Nenda kwa yaliyomo

Tawatur Ijmali

Kutoka wikishia

Tawatur Ijmali (Kiarabu: التواتر الإجمالي) ni moja ya vigawanyo vya Tawatur (hadithi iliyopokewa kwa kila njia na iliyokithiri mapokezi) ambayo mkabala wake ni Tawatur Lafdhi na Tawatur Maanawi. Tawatur Ijmali inatumika kwa ajili ya majimui ya hadithi na riwaya ambazo zinatofautiana katika maana na lafudhi lakini zinakubaliana na kuafikiana katika madhumuni yake jumla.

Istilahi ya Tawatur Ijmali ilitumiwa kwa mara ya kwanza na Akhund Khorasani katika mjadala wa Khabar Wahed (hadithi ambayo kutokana na idadi ya wapokezi wake hakuna uhakika kama imetoka kwa Maasumu). Baada ya hapo Maulamaa wengine wa Kishia wakalijadili hilo. Baadhi ya Maulamaa wa Kishia wametilia ishkali suala la Tawatur Ijmali.


Tawatur

Makala asili: Tawatur

Tawatur ina maana ya kunukuliwa hadithi kwa njia tofauti (na kwa wingi) kiasi kwamba, inaleta uhakika; kwani haiwezekani kusema kwamba, idadi yote hii ya wapokezi ni waongo au walifahamu kimakosa tukio.[1] Itibari ya tawatur inakubaliwa na wasomi na wanazuoni wa elimu ya Usul al-Fiq’h.[2]

Hadithi ya Mutawatir inagawanywa mara mbili, Mutawatir Tafsili na Mutawatir Ijmali. Tawatir Tafsili nayo inagawanyika mara mbili: Tawatur Lafdhi na Tawatur Maanawi.[3]

Utambuzi wa maana

Tawatur Ijmali ni mkabala wa Tawatur Lafdhi na Maanawi. Tawatur Lafdhi huundika pale sentensi maalumu inapokuwa na mambo ya kushirikiana katika kila ripoti na hadithi. Hadithi ya Thaqalayn imetajwa kuwa ni mfano wa Tawatur Lafdhi.[4] Tawatur Manawi yaani kuweko madhumuni maalumu katika riwaya, lakini kukawa na lafudhi tofauti. Mfano wa Tawatur Maanawi unatajwa katika ushujaa wa Imam Ali (a.s) ambao unachukuliwa kutoka katika riwaya na hadithi mbalimbali katika vita vya mwanzoni mwa Uislamu.[5]

Katika Tawatur Ijmali, hakuna ibara na madhumuni ya pamoja (hali ya kushirikiana katika hilo), lakini kupitia hadithi na riwaya kunachukuliwa matilaba ya pamoja baina yao; kama vile itibari ya Khabar Wahed ambayo inanukuliwa na Shia Imamiya ambaye ni thiqa na muaminifu ambapo madhumuni yake hayajaja na hayako katika hadithi na riwaya, lakini katika mujibu na kupitia majimui yake inaeleweka hivi.[6]

Wamesema: Kwa mara ya kwanza istilahi hii ilitumiwa na Akhund Khorasani katika maudhui na mjadala wa hoja za itibari ya Khabar Wahed.[7]

Itibari

Maulamaa wa Kishia na akthari ya Maulamaa wa Kisuni wameafikiana kuhusiana na itibari ya hadithi ya mutawatir;[8] lakini wametofautiana kuhusiana na Tawatur Ijmali.[9] Akthari ya wanazuoni na wasomi wa elimu ya Usul Fiq’h wanaikubali itibari yake;[10] lakini baadhi yao kama Shahidi Sadr na Muhammad Hussein Nainy ametilia ishkali aina hii ya mgawanyo wa Tawatur.[11]


