Tamko au ibara ya Haihata mina al‑dhilla
Tamko au ibara ya Haihata mina al‑dhilla “هَیهَاتَ مِنَّا الذِّلَّة” (hasha! kamwe hatutasalimu kwa udhalili): Ni sehemu ya khutba ya Imamu Hussein (a.s) aliyoitoa siku ya ‘Āshūrā, akilihutubia majeshi la Ibnu Sa‘ad. Kwa mujibu wa vyanzo vya kihistoria, Imam Hussein (a.s) alitamka kauli hii akimjibu Ibnu Ziad aliyempa hiari kati ya kusalimu amri au kuchukua maamuzi ya kupigana. [2] Katika hutuba yake hii, Imamu Hussein (a.s), alimjibu Ibnu Ziad kwa kuwambia kuwa; Kwa kuwa hakuna hata mmoja kati ya Mwenye Ezi Mungu na Mtume, na wala hakuna akili timamu inayokubali udhalili, basi kifo cha kufa kiheshima ni bora mno kwake, kuliko maisha ya fedheha. [3] Mas‘udi ambaye ni mmoja wapo wa wanahistoria wa karne ya nne Hijiria, ananukuu ibara hii kama ifuatavyo: «ألا وَإنَّ الدَّعيَّ ابنَ الدَّعيِّ قَد رَكَّزَ بَينَ اثنَتينِ بَينَ السِلَّهِ وَالذِلَّةِ وَهَيهاتَ مِنّا الذِلَّةُ» “(Eleweni ya kwamba; Mpachikwa nasabu isiyokuwa yake (mwana wa zinaa), na mwana wa mpachikwa nasabu isiyokuwa yake) amenihiarisha kati ya mambo mawili: ima upanga (vita) au (kukubali) udhalili; nasi kamwe hatukubali (kutumbukia katika) udhalili.” [5] Hata hivyo, baadhi ya vyanzo vimenukuu «القتلة» kwa maana ya vita, badala ya neno «السلة» lenye maana ya kuchomoa upanga kwa ajili ya vita, [6] pia vyanzo vyengine vimenukuu neno «الدَّنِیئَةُ» lenye maana ya uduni, badala ya neno «الذِّلَّة» lenye maana ya udhalili. [7] Katika zama za hivi sasa, ibara ya “Haihata mina al‑dhilla” imegeuka kuwa ni moja ya kauli mbiu muhimu ya kiupinzani katika muktadha wa kisasa. Waumini wa jumuia mbali mbali za Kishia, huinua sauti zao wakiitamka kauli hiyo katika maombolezo pamoja na maandamano yao mbali mbali, ili kutangaza kutosalimu kwao amri mbele ya ubeberu pamoja na kukataa aina mbali mbali za udhalilishaji. [8]