Sajjad (Lakabu)

Kutoka wikishia

Makala hii inahusiana na lakabu ya Sajjad. Ili kufahamu kuhusu Imamu wa ىne wa Waislamu wa Kishia angalia makala ya Imamu Sajjad (a.s).

Sajjad (Kiarabu: السَجّاد) ina maana ya mtu ambaye ni mwingi wa kusujudu (mwenye kusujudu sana), [2] na ni katika moja ya lakabu mashuhuri zaidi za Imam Zainul-Abidin (a.s). [3] Imamu wa nne wa Waislamu wa Kishia anajulikana kwa lakabu ya Sajjad kutokana na kufanya sana ibada, kumpenda Mwenyezi Mungu na kumkabidhi moyo wake na kutokana na kusujudu sana. [4]

Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imamu Muhammad Baqir (a.s) katika kitabu cha Ilal al-Sharayi’, Imamu Sajjad alikuwa akisujudu katika mambo haya:

  • Wakati alipokuwa akikumbuka neema miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu.
  • Aliposoma Aya yenye sijda ndani yake.
  • Wakati Mwenyezi Mungu anapomuepusha na jambo baya.
  • Wakati Mwenyezi Mungu anapomuweka mbali na kitimbi na mfanya vitimbi.
  • Baada ya Sala.
  • Wakati alipokuwa akifanikiwa kuleta upatanishi na maelewano baina ya watu wawili.

Katika maeneo yote yanayogusa chini wakati wa kusujudu kulikuwa na alama ya sijida na ni kutokana na sababu hiyo akaondokea kuwa mashuhuri kwa lakabu ya Sajjad (mwingi wa kusujudu). [5] Ibn Hammad mshairi na malenga wa Kishia wa karne ya 4 Hijiria ana beti kadhaa za mashairi zinazotoa wasifu wa sijida za Imamu Sajjad (a.s).

و راهب أهل البیت کان و لم یزل *** یلقّب بالسجاد حسن تعبد یقضی بطول الصوم طول نهاره *** منیباً و یفنی لیله بتهجّد فأین به من علمه و وفائه *** و أین به من نسکه و تعبّد



[Alikuwa mtawa na mchajimungu wa Ahlu-Bayt Alitambulika kwa lakabu ya Sajjad kutokana na ibada zake njema Alikuwa akiomba maghurifa katika masiku yote]


Mchana alikuwa mwenye kufunga Swaumu na usiku alikuwa akiamka na kusali Sala za usiku. Ni nani mithili yake mwenye elimu na utekelezaji ahadi kama yeye? Na wapi anaweza kupatikana mwenye kuabudu na kuomba dua mithili yake? [6]