Zaburi

Kutoka wikishia
Zaburi

Zaburi (Kiarabu: الزبور) ni kitabu cha mbinguni kilichoteremshwa kwa nabii Daudi (a.s). Zaburi haikuja na amri na sheria mpya kutoka kwa Alla, ila ndani mna nasaha na mawaidha, dua, na maombi mbali mbali. Kulingana na aya za Qur’an, Nabii Daudi amefadhilishwa zaidi na kupandishwa daraja zaidi kuliko manabii wengine kutokana na Zaburi aliyo teremshiwa na Mola wake. Kulingana na baadhi ya Hadithi, Zaburi ni moja ya amana na hazina za Maimamu ambayo ndani yake mmetaja ujao wa nabii Muhammad (s.a.w.w).

Baadhi ya watafiti wanaamini kwamba; Zaburi zilizopo katika Agano la Kale ndio Zaburi ya nabii Daudi, ambayo kiuhalisia ilikumbwa na wimbi la upotoshwaji. Zaburi za Torati ni miongoni mwa vyanzo vya kuaminika zaidi vya kidini na kiutamaduni kwa Wayahudi. Ndani yake mna jumla ya vitabu vitano na na vipengele 150 vya zaburi (kasida), ambapo zaburi (kasida) 73 kati ya vipengele hivyo zinahusishwa na nabii Daudi. Inasemekana kwamba; Aya ya 105 kutoka Surat Anbiyaa ndiyo nukuu pekee ya moja kwa moja kutoka Torati iliyopo katika Qur’an, ambayo bado ipo na inapatikana katika Zaburi.

Utambulisho na Umuhimu

Kulingana na baadhi ya Hadithi, Zaburi ni moja kati ya Sahifa (kurasa) 104 za mbinguni [1] ambazo ziliteremshwa kwa nabii Daudi (a.s) ndani mwezi 18 Ramadhani. [2] Kulingana na maelezo ya Nassir Makarem Shirazi, mwandishi wa tafsiri ya Nemune, ni kwamba; yaliyomo katika Zaburi ni jumla ya nasaha na mawaidha, dua, na maombi bila kuambaytana na amri au sheria mpya ndani yake. [3] Kulingana na baadhi ya Hadithi; Zaburi ni moja ya amana za Maimamu ambayo inahifadhiwa katika Jafru Abyadh. [4]

Kulingana na Imani za Mashia; Jafru Abyadh ni kitabu cha Imamu Ali (a.s) kilicho kusanya ndani yake Hadithi zote za bwana Mtume (s.a.w.w), ambacho alikiandika kupitia amri ya bwana Mtume (s.a.w.w). Kwa mujibu wa maelezo ya Hadithi iliyo nukuliwa kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), ni kwamba; jina la Mtume wa Uislamu katika Zaburi lilielezewa kwa jina la “Mahi” «ماحی» likimaanisha «anayeondoa na kufuta ibada ya masanamu duniani». [5] Katika baadhi ya Hadithi, pia kumekuwa na mazungumzo kuhussiana na kutajwa kwa jina la Imam Ali (a.s) katika Zaburi. [6] Kuna Hadithi isemayo kwamba; Mwenye Ezi Mungu badala ya Zaburi, alimpa Mtume wake Muhammad Sura maalumu za Qur’ani zijulikanazo kwa jina la Sura za Mathani. [7] Kuna vitabu kadhaa vilivyopewa jina la Zaburi kutokana na uzuri wake na madhumuni zake za kiibada, ikiwepo Sahifa Sajjadiyya na baadhi ya Mathnawi za Attar Nishapuri. [8] Neno «Zabur» katika lugha linamaanisha «yalioandikwa».[9]

Aya Zinazohusiana na Zaburi Ndani ya Qur’ani

Maandishi ya Aya ya 105 ya Surat Anbiya katika Haram ya Imamu Hussein (a.s)

Neno «Zaburi» limetajwa mara tatu katika Qur’an. Neno hilo linapatikana katika Aya ya 163 ya Sura An-Nisa na Aya ya 55 ya Surat Al-Isra, Aya mbazo zimeitambulisha Zaburi kama ni zawadi maalumu kwa Nabii Daudi (a.s). [10] Muhammad Hussein Tabatabai, mwandishi wa Tafsiri Al-Mizan, akirejelea Aya ya 163 ya Surat An-Nisa, anaamini kwamba; sababu ya ubora wa Nabii Daudi juu ya baadhi ya manabii wengine ni kushushiwa kwake kitabu cha Zaburi. [11] Katika Aya ya 196 ya Surat Ashuar’aa, neno Zuburi limetumika kama ni umoja wa neno (Zaburi) likiashiria vitabu vya mbinguni vilivyoteremshwa kwa manabii kabla yake, na sio tu kwa maada ya kitabu kilichoteremshwa kwa Nabii Daudi. Tukirudi Katika Aya isemayo:

