Wake za Imamu Hassan (a.s)

Kutoka wikishia

Wake za Imamu Hassan bin Ali al-Mujtaba (as) ni wanawake ambao wametajwa katika vyanzo vya historia kwamba, walikuwa wake za Imamu Hassan al-Mujtaba (as). Katika baadhi ya vyanzo, Imamu Hassan (as) ametajwa kwa jina la Mitlaq (yaani mtu anayetoa talaka sana) na hiyo imetokana na kudaiwa kwamba, Imamu huyu alio na kuacha sana. Mkabala na kauli hiyo, inaelezwa kuwa, Bani Abbas walitoa tuhuma ya mitlaq dhidi ya Imamu Hassan al-Mujtaba (as) kwa ajili ya kukabiliana na masharifu wa Kihassani (masharifu ambao nasaba yao inaishia kwa Imamu Hassan al-Mujtaba (as) na kama ripoti hizi zingekuwa sahihi basi Bani Umayyah wangetumia hilo kama silaha dhidi ya Imamu Hassan (as). Kutokuwa watu wa kuaminika wapokezi wa ripoti hizi kwa mujibu wa watalaamu wa Kishia na Kisunni wa elimu ya wasifu wa wapokezi wa hadithi ni ishkali nyingine na ukosoaji mwingine wa hadithi kama hizi. Kadhalika kutotajwa majina ya wake za Imamu Hassan (as) katika vyanzo vya historia, kutonasibiana idadi ya wake na watoto wa Imamu Hassan na harakati zake za kijamii na masuala ya dini na wingi wa ndoa anasonasibishwa nazo ni mambo ambayo kwa hakika yanakinzana na kutoakisi uhalisia wa mambo. Katika vyanzo wametajwa Khaulah bint Mandhur Fazari mama wa Hassan al-Muthanna, Ummu Is’haq binti ya Talha bin Abdallah Taymi, Ummu Bashir binti ya Uqbah bin Amru mama wa Zayd, Ja’dah binti ya Ash’tah, Nafilah au Ramla mama wa Qassim, Abdallah na Omar kuwa ni wake za Imamu Hassan (as).

Majina ya wake zake

Katika vyanzo kumetajwa wanawake 17 kuwa walikuwa wake za Imamu Hassan (as):

1. Khaulah bint Mandhur Fazari mama wa Hassan al-Muthanna.

2. Ummu Is’haq binti ya Talha bin Abdallah Taymi.

3. Ummu Bashir binti ya Uqbah bin Amru mama wa Zayd.

4. Hafsa binti ya Abdul-Rahman bin Abi Bakr.

5. Hind binti ya Suhail bin Amru.

6. Ja’dah binti wa Ash’ath.

7. Ummu Kulthum binti ya Fadhl bin Abbas bin Abdul-Muttalib.

8. Mwanamke kutoka katika ukoo wa Bani Thaqif.

9. Mwanamke kutoka katika familia ya wa Alqamah bin Zurarah.

10. Mwanamke kutoka katika kabila la Bani Kilab.

11. Mwanamke kutoka katika kabila la Bani Shayban kutoka katika ukoo ya Ibrahim Manqari.

12. Mwanamke kutoka katika Bani Shayban kutoka katika ukoo wa Hammam bin Murah.

13. Asmaa binti ya Atarud bin Hajib.

14. Binti ya Umair bin Ma’mun.

15. Binti ya Shalil bin Abdallah (mtoto wa kaka yake Jurair bin Abdullah Bajali). [1]

16. Nafilah au Ramla: Mama yake Qassim, Abdallah na Omar. [2]

17. Aisha Khath’amiyya. [3].


Kuitwa Imamu Hassan (as) kwa jina la “Mitlaq” (mtoa talaka sana)

Baadhi ya vyanzo vimemtaja Imamu Hassan (as) kwamba, alikuwa mtu mwenye kuoa sana na mwenye kutoa talaka sana “mitlaq”. [4] Katika vyanzo hivi idadi ya wake za Imamu Hassan (as) imetajwa kuwa ni 70, [5] 90, [6] 200 [7] na 250. [8]. Kwa mujibu wa Wilferd Ferdinand Madelung mtaalmu wa masuala ya Kiislamu na mtafiti wa Ushia wa Kijerumani ni kuwa, mtu wa kwanza ambaye alieneza uvumi kwamba, Imamu Hassan alikuwa na wake 90 ni Muhammad bin Kalbi na idadi hii ilitengenezwa na Madaini (aliaga dunia 225 Hijria). Pamoja na hayo, Kalbi alitaja majina ya wanawake 11 tu ambapo watano kati yao wanatiliwa shaka kama walikuwa wake za Imamu Hassan (as). [9] Kutokana na ripoti za vyanzo vilivyotajwa, Imam Ali (a.s.) alieleza wasiwasi wake kuhusu ndoa na talaka za mara kwa mara za Imam Hassan (a.s.) [10] na kwa ajili hiyo akawataka watu wa Kufa wasimpe mke. [11] Baqir Sharif Qurashi, mhakiki wa Kishia anasema kuwa, habari hii iliundwa na Bani Abbas kwa lengo la kukabiliana na masharifu waliokuwa wakitokana na kizazi cha Imamu Hassan [12] Kwa mujibu wa vyanzo vya kihistoria, wakati Mansour Abbasi alipomtia jela mjukuu wa Imam Hassan (as) yaani Abdallah Mahdh (al-Muthanna) kwa kutofichua maficho ya mwanawe Nafs Zakia, ambaye alianzisha uasi na mapinduzi dhidi ya Mansur alikuja na jambo hilo. [13] Kwa msingi huo, baadhi ya waandishi wamesema kwamba dai hili lilitolewa kwanza na Mansur Dawaniqi. [14] Na kama ripoti hizi zingekuwa sahihi Bani Umayya wangetumia hilo kama silaha dhidi ya Imamu Hassan (as) katika kipindi cha uhai wake. [15] Kadhalika kwa mujibu wa baadhi ya waandishi, mpokezi mkuu wa ripoti zilizotajwa, Abul Hassan Madaini, Abu Abdallah Waqidi Makki n.k ni miongoni mwa wanahistoria wa Ahlu-Sunna katika zama za Bani Abbas ambao walinukuu hadithi hizi kwa uadui au kwa wepesi wa kuamini mambo na kupitia kwao hadithi hizo zikaingia katika vyanzo vya Kishia [16] licha ya kuwa kwa mujibu wa wanazuoni wa Kisunni, hadithi za watu hawa si za kuaminika. [17] Kadhalika kutotajwa majina ya wake za Imamu Hassan (as) katika vyanzo vya historia, kutonasibiana idadi ya wake na watoto wa Imamu Hassan [19] na harakati zake za kijamii na masuala ya dini na wingi wa ndoa anasonasibishwa nazo ni mambo ambayo kwa hakika yanakinzana na kutoakisi uhalisi wa mambo. [20]