Tauthiq Aam
Tauthiq Aam “Uthibitisho au Uungwaji mkono wa Kiujumla” (Kiarabu: توثیق عام): Ni istilahi maalumu katika taaluma ya Hadithi na fani ya ‘ilmu al- rijal (Elimu inayotafiti maisha na sifa za wapokezi wa Hadithi). Istilahi hii huwa na maana ya kutangaza uaminifu na uungwaji mkono wa kijulma kwa mpokezi fulani au jumla ya wapokezi fulani wa Hadithi. Kwa mfano, pale azungumzwapo mpokezi fulani wa Hadithi, huku kukiwa na udadisi juu ya kuaminika au kutoaminika kwake, kisha mtu huyo akawa ni miongoni mwa wapokezi wa kitabu maalum, ambao wote wamechukuliwa kuwa ni waaminifu, katika hali hiyo, mtu huyo huchukuliwa kuwa ni mwaminifu kupitia uthibitisho huo wa jumla uliotambuliwa katika kitabu hicho. Mifano hai ya uthibitisho wa kiujumla, ni pamoja na; mtu kuwa ni wakili wa Imamu, kuwa na Hadithi nyingi, na kuwa Sheikh al-Ijaza ni (Shekhe aliye na uwezo wa kutoa ruhusa ya kupokea Hadithi kutoka kwake, yaani ni mwalimu aliyeruhusu wanafunzi wake kupokea Hadithi kutoka kwake).
Kinyume na uthibitisho wa kiujumla, kuna uthibitisho maalumu (uthibitisho makhususi), ambao unamaanisha kutangazwa kuaminifu wa mtu fulani binafsi kupitia jina na sifa zake maalum, baada ya kuchunguzwa sifa zake binafsi.
Wanataaluma wa fani ya ‘ilmu al-rijal wana maoni tofauti kuhusiana na vigezo vya uthibitisho wa kiujumla. Kwa mfano, Sayyid Abul-Qasim al-Khui anaamini; kuwa uthibitisho wa kiujumla uliothibitishwa na Ibn Qulawaih juu ya wapokezi wa kitabu chake "Kamil al-Ziyarat" unahusiana na walimu wake aliunukuu kutoka kwao moja kwa moja. Ila al-Hurr al-Amili anaamini kwamba; uthibitisho wa kiujumla wa Ibn Qulawaih unajumuisha wapokezi wote wa Hadithi za kitabu hicho.
Faida na matunda ya uthibitisho wa kiujumla husaidia pale unapokosekana uthibitisho maalumu; yaani, pale ambapo tutakuwa hatuna taarifa yoyote ile kuhusiana na udhaifu au umakini na uhalali wa mtu fulani. Hii ni kwa sababu ya kwamba; ikiwa mpokezi fulani atakuwa amepata uthibitisho maalum na makhususi, hapo hapatakuwa na hana haja tena ya kutumia uthibitisho wa kiujumla.
Ufafanuzi
Uthibitisho wa Kiujumla ni istilahi katika taaluma ya fani ya Hadithi, ambayo inamaanisha kutangazwa kwa uaminifu wa mtu au kundi la watu fulani miongoni mwa wapokezi wa Hadithi kwa mfumo wa kutakaswa kwa njia ya kiujumla. [1] Kinyume na uthibitisho wa kiujumla, kuna uthibitisho mwengine uitwao uthibitisho maalum au makhususi, ambao unamaanisha kutangazwa uaminifu wa mtu au watu kwa jina na kwa sifa zao maalum bila ya kutumia uthibitisho wa kiujumla. [2] Mfano mzuri wa uthibitisho na uungwaji mkono kwa njia binafsi na makhususi, tunaweza kuupata kutoka kwa Najashi, katika kitabu chake. Ambapo yeye kitabuni mwake amemtaja Muhammad ibn Abi Umair, kisha akampamba kwa sifa na hadhi maalumu mpokezi huyo kitabuni humo. [3]
Miongoni mwa mifano ya uthibitisho wa kiujumla, ni pale Najashi alipomtaja Ubaydullah ibn Ali ibn Abi Shu'ba, huku akiutaja ukoo wa Abi Shu'ba kuwa ni ukoo wa watu waaminifu. [4] Pia, Shahid Thani amesema kwamba; Mashaikh al-Ijaza (walimu waliruhusu wanafunzi wao kuchukuwa Hadithi kutoka kwao), kuwa ni miongoni mwa wapokezi waaminifu, na anaamini kwamba; mashekhe hao hawahitaji uthibitisho na ushahidi maalumu juu ya uaminifu wao. [5] Katika mifano miwili hii, ukoo wa Abi Shu'ba na Mashaikh al-Ijaza wamepata uthibitisho wa kiujumla.
