Mwenye Ezi Mungu na Nabii Mussa (a.s), ambayo yanasemekana kuwa yalifanyika moja kwa moja bila ya kupitia Malaika fulani au mfikishaji fulani wa ujummbe wa Mwenye Ezi Mungu. Suala hili la mazungumzo baina ya Mwenye Ezi Mungu na mja wake bila ya kutumika Malaika fulani, linahisabiwa kuwa ni sifa na hadhi maalumu kwa Nabi Musa peke yake. Suala hili limezungumzwa wazi ndani ya baadhi ya Aya za Qur'ani, miongo mwa Aya za Qur'ani, zilizo nukuu suala hili ni ile Aya ya 164 ya Surat al-Nisaa. Nabii Mussa husifika kwa sifa ya Kalimullah (yule ambaye Mungu alisema naye) ambayo ni mahususi kwa Nabii Mussa (a.s), na Mayahudi walimtabua kwa jina «Kalimi» kwa kutokana na sifa hii.

Baadhi ya wanazuoni wa Kishia kama vile Sheikh Tusi, wanaamini kwamba; mazungumzo yaliokuwa yakipita kati Mwenye Ezi Mungu na Nabi Musa, yalikuwa ni halisia yanayo fanana na mazungumzo ya kawaida. Katika Hadithi, maneno ya Mwenye Ezi Mungu yamezingatiwa ni maneno yanayozaliwa bila ya kutumia mdomo na ulimi. Kuna maoni tofauti kuhusiana na uhalisia wa maneno yenye sifa kama hizi: Baadhi ya wafasiri wa Shia wanaamini kwamba; Mwenye Ezi Mungu aliumba mawimbi ya sauti na maneno katika anga au katika vitu fulani. Baadhi ya wafasiri wengine wanaamini kwamba; Mwenye Ezi Mungu hakutaja wala hakutufahamis jinsi ya usemaji huo ulivyotimia, nasi hatuna mashiko yoyote yale kutoka katika Qur'ani, kuhusiana na namna halisi ya usemaji huo wa Mwenye Ezi Mungu.

Baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu wanaamini kwamba; pamoja na Mussa (a.s) pia Mwenye Ezi Mungu alizungumza moja kwa moja na Mtume wa Uislamu (s.a.w.w).

Nabii Mussa (a.s) Kupata Sifa ya Kalimullah

Kwa mujibu wa Aya ya 164 ya Surat al-Nisaa, ni kwamba Mwenye Ezi Mungu alizungumza na Mussa (a.s), Mwenye Ezi Mungu katika Aya hiyo Anasema: «کَلَّمَ الله مُوسی تَکْلیماً», Maana yake ni kwamba; "Na Mwenye Ezi Mungu alizungumza na Mussa kwa mazungumzo".[1] Pia mazungumzo haya baina ya Mwenye Ezi Mungu na Nabii Mussa yametajwa katika Aya ya 144 ya Surat A'raf.[2] Baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu[3] na Mayahudi[4] wanayachukulia mazungumzo aina hii, kuwa ni makhususi na maalum kwa Nabii Mussa (a.s) peke yake. Hivyo basi wao wamelirodhesha jambo hilo katika orodha ya sifa maalumu za Nabii Mussa (a.s).[5]

Wao wamesema kwamba Sifa ya Kalimullah ni makhususi kwa Nabii Mussa,[6] na wakasema kwamba; sifa hiyo hiyo ya Nabii Mussa ndiyo iliwafanya Mayahudi kuitwa «Kalimi».[7] Baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu wanaamini kwamba Mwenye Ezi Mungu pia alizungumza na Mtume wa Muhammad (s.a.w.w) katika safari yake ya Miraji, pia wamedai kuwa kuna Hadithi maalumu zinathibitisha usemi wao huo.[8] Wanazuoni hawa wanaamini kwamba; mawasiliano ya moja kwa moja na Mwenye Ezi Mungu, yalikuwa ni mahususi tu kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Mussa (a.s).[9]

Mazungumzo ya Mwenye Ezi Mungu yamezingatiwa kuwa; ni namna ya kunena bila kutumia na mwili; Kwa sababu kunena kwa kutumia ulimi na kwa njia ya sauti, ni dalili ya kuwa na kiwiliwili, hali ya kwamba Mwenye Ezi Mungu hana mwili.[10] Imamu Ali (a.s), kwenye moja ya vipengele vya hotuba zake, akizungumzia suala la mazungumzo baina ya Nabi Musa na Mola wake, ameyasifu mazungumzo hayo ya Mungu, kuwa ni mazungumzo na matamshi yasiyo haihitaji aina yoyote ile ya nyenzo au viungo vya kiwiliwili.[11] Pia Imamu Ridha (a.s) alizingatia unenaji huo wa Mungu, kuwa ni unenaji uliojiri bila ya kutumia mdomo na ulimi, jambo ambalo ni tofauti kabisa na mazungumzo ya viumbe.[12]

