Sayyid Murtadha Murtadha al-Amili
Sayyid Murtadha Murtadha al-Amili (Kiarabu: السيد مرتضی مرتضی الحسيني العاملي) ni alimu na mwanazuoni wa Kishia wa Lebanon. Sayyid Murtadha ni mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) na mubalighi wa Kishia nchini Kenya. Yeye ni nduguye Sayyid Ja’afar Murtadha al-Amili (aliaga dunia: 1441 AH), mwandishi wa sira na mwandishi wa kitabu mashuhuri cha al-Sahih min Sirat al-Nabii al-A’dham. [1] Sayyid Murtadha Murtadha alizaliwa katika kijiji kimoja kusini mwa Lebanon. Mwaka 1964 alielekea Iraq kwa ajili ya kujiendeleza katika uga wa masomo ya dini na kujishughulisha na masomo ya dini katika Chuo Kikuu cha Kidini (Hawza) cha Najaf, Iraq. Mwaka 1970 kutokana na hali ya kisiasa ya Iraq, Sayyid Murtadha Murtadha alielekea Qom, Iran na kujishughulisha na masomo ya dini katika Hawza ya mji huo. Baada ya Mapinduzi ya Kiislamu na katika mwaka 1982, Sayyid Murtadha alihajiri na kuelekea Afrika Mashariki katika nchi ya Kenya na kuanza kuishi huko. [2]
Inaelezwa kuwa, safari ya Sayyid Murtadha al-Amili nchini Kenya na hatua yake ya kuanzisha Madrasa ya Rasul al-Akram katika mji mkuu wa Kenya Nairobi ni mambo ambayo yalichangia kupanuka harakati za Mashia na kufahamika imani na itikadi ya Ushia katika eneo la Afrika Mashariki. [3]
Rasul Ja’afariyan mtafiti wa masuala ya historia anasema kuwa, Murtadha Murtadha alikuwa akimsaidia kueneza na kutarjumi kwa lugha ya Kifarsi athari na vitabu vya Ja’afar Murtadha. [4] Yeye ametarjumu kitabu cha “Abu Dharr; muslim am Shuyui” (Abu Dharr; Muislamu au msoshalisti) kilichoandikwa na Sayyid Ja’far Murtadha. [5]
Murtadha Murtadha ni mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) [6] na ni mjumbe pia katika Baraza Kuu la Jumuiya ya kimataifa ya kukurubisha pamoja madhehebu za Kiislamu. [7].