Nenda kwa yaliyomo

Sudair al-Sairafi

Kutoka wikishia

Sudair al-Sairafi: (Msimulizi Mashuhuri wa Kishia): Sudair al-Sairafi anajulikana kama ni mmoja wa wasimulizi maarufu wa Hadithi wa Kishia na ni miongoni mwa masahaba wa karibu wa Imamu al-Baqir na Imamu al-Sadiq (a.s). Familia yake pia ilikuwa na mchango mkubwa katika nyanja ya usimulizi wa Hadithi, kwani baba na watoto wake walikuwa ni miongoni mwa wasimulizi mashuhuri wa Hadithi na ni miongoni mwa Mashia. Takriban kuna kiasi cha Hadithi tisini zinazohusishwa na masimulizi ya bwana Sudair. Baadhi ya wataalamu wa elimu ya nasaba ya wapokezi wa Hadithi (elmu al-rijal), akiwemo Sayyid Abu al-Qasim al-Khoei, al-'Allama al-Hilli, na Mamaqani, walimhisabu bwana Sudair kama ni msimulizi mwenye kuaminika kuaminika. Kwa upande mwingine, pia baadhi ya wanazuoni wa upande wa Kisunni, kama vile Dhahabi walimtaja Sudair kuwa mtu wa kutegemewa na pia wametaja Riwaya kadhaa kuhusiana na uaminifu wake.

Isitoshe, pia kuna wasimulizi kadhaa maarufu walionukuu Hadithi kutoka kwa Sudair. Abd Allah bin Muskan, ambaye ni mmoja wanazuoni wanaokubalika mno miongoni mwa wanazuoni wa Hadithi, pia naye amenukuu masimulizi ya Hadithi zake kutoka kwa Sudair.

Hata hivyo, pamoja na sifa hizi, ila bado kuna baadhi ya Hadithi zilizoibuka Kumshutumu Sudair, ambazo zimesababisha baadhi ya wanazuoni kutilia shaka uaminifu wake.


Utangulizi na Nafasi ya Sudair b. al-Hakim b. Suhayb

Sudair bin al-Hukaim bin Suhaib, [1] anayejulikana pia kwa lakabu ya al-Sairafi [2] na kwa kuniya ya Abu al-Fadhli, [3] alikuwa ni mmoja wa wapokezi mashuhuri wa Hadithi za Imamu al-Baqir [4] na Imamu al-Sadiq (a.s). [5]. Baba yake, anayejulikana kwa jina la Hukaim, alikuwa mpokezi wa Hadithi anayenukuu Hadithi zake kutoka kwa Imamu al-Sajjad na Imamu al-Baqir (a.s), [6] wakati watoto wa Sudair, ambao ni Hannan [7] na Khalid, [8] pia walihusiana na masimulizi ya Hatihi za Imam al-Sadiq (a.s). Zaidi ya hayo, pia Khalid alihusiana na upokezi wa Hadithi kutoka kwa Imamu al-Kadhim (a.s). [9]

Kwa mujibu wa Mamaqani, mwandishi wa kitabu Tanqih al-Maqal, ni kjwamba; baba, babu, na mjomba wa Sudair walikuwa ni waumini wa madhehebu ya Mashia, na watu wa karibu wa Ahlul-Bait (a.s). [10] Ila Kushi (mtaalamu wa nasaba za wapokezi wa Hadithi), akitoa maelezo kusiana na Hannan, mtoto wa Sudair, amesema kwamba; baadae Hannan alijiunga na mrengo wa fikra za Waqifiyya, jambo lililoonyesha utofauti wa kimadhehebu ndani ya familia hiyo. [11]

Kwa ujumla, kuna kiasi cha Hadithi 68 zinahusishwa na Sudair kupitia nyaraka za wapokezi mbalimbali wa Hadithi, na kati ya hizo, kuna Hadithi 21 zilizonukuliwa moja kwa moja kutoka kwa Sudair mwenyewe yaani kupitia mdomo wake mwenyewe. [12] Hata hivyo, vyanzo vya kihistoria na vya elimu ya nasaba za wapokezi wa Hadithi (elmu al-rijal), vina taarifa chache mno kuhusiana na maisha binafsi na hali halisi ya Sudair. [13]


Uaminifu wa Sadir:

