Nenda kwa yaliyomo

Wiki ya Umoja

Kutoka wikishia
Nembo ya Ukumbusho wa Wiki ya Umoja, mwaka wa 1366

Wiki ya Umoja (Kiarabu: أسبوع الوحدة الإسلامية) ni kipindi cha baina ya tarehe 12 Mfunguo Sita Rabiul-Awwal na 17 Mfunguo Sita Rabiul Awwal. Waislamu wa madhehebu ya Suni wanasema, Mtume (s.a.w.w) alizaliwa tarehe 12 Mfunguo Sita (Rabiul Awwal) mwaka wa Tembo (570 Miladia) na Waislamu wa madhehebu ya Shia wanasema kuwa, mjumbe huyo wa Mwenyezi Mungu alizaliwa tarehe 17 Mfunguo Sita mwaka huo huo. Hivyo madhehebu haya mawili yametofautiana kuhusiana na tarehe ya kuzaliwa Mtume (saww). Wiki ya Umoja ilipendekezwa na Ayatullah Muntazeri 27 Novemba 1981 na kuidhinishwa na Imamu Ruhullah Khomeini.

Mkutano wa Kimataifa wa Wiki ya Umoja hufanyika kila mwaka nchini Iran katika Wiki ya Umoja. Mkutano huu huandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu.

Historia Fupi ya Umoja na Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu

Angalia pia: Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu

Makusudio ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu ni kukurubiana wafuasi wa madhehebu za Kiislamu kwa shabaha ya kufahamiana ambapo kuna misingi na mambo ya pamoja ya wazi ambayo Waislamu wanashirikiana.[1] Wazo hili limekuwa lengo la wanazuoni wa Kiislamu wa Shia na Sunni kwa miaka mingi. Lakini tangu mwanzoni mwa karne ya 20, wanazuoni kama Sayyid Jamaluddin Asadabadi, Muhammad Abduh, Muhammad Hussein Kashif al-Ghita, Abdul Majid Salim, Mahmoud Shaltut, Muhammad Taqi Qomi na Ayatullah Boroujerdi waliipa kasi zaidi.[2]

Kwa kutokea kwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran mwaka 1979 na kuanzishwa kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kutokana na umakini wa kiongozi wake, Imam Khomeini, aliliendeleza wazo la umoja na kulipa wigo mpana zaidi.[3]

Kuainisha Wiki ya Umoja

Baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, mwaka 1981, Ayatullah Muntazeri alimuandikia barua Waziri wa Miongozo wa wakati huo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akipendekeza kwamba ili kupata maelewano na kuungana na Waislamu wengine, kipindi cha kati ya tarehe 12 Rabiul-Awwal (kumbukuumbu ya kuzaliwa kwa Mtume wa Uislamu (s.a.w.w) kwa mujibu wa hadith za Sunni) na tarehe 17 Rabi-ul-Awwal (tarehe ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa mujibu wa hadithi zilizothibiti kwa Waislamu wa Madhehebu ya Shia), kinapaswa kutangazwa na kupewa jina la Wiki ya Umoja.[4] Baada ya hapo, Imam Khomeini alitumia neno na istilahi hiyo ya (Wiki ya Umoja) katika hotuba ya tarehe 29 Disemba 1981, akiunga mkono pendekezo lake[5][6]. Imamu Khomeini alisema katika sehemu ya hotuba yake: «Sisi tunapaza sauti ya kwamba, tuwe na umoja sote na tuwe na wiki moja. Dini yetu ni moja, na Qur'ani yetu ni moja, na Mtume wetu ni mmoja».[7]

Kulingana na ripoti, pendekezo kama hilo tayari liiliwahi kutolewa huko nyuma. Kwa mfano, mwaka 1356 Hijria, Ayatullah Ali Khamenei, alipokuwa uhamishoni katika mkoa wa Sistan na Baluchistan, alipendekeza kwa wanazuoni wa Kisuni wa eneo hilo kwamba, kufanyike maadhimisho na sikukuu na maulidi ya Mtume kati ya tarehe 12 Rabiul-Awwal na tarehe 17 Rabiul-Awwal.[8]

Matukio Yanayo Husiana

Hitimisho la Kongamano la 32 la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu mwaka 2017.

Kila mwaka katika Wiki ya Umoja hufanyika Mkutano wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu nchini Iran. Lengo ni kuhakikisha kwamba, kunakuweko mfungamano na mshikamano baina ya Waislamu[9] na kuweko pia fikra za pamoja baina ya wanazuoni wao.[10]

Mnamo 1369 Hijria Shamsia, baada ya mwaka wa nne wa kufanyika kwake, kwa amri ya Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, kukaundwa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu. Miongoni mwa malengo yaliyobainishwa ya jumuiya hii ni "kuinua kiwango cha kufahamiana na maelewano na hali ya kufahamiana kati ya wafuasi wa madhehebu za Kiislamu na kuimarisha nyuga za udugu wa Kiislamu miongoni mwa Waislamu.[11]

Rejea

  1. «Darbareye Majmau», Tovuti ya Jahani Taqrib Madhahib Islami.
  2. «Darbareye Majmau», Tovuti ya Jahani Taqrib Madhahib Islami.
  3. «Darbareye Majmau», Tovuti ya Jahani Taqrib Madhahib Islami.
  4. «Az Pishnahad Ayatullah Muntadhari Ta Hurumat Sab Sahaba», Tovuti ya Ilina.
  5. Imam Khomeini, Shahifah Imam, 1389 S, juz. 15, uk. 455.
  6. Imam Khomeini, Shahifah Imam, 1389 S, juz. 15, uk. 455-456.
  7. Imamu Khomeini, Shahifah Imam, 1389 S, juz. 15, uk. 456.
  8. «Riwayat Tarikh: Hafte Wahdat Chegune Nameghozari Shud?».
  9. «Si wa Chahromin Konfaransi Baina al-Milal wa Wahdat Islami», Tovuti ya Jahani Taqrib Madhahib Islami.
  10. «Darbareye Majmau», Tovuti ya Jahani Taqrib Madhahib Islami.
  11. «Darbareye Majmau», Tovuti ya Jahani Taqrib Madhahib Islami.

Vyanzo