Mazungumzo ya Moja kwa Moja na Bila ya Kiunganishi

Kulingana na nadharia za wanazuoni wa Kiislamu, ni kwamba; Mazungumzo yaliojiri kati ya Mwenye Ezi Mungu na Nabii Mussa (a.s) yalifanyika kwa njia ya moja kwa moja[13] na bila mwasilisha -ambaye ni Malaika-.[14] Tabrasi, mwandishi wa tafsiri ya Majma’u al-Bayan, akitoa ufafanuzi kuhsiana na tofauti kati ya mazungumzo ya Mwenye Ezi Mungu na Nabii Mussa (a.s) na manabii wengine, ameeleza ya kwamba; Mwenye Ezi Mungu alizungumza na Nabii Mussa (a.s) moja kwa moja bila kupitia mwasilishaji.[15] Katika aina hii ya mazungumzo, ujumbe hufikishwa kwa mkusudiwa (msikilizaji), huku mzungumzaji akiwa hawaonekani; hii ni kutokana na uwepo wa pazia maalumu la kiroho au kizuizi kinachozuia kumuona mzungumzaji huyo.[16]

Sheikh Tusi aliona kwamba; Mazungumzo ya Mwenye Ezi Mungu na Nabii Mussa (a.s) ni mazungumzo yenye sura ya mazungumzo halisi kabisa.[17] Baadhi ya wafasiri wakizingatia neno “takliman” «تَکْلیماً» lililoko katika Aya isemayo «وَ کَلَّمَ الله مُوسی تَکْلیماً» “Na Mwenye Ezi Mungu alimzungumza na Musa kwa mazungumzo”[18] wamedai ya kuwa neno hilo ni ushahidi wa kwamba Mwenye Ezi Mungu amezungumza kwa mazungumzo halisi kabisa, na wakasema kwamba; haiwezekani kutafsiri mazungumzo hayo kuwa ni ya “kimajazi” au kitamthili.[19] Kulingana na maelezo ya Allama Tabataba’i, mwandishi wa tafsiri ya al-Mizan, kuzungumza huko kwa Mwenye Ezi Mungu na Musa kulikuwa katika mfuma wa mazungumzo halisi kabisa na kulikuwa na athari sawa na mazungumzo ya kawaida, kama vile kufahamisha na kufikisha makusudio yake kwa wengine; lakini mazungumzo hayo yalikuwa ni tofauti na mazungumzo ya kawaida, na kwamba mazungumzo hayo hayakuwa kupitia njia ya ulimi au koo.[20]

Jinsi ya Mungu Alivyozungumza na Nabii Mussa (a.s)

Makarim Shirazi, ambaye ni mwanazuoni na mfasiri wa Kishia, anaamini kwamba; Mwenye Ezi Mungu alizungumza na Nabii Mussa (a.s) kwa kutuma mawimbi ya sauti angani au kwenye vitu fulani.[21] Sheikh Tusi pia ameandika akisema kwamba; Mwenye Ezi Mungu huzalisha maneno katika umbo (kiwiliwili) fulani ili kufikisha lengo lake kwa viumbe vyake.[22] Baadhi ya wafasiri wengine pia wameeleza kuwa; Mwenye Ezi Mungu aliumba sauti na maneno, na Mussa akayasikia maneno hayo yatokayo kwa Mola Wake.[23]

Kwa upande mwingine, Allama Tabataba’i anaamini kwamba Mwenye Ezi Mungu hajataja ni jinsi yeye alitima mazungumzo yake hayo, na wala sisi hatupati maelezo yale juu ya jinsi hiyo ya uzungumzaji kutoka katika Qur’ani Tukufu.[24] Muhammad Jawad Maghniyyah, mfasiri wa Kishia, yeye pia anaamini kwamba; Mwenye Ezi Mungu amekaa kimya bila ya kusema chochote kile kuhussiana na jinsi ya mazungumzo hayo. Hivyo basi sisi pia tunakaa kimya katika suala hili, na hatusemi chochote kuhusiana na asili ya maneno na mazungumzo hayo yalivyo.[25]

