Unajisi wa mbwa
Makala hii inahusiana na wasifu kuhusu mafuhumu na maana ya kifikihi na hivyo haiwezi kuwa kigezo cha amali na matendo ya kidini. Kwa ajili ya amali za kidini, rejea katika vyanzo vingine.
Unajisi wa mbwa ni ashirio la mbwa kuwa najisi na viungo vyake vyote. Wanazuoni na mafaqihi wa Kishia na Ahlu-Sunna aghalabu wametoa fat'wa ya kwamba, mbwa ni najisi. Kadhalika ni haramu kuuza na kunua mbwa isipokuwa mbwa wa kuwinda na mbwa wa kufanya ulinzi. Haijuzu kutumiai ngozi ya mbwa kwa ajiili ya kulia na kunywea na mambo ambayo yanahitajia tohara. Chombo ambacho kimelambwa na mbwa au amenywea maji humo kinapaswa kusuguliwa kwa udongo. Hukumu ya unajisi wa mbwa haijumuishi mbwa wa baharini (beaver). Sayyid Murtadha, mmoja wa mafakihi wa Kishia anaamini kuwa, nywele za mbwa na nguruwe kutokana na kuwa zinatokana na kiungo kisicho na uhai, sio najisi. Malik bin Anas, mmoja wa wanazuoni na mafakihi wa madhehebu nne za Kisunni mtazamo wake yeye ni kwamba, mbwa sio najisi.
Utambuzi wa maana
Unajisi wa mbwa maana yake ni kwamba, viungo vyake vyote hata viungo visivyo na uhai kama nywele, kucha na unyevunyevu wote vyote hivyo ni najisi. [1] Hata hivyo, Sayyid Murtadha, mmoja wa mafakihi wa Kishia anaamini kuwa, nywele za mbwa na nguruwe kutokana na kuwa zinatokana na kiungo kisicho na uhai, sio najisi. [2] Kwa mujibu wa Muhammad Hassan Najafi ni kuwa, fat'wa ya Sayyid Murtadha inapingana na mtazamo wa mafakihi wengine wa Kishia. [3] Hata hivyo, Malik bin Anas, mmoja wa wanazuoni na mafakihi wa madhehebu nne za Kisunni mtazamo wake yeye ni kwamba, mbwa sio najisi. [4] Hoja za kuthibitisha unajisi wa mbwa ni hadithi zilizonukuliwa kutoka kwa Maimamu Maasumu. Hadithi hizi zinapatikana katika kitabu cha Wasail al-Shiah, chini ya milango ya: " بَابُ نَجَاسَةِ الْکلْبِ وَ لَوْ سَلُوقِیا" (Mlango wa unajisii wa mbwa hata akiwa muwindaji) [5] na «بَابُ نَجَاسَة سُؤْرِ الْکَلْبِ وَ الْخِنْزِیرِ» [6]
Kupaka udongo
Makala asili: Kupaka udongo
Chombo ambapo kimelambwa na mbwa au amenywea humo maji au kikiminika kingine, ili kukisafisha na kukitoharisha, kwanza kinapaswa kupakwa na kusuguliwa kwa udongo na kisha kuoshwa kwa maji kidogo au maji ya kiwango cha kulateni. [7] Endapo kitaoshwa kwa njia nyingine bila ya kupakwa na kusuguliwa kwa udongo, hakitatoharika. [8]
Hukumu ya kununua na kuuza mbwa
Kwa mujibu wa rai ya mafaqihi, kununua na kuuza mbwa ni haramu; hii ni kwa sababu mbwa ni najisi halisi, na hana thamani ya kifedha na hivyo haiwezekani kuuza na kununua. [9] Hukumu hii inahusiana na mbwa mzururaji, [10] na haihusiana na mbwa wa kuwinda au mbwa wa ulinzi ambao kimsingi wana manufaa hivyo hawahusishwi na hukumu hii. [11]
Kufuga mbwa
Kwa mujibu wa fat'wa ya Ayatullah Makarim Shirazi, ni kuwa, hakuna tatizo kufuga na kulea mbwa ambao wana faida kama mbwa wa ulinzi, mbwa wa kuwinda, mbwa wa kutafuta watu walio hai (hasa katika matukio ya tetemeko la ardhi ambao wamekwama chini ya kifusi) na mbwa wa kunusa na kukamata madawa ya kulevya licha ya kuwa ni najisi. Lakini kuna ishkali katika kulea na kufuga mbwa kwa ajili ya mapambo, kwa ajili ya kuishii naye pamoja na kumfanya kama kiburudisho. [12] Na kwa hakika si katika hadhi na heshima ya Waislamu kulea na kumiliki mbwa kwa namna hii. [13] Baadhi ya Marajii Taqlidi wanasema, ni makuruhu kumuweka (kumfuga) mbwa nyumbani. [14]
Hukumu zingine
• Kitu ambacho kimegusana na mwili wa mbwa, kama unyevunyevyu umetoka katika mwili wa mbwa na kuhamia katika kitu hicho, basi kinanajisika. [15]
• Kwa mujibu wa fat'wa za mafaqihi wa Kishia, hukumu ya kwamba, mbwa ni najisi inahusiana tu na mbwa anayeishi nchi kavu na haijumuishi mbwa wa majini. [16]
• Ni haramu kulia chombo ambacho kimetengenezwa kwa ngozi ya mbwa. [17] Kadhalika kwa mujibu wa mafakihi ni kwamba, chombo kama hicho hakifai kutumika katika kazi ambazo tohara ni lazima ndani yake kama vile kutilia nacho udhu au kufanyia ghulsi (josho). [18] Akthari ya mafaqihi wanaamini kwamba; haifai kutumia katika mambo mengine hata yasiyokuwa ya kunywea na kulia kama chombo kimetengenezwa kwa ngozi ya mbwa au nguruwe. [19]
• Mbwa ni najisi halisi, na kwa msingi huo anatoharika tu kwa istihala (kubadilika najisi kuwa tohara) na haitohariki kwa kusafishwa na kwa kutumia vitoharishaji. [20]
• Kwa mujibu wa fat'wa ya mafakihi, kumsafisha mbwa au kumpiga rangi ya viatu, hayo hayapelekea atoharike; kwani hakuna dalili kwamba, unajisi wa mbwa unatokana na kuzurura kwake na kuwa kwake mchafu. [21]