Nenda kwa yaliyomo

Orodha ya makhalifa wa Bani Umayya

Kutoka wikishia

Orodha ya makhalifa wa Bani Umayya ni watu kutoka katika ukoo wa Bani Umayya ambao waliongoza na kutawala kwa muda wa miaka 91 (41-132 Hijria) katika ardhi za Kiislamu. Idadi ya makhalifa wa Bani Umayya ilikuwa 14. Mtawala wa kwanza wao alikuwa Muawiyya na wa mwisho wao ni Marwan bin Muhammad.

Makhalifa wa Bani Umayya kutoka ukoo wa Abu Sufiyan

Makhalifa wa Bani Umayya ambao nasaba yao inaishia kwa Abu Sufiyan ni:

1. Muawiyya bin Abi Sufiyan (41[1]-60 Hijria [2]).

2. Yazid bin Muawiyya (60-64 [3] Hijria).

3. Muawiya bin Yazid (alitawala kwa takribani siku 40 mwaka 64 Hijria [4]).


Makhalifa wa Bani Umayya kutoka ukoo wa Mar’wan

Makhalifa wa Bani Umayya ambao nasaba yao inaishia kwa Hakam bin Abi al-A's bin Umayya ambao kutokana na kuwa khalifa wao wa kwanza ni Mar’wan wameondokea kufahamika kuwa ni watu wa Mar’wan. Watawala hao ni:

1. Mar’wan bin al-Hakam bin al-A's bin Umayya (64 - 65 Hijria [5]).

2. Abd al-Malik bin Mar’wan bin al-Hakam (65- 86 Hijria [6]).

3. Walid bin Abd al-Malik bin Mar’wan (86- 96 Hijria [7]).

4. Sulayman bin Abd al-Malik bin Mar’wan (96- 99 Hijria [8]).

5. Omar bin Abd al-'Aziz bin Mar’wan (99- 101 Hijria [9]).

6. Yazid bin 'Abd al-Malik bin Mar’wan (101- 105 Hijria [10]).

7. Hisham bin Abd al-Malik bin Mar’wan (105- 125 Hijria [11).

8. Walid bin Yazid bin Abd al-Malik (Khalifa Fasiki (125- 126 Hijria [12).

9. Yazid bin Walid bin Abd al-Malik (Yazid mpungufu) (miezi 6 katika mwaka 126 Hijria [13]).

10. Ibrahim bin Walid bin Abd al-Malik (126-127[14]).

11. Mar’wan bin Muhammad bin Mar’wan (Mar’wan punda) (127-132 Hijria [15].