Mfano mwingine ni wa wanazuoni wanaokubaliana na mtazamo huu, ni Muhammad Fadhil Lankarani, akitete uthibitisho na uaminifu wa Abdul-Rahman ibn Hammad pamoja na uhalali wa Hadithi zake, ameandika akisema kwamba; Ingawa Shahid Thani katika kitabu chake "Masaalik", amemtaja Abdul-Rahman ibn Hammad huku akimsifu kwa sifa ya kutokuwa na uthibitisho, na kwamba ni mtu asiyejulikana, na kuhukumu kwamba, Hadithi zake hazina nguvu; ila kwa kuwa mtu huyu ni miongoni mwa wapokezi wa "Kamil al-Ziyarat" na ni miongoni mwa watu waliojumuishwa kwenye uthibitisho wa kiujumla wa Ibn Qulawayh. Hivyo basi, uthibitisho huu wa kiujumla ni uthibitisho halali kwetu sisi. Hivyo basi, Hadithi za Abdul-Rahman ibn Hammad ni Hadithi zenye nguvu na zenye kukubalika. [6]
Mfano wa Uthibitisho wa Kiuumla katika Kitabu "Kamil al-Ziyarat":
Hadithi zilizomo katika kitabu hichi nimezikusanya kutoka kwa wapokezi waaminifu kabisa wa Kishia. Na wala ndani yake, hakuna hadithi yoyote ile iliyonukuliwa kutoka kwa wapokezi nadra wasiojulikana ambao si wapokezi mashuhuri wala si wanazuoni, jambo ambalo lingeliweza kuharibu sifa za wapokezi haya. [7] |
Aina za Uthibitisho wa Jumla
Mohammad Kadhim Rahman-Setayesh katika kitabu chake "Touthiqat 'Aam wa Khaas" (Uthibitisho wa Kiuumla na Makhususi), amegauwa uthibitisho wa kiujumla katika makundi manne tofauti, hii ni kulingana na aina ya ushahidi na njia za uthibitisho zilivyo. Yeye katika kitabu chake ametaja vigao vinne kama ifuatavyo:
1. Uthibitisho wa Waandishi wa Vitabu: Katika aina hii ya uthibitisho, baadhi ya waandishi wa vitabu vya Hadithi, ambao wao wenyewe ni waaminifu, wamewathibitisha wapokezi waliomio vitabuni mwao, ambao ni walimu wao ambao wamewapokea Hadithi zilizomo vitabu mwao kutoka kwao. Kwa mfano, Ali ibn Ibrahim katika utangulizi wa tafsiri ya Qur’ani ya Qummi, amethibitisha waandishi wote wa Hadithi wa Kishia waliomo katika kitabu chake, ambao walinukuu Hadithi zao moja kwa moja kutoka kwa Imamu (a.s). [8] Ibn Qulawaih katika kitabu chake "Kamil al-Ziyarat" na Muhammad ibn Mashhadi katika "Al-Mazar al-Kabir" na Muhammad Ali Tabari katika chake "Bisharatu Al-Mustafa", ni miongoni mwa wanazuoni waliotumia njia ya uthibitisho wa kijumla katika uhalalishaji wa yaliomo vitabu mwao. [9]
2. Uthibitisho wa Walimu wa Wapokezi wa Hadithi: Watafiti baada ya kuchunguza wapokezi fulani, wamegundua kuwa; wapokezi hawa walikuwa wakinukuu Hadithi zao kutoka kwa walimu wao ambao walikuwa ni watu waaminifu. Hivyo kile kitendo cha kupokea Hadithi zao kutoka kwa waaminifu hao tu, kimekuwa kukitumika kama ni ithibati tosha ya kuthibitisha uhalali wa wapokezi hao. Aina hii ya uthibitisho hupatikana kupitia vitendo vya wapokezi, na si kupitia maneno yao. Kwa mfano, Kashshi anaamini kwamba; Hadithi zote zile zitokazo kwa Ashabu Al-ijmaa (kundi maalumu la wapokezi wlikubalika mbele ya wanazuoni) ni sahihi, hii ni kulingana na makubaliano ya viongozi (wanazuoni) wa Kishia. Kutokana na kauli hii, walimu wa Ashabu Al-ijmaa wanaaminika, na wanahisabiwa kuwa ni miongoni mwa wapokezi waaminifu. Mfano mwingine ni kwamba Najashi alionyesha mshangao mkubwa juu ya baadhi wapokezi waaminifu walinukuu kutoka kwa wasimulizi wasio waaminifu. Kutokana na kauli hii ya Najashi, watafiti hawa wanaamini kwamba; walimu wa moja kwa moja wa Najashi walikuwa ni watu waaminifu. [10]