Wataalamu wa elimu ya rijal (wataalamu wa uchunguzi wa wasimulizi wa Hadithi) katika vyanzo vya mwanzo na vya baadaye wameonekana kutoa hukumu ya kukubaliana na uamini wa Sudair, kwani wataalamu hawa wakimzungumzia Sudair wamesema kwamba; Sudair ni miongoni mwa wasimulizi wenye kuaminika. Allamah Hilli, katika kitabu chake Khulasat al-Aqwal, anaona kuwa; kilio cha Imamu Sadiq (a.s) juu ya Sadir, na dua yake kwa ajili ya kuachiliwa kwake huru kutoka gerezani mwa serikali ya wakati huo, ilikuwa ni dalili tosha inayoashiria hadhi na daraja yake ya juu aliyokuwa nayo. [15] Ayatollah Khui, katika kitabu chake Mu'jam al-Rijal, anasema kwamba; wasimulizi wote ambao majina yao yanaonekana katika mnyororo wa masimulizi ulioko katika kitabu Tafsir Ali ibn Ibrahim na kitabu Kamil al-Ziyarat, wanachukuliwa kuwa ni watu wa waaminifu. Na kwa vile Sudair naye ni mmoja wa wasimulizi ambao jina lake linaonekana katika minyororo ya masimulizi ya vitabu viwili hivi, basi pia naye atahisabiwa kuwa ni msimulizi mwaminifu. [16] Mamaqani, mtaalamu wa Kishia wa fani ya Rijal (fani ya uchunguzi wa wasimulizi wa Hadithi), pia anaandika katika katika kitabu chake Tanqih al-Maqal akieleza ya kwamba; tukiangalia Hadithi mbali mbali tunaweza kueleweka kutokana na masimulizi kutokana na Hadithi hizo ya kwamaba, Sadir alikuwa ni mmoja wa wasomi wakubwa wa Kishia, ambao walikuwa na masimulizi na nukuu nyingi mno. Na kuna watu kadhaa mashuhuri miongoni mwa masahaba wajulikanao kwa jina la “Ashabu al-Ijmaa” (walioko kwenye jopo la walikubaliwa uaminifu wao), walionukuu Hadithi zao kutoka kwake, akiwemo Abdullah ibn Muskan. [17] walisimulia

Muhammad Jawad Shubairi, msomi wa Kishia wa elimu ya rijal (elimu ya uchunguzi wa wasimulizi wa Hadithi), akielezea juu ya uaminifu wa Sudair alisema kwamba; wasomi wa Kisunni ni wenye tahadhari mno juu ya wasimulizi wa Kishia, na kukiwepo dosari ndogo kuhusiana na msimulizi fulani wa Kishia, bila kusita huamua kutojali masimulizi ya msimulizi huyo. Ila licha ya kutajika kwake kwa jila la Ushia, utakutia kwamba, wasomi mashuhuri wa Kisunni wa eleimu ya rijal, akiwemo; Aqiliy na Ibnu Uday, wametoa hukumu zisemazo kwamba, Sadir ni mtu mwenye kuaminika. Zaidi ya hayo, Imamu Baqir (a.s) alipokuwa akimzungumzia bwana Sudair anamtaja, huku akimtaja kwa njia ya mafumbo (njia isiyo ya moja kwa moja), mazungumzo yake (a.s) yalionesha kwamba; Sudair alikuwa mtu maarufu katika zama za Imamu huyu. [18]

Hata hivyo, baadhi ya masimulizi yanaashiria kuwepo kwa ukosoaji au lawama fulani dhidi ya Sudair, [19] jambo ambalo limesababisha kutokubaliana na khitilafu miongoni mwa baadhi ya wasomi wa Kishia wa elimu ya rijal (elimu ya uchunguzi wa wasimulizi wa Hadithi), kuhusu uaminifu wake. Ayatullahi Khui, akikataa nadharia ya ukosoaji dhidi ya Sudair, anasema kwamba; kutoelewa vyema makusudio yaliokusudiwa katika Riwaya zinazumzungumzia Sudair, ndiko kulikosababisha baadhi ya watu kuamini kwamba; Sudair alikosolewa ndani ya Riwaya hizo, ilhali masimulizi ya Hadithi hizo si tu hayana sura ya kumkosoa Sudair, bali yamekuja kumsifu kwa nia ya kumsifu mpokezi huyu maarufu. [20] Ukiachana na hayo, pia baadhi ya masimulizi hayo yanayodokeza ukosoaji dhidi ya Sudair hayana minyororo ya wapokezi wenye kuaminika ndani yake, bali ndani ya mlolongo wa wapokeze wake, kuna wapokezi dhaifu ndani yake. [21] Dhahabi, mmoja wa msomi maarufu wa Kisunni wa elimu ya rijal (elimu ya uchunguzi wa wasimulizi wa Hadithi), katika kitabu chake Mizan al-I'tidal, amesimulia Hadithi fulani ndani ya kitabu chake hichi, ambayo imekuja kumsifu Sudair kutokana na Uaminifu aliokuwa nao. [22]


Wasimulizi Wanaonukuu Hadithi Zao Kutoka kwa Sudair

Orodha ya wanazuoni na wasimulizi wa Hadithi waliopokea na kunukuu masimulizi yao kutoka kwa Sudair al-Sairafi ni ya kipekee na inajumuisha majina maarufu katika historia ya elimu ya Hadithi. Wasimulizi hao ni:

1.     Abdullah bin Muskan – Mmoja wa wapokezi wa Hadithi wa kundi la As'habu-Ijmaa (walioko kwenye jopo la walikubaliwa uaminifu wao). [23]

2.     Hussein bin Nu'aym Sah'haf [24]

3.     Hukm bin Zubayr [25]

4.     Khattab bin Mus'ab [26]

5.     Abi-l-Wafa al-Muradi [27]

6.     Ishaq bin Jarir [28]

7.     Bakr bin Muhammad al-Azdi [29]

8.     Jamil bin Salih [30]

9.     Hanan bin Sadir - Mtoto wa Sadir. [31]

10.   Ruzayq bin Zubayr [32]

11.   Sa'dan bin Muslim [33]

12.   Hashim bin al-Muthanna[34]

13. Yunus bin Ya'qub [35]

14.  Sulayman al-Daymuli [26]