Nenda kwa yaliyomo

Nawf al-Bikali

Kutoka wikishia

Nawf bin Fudhalah al-Bikali(Kiarabu: نَوف بن فُضالَة البِكالي) anayejulikana kwa jina la Nawf Bikali, ni mlinzi na mchunga mlango wa Imam Ali (a.s) wakati wa utawala wake. Nawf amepokea baadhi ya semi fupi na khutba za Nahj al-Balagha. Jina la Nawf halionekani katika vyanzo vilivyotangulia vya Mashia vya kuchambua wasifu wa wapokezi wa hadithi, lakini katika baadhi ya vyanzo vya hadithi vya Shia, kuna riwaya kutoka Imamu Ali (a.s) ambazo ananukuliwa yeye.

Maisha Yake

Nawfa bin Fudhala ni mmoja wa masahaba wa Imamu Ali (a.s), ambaye aliitwa Nawfa al-Bikali kutokana na kuwa na asili ya kabila la Bikalah au Bikkal, moja ya matawi la kabila la Himyar. [1] Baadhi ya watu walimchukulia kuwa ni mtu ya Bani Hamdan, ambao Mamqani amekataa mtazamo huo katika Tanqih al-Maqal. [2] Katika baadhi ya vyanzo, jina la baba yake limetajwa kuwa ni Abdallah. [3] Amru Bikali, sahaba wa Mtume (s.a.w.w), ambaye vidole vyake vilikatwa katika vita vya Yarmouk, anachukuliwa kuwa ndugu yake. [4]

Nawf alikuwa mtu wa Sham [5], na ndio maana ametajwa kuwa anatokana na watu wa Sham. Ibn Asakir amemtambuua Nawf kuwa ni mtu wa Sham na ametaja maelezo na ufafanuzi kkuuhusiana naye katika kitabu chake cha Tarilh Madinat Damascus. [6] Baadhi wamesema pia kuwa, alikuwa mtu wa Palestina. [7]

Kuniya ya Nawf ni Abu Yazid, [8] kama ambavyo Abu Amru imetajwa pia kuwa ni kuniya yake. [9]

Kwa mujibu wa nukuu ya Tarikh Tabari, mama yake Nawf, alioolewa na Kaa'b al-Akhbar baada ya baba yake Nawf kuaga dunia au kumpa talaka. [10]. Inaelezwa kuwa, Nawf aliuawa katika vita vilivyoibuka baina ya Muhammad bin Marwan na Waaremenia. [11]

Uhusiano Wake na Imamu Ali (a.s)

Nawf al-Bikali alikuwa mlinzi wa mlangoni wa Imam Ali (a.s.). Ametajwa kama Sahib, [12] Hajib [13] na sahaba maalumu wa Imamu Ali [14]. Amepokea na kusimulia baadhi ya minong'omo ya Imamu Ali [15] na baadhi ya khutba zake. [16] Nawf al-Bikali pia alimuomba Imamu Ali amshauri. Imamu Ali (a.s) alimshauri kuunga udugu, kutoshirikiana na madhalimu, kufanya urafiki na Ahlul-Bayt, kuacha usengenyaji na sifa nyingine za kimaadili zilizoamrishwa. [17]

Mamaqani anayachukulia mawaidha na nasaha za Imam Ali (a.s) kwa Nawf kuwa ni dalili ya ukubwa wa nafasi yake na nguvu ya imani yake, na anamchukulia kuwa ni miongoni mwa watu wema na kwamba, kuwekwa na Imam Ali (a.s) katika orodha ya watu wema ni ushahidi wa kauli yake. [18]

Hadithi

Katika vyanzo vya hadithi vya Kishia kuna hadithi zilipokewa na Nawf al-Bikal. Nawf amepokea pia baadhi ya semi fupi za Nahaj al-Balagha na khutba za Imamu Ali (a.s). [19] Kadhalika Nawf amepokea hotuba ya Hammam (ikiwa na tofauti kidogo) [20] kama ambavyo amenukuu hadithi kutoka kwa Imamu Ali (a.s) ambayo inaeleza sifa maalumu za Mashia. [21]

Nawf amesikia riwaya kutoka kwa Abdullah bin Amr As na Abu Ayyub Ansari, [22] Abu Ishaq Hamdani, Nusair bin Dhu'luq, Khalid bin Sabih, Abdul Malik bin Habib Juni, Amarah bin Juwayn Abdi, Shahr bin Haushab Ash'ari, [23] Abu Abdullah Shami, Abdul Ali [24] na Alqamah bin Qays [25] wamesimulia na kupokea hadithi kutoka kwake.

Jina lake halionekani katika vyanzo vya kale (vilivyotangulia) vya kueleza wasifu wa wapokezi wa hadithi wa Kishia; Ayatullah Khui ametosheka tu na kunukuu riwaya kutoka kutoka kwa Sheikh Saduq chini ya jina lake na hajatoa maoni yake kuhusu Nawf. [26] Katika baadhi ya vyanzo vya Sunni, imeelezwa kwamba kwa mujibu wa Nawf, maana ya Musa katika kisa cha Musa na Khidhr ndani ya Qur'an ni Musa mwingine asiyekuwa Mussa Mtume wa Bani Israil na ni kwa sababu hii ndio maana Ibn Abbas alimwita kuwa ni mwongo na adui wa Mwenyezi Mungu. [27]

Rejea

Vyanzo