3. Uthibitisho Kulingana na Vigezo Maalum: Baadhi ya wataalamu wa fani ya ‘ilmu al-rijal wamini kuwa; kule mpokezi fulani kupewa hadhi na sifa maalumu, ni moja wapo ya ishara za uthibitisho wa mtu huyo. Kwa mfano, kulingana na imani ya baadhi ya watafiti ni kwamba; miongoni mwa sifa zinazowe kuashiria uthibitisho na uaminifu wa mpokezi fulani, nipamoja na; mpokezi fulani kuwa ni wakili wa mmoja wa Maimamu, [11] kuwa Sheikh al-Ijaza, [12] kuwa na Hadithi nyingi [13], kuwa na kitabu msingi (Kitabu Asili) cha Hadithi, [14] na kuwa rafiki na mwandamani wa Ma'asum. [15]
4. Uthibitisho kwa Familia za Waandishi wa Hadithi: Baadhi ya familia ambazo zinajulikana kwa sifa nzuri zimepewa uthibitisho maalumu wa wataalamu wa ‘ilmu al-rijal, huku wakitambilwa kuwa ni miongoni mwa wapokezi waaminifu. Miongoni mwa familia hizi ni pamoja na; familia ya Abu Shu'ba Halabi, familia ya Rawwaasi, na familia ya Abu Jaham. [16]
Masharti Yanayoathiri Kukubalika kwa Uthibitisho wa Kiuumla
Watafiti mbali mbali wa Hadithi wameingia kazini katika kulifanyia kazi suala la uthibitisho wa kiujumla, pamoja na kuchunguza vipengele mbalimbali vinavyoathiri muktadha wa kukubalika kwa uthibitisho wa kiujumla, pamoja na namna ya ufanyaji kazi wake katika kuthibitisha uaminifu wa watu fulani. Baadhi ya vipengele hivi ni kama ifuatavyo:
1. Utafuiti wa Kiwango cha Upeo cha Ujumuishaji wa Uthibitisho wa Kiujumla
Kuhusiana na wigo wa kiwango cha uthibitisho wa kiujumla, ni muhimu kuzingatia namna ambavyo uthibitisho huu unahusiana na wahusika mbalimbali. Hata hivyo, kumekuwa na tafsiri tofauti kati ya wanazuoni wa fiqhi kuhusu jambo hili. Kwa mfano, Sayyid Abul-Qasim al-Khui anaamini kwamba; uthibitisho wa kiujumla ulioelezwa na Ibn Qulawaih katika utangulizi wa kitabu chake Kamil al-Ziyarat, unahusiana tu na walimu wake wa moja kwa moja, ambao yeye mwenyewe amepkea Hadithi zake kutoka kwao, bila ya kuwepo mpokezi mwengine katikati. Kinyume chake, al-Hurr al-Amili anaamini kwamba; uthibitisho huu ni sahihi kwa wapokezi wote wa Hadithi za kitabu hicho, hata wale ambao Qulawaih alipokea kutoka kwao huku wao wenyewe wakiwa wanamnukulia Hadhiti hizo kutoka kwa watu wengine. [17]
2. Uhalali Unaotegemea Msingi wa Itikadi za Wanazuoni wa ‘Ilmu Al-Rijal
Wanazuoni wa ‘ilmu a-rijal hutumia misingi na sababu tofauti katika kukubali uaminifu wa watu fulani. Misingi hii ni pamoja na:
- Uthibitisho unaojengeka kupitia itikadi juu ya uhalali wa habari zinazotolewa na mtu mmoja (hujiyyatu khabaru waahid).
