Yawmu Taghabun

Kutoka wikishia

Yawmu Taghabun (Kiarabu: يوم التغابن) ni mojawapo ya majina ya Siku ya Kiyama, ambayo maana yake ni siku ya kuweka wazi hasara na faida. Siku hii ya Kiyama imeitwa siku ya Hukumu; Kwa sababu siku hii itaweka wazi natija ya matendo ya wanaadamu waliyoyafanya ulimwenguni, na nani ni mshindi na mshindwa wa maamrisho ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake.

Maana ya msamiati (neno) Yawmu Taghabun

Maana ya "Yumul-Taghabun" iliyotajwa ndani ya Qur'an Tukufu ni Siku ya Kiyama; Kwa sababu siku hiyo itadhihirika kwa watu wote, Siku hiyo ni siku ya majuto. Siku ambayo Mwenyezi Mungu atawakusanya watu wote kwa ajili ya malipo na adhabu ya matendo yao mema na mabaya waliyoyafanya duniani. Yawmu at-Taghabun: Neno "Yawm al-Taghabun" limetumika katika aya ya tisa ya Surat at-Taghabun, na ndio maana sura hii inaitwa Taghaabun.[1] Siku ya Al-Taghabun ni miongoni mwa majina ya Siku ya Hukumu.[2] Sababu ya jina hili ni kwamba katika siku hii inajulikana ni nani amefuzu na nani amefeli katika maamrisho ya Mwenyezi Mungu.

Nadharia tofauti kuhusiana na (msamiati) wa Yawmu Taghabun

Kwa mujibu wa Fadhl Ibn Hassan Tabrasi katika tafsiri ya Majmaal al-Bayan, anasema. Makafiri wanaitwa Maghboon (wapotevu walioshindwa) kwa sababu ya kuacha manufaa ya Akhera na kufuata dunia tu, na Muumini anaitwa Ghabun (mshindi) kwa sababu ya kushughulika na kuzingatia Akhera yake. Kulingana na hadithi, baadhi ya waumini pia huhisi wamepata hasara Siku ya Kiyama; Kwa sababu hawakuitumia nafasi kwa ajili ya kufanya matendo mema zaidi.

Fadhl bin Hassan Tabrasi, anaendelea kusema kuwa; Taghaabun ina maana ya kuchagua kitu kisicho sahihi na kuacha kitu sahihi au kinyume chake. Kwa hiyo, kafiri ni mwenye hasara akwa sababu amewacha manufaa ya Akhera na amefaidika tu na dunia. Pia, Muumini ni Ghaabun (mshindi); Kwa sababu hakughilibika na anasa za dunia tu bali alitii maamrisho ya Mola wake kwa ajili ya kupata maslahi yake ya Akhera.[3] Tabarsi anaichukulia Siku ya Al-Taghban kuwa ni siku ambayo inabainishwa nani ni Ghaban (mshindi) na nani Maghbun (mshindwa).[4] Vile vile imenukuliwa kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) akisimulia kwamba Waumini wanaoingia peponi wataona udhaifu wao ikiwa wametenda dhambi) na watamshukuru Mwenyezi Mungu. Pia watu wa motoni wataona mahala pao peponi (kama hawakutenda dhambi) na watajuta.[5]

Allameh Tabatabai na Shahid Mutahari wanapendekeza maana nyingine ya Taghabun na kusema: Katika baadhi ya miamala, watu wote wa pande mbili hupata hasara; Kama pale watu wanapoamuwa kuwa wafuasi wa madhalimu ili wapate malipo, au watu wenye kiburi waliowaita na kuwahamasisha wafuasi wao kughilibika na anasa za kidunia na kuacha Akhera, katika hali hii, Siku ya Kiyama watu wa aina hiyo watakuwa ni miongoni mwa wale waliohasirika Taghabun ina maana ya kusababisha hasara kwa mtu, kudanganya kujutia, au kupata hasara katika muamala, na pia[6] Imetajwa katika Aya : ((...يوْمَ يَجْمَعُكُمْ لِيَوْمِ الْجَمْعِ ۖ ذَٰلِكَ يَوْمُ التَّغَابُنِ ; Kumbukeni siku atakayowakusanya nyinyi kwa ajili ya siku ya mkusanyiko)).[7]

Hisia za watu wa peponi

Kwa mujibu wa baadhi ya tafsiri, baadhi ya waumini Siku ya Kiyama pia watahisi hasara, kwa sababu walishindwa kutumia fursa ya kufanya matendo mema, na wamepoteza malipofursa hiyo.

Rejea

  1. Daneshnameh Quran wa Quran Pazuhi, 1377, juz. 2, uk. 1256
  2. Makarim Shirazi, Tafsir Nemuneh, 1374, juz. 24, uk. 194
  3. Tazama: Tabrasi, Majma' al-Bayan, 1372 HS, juz. 10 uk. 450
  4. Tabrasi, Majma' al-Bayan, juz. 10, uk. 450
  5. Tabrasi, Majma' al-Bayan, juz. 10, uk. 450
  6. Farhangge Mu'in, Neno غبن
  7. Surat at-Taghabun, aya: 9

Vyanzo

  • Thaalabi, Al-Kashf wa Al-Bayan, 1422 AH, Juzuu ya 9, uk.328; Tayeb, Atyab Al Bayan, 1378, juzuu ya 13, uk.40.
  • Thaalabi, Ahmad bin Muhammad, Al-Kashf na Al-Bayan, Beirut, Daru Ihya Al-Turath al-Arabi, 1422 AH.
  • Husseini Hamadani, Seyyed Mohammad Hussein, Anwar Derakhshan, imefanyiwa utafiti na: Mohammad Baqer Behbuudi, Tehran, duka la vitabu la Lotfi, 1404 AH.
  • Ensaiklopidia ya Qur'an Studies, cha Bahauddin Khorramshahi, Tehran, Dustane-Nahid, 1377.
  • Tabatabaei, Seyyed Mohammad Hussein, Al-Mizan fi Tafsir al-Qur'an, Qom, Ofisi ya Machapisho ya Kiislamu ya Jumuiya ya Walimu ya Seminari, 1417 AH.
  • Tabarsi, Fadhl bin Hasan, Majma al-Bayan fi Tafsir al-Qur'an, Utangulizi: Mohammad Jawad Balaghi, Tehran, Nasser Khusruw, 1372.
  • Tayyeb, Sayyed Abdul Hussein, Atyab al-Bayan fi Tafsir al-Qur'an, Tehran, Islam, 1378.
  • Qur'ani Tukufu, iliyotafsiriwa na Mohammad Mehdi Foladvand, Tehran, Dar al-Qur'an al-Karim, 1418 AH/1376.
  • Motahari, Mortdha, ufafanuzi wa Kuifahamu Qur'an, Qom, chapa ya Sadra, 2004.
  • Makarem Shirazi, Nasser, Tafsir al-Nashon, Tehran, Dar al-Kutb al-Islamiya, 1374.
  • Mui’n, Mohammad, Farhang Mui’n