Muhaddatha
Muhaddatha “المحدثة”: Ni mojawapo ya majina ya heshima yanayotumika katika kumtaja Bibi Fatima (s.a). Jina hili lina maana ya "Mwanamke Asemezwaye na Malaika." Pia jina hili limeonekana kunukiliwa katika masimulizi ya kidini katika kuwataja wanawake wengine, kama vile; Bibi Mariam (s.a) na Sara. Inasemekana kwamba; Malaika walikuwa wakimweleza Bibi Zahra (s.a) mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na; kumfarij, kumuarifu na kumjulisha hali za Waumini, pamoja na kumpa taarifa za matukio ya siku zijazo. Uwezokano wa Malaika kusemezana na Maimamu pamoja na Bibi Fatima (s.a) ni miongoni mwa kiini cha imani na itikadi za Mashia. Baadhi ya wafwasi fulani wa madhehebu ya Ahlu Al-Sunna wanadai kwamba; Mashia wanaamini juu ya unabii wa Maimamu wao. Lakini kwa mujibu wa maelezo ya Alamah Amini, mwandishi wa kitabu Al-Ghadir, ni kwamba; Suala la uwezo wa kusemezana na Malaika kwa wale wasio Mitume, ni miongoni mwa masuala yanayothibitishwa na pande zote mbili, Mashia pamoaja na Masunna; ila tofauti yao inahusiana na mifano tu ya watu waliobahatika kupata sifa hiyo. Muhaddatha “محدَّثه” Lakabu ya Bibi Fatima Muhaddatha" – kama ilivyobainishwa katika Hadithi za madhehebu ya Shia Ithna‘ashariyya – ni moja ya istilahi au majina 9 maalumu yanayomrejelea Bibi Fatima al-Zahra (s.a), linalomaanisha mwanamke anayesemezwa na Malaika [1] [2]. Istilahi hiyo, ambayo ni mojawapo ya lakabu za Bibi Fatima al-Zahra, pia inawahusiana na wanawake wengine ambao ni: • Sayyida Mariam (a.s.) (Mama wa Nabii Isa). • Yokabed (Mama wa Nabii Musa). • Sara (Mke wa Nabii Ibrahim). [3] Katika nakala za Mus-hafu Fatima (hati ya kiroho iliyoandikwa kupitia mafunzo ya Malaika, na kuandikwa na Imamu Ali), Bibi Fatima (s.a.) anathibitishwa waziwazi kuwa ni "Muhaddatha" (Msemezwa wa Malaika). [4] Pia jina hilo linaloashiria uwezo wake huo wa kiroho limetajwa katika kitabu kinachohisiana na Sala na salamu kwa bibi Fatima al-Zahra, ambapo ndani yake amepewa sifa ya "Muhaddatha al-‘Alima" (Mwenye Kusemezwa na Malaika na Mwenye Ufahamu wa Kipekee). [5] Maana ya Neno Muhaddatha Muhaddatha “مُحَدَّثه”: Ni neno linalomaanisha mtu anayezungumzishwa. [6] Msomi mashuhuri, Allama Amini, mwandishi wa Al-Ghadir, anasema kuwa; neno "Muhaddath" hutumika kumuelezea mtu ambaye si nabii, lakini huzungumza na malaika, au azungumzishwaye na Malaika. [7] Baadhi ya wanazuoni wameeleza kwamba; mazungumzo ya malaika na Bibi Fatima (a.s) yalikuwa yakihusiana na mambo makuu matano yafuatayo: • Kumpa faraja na kumliwaza • Kumletea habari kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) kuhusiana na nafasi yake huko Peponi • Kumjulisha matukio yatakayotokea baadae • Kumhabarisha kuhusiana na watawala • Kumfahamisha hali za waumini na makafiri. [8] Wapo pia wanaodai kuwa "Muhaddatha" kiuhalisia ni “Muhadditha” nayo ni sifa ya Bibi Fatima (a.s) inayomaanisha 'mzungumzaji', wakitoa hoja kwamba yeye alizungumza na mama yake akiwa bado yupo tumboni mwa mama yake. [9] [Maelezo 1: Qutb al-Rawandi, katika kitabu Al-Alqab al-Rasul wa Itratih, katika sehemu inayohusiana na majina ya Bibi Fatima, amemtaja Bibi Fatima akisema; "Mu'nisat Khadijah al-Kubra fi Batniha" (Mwenye kumtuliza Khadijah al-Kubra alipokuwa mjamzito huku akiwa tumboni mwake). [10]]
Uwezekano wa Malaika Kusemezana na Watu Wasio Manabii Makala ya Msingi: Ilhamu (Ufunuo kwa Njia ya Siri) Allamah Amini anabainisha akisema kuwa; imani ya kuwahusisha Bibi Zahra (a.s) na Maimamu Maasumina (a.s) na cheo cha "Muhaddathuna" (wale wanaosemezwa na Malaika) ni moja ya itikadi maalumu za Kishia. Kwa mtazamo wake, uwezekano wa Malaika kusemezana na watu wasio Manabii unathibitishwa na Mashia pamoja na Masunni. [11] Yeye anafafanua kwa kusema kwamba; tofauti katika jambo hili inahusiana tu na mifano hai ya watu waliotambuliwa kwa sifa hiyo, ambapo Washia, ni tofauti na Ahlu Sunna, wao hawamkubali Omar bin Khattab kama ni "Muhaddath" (miongoni mwa wasemezwa wa Malaika). [12] Abdullah Qasimi, mwandishi wa Kisalafi wa Saudi Arabia, katika kitabu chake As-Sira’a baina al-Islam wa al-Wathaniyya (Mapambano Kati ya Uislamu na Upagani), anawalaumu Mashia kwamba; Kule Mashia kudai kwamba, Bibi Fatima pamoja na Maimamu ni wenye kusemezwa na Malaika, kunawapelekea wao kuwafanya wao wawe na daraja sambamba na ile ya manabii. Ila Allamah Amini amekanusha madai haya. [13] Wanazuoni wa Kishia, wametumia Aya kadhaa, Ili kuthibitisha uwezekano kuwepo kwa mawasiliano kati ya Malaika na wasio Manabii. Miongoni mwa Aya zilizotumika katika suala hili, ni pamoja na; Aya ya 42 ya Suratu Al-Imran, Aya ya 71 hadi 73 za Suratu Hud, pamoja na Aya ya 7 ya Suratu Al-Qasas. Aya hizi ndizo ambazo zitoazo maelezo juu ya kuwepo kwa mazungumzo kati ya Malaika na baadhi ya wanawake waliotukuka katika jamii za kale. [14]