- Uthibitisho unaojengeka kupitia ushahidi unaotolewa na mashahidi fulani juu uaminifu wa mpokezi fulani.
- Uthibitisho unaojengeka kupitia yakini na umahiri binafsi (utaalamu wa mhusika) wa mwanazuoni mwenye bila ya kutegemea maelezo ya watu wengine juu ya uaminifu wa mpokezi fulani.
Kwa mtazamo huu, wanazuoni fulani wanaweza kukubaliana na uthibitisho fulani ambao haujafikia vigezo vya kisheria vya kukubalika habari za nukuu ya mtu mmoja (khabaru waahid), hii ni kutokana na iamani yao ya kwamba; sifa ya uaminifu juu ya mpkezi fulani, inaweza kufikiwa kupitia yakini binafsi inayofikiwa na mwanazuoni mwenyewe, inatosha katika kukubaliana na usahihi wa Hadithi fulani. [18] Kwa mfano, Sayyid Abul-Qasim al-Khui hakukubaliana na uthibitisho wa uaminifu uliotolewa na Muhammad ibn Mashhadi katika kitabu kiitwacho al-Mazar, kuhusiana na wapokezi wa Hadithi alizozinukuu kitabuni humo. Hii ni kwa sababu ya kwamba; kuna pengo kubwa la kiwango cha zama, kati ya Mashhadi na watu waliothibitishwa uaminifu wao ktabuni humo, hali iliyofanya taarifa hizo kuwa za kubahatisha. [19] Kwa mujibu maelezo ya Rahman-Setayeshi, ni kwamba; iwapo mwanazuoni fulani atakubaliana msingi wa uaminifu mpokezi fulani unaojengeka wa kupitia yakini yake yeye mwenyewe, hapo hapatakuwa na mashaka kuhusiana uthibitisho ulithibitisha na mwanzuoni juu ya wapokezi walioshi kindi cha kabla yake. [20] Hii ni kwa sababu ya kwamba; ikiwa sisi tutakubaliana na uaminifu unaothibika kupitia yakini ya mtu mwenyewe inayotegemea uchunguzi wake mwenyewe, hapo hapatakuwa na haja ya kuuliza swali, kwamba je mthibitishaji wa uaminifu wa mpokezi fulani yeye mwenyewe alikuwa kakiishi zama moja na mpokezi huyo au la? Kwa sababu ya kwamba; mtu anaweza kumtafiti mtu mwengine aliyeishi katika zama za kabla yake, kisha akatoa maoni yake kulingana na viashirio mbali mbali alivyovipata. [21]
3. Uhusiano kati ya Uthibitisho wa Kiuumla na Makhususi
Ufanisi hasa wa uthibitisho wa kiujumla hufanaya kazi pale ambapo hakuna uthibitisho makhususi au hakuna taarifa njema wala mbaya kuhusiana na mpokezi fulani. Hata hivyo, ikiwa mpokezi atakuwa ametakaswa kupitia uthibitisho makhususi, basi hapatakuwa na haja ya kutegemea au kutafuta uthibitisho wa kiujumla. [21] Aidha, endapo mpokezia fulani atakuwa na uthibitisho wa kiujumla, kisha wataalamu wa fani ya ‘ilmu al-ijal wakachunguza na kuibua mapungufu fulani juu ya mpokezi huyo, uaminifu wa mpokezi huyo unaweza kupoteza uhalali mbele ya baadhi ya wanazuoni wa fiqhi. [22]