Nenda kwa yaliyomo

Thaqalain

Kutoka wikishia
Makala hii inahusiana na neno Thaqalain (Vizito Viwili). Kama unataka kufahamu kuhusiana na Hadithi ya Thaqalain angalia katika Hadith Thaqalain.
Hadithi ya thaqalein

Thaqalain au Thiqlain (Kiarabu: الثَقَلَين أو الثِقْلَين) vizito viwili, na kinachokusudiwa ni Qur'an na Ahlul-Baiti(a.s). Katika hadithi ya Thaqalain, Bwana Mtume(s.a.w.w) ameuusia Umma wake ushikamane na viwili hivyo. Neno hili limechukuliwa kutoka katika hadithi hiyo.

Katika lugha ya Kiarabu Thiqlu ina maana ya mzigo[1], Thiqal ina maana ya uzito[2] na Thaqal ina maana ya kitu chenye thamani[3]. Ni kwa kuzingatia hilo ndio maana Thaqalain imekuwa ikitolewa fasiri na maana ya vitu viwili vyenye thamani kubwa. Neno Thaqalan lililokuja katika Aya ya 31 ya Surat al-Rahman na makusudio yake, wafasiri wameona na kutambua kuwa ni makundi mawili ya majini na watu,[4] katika hali ambayo baadhi wanaona kwamba, makusudio ya thaqalan ni Kitabu cha Qur’an na kizazi cha Mtume (watu wa nyumbani kwake).[5]

Bwana Mtume(s.a.w.w) Katika hadithi ya thaqalain, anawataka umma wake ushikamane na vitu viwili vyenye thamani: Anasema: (إنّي تاركٌ فيكم الثقلين ما إن تَمَسَّكتم بهما لن تضلّوا بعدي: كتاب الله وعترتي أهلَ بيتي، لن يفترقا حتى يردا عليّ الحوضَ) (Hakika mimi ninakuachieni vizito viwili ambavyo mkishikamana navyo kamwe hamtapotea)[6] baada yangu (navyo ni) Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu (watu wa nyumba yangu).))

Katika baadhi ya nukuu za hadithi hii, Mtume Muhammad (s.a.w.w) ameitambulisha Qur’an kama kizito kikubwa na watu wake wa nyumbani kuwa ni kizito kidogo.[7]

Rejea

  1. Ibnu Manzhur, Lisan al-‘Arab, 1414 H, juz. 11, uk. 85.
  2. Ibnu Manzhur, Lisan al-‘Arab, 1414 H, juz. 11, uk. 85.
  3. Qarashi, Qamus al-Qur'an, 1412 H, juz. 1, uk. 307-310.
  4. Ibnu Kathir, Tafsir al-Qur’an al-‘Azhim, 1415 H, juz. 4, uk. 447; Abul Futuh al-Razi, Tafsir Raudh al-Jinan, 1387 S, juz. 10, uk. 396.
  5. Al-Qummi, Tafsir al-Qummi, 1405 H, juz. 2, uk. 345; al-Bahrani, Tafsir al-Burhan, 1334 H, juz. 4, uk. 267.
  6. Al-Nasa’i, al-Sunan al-Kubra, 1411 H, juz. 5, uk. 45; al-Kulaini, al-Kafi, Dar al-Kutub al-Islamiyyah, juz. 1, uk. 294.
  7. Al-'Ayashi, Tafsir al-‘Ayasyi, 1380 H, juz. 1, uk. 5.

Vyanzo

  • Quran
  • Ibnu Kathir, Tafsir al-Qur’an al-‘Azhim, cetakan Ali Shiri, Beirut: Dar Ihya’ al-Turatshal-‘Arabi, (1415 H).
  • Ibnu Manzhur, Muhammad bin Mukarram. (1414 H). Lisan al-‘Arab, revisi Ahmad Faris, Beirut: Dar al-Fikr li al-Tihabaʻah wa al-Nashr wa al-Tauziʻ.
  • Abul Futuh al-Razi. (1387 S). Tafsir Raudh al-Jinan wa Ruh al-Jinan, revisi dan catatan Abul Hasan al-Syaʻrani dan Ali Akbar al-Ghaffari, Tehran: n.p.
  • Al-Bahrani, Hashim bin Sulaiman, Tafsir al-Burhan, revisi Mahmud bin Jaʻfar al-Musawi al-Zarandi, Tehran: Chapkhaneh Aftab, (1334 H ).
  • Al-‘Ayashi, Muhammad bin Masʻud, Tafsir al-‘Ayahyi, teliti ulang Sayyied Hashim al-Rasuli al-Mahallati, Tehran: Chapkhane Elmiyyeh, (1380 H ).
  • Al-Qurasyi, Sayyied Ali Akbar, Qamus al-Qur’an, Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiyyah, (1412 H).
  • Al-Qummi, Ali bin Ibrahim. (1405 H). Tafsir al-Qummi, revisi Thayyib al-Musawi al-Jaza’iri, Qom: Dar al-Kitab.
  • Al-Kulaini, Muhammad in Yakub, Al-Kafi, Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiyyah, (n.d.).
  • Al-Nasa’i, Ahmad bin Shuaib. (1411 H). Al-Sunan al-Kubra, Beirut: Dar al-Kutub al-‘Ilmiyyah.