Rejea

  1. Surat an-Nisaa: Aya ya 164.
  2. Tayyib, Atyab al-Bayān, juz. 5, uk. 453.
  3. Sheikh Tusi, at-Tibyān, juz. 3, uk. 394; Fakhrurrazi, at-Tafsīr al-Kabīr, juz. 11, uk. 267.
  4. Lakab Hadhrat Mussa Be Farsi Che Mi-Boshad waa Nubuwwat Ishan Chegune Bud? Site Wayahudi Iran.
  5. Qurashi, Tafsīr Ahsan al-Hadīth, juz. 1, uk. 470; Rashid Ridha, al-Manār, juz. 3, uk. 4.
  6. Fadhlullah, Tafsīr Min Wahy al-Qur'ān, juz. 20, uk. 202.
  7. Lakab Hadhrat Mussa Be Farsi Che Mi-Boshad waa Nubuwwat Ishan Chegune Bud? Site Wayahudi Iran.
  8. Banu Amin, Makhzan al-'Irfān Dar Tafsir Qur'an, juz. 2, uk. 379.
  9. Burujerdi, Tafsir Jami', juz. 2, uk. 426.
  10. Makarim Shirazi, Yek Sad wa Hashtad Pursesh wa Pasukh, uk. 75.
  11. Sheikh Saduq, at-Tauhīd, uk. 79.
  12. Majlisi, Bihār al-Anwār, juz. 4, uk. 152.
  13. Mughniyah, Tafsīr al-Kāshif, juz. 2, uk. 495.
  14. Tayyib, Atyab al-Bayān, juz. 5, uk. 452.
  15. Tabrasi, Majma' al-Bayān, juz. 3, uk. 218.
  16. Fadhlullah, Tafsīr Min Wahy al-Qur'ān, juz. 20, uk. 202.
  17. Sheikh Tusi, at-Tibyān, juz. 3, uk. 240.
  18. Surat an-Nisaa.
  19. Qurtubi, al-Jāmi' Li Ahkām al-Qur'ān, juz. 6, uk. 18.
  20. Tabataba'i, al-Mīzān, juz. 2, uk. 315 & 316.
  21. Makarim Shirazi, Tafsir Nemune, juz. 6, uk. 363.
  22. Sheikh Tusi, ar-Rasā'il al-'Ashr, uk. 95.
  23. Husseini Shirazi, Tabyīin al-Qur'ān, 1424 H, uk. 115.
  24. Tabataba'i, al-Mīzān, juz. 2, uk. 316.
  25. Mughniyah, Tafsīr al-Kāshif, juz. 2, uk. 495.

Vyanzo

  • Amīn, Nuṣrat Baygum. Makhzan al-ʿirfān dar tafsīr-i Qurʾān. Tehran: Naḥḍat-i Zanān-i Musalmān, 1361 Sh.
  • Burūjirdī, Muḥammad Ibrāhīm. Tafsīr-i Jāmiʿ. Tehran: Kitābkhāna-yi Ṣadr, 1366 Sh.
  • Faḍl Allāh, Sayyid Muḥammad Ḥusayn. Tafsīr min waḥy al-Qur'ān. Beirut: Dār al-Milāk li-Ṭabā'at wa al-Nashr, 1419 AH.
  • Fakhr al-Rāzī, Muḥammad b. al-ʿUmar al-. Mafātīḥ al-ghayb (al-Tafsīr al-Kabīr). Chapa ya tatu. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1420 AH.
  • Ḥusaynī Shīrāzī, Sayyid Muḥammad. Tabyīn al-Qurʾān. Beirut: Dār al-ʿulūm, 1423 AH.
  • Ibn Kathīr, Ismāʿīl b. ʿUmar. Tafsīr al-Qurʾān al-ʿaẓīm. Mhariri: Muḥammad Ḥussein Shams al-Dīn. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1419 AH.
  • Ibn Qayyim al-Jawziyya, Muḥammad ibn Abī Bakr. Ḥādī al-arwāḥ ilā bilād al-afrāḥ. Beirut: ʿĀlam al-Kutub, [n.d].
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Chapa ya pili. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
  • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tafsīr-i nimūna. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1374 Sh.
  • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Yikṣad-u hashtād pursish wa pāsukh. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1386 Sh.
  • Mughnīyya, Muḥammad Jawād al-. Tafsīr al-Kāshif, Qom: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1424 AH.
  • Qurashī, Sayyid ʿAlī Akbar. Tafsīr-i aḥsan al-ḥadīth. Chapa ya tatu. Tehran: Bunyād-i Biʿthat, 1377 Sh.
  • Qurtubī, Muḥammad b. Aḥmad al-. Al-Jāmiʿ li-aḥkām al-Qurʾān. Tehran: Intishārāt-i Nāṣir Khusraw, 1364 Sh.
  • Rashīd Riḍhā, Muḥammad. Tafsīr al-manār. Cairo: al-Hayʾat al-Misrīyya al-ʿĀmma li l-Kitāb, 1990.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Al-Tawḥīd. Mhariri: Hāshim Ḥusseinī. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1398 AH.
  • Shāh ʿAbd al-ʿAẓīmī, Ḥussein. Tafsīr ithnā asharī. Tehran: Mīqāt, 1363 Sh.
  • Ṭabāṭabāʾī, Sayyid Muḥammad Ḥussein al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1417 AH.
  • Ṭabrisī, Faḍl bin al-Ḥassan al-. Majmaʿ al-bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Tehran: Naṣir Khusruw, 1372 Sh.
  • Ṭayyib, ʿAbd al-Ḥussein. Aṭyab al-bayān fi tafsīr al-Qurʾān. 2nd ed. Tehran: Intishārāt-i Islām, 1378 Sh.
  • Ṭūsī, Muḥammad bin al-Ḥassan. Al-Rasāʾil al-ʿashr. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1414 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad bin al-Ḥassan al-. Al-Tibyān fī tafsīr al-Qurʾān. Mhariri: Aḥmad Qaṣīr al-ʿĀmilī. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, [n.d]

.