«وَلَقَدْ کتَبْنَا فِی الزَّبُورِ مِن بَعْدِ الذِّکرِ أَنَّ الْأَرْضَ یرِثُهَا عِبَادِی الصَّالِحُونَ»
Na kwa hakika tulishaandika (tumesha hukumu) katika Zaburi, baada ya Ukumbusho, kwamba bila shaka ardhi watairithi waja Wangu walio wema. [12]

Tutakuta kwamba pia ndani yake kumetajwa kumetajwa neno «Zaburi». Ingawaje neno «Zaburi» limetajwa na linapatikana katika Aya hii, lakini kuna uwezekano nadhana mbalimbali ziliojadiliwa kuhusiana na maana halisi iliyo kusudiwa katika neno hilo. Allama Tabatabai kwa kutegemea Aya nyingine, anaamini kwamba; makusudio ya Ayo hiyo ni kitabu cha Nabii Daudi (a.s).[13] Baadhi ya watafiti wanachukulia maelezo ya Aya 105 ya Surat Anbiyaa kama ndio nukuu pekee ilionukuu moja kwa moja kutoka Agano la Kale katika Qur'an.[14] Muhammad Sadiq Tehrani na Nasir Makarem Shirazi, ambao ni wafasiri wa karne ya kumi na tano, baada ya kuchunguza Zaburi (kasida au nyimbo) za Torati, wamefikia hitimisho lisemalo kwamba; maelezo na madhumini ya Aya hii yanapatikana maandiko ya Zaburi (kasida) zilizomo katika Torati.[15]

Mawafikiano Kati ya Yaliomo Ndani Zaburi na Baadhi ya Yaliomo ndani ya Taurati

Picha ya nakala ya zamani zaidi ya zaburi ya Daudi, ya karne ya 4 BK, iliyohifadhiwa katika Jumba la Makumbusho la Coptic la Misri[17]

Baadhi ya wafasiri kama vile Makarim Shirazi na Sadiqi Tehrani, wameilinganisha Zaburi ya Nabii Daudi na sehemu za Taurati (Kasida za Taurati), ila bado wao wanaamini kwamba sehemu hizo za Taurati pia kumefanyika upotoshaji. [18] Hata hivyo, Sadeqi Tehrani anaamini kwamba; baada ya Qur’an, hakuna kitabu chengine cha mbinguni kilichobaki bila kupotoshwa kama Zaburi, na upotoshaji uliofanyika ndani yake ni mdogo mno. [19] Kulingana na baadhi ya watafiti,ni kwamb; kuna sifa zinazofanana kati ya Qur’an na Zaburi, kama vile mifano mashabihisho yaliomo ndani yake, na baadhi ya maneno au herufi zisizo wazi ambazo zinaashiria chanzo cha pamoja cha vitabu viwili hivyo. [20] Kifungu cha Zaburi (kasida) ya 45 ya nabii Daudi, kinazungumzia kuhusiana na Mtume wa Uislamu na masahaba zake. [21]

Zaburi kwa jumla ina vitabu vitano [22] na vifungu vya zaburi (kasida) 150 [23] ambavyo zaburi au kasida 73 kati yake zinahusishwa na nabii Daudi, [24] pia baadhi ya zaburi zimehusishwa na nabii Sulemani na nyingine zimehusishwa na watu wengine wanaojulikana au wasiojulikana. [25] Zaburi zina muundo wa ushairi [26] na ni miongoni mwa vyanzo vya kuaminika zaidi vya kidini na kiutamaduni mbele ya Wayahudi. [27] Sehemu kubwa ya maombi ya kila siku, ya kila wiki, sikukuu, na sherehe nyingine za Kiyahudi zinatokana na Zaburi, [28] na hakuna kitabu chengine chochote kile katika Biblia -ukiachana na Injili- kisomwacho zaidi kama Zaburi. [29]

Maudhui zinazo funagamana