Ishkali Nainy

Muhammad Hussein Naini anaitambua Tawatur kwamba, inaishia tu katika migawanyo mwili ya Tawatur Lafdhi na Maanawi. Ishkali yake katika Tawatur Ijmali ni kuwa, kama kuhusiana na Tawatur Ijmali itawezekana kufikia maana jumuishi na ya pamoja, hii ndio ile Tawatur Maanawi; lakini kama haitawezekana kufahamika kitu kama hicho, katika hali hii hakutakuwa na Tawatur na natija ya hilo hakutakuwa na itibari.[12]

Kumetolewa majibu kwa ishkali hii. Sayyid Abul-Qassim Khui mwanafunzi wa Naini anasema: Ishkali hii kama itakuwa ya mahali pake, basi Tawatur Lafdhi na Tawatur Maanawi navyo vitakuwa na ishkali pia; kwa sababu viwili hivi pia kuna uwezekano wa uongo kwa kila moja kati ya riwaya kwa sura ya kujitegemea.[13]


Rejea

  1. Mudhaffar, al-Muntiq, 1424 AH, uk. 333
  2. Tazama: Tusi, Al-Ida, 1417 AH, uk. 7; Mudhaffar, al-Mantiq, 1424 AH, uk.333; Sadr, Durus fi ilm al-usul, 1418 AH, uk. 270.
  3. Swafi, Bayan al-Asul, 1428 AH, juz. 2, uk. 152.
  4. Naraqi, Anis al-Mujtahidin, 1388 S, juz. 1, uk. 197
  5. Swafi, Bayan al-Usul, 1428 AH, juz. 2, uk. 154
  6. Maleki Esfahani, Farhange Istilahi Usul, 1379 S, juz. 1, uk. 309.
  7. Moruj, Muntaha al-Darayah, 1415 AH, juz. 4, uk. 423.
  8. Tusi, Al-Ida, 1417 AH, uk. 7.
  9. Valai, Farhange tashrihy istilahat usul, 1387 S, uku. 181.
  10. Valai, Farhange tashrihy istilahat usul, 1387 S, uku. 181.
  11. Husseini Haeri, Mabahith al-usul, 14087 AH, juz. 2, uku. 482-484
  12. Khui, Ajuwad al-Taqarirat, 1352 S, juz. 2, uk. 113.
  13. Husseini Ha'eri, Mabahith al-usul, 1408 AH, juz. 2, uk. 483.

Vyanzo

  • Husseini, Hairi, Sayyied Kadhim dan Sayyied Muhammad Baqir Shadr, Mabahis al-Ushul, Qom: Cetakan Markaz Nashr dan Maktab al-I'lam al-Islami 1408 H
  • Jazairi, Muhammad Ja'far, Muntaha al-Dirayah fi Taudhih al-Kifayah, Qom: Yayasan: Dar al-Kitab 1415 H
  • Khui, Sayyied Abu al-Qasim dan Muhammad Hussein Nainy, Ajwad al-Taqrirat, Qom: Irfan 1352 S
  • Maliki Ishafahani, Mujtaba, Farhangge Istilahat-e Ushul, Qom: Alimah 1379 S
  • Mudhafar, Muhammad Ridha. al-Mantiq, Qom: Yayasan al-Nahsr al-Islami 1424 H
  • Naraqi, Muhammad Mahdi bin Abi Dzar, Anisu al-Mujtahidin fi Ilmi al-Ushul, Qom: Yayasan Bustan-e Kitab 1388 S
  • Shadr, Muhammad Baqir, Durus fi Ilmi al-Ushul, Qom: Yayasan al-Nashr al-Islami 1418 H
  • Shafi, Luthfullah, Bayan al-Ushul, Dairah al-Taujih wa al-Irshad al-Dini fi Maktab al-Marja' al-Dini Ayatullah al-Udhma al-Sheikh Luthfullah al-Shafi al-Gulpaigani, Qom: 1428 H
  • Tusi, Muhammad bin Hassan, Al-'Uddah fi Ushul al-Fiqh, Qom: 1417 H
  • Wilai, Issa, Farhangge Tashrihiye Istilahat-e Ushul, Teheran: Penerbit Ney 1387 S