Kafara

Kutoka wikishia


Kafara (Kiarabu: الكفارة) ni faini ambayo inapaswa kutolewa kama mbadala kutokana na kufanya baadhi ya mambo ya haramu au kuacha baadhi ya mambo ya wajibu. Kumuachilia huru mtumwa, kulisha au kuvisha mafakiri, kufunga swaumu na kuchinja ni miongoni mwa kafara na faini muhimu. Baadhi ya mambo kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu ambayo mtu analazimika kutoa faini au kafara ni: Kumuua mtu, kufungua kwa makusudi swaumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, kuvunja ahadi, nadhiri na kiapo na kufanya baadhi ya mambo ambayo ni haramu kuyafanya mtu akiwa katika vazi la ihramu.

Aina ya kafara na namna ya kuitekeleza kuna tofauti kulingana na jambo alililofanya mtu; Baadhi ya matendo yameainishwa kafara maalumu na inayoeleweka, baadhi ya mengine yana kafara kadhaa ambapo mukallafu(mwenye kuwajibishw) ana hiari ya kufanya moja kati ya hayo; baadhi ya matendo pia yana kafara kadhaa kwa utaratibu na mtu anapaswa kutekeleza kwa mujibu wa kipaumbele. Aidha baadhi ya matendo pia yana kafara ya kukusanya (kuzitekeleza zote kwa pamoja); kwa maana kwamba, yameainishiwa kafara na faini kadhaa na mukallafu anapaswa kuzitekeleza zote.

Utambuzi wa maana

Faini ya kifedha na kimwili ambayo ni mbadala wa kutenda baadhi ya madhambi na ambayo ni lazima kuitekeleza, katika mafundisho ya Kiislamu inafahamika kwa jina la kafara au faini. [1] Kafara aghalabu hupelekea kuondolewa au kupunguziwa adhabu ya akhera ya dhambi. [2] Kafara inatokana na neno la Kiarabu (کَفر) lenye maana ya kufunika au kuficha. [3] Kwa kuwa Kafara hupelekea kufunika na kufumbiwa macho dhambi, ndio maana imeitwa kwa jina hili. [4] Wakati mwingine katika mazungumzo ya watu katika jamIi kafara inajulikana kwa maana ya fidia. Kwa mfano kibaba kimoja cha chakula (gramu 750 za ngano na kadhalika) hutajwa kama ni kafara ya swaumu; [5] hii ni katika hali ambayo kimsingi ni fidia ya swaumu; yaani ni mbadala wa siku ambayo mtu hakufunga kutokana na sababu na udhuru wa kisheria kama ugonjwa na kadhalika. [6]

Aina za kafara na zinapohusika

Kwa mujibu wa vitabu vya fikihi, kafara ni:

  • Kumuachiliia huru mtumwa. [7]
  • Kuwalisha masikini kumi. [9]
  • Kufunga swaumu miezi miwili. [10]
  • Kufunga swaumu siku tatu. [11]
  • Kuchinja kondoo. [12]
  • Kuchinja ngamia. [13]
  • Kuchinja ng'ombe au kondoo. [14]
  • Kutoa kibaba kimoja cha chakula. [15]
  • Kulisha mafukara sita. [16]

Madhambi ambayo yana kafara

Katika vitabu vya fikihi matendo ambayo yanapelekea kafara hujadiliwa katika mlango wa dhihar; [18] hata hivyo ukiacha kafara ya mambo ya haramu ambayo mtu hapaswi kuyafanya akiwa amevaa vazi la ihramu ambayo hubainishwa katika mlango wa Hija. [19] matendo ambayo yana kafara yanatofautiana kulingana na aina ya kafara yenyewe na namna ya kuitekeleza: Baadhi matendo hayo yana kafara maalumu (Kaffara Muayyanah). Katika baadhi ya matendo mengine kuna kafara kadhaa zilizoainishwa na mukallafu ana hiari ya kuchagua moja kati ya hizo (Kaffara Mukhayyarah).

Sehemu nyingine kuna kafara ambazo mtu anapaswa kuzitekeleza kwa mujibu wa mpangilio na kipaumbele; kwa maana kwamba, kama hakuwa na uwezo wa kutekeleza ya kwanza anatekeleza ya pili na hii inafahamika kwa jina la Kaffara Murattabah. Vilevile kuna baadhi ya matendo akiyafanya mtu anawajibika kutekeleza kafara zote yaani anajumuisha kafara zote, hii inajulikana kwa jina la Kafara ya kukusanya(Kaffaratul-Jam'). [20]